Mke wangu alisajili line mpya bila Mimi kujua,Jina lake Jenifa
Godson.
Jana usiku nimerudi home akaniomba Tshs 10,000/= akasuke
nywele nikamwambia sina ila nakupa Tshs 7,000/=
Wakati tumelala,message ikaingia katika simu yangu "Hi,my
Love!",Nikatoka nje(toilet) nikamjibu,"We ni nani?"
MESSAGE:
"Ni mimi Jen Msambwanda" kusikia sambwanda, Mshipa wa
"Samsing" ukanicheza!
MIMI:
Jen Msambwanda wa wapi tena?
MESSAGE:
"Buana baby,nawe,si pale unapokulaga kila siku?"
MIMI:
"Oooh,kumbe unaitwaga Jenifa!Namba yangu umeipata
wapi?
MESSAGE:
Nimepewa na rafiki yako DJ Tipwili.
Nakupenda sana handsome, sema huwa naogopaga kukwambia.Fahamu
mi sijiwezi juu yako,yaani kila ukija kula, natamani usiondoke,nikwambie
yaliyomo moyoni mwangu,Unanitesa mwenzio!"
MIMI:
Ooh,Jamani pole mpenzi!
Hata Mimi nilikuwa nakupenda,yaani kila nikiona hilo
"tako",nahisi mzunguko wa damu ku-change! I love you too Honey!
MESSAGE:
Basi mpenzi,Nikuombe kitu?
MIMI:
Aaah,sema tu.
Message:
Naomba Tshs 50,000/-
MIMI:
Nakutumia sasa hivi.(Nikatuma)
MESSAGE:
Wow!
Asante mume wangu,haya rudi ndani tulale.Ni mimi mkeo Mama
Kiduku hapa!
♂♂♂
Basi mwenzenu leo nimezuga zangu mlinzi nipo nje hata ndani
sitaki kwanza hakuna hata feni alafu mbu wengi Acha awake mwenyewe
!
0 comments:
Post a Comment