MKATABA WA WAFANYA KAZI WA TAWI LA BARANI LA KUUZA NGUO. Mimi mwenye kutia sahihi hapa chini ya mkataba huu, nimekubali kufanya kazi yoyote katika tawi la Barani la kampuni ya kuuza nguo kwa mshahara wa kila mwezi shilingi mia. Nimekubali ya kuwa nikiharibu kitu humo kazini lazima nikilipe. Nimekubali kuwa nyumba au shamba yangu ikamatwe na iuzwe nikataapo kulipa chochote nitakacho kiharibu.
Sahihi ya mfanya kazi .
Shahidi
Tarehe
Watu wengi hawakupenda kufanya kazi huko, lakini ilivyokuwa huko kulikuwa na upungufu mkubwa wa kazi, baadhi ya watu walitia sahihi zao katika mkataba na kufanya kazi. Mara nyingi Bwana Peku aliwalipisha watumishi wake kwa kuvunja au kuharibu kitu bila ya kukusudia, na alikuwa hasikilizi maneno ya mtu yeyote ila lazima alipe tu anapoharibu. Mara moja mwendeshaji motakaa wa hapo kazini alifikiliwa na ajali ya motakaa ya kuchopoka usukani. Motakaa hiyo iliacha njia na kwenda kujigonga kwenye shina la mti uliokuwepo karibu. Gari hiyo iliumia sana na haikuwezekana kutengenezwa. Kwa mujibu wa mkataba, nyumba ya mtu huyo iliuzwa ili ilipwe gari iliyovunjika. Huyo mwendeshaji gari iliyovunjika alisema kuwa yeye hakuigonga gari hiyo kwa makusudi bali ilikuwa ni ajali tu na ajali haikimbiliki, lakini hakusikilizwa. Bwana Peku alisema kuwa hataki maneno ya upuuzi. Watu wengi waliokuwa wakifanya kazi huko walipoteza majumba na mashamba yao kwa kuharibu mambo huko kazini. Bwana Peku hakupata amri kutoka ofisi kuu ya kuwatilisha watu sahihi za kuuziwa majumba yao au mashamba yao wanapoharibu kitu humo kazini. Alijifanyia hivyo kwa kuona watu hapo walikuwa wahitaji mno wa kazi. Mara nyingi watumishi wa Bwana Peku wakisema, 'Ajali haikimbiliki', wanapoharibu kitu hapo kazini, lakini Bwana Peku hakukubali kuwa ajali haikimbiliki na akisema, 'Sitaki maneno ya kipuuzi.' Mara moja Bwana Peku alilala na akaota kuwa atakufa kwa kuumwa na nyoka kipilili. Nyoka kipilili ni mdogo kuliko nyoka wote, lakini ana sumu kali. Alipoamka Bwana Peku aliogopa sana alitafutatafuta humo nyumbani mwake, kwani alidhani labda nyoka kipilili amejificha. Bwana Peku aliingiwa na wasiwasi mkubwa kila anapoifikiri ndoto aliyoiota. Kwa hivyo alikuwa hatembei misituni wala vichochoroni anamokaa nyoka huyo. Wasiwasi huo alikuwa nao kwa miaka mingi mwishoni ulimfanya kama hana akili. Siku moja Bwana Peku alikwenda karamuni. Huko watu walikaa chini juu ya majamvi. Basi alipofika hapo alianza kunyanyua majamvi na kuchungulia chini badala ya kukaa tu kama wenziwe. Watu walimwuliza kwa nini kufanya hivyo. Alisema kuwa aliota atakufa kwa sababu ya kuumwa na nyoka kipilili, basi hivyo kunyanyua majamvi alikuwa na shaka kuwa nyoka kipilili amejificha huko chini. Hao watu walisema kuwa hawajapata kumuona nyoka wa namna hiyo. Hapo Bwana Peku aliwachorea hao watu sanamu ya nyoka kipilili kwenye mchanga kwa kutumia kidole chake. Wakati alipokuwa akimtia meno alirusha mkono wake kwa upesi sana na kusema, 'Aa!! Nimechomwa na kitu kama shindano hapa kidoleni.' Hapo hapo sura ya Bwana Peku ilibadilika na akawa mweusi na alianza kutoa na kuvuta puma kwa namna ya mtu anayezimia. Watu walimpeleka hospitali kwa haraka na alipofika kwa daktari alikuwa amekwisha kuzimia. Watu walimwelezea daktari ile hadithi ya nyoka kipilili na namna alivyorusha mkono hapo alipokuwa akichora hiyo sanamu. Daktari alikitazama kile kidole cha Bwana Peku alichokuwa akikichorea sanamu akakiona kina meno ya nyoka. Daktari alijaribu kuyatoa meno hayo lakini, wapi! Ajali haikimbiliki, Bwana Peku, maskini, alikufa hapo hapo. Daktari alitaka kupatazama hapo alipokuwa akichora hiyo sanamu. Basi daktari alipooneshwa hapo pahali aliondoa mchanga wa pahali hapo. Kwa kufanya hivyo aliona baadhi ya
mchanga unadidimia chini kwenye kishimo kidogo. Alipozidi kuondoa mchanga hapo mara alimuona mnyama anatoa kichwa chake kidogo na kukirudisha ndani ya kishimo. Daktari alitoa amri ya kufukuliwa mnyama huyo. Hapo alifukuliwa kwa majembe, na alipoona hana budi na kuonekana, pale pale, alitoka kwenye shimo mbele ya watu naye alikuwa ni nyoka kipilili. Kumbe Bwana Peku alitafunwa na yule yule adui yake aliyemuota usingizini na akawa anamkimbia. Daktari alimchukua nyoka huyo na kumtia ndani ya chupa yake ya hospitali. Daktari aliwaambia watu kuwa Bwana Peku alikufa kwa sababu ya kutafunwa na nyoka huyo hapo alipokuwa akichora sanamu yake. Watu walisema, Ama kweli ajali haikimbiliki, hadhari yote aliyokuwa nayo Bwana Peku ili asiumwe na nyoka kipilili haikufaa kitu, ameuliwa na jambo lile lile alilokuwa akilikimbia. Habari ya kifo cha Bwana Peku ilifika huko ofisi kubwa ya kampuni ya nguo. Wakubwa wake walikuja upesi kwa kumzika. Baada ya maziko walitazama mabuku yote ya hesabu, wakaona ndani ya mabuku hayo, dhuluma na unyang'anyi wote alioupitisha Bwana Peku kwa wafanya kazi wa tawi la Barani. Mkubwa wa kampuni hiyo aliwaita watu walionyang'anywa mali zao na Bwana Peku kwa kuharibu bila ya kukusudia, vitu vya hapo kazini. Watu wote hao walirudishiwa mali zao na walishukuru sana. Mkubwa wa kampuni aliwaambia watu kuwa angejuwa vitendo vibaya vile vya Bwana Peku angalikwenda huko Barani na kuzuia vitendo hivyo, kisha naye angemfukuza kazini. Mkubwa huyo alimweka mtu mwingine hapo pahala pa Bwana Peku, na ule mkataba wa Bwana Peku wa kutia watu kazini uliondolewa
Hapo zama za kale palikuwa na nchi iliyokuwa na wafalme wawili mbali mbali. Mmoia alitawala sehemu ya Kaskazini na mwengine sehemu ya Kusini. Wafalme hao hawakuwa wakigombana bali walikuwa wakipelekeana barua na zawadi pia. Mfalme wa Kaskazini akiitwa Matora na yule wa sehemu ya Kusini akiitwa Mamboni. Hapo mpakani baina ya nchi ya Matora na Mamboni ilikuwepo chemchemi ya maji ambayo ilikuwa na maji mengi sana na matamu. Kila mmoja katika wafalme hawa wawili alidai kuwa chemchemi hiyo ni yake, hapo walianza kuchukiana na kugombana. Mfalme Mamboni alikuwa na nguvu zaidi kuliko Mfalme Matora, kwa sababu alikuwa na askari wengi sana, mali na watu. Ugomvi wa chemchemi hiyo uliposhika nguvu, Mfalme Matora alimwandikia Mfalme Mamboni barua ifuatayo: Mpenzi mfalme Mamboni, siku nyingi zilizopita tumekaa, mimi na wewe, kwa wema na kupendana. Heshima yangu ni kubwa kwako wala sipendi kukuondolea kadiri yako. Natumai na wewe hupendi, vile vile, kuniondolea heshima yangu. Kwa hivyo, nakupa habari kuwa chemchemi iliyoko mpakani ni yangu wala wewe huna haki juu ya chemchemi hiyo. Ninayo shahada kamili inayoonesha kuwa chemchemi hiyo ikitumiwa na kutunzwa na watu wa nchi yangu tokea miaka mia iliyopita. Babu yangu aliyekufa kwa miaka kumi iliyopita alinihadithia kuwa ilipokuwa ikitaka kujengwa nyumba hii ninayokaa, baba yake, aliyekuwa mfalme kama mimi, alipeleka watu hapo penye chemchemi kuchimba mawe. Hapo jiwe moja kubwa lilipovunjwa palitoka maji mengi yenye nguvu sana, na maji hayo ndiyo chemchemi hii. Kwa hivyo huna haki ya kudai kuwa chemchemi hiyo ni yako. Ni mimi hapa, Matora wadi Kipande wadi Sharambua. Barua hii ilipomfikia Mfalme Mamboni, alihamaki sana, na kwa vile alivyokuwa ana nguvu za kutosha za kupigana na Mfalme Matora, aliijibu barua hii kwa haraka na kwa ujeuri. Aliandika: Kwa Matora wadi Kipande, Mimi sina habari kuwa wewe ni mfalme ingawa watu wanakuita hivyo. Barua yako inayohusu habari ya chemchemi ni ya upuuzi mtupu. Nakupa habari ya kuwa mimi sidai chemchemi tu kuwa ni yangu bali nchi yote unayodai kuwa ni yako, ni yangu. Kwa haraka, uhame kwenye sehemu ya Kaskazini ya nchi yangu, ikiwa unajidai kuwa wewe ni mfalme wa huko. Ikiwa hukuondoka kwa muda wa siku saba, nitakuondoa kwa nguvu. Ni mimi mfalme, Mamboni wadi Sinatoa. Barua hii ilimshtusha sana Mfalme Matora na ilimuakinisha kuwa vita vi tayari. Mfalme Matora alikuwa ni mfalme mwenye akili na busara ya kutosha. Alipojiona kuwa hana nguvu za kutosha za kumwezesha kuvikabili vita vya Mfalme Mamboni, aliazimia atumie akili na siasa. Kwa hivyo alijibu barua ya Mfalme Mamboni kama ifuatavyo: Kwa mpenzi Mfalme Mamboni wadi Sinatoa, Barua yako tukufu imeniwasilia, nayo imenifahamisha kuwa umehamaki sana, na kuwa utanipiga vita. Basi hapana haja ya mimi na wewe kupigana bora useme unalotaka kwangu nikupe. Ni mimi mpenzi wako wa daima, Matora wadi Kipande wadi Sharambua. Ingawa barua hii ni ndogo lakini ilikuwa na maana makubwa. Mfalme Matora alijua kuwa barua hii, kwa vile ilivyoandikwa kwa upole na wingi wa adabu, itampoza Mfalme Mamboni, wala hatakuwa na hamaki kubwa. Vile vile alijua kuwa ijapokuwa mfalme anayo azima ya kumpiga vita, kwa kumpelekea barua ile, mfalme atachelewesha azima yake ya vita. Tena jinsi Mfalme Matora alivyoiandika barua hii kwa hadhari, hakutia neno lolote lililoonesha kuyakubali madai ya Mfalme Mamboni. Siku ilipopelekwa barua hii kwa Mfalme Mamboni, Mfalme Matora alipeleka watu kumi huko nchini kwa mfalme Mamboni, kwa ajili ya kupeleleza habari, ili wamuarifu Mfalme Matora kama watakalolisikia. Watu hao walikuwa mahodari sana kwa kazi ya upelelezi. Mmoja alivaa nguo mararuraru na akaenda moja kwa moja kwa Mfalme Mamboni kuomba kazi ya utumishi wa nyumbani. Jinsi alivyokuwa na bashasha na adabu, alikubaliwa kufanya kazi nyumbani kwa mfalme. Mwengine alikwenda kwa mfalme kuomba kazi ya kuendesha motakaa, huyo naye alipata kazi hiyo aliyoitaka. Wanane waliobaki walitawanyika nchini kwa kazi mbali mbali. Yule aliyekuwa mtumishi wa nyumbani alipendeza sana kwa mke wa mfalme na yule aliyekuwa mwendeshaji wa gari alipendeza kwa mfalme mwenyewe. Watu hawa walifika sawasawa na barua ya Mfalme Matora huko nchini kwa Mfalme Mamboni. Mfalme Mamboni alipoipata barua hii ya mwisho, alipoa kidogo lakini azma ya kumpiga vita Mfalme Matora alikuwa nayo, wala barua hii hakuijibu. Kila wakati Mfalme Mamboni alikuwa akifikiri namna ya kumhujumu Mfalme Matora na lini amhujumu. Mara mojia alimwambia muendeshaji gari, yaani yule mpelelezi habari wa Mfalme Matora, ampeleke pahali fulani. Katika kwenda safari hiyo, mfalme alikuwa akifikiri mambo ya vita tu hata hakuweza kustahamili bali alianza kumwambia muendeshaji wake wa gari kuwa ni lazima ampige vita Mfalme
Matora na aikamate nchi yake na mali yote. Mwendeshaji gari alimwuliza mfalme, 'Lini bwana?'
