"
KAMANDA "
NGURUMO
za radi zilizoambatana na miale kadha wa kadha hazikutofautiana sana na ile
mizinga iliyopigwa miaka mingi nyuma.
Ni miaka mitano sasa imepita, awali nilikuwa nikija peke yangu katika udongo huu ulionyanyuka juu katika namna ya kuunda tuta la aina yake lisilopendeza sana kutazama machoni.
Sipo peke yangu leo katika tuta hili nipo na kiumbe mwingine ambaye angalau siku hii ya leo anaanza kupata maana halisi ya tuta hili.

Naam
ni kaburi ambalo walizikwa wanajeshi wapatao kumi na watano waliokufa katika
vita huko Somalia, miili yao iliharibika vibaya kiasi kwamba haikutamanika kuaga
na hivyo serikali ilitusihi sana tukubaliane na matokeo.
Wanajeshi wote wakazikwa katika kaburi moja kubwa.
Kati ya miili hiyo mmoja ulikuwemo mwili wako mume wangu, mume niliyelisahau jina lako la Amata na kukubatiza jina la Kamanda tangu ulipojiunga na jeshi na hatimaye kuwa mwanajeshi kamili.
Hakika ulikuwa kamanda, sio tu kwa sababu ya gwanda ulizokuwa unavaa bali jinsi ulivyopigana kiume ilimradi familia yako iweze kuja kuishi maisha mazuri, ulisaidia upande wa familia niliyotoka ya kimasikini bila kujal;i nduguzo watasema nini. Hatimaye ukanioa il;i wakae kimya.

Ukamanda
wako haukuishia hapo, wakazi wa Mbagala wanakulilia hadi hivi sasa, kwa jinsi
ulivyojitoa muhanga wakati ule lilipotokea tukio la mlipuko wa mabomu, watoto
uliowaokoa hivi sasa wapo shule ya msingi, usingekuwa wewe wangekuwa chini ya
madongo haya yaliyokufunika wewe.
Kamanda!! Leo hii nimekuja hapa na ninayazungumza haya nikiwa na kamanda mwingine chipukizi, kamanda ambaye haukuwahi kumuona wala yeye hajawahi kukuona zaidi ya picha zako tu zilizojazana tele ndani ya ile nyumba uliyoijenga.
Mara yako ya mwisho ulilibusu tumbo langu lililokuwa kubwa kiasi kutokana na ujauzito, ukasema kuwa iwe isiwe lazima nitazaa mtoto wa kike..... nikabisha nikasema nazaa kamanda wa pili.
Amata mume wangu huko ulipo tambua kuwa nimekuzaa wewe tena na leo hii nipo na wajina wako aliyeniuliza sana juu ya wapi ulipo na nini kilikutokea.
Amata!! Siamini kama kweli upo chini ya madongo haya kwa sababu sikuwahi kuushuhudia mwili wako uliodaiwa kuwa umeharibika vibaya mno.

Kamanda
nahisi upo hai na siku moja utarejea nyumbani ili umfunze wajina wako mambo
mengi kuhusiana na jeshi, kwa sababu maswali anayoniuliza nakosa majibu,
ananiuliza nini maana ya nyota, ananiuliza nini maana ya saluti. Nakosa majibu
kabisa namjibu uongo leo, kesho anakuja na swali jingine.
Na kinachonifanya niamini kuwa bado upo hai ni kitendo cha wajina wako kujitamba kila siku shuleni kuwa baba yake ni mwanajeshi na ni shupavu sana.
Kamanda!! Naumia sana moyoni mwangu kwa maneno makali niliyiopewa na ninayoendelea kupewa kutoka kwa ndugu zako, Kamanda huwezi amini eti wanadai nahusika katika kifo chako eti kisa tu ile nyumba uliyoijenga uliandika jina langu hivyo hawana haki ya kunifukuza.
Nakukumbuka sana kamanda uliniambia kuwa mtu akinikera basi sitakiwi kujifungia ndani na kuugulia huku machozi yakinibubujika badala yake nitembee na kukutana na watu ambao wapo upande wangu nizungumze nao na hapo nitapata faraja ya moyo.
Basi sina haja ya kuwa nazunguka sana faraja yangu ni huyu wajina wako, kila nikikereka nakaa karibu naye na kumsikiliza jinsi anavyonisimulia sinema alizoziona......

