
Abunuwasi ni pale alipokuwa na
shida na Sultani. Kufika mlangoni kwa sultani wale mlinzi akakataa kumruhusu
aingie kumwona. Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe kumwona Sultani maana alikuwa
na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa abunuwasi akiingia kwa sulatani atapata
anachotaka maana alipendwa sana na sultani. Mkwara aliompa ni kwamba aahidi kuwa
atakachopata kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi
akakubali na akaingia kwa sultani. Kufika ndani sulatani anamuuliza sema shida
yako abunuwasi maaana leo unaonyesha una huzuni. Abunawasi akasema Seyidina
wangu naomba unichape viboko mia, Sultani akashangaa, kwa kosa gani? Abunuwasi
akasema nichape tu Seyidina wangu na akasisitiza kuwa haondoki mpaka achapwe.
Sulatani akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu
sana viboko mia. Walipomchapa mpaka viboko hamsini Abunuwasi akasema vimetosha
maana mlinzi wa pale getini tumekubaliana kuwa nitakachopata humu ndani kwa
sultani lazima na yeye apate nusu yake kwa hiyo hivyo hamsini vilivyobaki
atandikwe mlinzi. Sulatani kusikia hivyo akaghadhabika sana na kuamuru mlinzi
aletew apigwe viboko hamsini tena vya uhakika. Mlinzi alijuta kuzaliwa, na
hakurudia tena kuomba rushwa
0 comments:
Post a Comment