Mfalme alisema, 'Kwa siku za karibu, kiasi baada ya miezi mitano hivi, sababu ni lazima nitengeneze mambo ya vita kama vile chakula, askari na kadhalika.' Mke wa mfalme naye alimwambia yule mtumishi wa nyumbani kuwa mumewe, mfalme, atampiga vita Matora wadi Kipande kwa siku za karibu sana. Yule mtumishi alimwuliza mke wa mfalme, 'Lini bibi?' alijibiwa, 'Sijui, lakini haipiti miezi mitatu.' Tokea siku Mfalme Matora alipopeleka ile barua ya mwisho na kupeleka wapelelezi wake huko kwa Mfalme Mamboni, Mfalme Matora alikuwa akijitengeneza kwa ajili ya vita. Aliongeza askari, silaha, vyakula na kadhalika. Kwani alijua kuwa lazima Mfalme Mamboni atapigana naye. Mwendeshaji gari ya mfalme na mtumishi wake wa nyumbani walijitahidi kwa kutafuta nafasi ya kwenda kwa Mfalme Matora kupeleka habari waliyoipata. Walipopata nafasi, mara tu, walimfika Mfalme Matora na kumwambia aliyosema Mfalme Mamboni na mkewe. Wale wanane wengine vile vile walipeleka habari kuwa mnong'ono umeenea nchini kwa Mfalme Mamboni kuwa nchi ya Mfaime Matora itachukuliwa na Mfalme Mamboni. Baada ya miezi mitano hivi, Mfalme Mamboni alipeleka barua ya vita kwa Mfalme Matora. Barua alisema hivi: Kwa Matora wadi Kipande, Nakupa habari kuwa siku ya Jumatatu mwezi kumi na mbili Julai mwaka huu, nitafika kwenye nchi yangu iliyopo Kaskazini kuikabidhi. Sitaki kukuona wewe wala jambo lolote lako huko nchini. Ikiwa hukuondoa mambo yako, basi sitochukua dhamana ya kitu chochote kitakachoharibika. Ni mimi mfalme, Mamboni. Ilipopelekwa barua hii kwa Mfalme Matora, zilibakia siku nne tu kufika siku hiyo aliyoitaja Mfalme Mamboni katika barua yake. Mfalme Mamboni alikuwa na mawaziri wane, mmoja katika hao alikuwa waziri wa mambo yahusuyo ulinzi wa nchi na mapigano. Waziri huyo alikuwa akiitwa Jabiri. Bwana Jabiri alikuwa akitembelea sana huko nchini kwa Mfalme Matora na mara nyingi alikuwa akialikwa na Mfalme Matora kwa chai au chakula wakati alipokuwa akitembelea huko. Bwana Jabiri na Mfalme Matora walikuwa na urafiki kidogo. Baada ya Mfalme Matora kupata barua ya vita, aliona nguvu zake zingali ndogo bado, kwa hivyo alifikiri ni lazima atumie akili kubwa juu ya vita hivyo vilivyo mkabili. Kwa hivyo alifanya akili na busara hata akampata rafiki yake Bwana Jabiri. Bwana Jabiri kumuona Mfalme Matora tu alimdakiza, 'Rafiki yangu Mfalme Matora, sina budi kukupa habari kuwa kesho kutwa tutakamata nchi yako na pindi Mfalme Mamboni akijua kuwa mimi leo nimeonana nawe, lazima nitapata adabu. Kwa hivyo niambie uliloniitia nipate kurudi kwani nimeshughulika sana kwa kutengeneza majeshi yangu.' Mfalme Matora alimjibu, 'Bwana Jabiri, rafiki yangu mpenzi wangu, hatari imenikabili mimi rafiki yako. Ukipenda, sipati madhara yoyote ya vita vyenu. Ninajua yakini kuwa kupona kwangu na nchi yangu kuko ndani ya mikono yako.' Bwana Jabiri alisema kuwa yeye ni mwenye kuamrishwa tu kwa hivyo, hana amri ya jambo lolote. Mfalme Matora alimwambia Bwana Jabiri aseme analopenda ampe ili amsaidie katika vita hivi. Bwana Jabiri alijibu kuwa hawezi kufanya khiana kwa mfalme wake. Mfalme Matora alimwambia, 'Ukininusuru mimi na watu wote waliomo ndani ya nchi yangu ni bora kwa Mungu kuliko kuuwa maelfu ya watu kwa kumnusuru mfalme wako tu ambaye ni dhalimu. Nakupa ahadi, ikiwa utaniacha nimkamate mfalme wako siku hiyo ya vita nitakuachia hiyo nchi yenu uitawale, na tokea leo nitakupa shilingi elfu tisini.' Bwana Jabiri aliinamia chini na kufikiri kidogo, kisha akasema, 'Nimekubali.' Hapo hapo Mfalme Matora alimpa Bwana Jabiri shilingi elfu tisini. Bwana Jabiri, pasi na kuambiwa na Mfalme Matora, alikula kiapo kuwa atatenda alivyoahidi. Mfalme Matora naye alikula kiapo na kusema kuwa kama alivyosema ndivyo atakavyofanya. Bwana Jabiri tena alianza kumwambia Mfalme Matora mpango wa vita. Alisema, 'Nitamwambia mfalme mwenyewe aje huku nchini kwako siku ya vita. Tutafika huko saa za usiku na kupiga kambi kiasi cha maili mbili kutoka mjini kwako. Hema la mfalme litakuwa na bendera juu yake. Nitaweka askari wawili tu kushika zamu. Basi wewe na askari wako kiasi cha mia hivi unaweza kuja kwa ghafla, kiasi cha saa kumi za alfajiri na kututeka.' Mfalme Matora alimuuliza Bwana Jabiri, 'Jee askari wako wengine watakuwa wapi?' Alijibiwa, 'Watakuwa kando kabisa na hawatokuwa macho wakati huo.' Bwana Jabiri aliongeza kusema, 'Lakini fahamu sina budi kuuwa watu wawili watatu hivi.' Hapo Bwana Jabiri alimuaga Mfalme Matora na akaenda zake. Mfalme Mamboni hakujua kitu chochote kilichokuwa kati ya Bwana Jabiri na Mfalme Matora. Siku ya kwenda kumpiga vita Mfalme Matora ilipofika, Mfalme Mamboni pamoja na mkubwa wa jeshi Bwana Jabiri waliondoka kwenda kwa Mfalme Matora pamoja na jeshi lao la askari mia sita. Walipofika huko, walifanya kama alivyosema Bwana Jabiri. Basi mfalme Matora alichagua jemadari hodari sana wa vita na akampa jeshi la askari mia nne tu ambao walikuwa hodari sana. Mfalme Matora aliwaelekeza, barabara, namna ya kumteka Mfalme Mamboni na askari wake. Yeye mwenyewe, Mfalme Matora hakwenda vitani, lakini alijiweka tayari kabisa hapo pake pindi vita vikiendelea na kufika huko aliko, aweze kuvikabili. Jemadari wa mfalme Matora alifika kule alikokuweko