
Hapo zamani za kale katika nchi
moja Afrika, paliishi mama mmoja ambaye alikuwa mjane. Muda mfupi tu kabla ya
mumewe kufariki walijaliwa mtoto mmoja wa kiume ambaye huyo mama alimlea kwa
shida na taabu nyingi. Hata hivyo mama na mtoto wake walipendana ipasavyo. Hapo
katika kijiji chao kulikuwa pia na tajiri mmoja ambaye alikuwa bahili na katili
kweli. Yule kijana maskini alikwenda kwa tajiri kuomba kazi. Tajiri alimwambia
kwamba alikuwa na kazi kwake na angemlipa vizuri sana. Kijana alifurahi kusikia
hivyo na akamwuliza tajiri kwa furaha. "Kazi gani hiyo utanipa mheshimiwa? Mimi
nitaifanya vizuri mpaka hata wewe utafurahia." Tajiri akamwambia, "Ukilala
katika maji baridi sana usiku mzima, nitakupa shillingi laki moja." Ulikuwa
wakati wa baridi sana kwamba maji ya ziwa karibu yagandamane kuwa theluji kwa
baridi. Lo! Kijana hakufikiria angeweza kuwa na pesa nyingi hivyo katika maisha
yake. Tamaa ya kutaka kumsaidia mama yake ambaye wakati huo alikuwa mgonjwa na
mzee, ilikuwa kubwa sana kwa hivyo akakubali bila kufikiria. Mama aliposikia
habari hizo karibu azimie kwa wasiwasi na huzuni. "Mwanangu sitaki uhatarishe
maisha yako kwa sababu ya pesa. Mungu yuko nasi na hajatuacha hata siku moja
tukalala njaa. Atazidi kufanya hivyo hivyo. Je, ukifa nitabaki na nani mwanangu?
Mimi mzee sasa wala sijiwezi!" Kijana alimjibu, "Mama usiwe na wasiwasi wala
woga wo wote! Nitaweza kabisa kulala kwenye maji baridi mpaka asubuhi na siwezi
kufa" Mama bado alizidi kubisha, lakini kijana alisisitiza kabisa kwamba lazima
afanye hiyo kazi ambayo itawaondolea shida zote za kifedha, kama alivyoona yeye.
Kwa huruma ya mama na wasiwasi juu ya mtoto wake, alikwenda karibu na ziwa pale
alimotumbukizwa mtoto wake kwenye maji baridi kama barafu, Alimwona kichwa tu
kimelea juu ya maji. Mama aliwasha moto mkubwa karibu na ziwa lile kwenye ufa,
ili aweze kumwangazia angalao mwangaza na kumwona. Usiku kucha mama mtu
hakufunguka jicho hata dakika moja. Alimlilia Mungu amtunze mwanae asife kwa
baridi. Kwa huruma ya Mwenyezi Mungu, kijana alistahimili baridi yote ile mpaka
alfajiri siku ya pili. Alikwenda kwa tajiri kupokea malipo yake lakini tajiri
akamwambia. "Hupati hata ndururu ng'o!" "Kijana alishangaa akamwuliza, "Kwa nini
mheshimiwa? Uliniahidi kunipa shillingi laki moja nikilala katika maji yabaridi
usiku mzima. Usiku mzima nilikuwa ndani ya maji hayo na shahidi wako
wameshuhudia na pia mama yangu." "Ehe, hapo sasa umenena. Mamako aliyekuwashia
moto ili upate joto usiku mzima. Hayo ndiyo yalikuwa maagano yetu? Sikumbuki
tukiagana kwamba mama yako atakuja na kuwasha moto mkubwa wa kukupa joto kisha
unidanganye umelala kwenye maji ya baridi. Unaniona mimi bwege sio? Nenda zako,
sikulipi cho chote." Kijana alikasirika kweli na akamweleza jirani yake mzee
Abunuasi. Kama kuna watu Abunuasi aliowazira, ni matajiri waliopenda
kuwaangamiza maskini badala ya kuwasaidia. Abunuasi akamwambia kijana asiwe na
wasiwasi kwamba rafiki yake Sultan atamsaidia. Akamwambia aende kwake na
kumweleza habari zote. Kijana alifuata ushauri wa Abunuasi, lakini Sultani
aliposikia kisa chote kutoka pande zote mbili aliamua kwamba kijana asipate
malipo kamwe. Abunuasi alishangaa na uamuzi huo wa Sultani mzima wa nchi
akamwambia kijana bado asiwe na wasiwasi atapata hela zake. Kijana alimwahidi
Abunuasi kumpa shillingi elfu ishirini akimsaidia. Abunuasi aliandaa karamu
kubwa na akawaalika watu wengi pamoja na Sultani na yule tajiri pia. Alichinja
mbuzi akatayarisha vitu vyote, mchele, mboga zikakatwakatwa na kuwekwa kando.
Moto mkubwa uliwahswa na kila kitu kikawekwa kando ya moto, nyama ya mbuzi
katika sufuria pamoja na vitunguu na viungo. Mboga, mchele, zote zikawekwa kando
ya moto na Abunuasi akaenda kuwakaribisha wageni wake. Wageni walingojea chakula
siku kutwa hawakuona hata maji ya kunywa. Abunuasi aliwaambia kwamba chakula
bado kinapikwa jikoni na wala hakijawa tayari. Itabidi wangojee. Mwisho
walikasirika na kuingia wote katika jiko. Walikuta moto unawaka vizuri na kando
ya huo
0 comments:
Post a Comment