Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

BINAADAMU HATUNA FADHIRA

 





    KATIKA tawala ya MAPAMBANO palikuwa na walinzi 12 waliokuwa wakilinda ghara la chakula ambacho wanannchi walikuwa wakikiifadhi pindi njaa itakapotokea basi watumie chakula hicho.
    Walinzi hao walilinda ghala hilo kwa takribani miaka 10 wakipigana na wezi mbali mbali pia na wavamizi mbalimbali kutoka tawala jirani waliotaka kuiba chakul a hicho kwa manufaa yao.
    Katika walinzi hao 12 palikuwa na mlinzi mmoja mvutaji wa sigara.Siku moja wakiwa wamengia lindo la usiku yapata majira ya saa 1 jioni waliingia ndani ya ghala ili kuhakikisha kuwa chakula kipo salama.Wakati wanakagua yule mlinzi mvuta sigara alikuwa anavuta sigara wakati huo.Mmoja kati ya walinzi wenzake alimwambia"Zima sigara usije ukasababisha moto".Yule mlinzi alimjibu mwenzake"Nipo makini siwezi kuunguza".

    Wakati wanatoka mlangoni jivu la sigara lililokuwa na moto lilipepeluka na kutua kwenye gunia la chakula.Pasipo wao kujua walifunga ghala na kuanza kulinda.Usiku baada ya muda kidogo kupita wakiwa wamepitiwa na usingizi kidogo mmoja wa walinzi wale aliamka na kwa mshangao aliona moto mkubwa sana ukiteketeza ghala.Walipiga kelele hatimae wanannchi waliamka na kuanza kuuzima moto.Walifanikiwa kuuzima lakini nusu ya chakula ghalani kilikuwa kimeteketea.Msako wa nani aliesababisha moto ulianza na hatimae walinzi wenzake na yule mvuta sigara walimtaja mwenzao kuwa ndie chanzo kwa sababu aliingia na sigara mle ndani.
    Wanannchi wakiwa na hasira kali sana walimchukua yule mlinzi huku wakimpiga na kumdhihaki kwa matusi kutokana na kusababisha hasara wakaamua kumpeleka mbele ya mfalme akapate hukumu.Walipofika kwa mfalme kila mmoja alipiga kelele kuwa yule mlinzi anatakiwa auwawe kwa sababu ya hasara aliyosababisha ya chakula.Mfalme alimtazama yule mlinzi ambae nguo zake zimejaa damu kutokana na kipigo cha wanannchi.Kisha akanyanyua macho yake pia kuwatazama wanannchi waliokuwa na hasira wakisubiri hukumu ya mlinzi kuuawa.Mfalme alipokuwa akipepesa macho yake kwa wanannchi mara alimuona mtoto mmoja mdogo mwenye miaka kama 10 akiwa pale nae akisubiri hukumu ya yule mlinzi
    Mfalme alimfuata yule mtoto kisha akachuchumaa na kumpapasa mashavuni kisha akaagiza vipanda vya fedha vyenye thamani kubwa viletwe.

    Mfalme alimuuliza yule mtoto"Baba yako yuko wapi".Mtoto alinyoosha kidole kuonyesha baba yake alipo ambae nae alikuwa mmoja wa waandamanaji wa hukumu ya yule mlinzi.Mfalme aliamuru vile vipande vya fedha vyenye thamani kubwa apewe yule mtoto.

    Mtoto alifurahi sana kuona kapewa fedha ambayo angeweza kununua kitu chochote kitamu akipendacho.Kisha mfalme akamuuliza tena yule mtoto"Kati ya mimi na baba yako unachagua kuishi na nani".Mtoto bila kupindisha maelezo na kwa sauti kubwa alisema anachagua kuishi na mfalme.
    Pale pale mfalme alimgeukia yule baba wa mtoto na wanannchi kwa ujumla na kuanza kuwapa somo."Angalieni nyinyi wenyewe mashahidi mtoto huyu amekaa na baba yake zaidi ya miaka kumi.Baba yake amehangaika kumlisha na kumvisha mpaka kufikia umri huo.Baba yake amepoteza mali na mali amepoteza usingizi na usingizi ili mladi tu kumpigania mtoto huyu akue.Baba yake amehangaika kutafuta dawa pindi mtoto huyu alipokuwa anaumwa,Alihangaika kumbembeleza pindi mtoto huyu alipokuwa analia lakini cha ajabu leo nimempa vipande vichache vya fedha ambavyo havina kabisa thamani yoyote ya gharama ambayo mzazi wake amemtuza mpaka kufikia hapa lakini mtoto huyu ameniona mimi ni wadhamani kuliko hata mzazi wake aliemtuza miaka 10 na kufikia hatua ya kumkana mzazi wake mbele ya umati wa watu na kuchagua kuishi na mimi kisa kaona kapewa vipande vya fedha ambavyo angeweza kununua chochote kitamu akipendacho."Mfalme aliendelea kusema."Ndivyo ilivyo leo kwa mlinzi huyu ambae amelinda ghala lenu la chakula zaidi ya miaka 10 na kupigana na wezi na majambazi wa kila aina kwa ajili ya kupigania chakula chenu lakini leo kosa moja tu alilolifanya mnataka msahau mazuri yote ya miaka kumi aliyoyafanya mlinzi huyu kama vile mtoto huyu alivyosahau mazuri yote ya mzazi wake aliyotendewa kwa miaka kumi kisa vipande vya fedha vya siku moja.Je sisi ni watu wa roho gani wa kupenda kukumbuka mabaya tu na kusahau mazuri.?"

    Taratibu wanannchi walianza kutupa mawe na siraha za kuulia walizokuwa wamebeba kwa ajili ya kumuuwa mlinzi huyo walianza kusogea nyuma kwa aibu na kujiona ni wakosaji sana.
    MFALME alitoa mamlaka kuwa mlinzi yule hatouwawa na badala yake mfalme alimpandisha cheo mlinzi yule na kuwa mkuu wa ulinzi katika nnchi yake na kumtahadhalisha awe makini na kazi siku nyingine ili yasije yakamtokea mabaya zaidi ya yale.
    TURUDI KATIKA JAMII YETU SISI
    ....MUDA mwingine kwenye ndoa zetu,mtaani kwetu,au katika jamii yetu watu wamekuwa wepesi sana wa kusahau yale mazuri machache machache tunayoyatenda.Badala yake wamekuwa bora sana wa kuangalia kosa moja la bahati mbaya ulilolitenda na kukusema kila sehemu mbaya zaidi wale uliokuwa nao karibu ndio wanakuwa watu wa kwanza kukusema na kukudhihaki kama wenzake na huyo mlinzi.

    Nauliza je katika jamii yako au hapo unapoishi watu wa hivi kama hawa wanannchi wa kwenye tawala ya MAPAMBANO hawapo??.

    Mungu akusaidie sana kukuepusha mbali na hawa watu

    AMEN.


    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG