Alikuwepo
mtoto mmoja wa kimaskini jina lake Muhsin, tabia yake alikuwa hasemi sana ila
kwa haja tu. Wazee wa mtoto huyo walikufa zamani wakati alipokuwa na umri wa
miaka minane. Mara moja Muhsin alikaa peke yake na huku anafikiri mambo ya
kufanya ili yamsaidie katika maisha yake. Katika kule kufikiri kwake, alimpitia
mtu na kumtolea salamu, Muhsin aliitikia, 'Waalaykumu ssalaam, jee unakwenda
wapi?' Yule mtu alimwambia Muhsin kuwa alikuwa akienda kujifunza elimu ya hesabu
kwa mwalimu mmoja anayekaa pahali pa maili kumi kutoka pale alipo. Muhsin
alisema ya kuwa naye angependa kujifunza elimu hiyo. Yule mtu alimwambia kuwa
yeye atakwenda huko kwa kupanda gari la moshi, kwani ni mbali. Muhsin alimwambia
amuelekeze pahali penyewe naye atakwenda kwa miguu. Yule mtu alimuelekeza akisha
akaenda zake. Muhsin naye aliiandama njia kwa miguu na alifika huko baada ya
mwendo wa kutwa nzima, kwani njia hiyo ilikuwa mbaya sana. Njia hiyo ilikuwa na
milima mikubwa, mabonde na mito, kwa hivyo alipata taabu kidogo katika safari
hiyo hasa vile alivyokuwa pweke, lakini juu ya hivyo alifika salama. Alipofika
huko alimuona yule mwalimu na alimuomba amsomeshe elimu ya hesabu. Yule mwalimu
alikubali lakini lazima yule Muhsin atoe malipo maalumu kwa mafunzo hayo. Muhsin
alisema kuwa hana kitu cha kulipa lakini atalipa nguvu zake yaani atamfanyia
huyo mwalimu kazi yoyote apendayo ili amsomeshe. Yule mwalimu alimpenda Muhsin
kwa ile tabia yake ya ukimya, basi alikubali kumsomesha Muhsin ambaye alifanya
kazi za huyo mwalimu wake, kama vile kufyagia, kufua nguo, kupiga pasi na
mengineyo. Muhsin alianza kusoma hesabu na alitokea kuwa mhodari kuliko
wanafunzi wote, kwa hivyo mwalimu wake alizidi kumpenda. Kwa bahati nzuri
alifahamu tambo nyingi za hesabu baada ya miaka michache tu. Muhsin alipoona
ametosheka na alichopata katika elimu hiyo alimuaga mwalimu wake na akarejea
kwao. Huko kwao Muhsin, alikuwako Mfalme aliyepelekewa suala la hesabu na Mfalme
mwenziwe aliyekuweko mbali na hapo. Suala lenyewe ni hili: 'Shilingi kumi na
mbili zinataka kugaiwa kwa watu wawili, mmoja haki yake ni nusu ya hizo na yule
wa pili haki yake ni fungu moja katika mafungu sita ya shillingi hizo. Baada ya
kwisha kuwapa haki zao hizo, kitakacho bakia uwarudishie hao hao kwa mujibu wa
mafungu yao, kila mtu atapata kiasi gani na pesa hizo zisibakie?' Suala hili
lilimshinda kabisa yule Mfalme na aliona aibu kubwa kusema haliwezi. Aliwaita
Mawaziri wake, akawaambia waifanye hesabu hiyo, na hata mawaziri walishindwa-
Hapo Mfalme alitoa mtu azunguke mjini na kusema kuwa Sultani
ana
hesabu atakayeijua amuombe Sultani anachotaka na atapewa. Mfalme alisema kuwa hataki watu ovyo tu, mpaka wanaojulikana kuwa wana elimu ya hesabu, ndio watakaopata ruhusa kwenda kwa Mfalme. Watu wengi sana walifika huko kwa Mfalme, lakini wengine hawakupewa ruhusa kufika alikokuwa Mfalme kwani walidhaniwa kuwa hawajui kitu. Muhsin naye alikwenda, lakini kwa ile tabia yake ya ukimya, alijiweka mwisho. Alipoonekana anakuja kwa upole na kuomba apewe ruhusa aende aliko Mfalme, alisukumiliwa mbali na kuambiwa, 'Ondoka hapa wee, watu kweli hawakufaulu je wewe!!' Baadhi ya watu wa hapo kwao walijuwa kuwa Muhsin ana elimu ya hesabu kidogo, lakini ule unyonge, ukimya na umaskini ndiyo yaliyomsabibisha kufukuzwa na kutoonekana kitu. Wale walioachiwa kwenda kwa Mfaime, walikuwa wakijigamba kuwa wao ni mahodari kwa hesabu na kuwa watafuzu. Basi makelele yao na ghasia zao hazikufaa kitu kwani walipopewa ile hesabu hapana hata mmoja aliyeijuwa. Muhsin aliposikia hivyo alikwenda tena kuomba aende kwa Mfalme, vile vile hakuachiliwa. Mfalme aliingia katika huzuni kubwa kwa vile kushindwa na jawabu ya hesabu ile kwani mfalme mwenzake atamcheka. Basi Muhsin alipoona kuwa hapewi ruhusa kwenda kwa Mfalme alimuandikia barua na kumuomba Mfalme atoe amri aachiliwe kuonana naye, ili aende akaifanye hesabu hiyo. Vile vile alitia ndani ya barua hiyo kuwa amerudishwa mara mbili na kusukumwa alipotaka kuonana naye. Mfalme alipoipata barua hiyo alifurahi kidogo kwa tamaa ya kuwa labda mtu huyo ataweza kuijua hesabu hiyo. Mfalme alitoa amri atafutwe Muhsin na