Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

BINADAMU HATUNA UTU

 





    KISA CHA KWELI

    Source : https://en.wikipedia.org/wiki/Kevin_Carter



    Ndege aina ya tai akisubiri mtoto afe ili aweze kupata kitoweo picha hii ilipigwa mnamo mwezi marchi ya mwaka 1993. Mpiga picha raia wa Southafrica wa kuitwa Kelvin Carter alifanya safari pamoja na shirika la kugawa chakula cha msaada huko Sudani ya Kusini katika kijiji cha Ayod.

    Wazazi wa mtoto walikuwa busy wakipokea chakula cha msaada, Kelvin Carter alisogea eneo alilopo mtoto taratibu ili asiweze kumfurumusha tai, alitumia takribani dakika 20 kupata picha aliyoitaka kabla ya kumtimua tai.

    Mnamo mwaka 1994 Kelvin alishinda tuzo ya pultizer baada ya kuipeleka picha hiyo katika gazeti la Marekani liitwalo "The New York Times" na picha hiyo ilichapwa katika gazeti mwaka wa 1993. Ingawaje picha hiyo iliibua mijadala mikubwa miongoni mwa jamii ya watu na mashirika ya haki za kibinadamu.

    Kelvin Carter alijiua.

    Ripoti zinasema kuwa Kelvin alipokea upingwaji mkubwa kuhusiana na hiyo picha na alitupiwa kila aina ya lawama. Wengi walilaumu kuwa hakuwa na sababu ya kupiga hiyo picha, bali alichotakiwa ni kutoa msaada kwa mtoto huyo. Gazeti la New York Times linasema msichana hakufanikiwa kufika eneo la ugawaji wa chakula ingawa hakuna anaejua nini kilitokea baada ya hapo.

    Mnamo tarehe 27 Machi ya mwaka 1994 Kelvin alielekea eneo la Braafontein Spruit River eneo ambalo alipenda kucheza alipokuwa mtoto, alijiua eneo hilo kwa sumu ya Carbon Monoxide akiwa na umri wa miaka 33

0 comments:

Post a Comment

BLOG