Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

NISINDIKIZENI KWA AMANI

 





    Ndugu zangu nioneeni huruma Mimi ndugu yenu nawaona Leo mkiwa katika hali ya umoja uku mkinisindikiza katika safari yangu ya mwisho hapa Duniani, sikutegemea kama ipo siku nitawekwa ndani ya jeneza uku nikibebwa kama mtoto mchanga, ama kweli Duniani tunapita.



    Namuona mwanangu Rehema akilia kwa uchungu sana mpaka anapoteza fahamu ameshindwa kuamini kabisa kwamba Leo Baba yake aliyempenda anafukiwa katika udongo na tumaini la kuonana nae tena likipotea.



    Jamani ndugu zangu naomba mnishushe taratibu katika makao yangu ya milele kwani sikuamini kabisa kwamba ipo siku nitaitwa marehemu ila Leo nafsi imenisaliti na pumzi ya uhai imetoweka kabisa, kweli Duniani sote ni wakimbizi, naumia sana kuona familia yangu ikinililia kwa uchungu sana mpaka baadhi ya ndugu zangu kupoteza fahamu.



    Jamani majirani nishusheni taratibu katika kaburi langu kwani adhabu nayoenda kuipata ni kubwa sana, niliwadharau masikini, niliwatumikisha mabinti wadogo kingono na mpaka wengine niliwatenda Hata kinyume na maumbile yao sikujua kama ipo siku viungo vyangu vitakoswa nguvu na kuitwa marehemu, naomba mnisamehe jamani niliwabaka watoto wadogo ili nipate pesa, niliwauwa mpaka ndugu zangu ili niwe na majumba ya kifahari kumbe nilikuwa najidanganya, ebu nitazameni Leo nikiwa ndani ya jeneza nashushwa taratibu bila Hata ya huruma sikutambua kwamba ipo siku nitaupoteza uhai wangu.



    Acheni nitangulie katika makao yangu ya milele japo sistahili hata kupokelewa katika hali ya neema. Pesa zangu zilinipa jeuri hasa kipindi Kile nikiwa kiongozi Mkubwa serikalini kila aliyenipinga niliweza kuuchukua uhai wake katika hali ya maumivu sana.



    Jamani siamini kama Leo nafukiwa tena katika mavumbi kwanini lakini siku ya kufa haijulikani Labda ningetubu mapema ingekuwa bora kwangu ningekufa kifo chema. Kwa pembeni nakuona jirani yangu Mzee Peter ukiwa unaachia kamba uku ukijawa na hasira naomba unisamehe najua bado unakinyongo kwangu toka nilipompata binti yako mimba akiwa kidato cha tatu.



    Jamani ndugu zangu naomba mnishushe taratibu katika kaburi langu mnisamehe makosa yote niliyowatendea kwani Sikujua kama ipo siku mdomo wangu utajazwa pamba uku mwili wangu ukiwekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti naomba mnionee huruma na kunisamehe makosa yangu.



    Mwanzo niliamini kwamba pesa zangu zinaweza kunisaidia na ndio maana Hata kwenye misiba ya jirani zangu sikuweza kufika nikiamini pesa zangu zitanilinda, lakini Leo eti nimekuwa mfu niliyewekwa ndani ya jeneza jamani naomba mnisamehe sikujua kwamba Duniani tunapita Leo naelekea katika mateso ya milele.

0 comments:

Post a Comment

BLOG