apelekwe mbele yake. Muhsin alipofika mlangoni kwa Jumba la Mfalme, wale waliomsukuma walimtolea macho ya uadui na dharau na kumwambia kuwa watu kweli hawakufaulu licha yeye. Muhsin alifika mbele ya Mfalme na kuamkia, 'Sabalkheri Maulana.' Mfalme akaitikia, 'Labulkheri mtoto, karibu.' Mfalme alimuuliza Muhsin kama yu tayari kuifanya hesabu. Muhsin alijibu, 'Naam bwana.' Mfalme alimpa Muhsin ile hesabu. Muhsin hakuwa mtu wa kucheka ovyo au kusema ovyo lakini alipopewa hesabu hii alicheka kidogo kwani alifurahi sana kwa jinsi alivyoiona kuwa ni nyepesi. Mfalme alimuuliza, 'Mbona unacheka baba?' Muhsin alijibu, 'Nimefurahi kwa kunipa hesabu ambayo nina hakika nitaijua.' Mfalme aliposikia haya alifurahi kabla hesabu haijafumbuliwa. Basi Muhsin alianza kuifanya ile hesabu akasema, 'Katika shilingi kumi na mbili kwanza nitampa shilingi sita yule mwenye nusu na nitampa shilingi mbili yule mwenye fungu moja katika mafungu sita ya shilingi hizo, na hapo tena zitabakia shilingi nne. Katika hizo shilingi nne nitampa shilingi tatu yule niliyempa shilingi sita, hapo zitakuwa zake ni shilingi tisa, na nitampa tena shilingi moja yule niliyempa shilingi mbili zitakuwa zake ni shilingi tatu. Shilingi kumi na mbili zimekwisha kugawika bwana.' Mfaime alimwambia amfahamishe kwa nini yule aliyempa shilingi sita kumuongeza shilingi tatu na yule aliyempa shilingi mbili kumuongeza shilingi moja. Muhsin alimfahamisha kwa kumwambia, 'Ukitazama yule niliyempa shilingi sita amemzidi yule naliyempa shilingi mbili
kwa mara mbili basi katika kuwagawia hizo shilingi nne zilizobaki, lazima nimpe shilingi tatu yule naliyempa shilingi sita ili amzidi yule mwenzake kwa mara mbili kama hapo kwanza, na yule mwengine nimpe shilingi moja tu ili azidiwe kwa mara mbili kama hapo kwanza. Hivi ndivyo hesabu hii inavyofanywa.' Mfalme alifahamu vizuri sana na akafurahi kupita kiasi. Mfalme aliisoma tena ile barua aliyopelekewa na Muhsin kwa kutaka kuonana naye ili afanye hesabu hiyo. Alipokwisha kuisoma, aliwaita wale mabawabu waliokuwa wakimzuia Muhsin kuonana naye na kumsukuma, nao walikuwa ni watu watatu. Mfalme alipowaona aliwaambia, 'Siku nyingi nimelala na majonzi na huzuni kwa kufikiri atakayeweza kuifanya hesabu hii. Taabu yote hii iliyonipata ni kwa sababu yenu nyinyi, kwani mngalimuachia huyu Muhsin kuja pamoja na watu wengine nisingalipata udhia wowote ule ulionipata, basi lazima mpate adabu kwa kufanya jambo ambalo sikukwambieni mlifanye.' Mfalme aliamrisha wapigwe fimbo sita sita, na walipokwisha kupigwa walifukuzwa kazini. Mfalme, tena, alimwambia Muhsin aseme lo lote analolitaka ili apewe. Muhsin alisema kwa adabu na heshima, 'Nakuomba unipe kazi yoyote bwana.' Mfalme alifurahi kumuona Muhsin si mtu aliyejitakia makuu na hali alikuwa na nafasi ya kutaka chochote. Basi Mfalme alimwambia Muhsin kuwa hilo atakalompa, atampa mbele ya watu wote walioshindwa kuifanya hesabu ile. Mfalme aliwaita watu wote wa hapo mjini na mawaziri wake pia. Hapo alimpa Muhsin nguo nzuri sana avae kabla hajatoka mbele ya watu. Muhsin alivalia vizuri sana na ilimjaa haiba kwa namna alivyovalia. Mfaime alikaa juu ya kiti chake na kumuweka Muhsin juu ya kiti kilichokuwa karibu yake. Hapo Mfalme alianza kuwahutubia watu, alisema, 'Leo ni siku ya furaha yangu na furaha ya Muhsin ambaye ndiye aliyeweza kuifanya ile hesabu niliyokupeni ambayo iliwashinda mawaziri wangu wote na nyinyi kuifanya. Muhsin aliyekuwa akizuiwa kuonana nami, kwa tabia yake ya ukimya ndiye aliyeifanya. Nimemwambia Muhsin aseme analolitaka ili nimpe, naye ameniomba nimpe kazi yoyote. Nilidhani Muhsin atataka jambo nisilolimiliki lakini kataka jambo dogo sana. Basi kwa hivyo nakushuhudizeni huku ananyosha mkono wake kumpa Muhsin 'kuwa toka leo Muhsin ni mmoja katika mawaziri wangu na ndiye mkubwa wao. Mawaziri wengine hawana ruhusa kufanya jambo lolote bila ya kumshauri yeye.' Hapo Muhsin alipewa mikono na watu wote, na tokea siku ile alikuwa Waziri Mkuu wa Mfalme. Basi ile tabia yake ya ukimya hali ya kuwa ni mwerevu, ndiyo iliyompa daraja tukufu, kama yule simba anayekula nyama nono kwa kwenda kimya kimya humo misituni

0 comments:
Post a Comment