Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

JINSI YA KUIPATA FURAHA

 





    SIMULIZI FUPI SANA: JINSI YA KUIPATA FURAHA



    Kundi la takribani watu hamsini, wanaume kwa wanawake walihudhuria semina ya mambo ya kijamii.

    Lakini baada ya kufika katika hiyo semina mtangazaji mwenyekitii akaifungua hiyo semina kwa zoezi dogo.

    Akakusanya mapulizo (balloons) hamsini, akamkabidhi kila mmoja la kwake kisha akawapatia kalamu (marker pen) zinazofanana wino na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake katika pulizo lake.

    Baada ya kila mmoja kuandika, mapulizo yale yakakusanywa na kuwekwa katika chumba kimoja kikubwa.

    Kisha mtangazaji akawaambia ndani ya dakika tano kila mmoja awe amepata pulizo lenye jina lake.

    Watu waligongana, wakakanyagana, kila mmoja akilalamika kivyake akishika hili na kuliacha akienda huku na kule bila mafanikio. Hakuwepo wa kumuuliza maana kila mmoja alijikita katika kutafuta la kwake!!

    Baada ya dakika tano hakuna hata mmoja aliyekuwa amepata pulizo lenye jina lake.

    MWENYEKITI akabadilisha zoezi, akasema kila mmoja achukue pulizo lolote kisha amtafute mwenye jina hilo na kumpatia pulizo lake.

    NDANI ya dakika tano kila mmoja alikuwa ameletewa pulizo lake na yeye alikuwa amepeleka lisilokuwa lake kwa mwenye jina husika. Kila mmoja akafurahi na kuridhika.

    HAYA YANATOKEA katika maisha yetu… kila mmoja amejikita katika kuitafuta furaha yake na kamwe asiipate kisha anabaki kunung’unika.

    IPO HIVI!! FURAHA yetu imeegemea katika furaha za watu wengine.

    WAPE WATU FURAHA WANAYOHITAJI NA WAO WATAKUPA FURAHA YAKO!!

    **Barikiwa sana siku ya leo ewe mdau huku ukiamini kuwa huwezi kujitafutia furaha yako iwapo wewe unawanyima wengine furaha yao!!!

0 comments:

Post a Comment

BLOG