Mfalme Mamboni saa kumi juu ya alama. Alipeleka askari mia tatu kuyateka mahema ya skari wa Bwana Jabiri, na askari mia moja pamoja na yeye mwenyewe walikwenda kumteka Mfalme Mamboni. Basi hapo mara tarumbeta ya kuteka ililia na kwa ghafla Mfalme Mamboni alikamatwa pamoja na baadhi ya askari wake. Bwana Jabiri pamoja na askari washika zamu walipiga bunduki, na askari watatu wa Mfalme Matora waliuawa. Askari wengi wa Mfalme Mamboni walikimbia, kumi na mbili waliuawa, na kiasi cha askari mia mbili walitekwa. Maskini Mfalme Mamboni pamoja na bwana Jabiri walichukuliwa hali wamefungwa mikono nyuma. Wakati huo, macho ya Mfalme Mamboni yalikaa kama yatakayotoka vishimoni mwake, uso wake ulionesha ni mwenye fikira nyingi za kuhuzunisha. Ukanda wa suruali yake aliyoivaa ulikatika, kwa hivyo mguu mmoja wa suruali uliteremka na alikuwa akiukanyaga alipokuwa akibururwa kwenda huko kwa Mfalme Matora. Kule kubururika kwa mguu wa suruali yake, kulimsabibisha kuanguka kiasi cha mara mbih tatu hivi, na hapo akianguka, akinyanyuliwa kwa kupigwa mateke ya viatu na ****** ya bunduki. Bwana Jabiri alijidai kuwa naye ni mwenye huzuni kuliko mfalme mwenyewe, lakini kwa kweli alikuwa na furaha kwani alikuwa na tamaa kubwa kuwa Mfalme Matora atampeleka huko kwao na kumtawalisha. Mateka yalipelekwa mbele ya Mfalme Matora ambaye alimtisha kuwa Mfalme Mamboni na Bwana Jabiri watiwe korokoroni. Askari waliotekwa walifungwa katika gereza la peke yao. Mfalme na Bwana Jabiri walipokuwa wakichukuliwa, Bwana Jabiri alimtolea macho Mfalme Matora, kama anayemuuliza kuliko habari ya ahadi yao. Mfalme Matora alicheka kidogo, halafu akamgeuzia uso. Siku ile ile ya vita, Mfalme Matora alipeleka jeshi la askarimia mbili, chini ya uongozi wa jemadari wake yule aliyeshinda vita, huko nchini kwa Mfalme Mamboni, ili kuikamata nchi hiyo iwe ndani ya mamlaka yake. Huko, nchi ilikamatwa bila ya taabu yoyote na bendera ya mfalme Matora ilipepea. Baada ya siku nne kupita Mfalme Matora alimpeleka mtoto wa baba yake mdogo, aliyekuwa akiitwa Jodari, huko nchini alikokuwepo Mfalme Mamboni, kuwa mtawala wa nchi hiyo, yaani awe Naibu wake katika nchi ile. Kwa siku ya tano baada ya vita, Mfalme Matora aliamrisha kuwa Mamboni na Jabiri wapelekwe mbele yake kwa hukumu. Walipofika mbele yake Mfalme Matora aliwaambia, 'Wewe Mamboni na wewe Jabiri lazima nikuuweni. Mnayo maneno mnayotaka kusema?' Mamboni alisema kwa uchungu mkubwa, 'Sina.' Jabiri alisema kwa upole, 'Bora utuachilie Bwana.' Hapo Jabiri alipokuwa akisema na mfalme, alikuwa akimbiruzia mkono kwa kumwuliza, 'Vipi ahadi yetu?' Jabiri alipokuwa akifanya hivyo Mamboni alikuwa hamuoni, kwani Jabiri alisimama nyuma yake. Mfalme alijua kuwa Jabiri anamkumbusha ile ahadi yake ya kumtawalisha huko kwao, lakini mfalme hakukubali kitu kwani hakuwa na azma ya kuitimiza ahadi hiyo. Mfalme aliwaambia Mamboni na Jabiri,'Ningependa nikunyongeni nyote wawili, lakini nakuoneeni huruma. Najua kwa yakini kuwa mngalinishinda mngeniua. Basi wewe Mamboni nimekufunga bila ya muda maalum, na wewe Jabiri nimekufunga muda wa miaka kumi na tano.' Hapo Jabiri alikata tamaa ya kupata aliyoahidiwa na mfalme. Hapo tena, moja kwa moja, waliongozwa na askari na kupelekwa gerezani. Watu waliokuwepo nchini kwa mfalme aliyetekwa walisikitika sana kusikia kuwa mfalme wao kakamatwa na kufungwa. Lakini baada ya siku chache, walianza kufurahi kwani yule mtawala mpya yaani Naibu wa Mfalme Matora, alikuwa mtu mwema sana na mwenye akili. Alianza kuutengeneza mji na nchi nzima. Kazi huko zilikuwa nyingi sana na neema ilitapakaa kila pahala. Watu wote walimpenda Bwana Jodari kuliko huyo mfalme wao wa zamani. Tukirudi kwenye fumbo letu lisemalo 'kikulacho kimo nguoni mwako' tutaona kuwa mfalme Mamboni atiliwe na watumishi wake waliokuwa wakipeleka habari ya matengenezo ya vita kwa Mfaime Matora. Vile vile aliyekuwa akimla hasa ni yule waziri wake, Bwana Jabiri aliyemkamatisha. Huyo Bwana Jabiri naye alikuwa na mfalme Matora, kwani alidhani akimkamatisha mfalme wake, atatawala yeye, kumbe vile Mfalme Matora alikuwa na azma nyengine asiyoijua mtu yeyote. Basi huu ndio mwisho wa hadithi yetu hii. Mfalme Matora alikuwa mfalme wa nchi mbili, yaani nchi ile ya Kaskazini na ya Kusini, na Mamboni aliyekuwa akijigamba, aliishi kifungoni. Jabiri naye aliyefanya khiana kwa mfalme wake alifungwa kwani Mfalme Matora alimjuwa kuwa mtu mbaya asiyeaminika

Alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa akitamani sana apate mtoto. Bibi huyo alikaa muda mrefu, alifika umri wa miaka arobaini hajapata mtoto, basi alikata tamaa. Alipofika umri wa miaka arobaini na tatu alipata mtoto mwanaume. Kwa bahati mbaya, baba yake huyo mtoto, yaani mume wake huyo mwanamke, alikufa wakati mtoto huyo alipokuwa na umri wa siku thelathini. Mapenzi ya bibi huyo juu ya mwanawe huyo yalikuwa ya hatari kwani alikaribia kuingia wazimu kwa kumpenda. Bibi huyo alikuwa halali usiku ila akimtazama yule mtoto wake wakati anapokuwa ndani ya usingizi mpaka asubuhi anapoamka. Basi yule mtoto aliendelea kukua na tabia ya kupendwa huko kijinga. Mtoto huyo hakukatazwa jambo lolote alilopenda kufanya. Wala hakujua kuwa kiko kitu kukatazwa. Yule mtoto alianza tabia ya kuudhi majirani, yaani akiharibu vitu vyao na kuudhi wanyama wao mpaka watoto wenzake wa hao majirani. Basi majirani wakishtaki kwa mama yake, ambaye alikuwa akigombana na yule aliyekuja kushtaki au ikiwa kaharibu kitu akilipa thamani ya kitu hicho. Almuradi huyo mama mtu alikuwa katika taabu kubwa lakini alikuwa hajali kitu wala hakumkataza mwanawe vitendo hivyo vibaya kwa jinsi alivyokuwa akimpenda. Yule mama mtu alipoona taabu ya majirani na hasara imezidi, alihama pale alipokuwepo akaenda akahamia pahali mbali na majirani. Wakati huo yule mtoto alikuwa na umri wa miaka minane. Walipokaa huko walikohamia, taabu ya yule mama ilipungua kidogo ilibaki taabu baina yake na mwanawe tu kwani ile tabia ya yule mtoto ya kufanya anavyotaka haikupungua. Huko alikohamia kulikuwa ni pahali pa malisho ya wanyama. Yaani ndiko watu walikokuwa wakichungia wanyama wao. Yule mtoto alipenda sana kuona makundi ya ng'ombe, kondoo na mbuzi wanakula majani. Naye alitamani awe mchunga ng'ombe. Alimwambia mama yake kuwa angependa naye awe mchunga ng'ombe, mama yake alimpeleka kwa mchunga ng'ombe mmoja ili amfundishe kazi ya kuchunga ng'ombe. Yule mtoto aliendelea kuchunga ng'ombe mpaka akafika umri wa miaka ishirini na tano lakini vile vile huko alikokuwa akichunga ng'ombe hakuacha kuudhi watu na kuharibu mali za watu. Lakini hao aliowaharibia mali zao na kuwaudhi walikuwa nao wakimuudhi
kwa kumpiga magongo na ngumi. Siku moja yule mtoto ulimpanda umaluuni akamkata ng'ombe mmoja mkia. Loo!!! Mwenye ng'ombe akahamaki bila ya kiasi. Yule mtu mwenye ng'ombe alikimbilia kwa mama wa yule mtoto na kumshitakia kitendo hicho cha ukatili alichofanya mwanawe na kumwambia mama amlipe ng'ombe, badala ya ng'ombe wake aliyekatwa mkia na asipolipwa basi naye atamkata yule mtoto kidole. Mashitaka haya yalimkalia sana yule mama mtu, basi hapo aliondoka akaenda alipokuwepo huyo mwanawe na kuanza kumgombeza kwa jambo hilo alilolifanya. Hii ndiyo mara ya kwanza kumgombeza tokea kumzaa kwake, wala asingalimgombeza lakini ile fikira ya kukatwa mtoto wake kidole ilimbadilisha tabia yake ya mapenzi ya kijinga juu ya mwanawe. Ilivyokuwa kule kugombezwa na mama yake ni kitu kigeni kwa yule mtoto, yule mtoto alihamaki sana na hapo alikata fimbo ya mti uliokuwepo karibu yake na akaanza kumpiga yule mama yake fimbo nyingi. Watu waliokuwepo walimsaidia yule mama mtu ambaye, baada ya kuachiwa alikimbia mpaka kwa bwana mmoja aliyekuwa na akili na elimu nyingi hapo mtaani. Kufika huko, yule mama mtu alimwelezea yule mtu yote yaliyompata kwa mwanawe. Yule mtu alimwuliza, 'Mtoto wako alipofika umri wa miaka saba ulimpa kazi gani?' Mama alijibu, 'Sikumpa kazi yoyote lakini alipofika umri wa miaka minane nilimpeleka kwa wachunga ng'ombe kufanya kazi ya kuchunga ng'ombe.' Yule mtu alimwambia, 'Basi mtoto wako hakufanya vibaya hata kidogo, kwani alipokuwa akikupiga alidhani anapiga ng'ombe tu wala hakujua kuwa anakupiga wewe mama yake, sababu watu wanasema udongo upatize ulimaji. Wewe ulimwachia mtoto wako tokea alipokuwa mchanga hukumlea vizuri na kumpeleka shuleni alipofika umri wa miaka saba, kwa hivyo ni lazima
afanye apendavyo. Haya nenda zako na ujinga wako." Kwa kuona huruma ya mwanawe asikatwe kidole, yule mama alilipa ng'ombe, badala ya yule aliyekatwa mkia. Basi tokea siku ile mapenzi ya mwanawe yalimtoka. Yule mtoto ambaye alikuwa ameshakuwa mtu mama hawakusikizana kabisa na mama yake wala mama mtu hakupata manufaa ya mwanawe kwa kutomlea malezi mazuri tokea alipokuwa mchanga.
"Hapo zamani alikuwepo mtoto aliyelelewa na babu yake mzaa baba tokea alipokuwa mdogo mpaka akawa mkubwa. Baba wa mtoto huyo alikufa ikabidi alelewe na babu yake. Mtoto huyo alirithi kiwanja kizuri chenye thamani kilichokuwa katikati ya mji. Babu yake alipewa shilingi elfu arobaini akiuze, asitake. Alisema hawezi kuuza mali ya mjukuu wake mdogo, mpaka awe mkubwa aje afikiri mwenyewe jambo la kufanya juu ya kiwanja chake hicho. Mtoto huyo aliishi na babu yake, kama hivi ninavyoishi nanyi, wajukuu zangu, hata akawa mkubwa. Babu yake huyo hakuwa hodari wa kumfundisha mjukuu wake mambo mazuri tokea alipokuwa mdogo, bali akimuachia kwenda mwendo aliopenda. Kwa bahati mbaya mtoto huyo alikuwa akipenda kutumia fedha sana na akinunua vitu vingi visivyokuwa na haja, kama vile matunda ya kutegea ndege, panda za kupigia ndege, matunda machanga, muradi alikuwa na tabia ya kununua ambacho alikuwa na haja nacho, na asichokuwa na haja nacho. Mtoto huyo aliendelea na tabia hii mbaya hata akawa analewa. Alikuwa akifanya kazi ya kibarua na kupata kutwa shilingi nne, lakini kwa tabia yake mbaya hii alikuwa habariki na mwisho hata chakula na nguo zake za kuvaa vilimfanyia taabu, yaani alikuwa akivaa matambara kila wakati na akila chakula cha ovyo cha kiasi cha kujaza tumbo lake tu akaishi. Mwishoni mtoto huyo ilimjia fikira kuwa lazima akiuze kile kiwanja chake alichorithi kwa baba yake, ili aweze kuendesha maisha yake. Babu yake alimkataza kufanya hivyo kwani alijua ya kuwa hatanunua kitu cha maana badala ya kiwanja chake. Yule mtoto hakumsikiliza babu yake kabisa, basi alianza kukitembeza kiwanja chake kwa matajiri.