Kamanda!!
Huko ulipo napenda pia kukushirikisha hili jambo ambalo nashindwa kulikemea kwa
sababu sina nguvu katikati ya umma.
Ni kuhusu thamani ya mtu baada ya kifo chake, Kamanda, eti licha ya kujitolea kote kule, kaburi lako wewe na wanajeshi wenzako mliokufa mkipigana vita katika nchi isiyokuwa yenu hata hayajasakafiwa, ninapozungumza na wewe haya mvua inanyesha na ni matope yametapakaa, natumia uzoefu tu kulitambua kaburi hili kwa sababu huwa nakuja mara kwa mara kukusalimia maana sina pengine pa kukupata na kukupa salamu hizi.
Kamanda!!! Miaka yote nilikuwa nikifika hapa na kukueleza kuwa nimeukumbuka sana uwepo wako huku nikilikosa penzi lako maridhawa, lakini sikuwa hi kukueleza mengi yaliyojitokeza baada ya tukio hilo lililohusisha kifo chako na makamanda wenzako.

Kamanda!
nilikuwa Mwanza kwa ndugu zako, nadhani unajua jinsi gani ambavyo hawakuwa
upande wanguy mara zote lakini kumbuka mimi tayari nilikuwa katika ukoo wako
hivyo sikuwa na namna zaidi ya kwenda kuwajulia hali, na baada ya tukio ndipo
nikatambua ni kwa nini ulinikataza kata kata nisiende kwa ndugu zako bila uwepo
wako.
Awali nilitengwa na dada zako, hadi mama yako alikuwa akinitazama kwa jicho la tofauti.... ila haya yote niliyapuuzia japokuwa nilikuwa naumia sana.
Sasa ilipotumwa ile taarifa kuwa mmeuwawa mkiwa vitani, hapo kila mtu akanigeukia mimi kana kwamba ni mimi nilikulazimisha uende vitani!!
Kamanda! nisiendelee kuzungumza haya kwa sababu yananiumiza sana, ila cha msingi elewa kwamba baadhi ya watu walinishauri niitoe hii mimba uliyokuwa umeniachia eti mimi bado kigoli niweze kuolewa na mtu mwingine kwa sababu nduguzo walikuwa wamenitenga kabisa.

ningeweza kufanya kila kitu lakini sio kutoa kumbukumbu hii, hadi familia yangu
ilinisihi kuhusu jambo hilo na hadi wakafikia hatua ya kusema kuwa hawatamlea
mtoto ambaye ukoo wake umemkataa hata kabla hajazaliwa.
Nikaamua kusimamia uamuzi wangu, yaani laiti kama ile nyumba ungekuwa haujaandika jina langu sijui tu ningepitia wakati mgumu kiasi gani.....
Niliilea mimba hadi nikajifungua Kamanda, na hatimaye nikajiona nikiishi nawe tena katika mwili wa huyu mtoto wako.
Ni miaka mitano na miezi kadhaa sasa Kamanda!
Sijawahi kufikiria kuwa na mwanaume mwingine, nimeamua maisha yangu yote kumkabidhi Mungu.... nakumbuka uliwahi kuniambia sijui kuimba eti nina sauti mbaya... nahisi ulikuwa unanitania tu huwezi amini sasa naimba kwaya kanisani. Na wanakwaya wanasema najua kuimba....
Basi hiki ndicho nilichoamua, nimeamua kumuimbia Mungu kwa mema yote ambayo ananitendea na ninamshukuru kwa yote yaliyopita.....

Amata! Ningeweza kuwa na mwanaume mwingine, lakini hakuna mwanaume kama wewe na
simwoni akitokea mbele yanguhadi nitakapokutana nawe huko ulipo ama la ukirejea
kutoka ile safari uliyoondoka miaka mitano iliyopita huku ukinipa ahadi kedekede
kuwa utaniletea zawadi kutoka huko unapokwenda.
Nazisubiri zawadi zangu Kamanda kwa sababu bado naamini upo hai, ila basi tu haujataka kurudi nyumbani kwako.
Nimezungumza mengi sana Kamanda, naamini umenielewa na si jambo jipya wewe kunielewa ila siku hii ya leo mtoto wako wajina wako na kamanda mwenzako amenisihi sana kuwa kuna neno anahitaji kuzungumza na wewe, amesihi kuwa nisimwache nyumbani bali nije naye hapa anataka kusema na wewe.
“Amata mwanangu, baba yako anaishi chini ya udongo huu, zungumza ulichotaka kuzungumza atakusikia na atakujibu sawa mwanangu!!!” nilimweleza mtoto wangu, mtoto ambaye naweza kukiri kuwa alikuwa wa aina yake akiwa na uwezo wa kufikiri mambo makubwa sana tofauti na umri wake wa miaka mitano, ni kweli hakuwa mzuri katika kuunganisha visa olakini alikuwa anaongea na kueleweka.

