...SAUTI kutoka sebureni ilisikika ikiita "Danny njoo hapa".Alikuwa si mwingine bali ni mama yake mdogo mke wa baba mdogo wake."Sogea hapa karibu yangu.....Aliekuambi kwamba upakue mboga nyingi ni nani?..".Alipewa swali na mama yake yule mdogo huku akiwa ameshika kiuno."Mamdogo mimi nimechukua vipande viwili tu vya nyama aliechukua vingi ni Devy"Danny aliongea akimaanisha Devy ambae ni mwanae na mama huyu ambae ni mama yake mdogo ndie aliechukua vipande vingi vya nyama wakati wanakula.
Mara ilisikika "Pwaaaaaah"kilikuwa ni kibao kizito cha mdomoni kilichompata Danny na pale pale meno yake mawili ya juu yalitoka yakiambatana na damu nzito."Nimeshakwambia usiwe unanijibisha sogea hapa karibu nikufundishe si unajifanya husikiagi wala huelewi"Mama yule aliongea na kumshika mikono Danny iliyojaa makovu na vidonda mbalimbali kutokana na vipigo vya kila siku.
"Davvvvvvvy"Sauti iliita ya mama yule akimwita mwanae.Davvy alikuwa ni mtoto wa miaka takribani 15 alikuwa akilingana miaka na Danny.Mara nyingi alifurahi sana kumuona Danny anaadhibiwa kwa sababu alikuwa hampendi hata kidogo hivyo hata kuchukua vipande vya nyama vingi alifanya makusudi ili mladi tu Danny aadhibiwe.Alikuwa hapendi kabisa kumuona yatima Danny pale nyumbani kwao.Davvy alielekea kule alikoitwa na mama yake na kumkuta Danny kashikwa na mama yake."Niletee nyasi na kiberiti"Amri ilitolewa na Davvy alitoka mbio kwa furaha kuleta kile alichoagizwa.
Maskini Yatima huyu nyasi zile zilifungwa kikamilifu katika mikono yake yote miwili kisha mafuta ya taa yarifuata juu ya zile nyasi."Na ole wako uchomoe mikono kwenye hizi nyasi we si unajifanya mzuri sana wa kukomba mboga sasa ngoja tuikomeshe hii mikono yako.Ukichomoa tu mikono ujue unakufa leo hapa"Danny alipewa onyo hilo na yule mama kitendo kilichofanya azidi kuogopa zaidi.
Kiberiti kilipigwa kwenye zile nyasi na hatimae moto ukapamba.Danny aliishia kutoa chozi zito huku akimkumbuka baba yake moto ulilindima katika mikono ya Danny na kusababisha maumivu makali.Hatimae Danny uvumilivu wa kulia kimya kimya ulimshinda na akaamua kufumbua mdomo ili alie kwa sauti.Masikini mdomoni bado alikuwa ameyabunda yale meno yake mawili ya mbele yaliyokuwa yamevunjika,Licha ya hivyo bado pia mdomoni na shati lake lilijaa damu zito iliyotoka mdomoni.Aliangusha kilio cha moto mikononi wakati huo Davvy alikuwa anachekelea na ubonge wake ule aliokuwa nao kutokana na kula hovyo hovyo.Walikuwa wakimshangaa jinsi anavyoteseka mtu na mama yake pasipo kutoa msaada wowote.
Mungu akasaidia hatimae moto ukaisha na kumuachia vidonda vingine vingi mikononi.
Hiyo ndio sawa yako haya kwenda kwenye chumba chako na bado baba yako mdogo akiludi utaeleza zaidi.Chumba alichokuwa akikaa ni afadhali hata ya chumba cha mbwa,Alikuwa akifungiwa kama vifaranga wa kuku wakizungu wanaohitaji joto,chumba kilikuwa na dirisha dogo lililopo kwa juu na ndani alipewa blanketi moja tu wala hapakuwa na kitu kingine.Aliingia kwenye chumba hicho na kufungiwa kama ilivyo kawaida yao kumfungia ili asitoke nje kuonana na watu na akawasimulia yanayompata.
Jioni baba yake mdogo aliejulikana kwa jina la Mzee Koyanza alilejea kutoka kazini katika kampuni kubwa alilokuwa anaendesha.Koyanza alikuwa ni mdogo wake na baba yake na Danny aliefariki Miezi sita iliyopita.Walizaliwa wawili tu yaani Koyanza na baba yake Danny wala hapakuwa na ndugu mwingine hivyo Koyanza alimchukua Danny kuishi nae kwa sababu hakuna na pakwenda.Alipofika tu baada ya salamu kwa mke wake na mwanae Davvy aliulizia"Huyu mbwa yupo?".Alimaanisha Danny kama yupo.Hapo hapo ndipo mke akaanza kufunguka maneno ya uongo na kweli kuhusu alichokifanya Danny mchana.Mzee Koyanza alijawa na hasira na akaamulu ziko la mkaa liwashwe,Alienda moja kwa moja kwenye kile chumba na kumtoa Danny ndani kisha bila maelezo alianza kumpiga"hivi bado unajifanya mtukutu et?...Wewe ni kichwa ngumu usieelewa?"Danny hakuwa na lakusema maana hata kama angesema isingemsaidia kitu,Zaidi alilia kutokana na maumivu ya kuchapwa na mkanda wenye chuma.Hakika alitoa kilio kizito sana.