Matajiri walipomuona muhitaji sana wa fedha hawakumpa bei kubwa. Mmoja alimpa shilingi elfu saba, mmoja shilingi elfu nane, na huyo aliyekuwa na haja nacho sana alimpa shilingi elfu kumi. Basi kilifika robo ya thamani ya hapo zamani tu yaani shilingi elfu arobaini. Basi hapo alikiuza na akazichukua fedha zote. Alipopata hizo fedha hakwenda tena kwa babu yake, alikimbilia madukani kununua kila aina ya nguo. Wenye maduka hawakuwa wakimuuzia nguo kwa ughali sana. Suruali ya shilingi thelathini wakimpa kwa shilingi ishirini. Basi siku hiyo ya kwanza alitumia shilingi elfu moja kwa nguo na viatu. Rafiki zake waovu waliposikia ana fedha walimjia kwa kikundi na ikawa anafuatwa kila anapokwenda kama mfalme. Baada ya wiki moja fedha hiyo ilibaki shilingi mia tano tu. Basi hapo ilimjia fikira akainunulie baisikeli. Kabla ya kununua hiyo baisikeli alifuatana na rafiki zake kwenda kulewa katika saa za usiku; basi alilewa sana hata asijifahamu, hapo rafiki zake waliiba ile fedha aliyokuwa nayo na aliamka asubuhi hana fedha wala hana rafiki. Tena yule mtoto aliingilia kuuza zile nguo na vitu vinginevyo alivyonunua. Mwishoni alirudia kuvaa matambara yake. Yule aliyemuuzia kiwanja chake alianza kujenga nyumba kwenye kiwanja hicho, basi, naye akenda kuomba kazi ya kibarua, akapewa. Siku moja alikuwa akichukua mawe kichwani, jiwe moja kubwa likamponyoka na kumpiga mguuni akaumia, akachukuliwa akapelekwa hospitali. Babu yake alikwenda huko kumtazama, kumuona babu yake tu alilia na babu yake naye pia akalia. Yule mtoto alilia kwa sababu mali yake yote amekwisha kuipoteza na akitoka hospitali hajui cha kutumia, na yule babu mtu alililia hilo hilo. Yule mtoto alipotoka hospitali, hakuweza kufanya kazi yoyote kwani alikuwa akichechea. Alipata taabu kubwa ya kutunza maisha yake. Ilimbidi kuomba chakula na nguo pia. Kwani babu yake naye alikuwa maskini. Babu yake alimwambia, 'Mjukuu wangu, mara nyingi nilikuwa nikikupa shauri nzuri za kutunza mali yako, ili usije ukapata dhiki kama uliyonayo hivi sasa, nawe ulikuwa kabisa hunisikilizi, basi haya ndiyo matokeo ya mtu asiyesikiliza la mkuu. Watu wamesema, “Asiyesikia la mkuu huvunjika mguu,” si kuwa huvunjika mguu kweli, bali maana yake mambo yake na maisha yake yote humharibikia na pengine ikawa ile dhiki itakayompata ndiyo sababu ya mauti yake. Basi sasa mjukuu wangu, sina la kukufanya ni wewe na bahati yako katika maisha yako.

Palitokea Mwanamke, aliyekuwa ametolewa, akashindwa kuishi vizuri na mumewe. Kwa hivyo mumewe hakuridhika naye akaamua atafute mwanamke atayemfaa zaidi, aishi naye. Kwa wivu, yule mke wa kwanza, akatafuta dawa ya kuweza kumrudisha mume wake. Akatafuta dawa aina nne. Aina ya kwanza, ilikuwa ya kujipaka mwilini, aina ya pili, ya kutilia yule mawanaume kwenye chakula, aina ya tatu, ilikuwa ya kuoganayo, aina ya nne, ilikuwa ya kuchoma kwa moto. Hizo dawa aliamini zitamfanya mume wake, amwache mke wa pili, na kwamba mapenzi yao yataongezeka, kwa hivyo wataishi pamoja tena. Baada ya kuzipata dawa hizo na kuzitumia kikamilifu, bado hali ikawa ile ile, hakuna lililobadilika. Mumewe akaendelea kuishi na mkewe wa pili.
Yule mke wa kwanza, akaenda kwa bibi kizeemmoja ambaye alisifiwa kuwa mganga hodari akamwomba amsaidie. Bibi kizee hakusita akamwambia akatafute ubongo wa Fisi, yaani akamuue Fisi ampasue na kuuleta ubongo ukiwa bado mzima! Ubongo huo, ndio utatumika kutengenezea dawa ya mapenzi.
Mwanamke akarudi nyumbani akaanza kufikiria jinsi atakavyomtega Fisi na kumuua. Akapata wazo la kununua nyama na kuikata vipande, kuviweka njiani ambapo fisi hupendelea kupita mara kwa mara. Kesho yake akakuta ule mtego mtupu, na nyama imeliwa. Akanunua nyama kwa wingi akaiweka toka pale alipotega jana yake njiani pote mpaka nyumbani kwake. Fisi walipofika, kwa uroho na ujinga wao kana tunavyowafahamu, wakaanza jula vile vipande vya nyama mpaka ndani ya nyumba ya yule mwanamke. Akamkuta yule mwanamama amejitayarisha vizuri na shoka. Kwa nguvu zake zote. Akampiga kipigo kimoja tu na yule Fisi akafa hapo hapo. Akampasua kicwani akatoa ubongo, na akaenda nao kwa bibi kizee mganga.
Alipofika, bibi kizee akauliza: “Mwanangu, umeniletea ile dawa niliyokutumia?” Mwanamama akajibu. “Ndiyo mama, lakini nimeipata kwa shida sana!” Akamkabidhi bibi kizee ule ubongo wa Fidi. Alipokwisha upokea akakaa kitako akafikiri sana. Halafu akasema: “Mwanangu, sasa nitakueleza kila kitu vizuri sana umetumie akili na ujuzi mwingi, kutega Fisi na kumwua. Sasa nenda ukatumie akili na ujuzi wako wotw ulionao, ili uweze kupata mapenzi ya mumeo, ili uweze kupata mapenzi ya mumeo tena. Nina maanisha kusema, lazima uwe msafi, uvae vizuri na upikie chakula kizuri mume wako. Vile vile, jaribu kujipendezesha kwa mume wako kwa kila hali. Utaona mumeo anarudi nyumbani na kumuacha mke aliyekuwa naye sasa hivi, na mataishi kwa amani na furaha.