Amata
alisogea mbele ya tuta lile akapiga magoti akiniiga nilivyokuwa nimefanya mimi
na hapo akaanza kuzungumza kwa sauti ya kitoto sauti iliyoniumiza sana hasahasa
kile alichokuwa anakisema.
“Baba kwa nini unaishi huku peke yako huku porini... nimekuja nikuchukue twende nyumbani.
Nilimwambia rafiki yangu Lameck baba yangu ni mwanajeshi akabisha... nataka aje akuone, nikimleta lameck utatoka humu baba ili na yeye akuone... halafu baba nataka na mimi nikiwa mkubwa niwe mwanajeshi kama wewe.
Nakusubiri utoke baba... kama mimi ni mtoto wako toka twende nyumbani.....”

Alimaliza
kuzungumza mwanangu Amata na kama masihara vile nilidhani tutaondoka, mtoto
akagoma kuondoka kabisa alikuwa analia akiita babaa babaa!!
Nilijaribu kumsihi sana nilimwongopea mambo mengi ilimradi tu aamini lakini kilio kilizidi kuwa kikubwa.
Kilio cha mtoto huyu kulilia kuwa anamtaka baba yake kiliniumiza sana na mwishowe na mimi nikajikuta nalia nikimsihi Kamanda kama anakisikia kilio cha mtoto wake basi atoke na kumtuliza walau mara moja tu!!
Lakini zaidi ya kelele za miti na ndege waliokuwa wanaruka hapa na pale hakuna jibu lililotoka. Palikuwa kimya... kimya kabisa!!
Kamanda hakuwa pamoja na sisi!!
Nikiwa sijajua nini cha kumfanya mtoto yule mara alianza kushangaa huku akirejewa na tabasamu.... na mara akazungumza.

“Mama...
baba amesema tutamkuta nyumbani... twende nyumbani mama twende!!” alinisihi
mwanangu huku akinivuta mkono.
Ilikuwa inastaajabisha sana hali ile, nikamfuata alichohamasisha tukaondoka.......
Uzuri ni kwamba tulipokuwa garini alisinzia nadhani hii ilisababisha akasahau alichokuwa amesema tutakikuta nyumbani......
Nilipofika nyumbani hata mimi roho ilikuwa inadunda nikitarajia kukutana na Kamanda wangu akiwa yu hai na tabasamu lake lile tamu la kupendeza.
Lakini palikuwa kimya sana na hapakuwa na dalili ya mtu pale ndani.

Nilipiga
goti na kumshukuru Mungu kwani niliamini kuwa mwanangu alikuwa walau ameisikia
sauti ya baba yake!!
Nikamwandalia chakula akala kisha akalala.
Nikaifunua ‘albamu’ nikazitazama picha kadhaa za hayati kamanda na kisha namimi nikaingia kulala.
Nililala nikiwa naamini kuwa alipangalo mola haliwezi kuepukika na linakuwa na makusudi yake.....
Nikaukumbusha moyo wangu kuwa usisononeke upya tena kwa sababu ya kukipoteza kipenzi cha moyo wangu!!!
Wakati nataka kuzima taa nikageuka kumtazama yule mtoto wangu..... nikaiona sura ya baba yake tupu katika uso wake.
“Kamanda Amata!!!” nikaita lile jina.... mtoto akatabasamu.
Nikafarijika moyoni kuwa nilikuwa nimezaa mwanajeshi mwingine ambaye atashabihiana na baba yake kila kitu!!!

LALA
KAMANDA LALA UPUMZIKE UMEZALIWA UPYA TENA!!
MWISHO!!!
0 comments:
Post a Comment