Jiko hatimae lilipamba moto na mzee yule alichukua chuma na kukiweka katika jiko kisha kumchukua Danny na kumlaza katika mbao na kumfunga miguu na mikono kifudifudi."Sasa leo nataka nikuonyeshe kuwa mimi huwa sipendi upuuzi nyumbani kwangu,Kama hizi tabia za ajabu ajabu ulikuwa nazo ni kwenu na wala sio hapa kwangu mpumbafu mkubwa wewe,Hapa kwangu ukileta ujinga utaumia tu".Chuma kilitolewa kwenye moto kikiwa chekundu kisha bila huruma kiliwekwa mgongoni mwa Danny aliekuwa kalala kifudifudi.Danny alipata maumivu makali sana,Alilia kwa sauti kubwa sana kitendo ambacho Koyanza aliona kitajaza watu hivyo moja kwa moja kupitia soksi alizokuwa amebaki nazo miguuni baada ya kuvua viatu mlangoni alizichomoa na kumziba mdomo Danny.Danny alibaki anatoa sauti ya mauvivu kwa kuungulumia tumbo kutokana na sauti kushindwa kutoka.Moshi wa kama vile mtu alikuwa anachoma mshikaki ulifuka kuelekea juu.Harufu ya nyama inayoungua ilitokea mgongoni kwa Danny.Baada ya wao kujilizisha sasa wamemkomesha walikitoa kile chuma mgongoni,Shimo la kidonda cha kuungua kilionekana mgongoni kikitoa damu."Hili ni onyo la mara ya mwisho siku nyingine ukirudia sintakufanya hivi bali nitakukata mikono kabisaaa".Onyo lilitoka kwa baba yake mdogo na kurudishwa katika kile chuma.
Usiku Danny akiwa katika kile chumba huku maumivu ya vidonda yakipamba moto.Alinyanyua macho yake kumshukuru Mungu na kusema"Asante Mungu wa mbinguni uishie milele,Mimi si kitu bila wewe Tazama mali na kampuni alizoacha baba yangu kwa ajili ya urithi wangu leo vimegeuka kuwa mateso kwangu,Lakini niseme nini Eeh Mungu zaidi ya kukurudishia sifa na utukufu,Najua wapo yatima wanaoteseka zaidi yangu mimi si wa kwanza lakini kabla hujaniangalia mimi Mungu waangalie hao yatima wanaoteseka zaidi yangu,Pengine afadhali hata ya mimi napata mateso lakini napewa chakula huenda wao wanapata mateso na chakula hawapewi Uwaguse na kuwalinda zaidi Maana wewe ndie baba yao na mama yao"
Danny alimaliza sara hii kisha akaegamia ukuta huku akilia kwa maumivu zaidi.
Akiwa analia ghafla katika kile chumba pembeni ya ukuta aliona mtu kama kavalia mavazi meupe na yenye kung'aa.Alitazama kwa shida na kugundua walikuwa watu wawili.Maumivu hakuyasikia tena bali wasiwasi ulitanda huku akitetemeka,Alikaza macho zaidi kuwaangalia na ndipo kwa mwanga wa kuchoma machoni aliona nyuso za baba na mama yake waliofariki miezi 6 iliyopita wakiwa wanalia huku wanamwangalia kwa huruma.zilikuwa ni roho za wazazi wake zilizouvaa mwili kwa nguvu ya Mungu na kuja Duniani.........
JE NINI KITAENDELEA
.....TUKUTANE katika kipande cha pili na huenda kikawa cha mwisho cha simulizi hii ya msisimko
Usisahau ku-Like na Kumoment kama kutoa maoni juu ya simulizi hii fupi inayoelezea maisha ya Danny
UJUMBE WANGU
....Mpaka kuandika kisa hiki mimi mtunzi nimeona Jinsi yatima wanavyoteseka sana.Nimeshuhudia wengine wakipata mateso ni afadhari hata ya Danny hivyo kwa uchache na utunzi niliojaaliwa nimeona niseme na jamii japo hata kwa simulizi hii.Huenda ikamfikia na yule nae akaelimisha jamii na hatimae vita zidi ya mateso kwa yatima tukawa tumeipunguza japo ni ngumu kuisha.
Mimi mtunzi nimeileta kwa njia ya kuandika sio mbaya nawe ukaipeleka mbali zaidi kwa njia ya Ku-Share na hatimae kwa namna moja ama nyingine tukawa tumetengeneza jamii salama na MUNGU ATAKUBARIKI kwa kazi yako ya KUSAMBAZA UJUMBE.
0 comments:
Post a Comment