Aliporudi nyumbani, akafanya, yote aliyoambiwa na yule bibi kizee. Haukupita muda, mumewe akamfukuza mke wa pili na akarudi nyumbani kwa mke wake wa kwanza. Wakaishi vyema kwa mika mingi sana mpaka vifo vikawatengenisha.
FUNDISHO:- Inaaminika kuwa, watu wanapoishindwa kuishi pamoja katika ndoa, hutumia dawa za kienyeji kwa sababu ya kusitawisha maisha yao.
Wapo akian mama wengi amabao wanaamini kabisa kwamba kuna dawa ya mapenzi.
Lakini ukweli ni kwamba, dawa ya mapenzi ni moja tu nayo ni: Kuhakikisha kwamba, kina mama wanaheshimu ndoa zao na kutii waume zao. Nyumba yenye mapenzi, inamfanya mume apende kukaa nyumbani, na asitembee tembee ovyo.

Ilikuwa ni asubuhi siku ya Jumamosi. Guyo, babake Nuru, alikuwa tayari ameondoka na wavuvi wenzake kutafuta riziki ya kila siku katika Mto Tana. Gumato, mama yake pia alikuwa ameenda sokoni. Nuru alikuwa nyumbani na ndugu zake wadogo, Munga na Habuko. Sawa na Jumamosi nyingine, kazi yake Nuru ilikuwa kufua nguo za familia yake yote. Alikusanya nguo hizo na kuzikunjia kwenye shuka moja, akaziweka kwenye karai kisha akaelekea Mto Tana . Alitembea kilomita nane hivi.
Alipofika, aliyarusha mawe madogo majini kuhakikisha kwamba hakukuwa na mamba mle ndani. Mto huo ulijulikana kuwa na mamba walio washambulia wanyama na watu sawa na kuwazamisha majini kabla ya kuwala. Hakuona dalili ya mamba au nyama yeyote halifu majini. Hivyo basi alizibwaga nguo zile na karai pale na kuanza kufua nguo. Hatimaye, alitazama maji kwa uangalifu kwani alikuwa bado na wasiswasi. Goliathi naye alikuwa akiota jua katika ukingoni upande huo mwingine wa Mto Tana. Goliathi hakuwa mtu, bali mamba mzee wa kiume aliyesemekana kuwa na nguvu kupindukia. Alipomwona Nuru, alimshukuru Mola wake kwani alikuwa na njaa sana. Alianza kuogelea pole pole kama mzee kobe akielekea Nuru alipokuwa. Nuru hakuelewa kwa nini siku hiyo wasiwasi wake haukutoweka lakini hakuwa na budi ila kuendelea na kazi aliyopewa na wazazi wake. Angali chini ya maji, Goliathi alisogelea windo wake kwa tamaa. Hangeonekana na yeyote yule kwani maji hayakuwa na uwazi wa kioo: yalikuwa mchanganyiko wa rangi nyeusi, hudhurungi na kijivu. Kwake Nuru, masaa yalikimbia kweli kweli na aling'ang'ana kumaliza kazi ile iliakatafute kuni kabla ya kusoma. Nuru alipenda kusoma sana kwani alikuwa msichana mwenye matumaini kabambe maishani. Goliathi alisogea taratibu bila kusumbua maji hata kidogo. Huku Nuru amezama katika fikira za kazi alizopaswa kutimiza. Ghafla kama mshale, Goliathi aliruka kutoka majini na kumshambulia Nuru kwa jikia lake lenye magamba. Pigo hilo lilimuinua Nuru kijuujuu kama mpira uliopigwa shuti kali na akaanguka majini chubwi!, kichwa kikitangulia. Goliathi alimfuata majini huku amepanua kinywa chake kipana tayari kumrarua Nuru kwa mijino yake ya msumeno. Alilenga paja lake la kushoto na akakwamisha meno yake mwilini mwake Nuru. Alifahamu vizuri nia ya mshambulizi wake; alitaka kumzamisha majini ili afe. Huku damu ikimtirika tiriri, Nuru alipambana na Goliathi vilivyo. Alipiga nyende kadhaa akitumai kuokolewa lakini wapi! Baada ya robo saa hivi, Nuru alishindwa kupambana naye tena, kwani nguvu ilianza kumwishia. Kwa sababu ya damu aliyopoteza, alijua kwamba muda si muda, angezirai na Goliathi angemmaliza. Nuru alikata tamaa papo hapo na Goliathi akaanza kumvuta kuelekea katikati ya mto. Ni katika mapambano hayo ya wapinzani wachovu ambapo Nuru alikumbuka visa alivyosikia kuhusu tabia za mamba. Kati ya masimulizi mengi, alikumbuka tukio moja alipomsikia nyanya yake akisema kuwa mamba huogopa sana kuguswa jichoni. Hakujua iwapo habari hizi zilikuwa za kubuni au zilikuwa na ukweli fulani. Aliyoosha mkono wake wa kushoto na kutia kidole chake jichoni la Goliathi, huku akitumia nguvu yote aliyobakisha. Ghafla Goliathi alimwachilia Nuru na kwa mara ya kwanza walionana ana kwa ana. Kwa uchungu mwingi, Nuru aliogelea akielekea ufuoni. Goliathi naye alimfuata unyounyo huku amemkondolea macho kwa hasira. Nuru husema hakumbuki lingine lililotokea alipofika hapo ufuoni ila alimwona mvuvi mmoja akimwendea kwa mbio. Alipopata fahamu, alijipata katika hospitali aipouguza majeraha kwa muda wa miezi miwili. Baada ya siku kadha, alirudi shuleni na kuanza kufanya mazoezi ilikufufua viungo vyake vya mwili vilivyokuwa vimeganda. Wiki chache baadaye, alianza kukimbia kama awali kwani alikuwa bingwa katika timu shuleni. Miezi tisa baada ya tukio hili, Nuru aliibuka mshindi katika mbio za vijana wa kike duniani. Hakuwa tu ameshinda dhahabu katika mbio hizo za mita mia nane, bali pia alikuwa amevunja rekodi duniani. Bila shaka alikuwa ni kielelezo kizuri kwa vijana wengi ulimwenguni ambao wakati mwingine hukumbwa na dhiki na kuanza kukata tamaa.
