Walikuwepo ndugu wawili
wanaume, mmoja jina lake Shauri na mmoja Taabu. Ndugu hawa walipelekwa shuleni
tokea walipokuwa wadogo, Taabu alikuwa na umri wa miaka saba na Shauri alikuwa
na umri wa miaka minane. Watoto hao walikuwa mahodari sana huko shuleni,
walikuwa na jitihada kubwa sana ya kusoma. Wakirudi huko shuleni wakichukuwa
madaftari yao na penseli zao na wakifika nyumbani walikuwa hawashughulikii jambo
lolote ila kusoma na kuandika. Jinsi walivyokuwa wakitumia wakati wao wote
katika kusoma na kuandika mama yao aliona kuwa watoto wake wataumia kwani
hawaoni katika kucheza hata mara moja. Basi alikuwa akiwaambia, 'Kwa nini
hampumziki ninyi?' Wakamjibu, 'Tukipumzika wenzetu huko shuleni watatupita nasi
hatutaki kupitwa kwa hivyo tuache tu, mama.' Mama yao alipowaona watoto wake
wanasema maneno ya halali yaani ya kweli, alijinyamazia. Watoto hao walikazana
sana, na aghalabu, Shauri akitokea wa kwanza katika mtihani na Taabu wa pili au
kinyume cha hivyo, haikupata kutokea wa tatu hata mmoja katika wao. Watoto hao
walisoma mpaka wakafika darasa la kumi na mbili. Hapo walifanya mtihani unaoitwa
Cambridge. Kwa bahati mbaya Shauri hakupasi lakini Taabu alivuka yaani alifuzu.
Serikali ilimsaidia Taabu kwa kumpeleka Ulaya Uingereza kwa ajili ya masomo ya
juu. Shauri alisoma tena darasa la kumi na mbili. Taabu alipofika Ulaya mambo
yote yalimbadilikia. Aliona mambo yote ya huko yametofautiana na yale ya kwao.
Jambo lililompendeza kuliko yote ni mchezo wa dansi. Taabu alichukuliwa na
wanafunzi wenzake kwenda kutazama dansi, ua alipofika huko alikaribishwa vizuri.
Kwanza waliletewa viburudishaji na huku mdundo unaendelea. Dansi ilikuwa
ikichezwa baina ya wanawake na wanaume. Waliokuwa wakicheza walipendeza sana
kwani aliyekuwa mkubwa zaidi alikuwa na umri wa miaka kumi na nane na mdogo wao
alikuwa na umri wa miaka kumi na nne. Taabu tu ndiye aliyekuwa katika umri wa
miaka ishirini. Mmoja katika wale rafiki zake Taabu, alimleta mtoto mmoja wa
kike aliyekuwa mzuri sana na akamjulisha na Taabu kisha, yule mwanamke,
akamuomba Taabu wacheze pamoja. Taabu alifurahi kupita mpaka, kwani alikuwa
akijuajua kucheza, kabla ya kwenda Ulaya, lakini hakupata kucheza na mtoto wa
Kizungu. Basi Taabu alijikunjua vyema kwenye dansi. Dansi ilipovunjika Taabu
alirudi nyumbani pamoja na rafiki zake. Usiku ule Taabu hakupata usingizi kwa
kufikiri utamu wa dansi. Asubuhi Taabu alikwenda shuleni hali fikira yake yote
iko kwenye dansi ya jana. Mwalimu alipokuwa akisomesha, mengine alikuwa
akiyasikia na mengine yalikuwa yakimpita. Kama tulivyoona kuwa Taabu
alipendezewa na dansi kuliko yote aliyoyaona huko Ulaya. Siku zote akiwauliza
rafiki zake wamwambie pahali penye dansi. Taabu alipoteza wakati wake wote
kwenye madansi. Taabu aliazimia asome namna ya kucheza dansi yaani ajue namna
zote za michezo. Taabu hakushughulika na masomo yake kabisa ila dansi tu. Kwa
hivyo kila mara alikuwa anafeli yaani hapasi katika mtihani. Ndugu yake Shauri
alifuzu katika mtihani wake wa Cambridge mwaka wa pili na Serikali ilimsaidia
kumpeleka Amerika kusoma udaktari. Huko Amerika Shauri aliona mambo mengi ya
kumfurahisha kuliko yale aliyoyaona Taabu huko Ulaya Uingereza. Katika mambo
aliyoyaona Shauri ni mambo mawili tu yaliyomfurahisha kuliko yote nayo ni dansi
na mashindano ya farasi. Walimu wa yule Taabu aliyekuwepo Ulaya Uingereza
walipeleka habari ya Taabu huko kwenye Serikali yao kuwa Taabu haendelei katika
masomo yake. Kwa hivyo Serikali ilimpelekea barua kuwa arudi. Masikini Taabu
alirudi pasi na kupata shahada yoyote ya masomo isipokuwa uhodari wa kucheza
dansi. Serikali yake ilimlaumu na watu pia huko kwao walimsikitikia. Huko kwao
Taabu alipewa kazi ya ukarani wa kupokea kodi za viwanja vya serikali. Taabu
hakuipenda kazi hiyo lakini hakupewa nyingine kwani hakuwa na elimu ya kutosha
ya kumwezesha kufanya kazi bora. Mshahara wake ulikuwa hautoshi lakini akiishi
hivyo hivyo. Shauri, kama tulivyoona kuwa alipenda sana dansi na mashindano ya
farasi huko Amerika lakini juu ya hivyo alishughulikia masomo yake zaidi. Mara
moja Shauri alikwenda kwenye dansi na alikaa huko mpaka saa nane za usiku ndipo
aliporudi kwenda kwake kulala. Alipoamka alikuwa na usingizi mwingi na siku ile
hakuweza kufanya kazi vizuri huko shuleni. Walimu wake walimlaumu na kumshitakia
sana kwa kazi zake mbaya za siku ile. Kwa hivyo tokea siku ile alianza kuichukia
dansi na michezo yote hasa ile ya usiku. Alikuwa na azima ya kujifundisha
kupanda farasi na kujua kushindana pia, lakini alifahamu kuwa mambo hayo
yatampotezea wakati wake wa kusoma. Kwa hivyo aliacha kila kitu cha mchezo na
akaendelea na masomo yake tu. Shauri alitokea kuwa mtoto hodari sana na kwa
bahati nzuri na kwa jitihada yake alifuzu. Alipata Shahada nzuri ya udaktari.
Shauri alirudi kwao kwa furaha kubwa. Watu wote hapo kwao walimfurahia na
serikali pia. Shauri alitokea kuwa daktari mashuhuri sana na maisha yake
yalikuwa mazuri kabisa. Taabu aliyeshughulikia dansi huko Ulaya Uingereza
hakupata kusoma ila alipata hiyo dansi isiyomsaidia kitu. Lakini Shauri, ingawa
alifeli mara moja, alijitahidi na kusoma tu na alifuzu. Kwa hivyo watu husema
muangaza mbili moja humpona, basi Taabu aliponwa na elimu akapata
mchezo.
Menu
Blog Archive
-
▼
2022
(50)
-
▼
December 2022
(50)
- HADITHI YA MVUVI MASKINI
- Ukupigao Ndio Ukufunzao
- Mshika Mawili Moja Humponyoka
- Mchimba Kisima Huingia Mwenyewe
- Simba Mwenda Pole
- Abunuwasi Na Mkono Wa Ajabu
- Wajinga Ndio Waliwao
- Abunuwasi Na Viatu
- Abunuwasi Na Hukumu Ya Kijana
- Abunuwasi Na Mlinzi
- Maji Yakimwagika Hayazoleki
- Mtaka Cha Uvunguni
- Ajali Haikimbiliki
- BINTI NURU
- IMANI YENYE KUFUFUA
- BINTI YANGU JOANITHA
- UA JEKUNDU
- SIKU MBAYA KAMA HII
- SARAFINA
- THE WICKED DEMAND (HITAJI LENYE UOVU)
- FAITHFULNESS
- HYUNG NIM
- JERAHA LA MOYO
- AMKA MAMA
- BINADAMU HATUNA UTU
- FADHILA
- NILIKATAA UCHUNGAJI NIKAWA MKUU WA WACHAWI
- NISINDIKIZENI KWA AMANI
- NATAMANI MAMA ANGERUDI HATA KWA DAKIKA TANO
- KWANINI MAMA…LAKINI KWANINI MAMA?
- BINAADAMU HATUNA FADHIRA
- KIFO CHA YATIMA DANNY
- KIJANA MCHOKOZI NA KICHAA
- KISA CHA BIBI MCHAWI
- MKONO WA FARAJA
- FUKARA WA FIKRA
- WATOTO 100
- NATAMANI MAMA ANGEKUA HAI NIMUOMBE RADHI
- JIJINI DAR ES SALAAM…!
- MSAMBWANDA !!
- KIPANDAUSO
- OMBA OMBA
- KAMANDA
- BALAA
- NILIFANYA BIASHARA YA VIPODOZI NA MISUKULE
- BARUA YA MTOTO KWA MAMA YAKE
- CHOZI LA MILELE.
- UWE SAUTI YAO
- JINSI YA KUIPATA FURAHA
-
▼
December 2022
(50)
-
►
2023
(147)
- ► January 2023 (147)
0 comments:
Post a Comment