UKARIMU UNA MALIPO MAZURI
Siku joka kubwa lilipotaga almas na dhahabu na kunilazimu kuchagua kimoja
Mtu mmoja aliwasili katika kijiji kimoja kilichopo kusini mwa Tanzania katika lengo la kununua ng'ombe wa kuwasafirisha kwenda kuwauza katika mikoa ya Dar, Arusha na Morogoro.
Baada ya kufika mwisho wa basi ilimlazimu kutembea zaidi ya umbali wa kilomita kumi na tano kwa miguu mpaka alipofika kijiji ambacho aliambiwa angeweza kupata ng'ombe wengi kwa kufutana na mahitaji yake.
kile kijiji hakukuwa na hotel wa nyumba ya kulala wageni zaidi ya club ya pombe za asili ambazo wenyeji wa kijiji kile walikuwa wakipata baada ya shughuli za shamba.
Akafika pale na muda huo giza lilishaanza hivyo akaongea na mama mmoja ambaye ni muuzaji wa kibanda kile cha pombe na mama akamwambia asiwe na wasiiwasi kwani atamsaidia sehemu ya kulala.
Baada ya kuridhishwa kuwa atapata sehemu ya kulala basi akala chakula na akaendelea kunywa pombe za kienyeji na wenyeji wale huku akiwa kakaa na mzee mmoja ambaye kwa mavazi alionekana dhairi kuwa ni fukara na hutumia pombe kama njia ya kujituliza kimawazo huku akisubiri siku zake ambapo mtoa roho ataichukua roho yake na kumpunguzia maumivu ya dunia.
Wakanywa kwa muda huku hadithi za hapa na pale zikipamba moto na mgeni akijaribu kupeleleza habari za kijiji kile ili siku ya pili biashara yake iende salama bila kokoro na amalize kazi zake na kurejea mjini kwa ajili ya biashara zake.
Mazungumzo yaliendelea mpaka akaja kujikuta kabaki yeye na yule mzee tuu na kilabu kimebaki kimya ikimaanisha hakuna aliyebakia pale zaidi yao jambo lililomfanya amhoji mwenyeji vipi huyu mama anayetuuzia atakuwa wapi?
Mzee akamjibu kuwa kashaondoka mida hii na yeye hufanya biashara mbili, hujiuza yeye na pia huuza vinywaji sasa akipata mtu wa kulala naye huwai kulala, ila kama hutajali kwa kuwa alikuahidi uende kwake basi mimi naweza kukukaribisha kwangu kama utapaweza.
wakaondoka na kwenda kwa huyo mzee ambaye yeye mke wake alifariki miaka mingi iliyopita na kumwacha na mtoto mmoja wa kiume ambaye alikua anasoma shule ya msingi wakati huo.
Wakafika na kuona kijana amesha lala na mwenyeji akatandika mkeka sebuleni na wakalala mpaka siku ya pili yake. Nyumba ilionyesha hali ya upweke na kuwa maisha hayakua mazuri.
Asubuhi wakawahi kuamka na baada ya kuamka wakaagana na kutokomea kazini baba akielekea shambani, mtoto shuleni na mgeni kusaka ng'ombe.
Jioni wakakutana na kumwacha kijana akipika chakula mgeni alichonunua na kwenda kupata pombe za kienyeji na katika maongezi ikaonyesha mgeni alifanikiwa kukusanya ng'ombe 150 na baada ya mazungumzo wakarudi waka na kulala.
Siku ya pili mgeni akakusanya pia ng'ombe 150 na siku ya tatu pia 150 jumla ikawa ng'ombe 450. Siku ya nne magari yakawasili pale na kuwabeba tayari kwa safari ya kurudi mjini.
Jioni ile ambapo siku ya pili yake alfajiri mgeni alitarajia kuondoka, wakatoka tena na kwenda kupata pombe na waliporudi mgeni aliwashukuru sana na kumwambia mzee ya kuwa kamwe hakutegemea kama angepata sehemu ambayo angeishi kwa furaha akiwa kijijini pale kama nyumba ya mzee huyo aishie na kijana wake.
Akawashukuru kwa ukarimu wao na jinsi walivyoishi kwa amani na furaha pamoja na hali zao. Akasema hana fedha za kuwapa ila anawashukuru kwa moyo wao. Akamwomba mzee azunguke kwenye bustani yake pale nje na kumuuliza kama ameona kitu, mzee akajibu hakuna kitu.
Akamwambia kesho nitaondoka asubuhi sana na baada ya kuondoka masaa mawili baadae katika hiyo bustani utaona chungu kikubwa sana na ukiufunua mfuniko utaona kitu cha ajabu usitishike wewe kichukue na kitupe pembeni na chini yake utaona vitu viwili wewe chagua kimoja tu ukichukue na ndio itakuwa zawadi yako. Mzee hakupata usingizi akiisubiri siku ya pili ifike.
Siku ya pili asubuhi yule mgeni baada ya kuondoka mzee akasubiri kwa hamu masaa mawili yapite kisha akazunguka kwenye lile shamba na kukiona kile chungu kama alivyoelekezwa na mgeni wake.
Alipofungua chungu joka kubwa likatoa kichwa chake, kwa hofu nyingi yule mzee akalishika kichwani na kulitupia pembeni nalo likatokomea vichakani.
Pale chini akaona lile joka lilikuwa limekalia kipande kikubwa cha dhahabu na kipande kikubwa cha almasi pia.Mzee yule akaichukua almasi na baada ya kupiga hatua mbili tu, chungu kile kikatoweka zake nae akaingia ndani na almasi yake na kuificha.
Siku ya pili yake mzee akajiandaa na kwenda mjini ili akaiuze ule almasi, na kwa kuwa alikuwa hana wazo la wapi kwa kuuza akaenda duka la mfanyabiashara maarufu katika mji ule mwenye asili ya kiasia na kumwonyesha kwa mashangao mkubwa yule mfayabiashara akaamua kumpa visima viwili vya mafuta na duka lake na magari ya mafuta pamoja na magari ya kutembelea na nyumba ya kuishi na mzee akakubali.
Siku chache baadae baada ya yule mzee kukabidhia zile mali zake... Akaanza kuumwa na kukaa ndani kwa miezi miwili mpaka alipokuja kupona na kuona baadhi ya mali zimeibiwa ila kwa maajabu wiki moja baaadae kila aliyeiba alivirudisha na yule mwafanya biashara akaja na kumwambia hakumtendea haki akamwongezea tena fedha nyingi.
Mpaka leo yule mzee ni mtu tajiri sana na mwanae amesoma na sasa ni msimamizi mkuu wa biashara zake na kile kijiji chake kakibadilisha na umekuwa mji mdogo wenye kila hitaji la muhimu na yeye hadi leo hajui yule mtu aliyekuja pale kijijini kununua ng'ombe alikuwa wa aina gani..............????????????
UKARIMU UNA MALIPO MAZURI
0 comments:
Post a Comment