Asili
ya neno ajali ni neno la Kiarabu na maana yake ni, muda'. Tukifasiri kwa
Kiswahili ni kuwa jambo lo lote, likifika muda wa kutuka, muda huo haupiti, na
ikiwa jambo hilo ni la kumfikia mtu, mtu huyo hawezi kulikimbia, yaani ni lazima
limfikilie. Wakati mwengine tunalifasiri neno 'ajali' kwa maana ya mauti, kwa
hivyo tukisema ajali haikimbiliki, maana yake mtu yeyote hawezi kuikimbia ajali
yake, yaani mauti yake. Undani wa fumbo hili ni kuwa kila jambo alilolitakia
Mungu likufikilie, lazima litakufika.' Bibi Maahira alianza hadithi kwa kusema,
"Hapo zamani palikuwa na watu walioshirikiana kwa kufanya biashara ya kuuza
nguo. Biashara hiyo ilifanya baraka sana na iliendelea vizuri. Ilikuwa kama
biashara za kampuni, kwa hivyo, iliwabidi wafungue matawi kwenye miji mingine.
Tawi moja kubwa lilifunguliwa kwenye mji unaoitwa Barani. Barani ulikuwa mji
mkubwa wenye watu zaidi ya laki moja. Mji huo ulikuwa na majumba mengi ya mawe
na yasiyokuwa ya mawe. Ulikuwa na njia nyingi za magari ya motakaa na magari
mengineyo. Kwenye tawi la huko Barani alipelekwa mtu mmoja mkubwa wa tawi hilo
aliyekuwa akiitwa Bwana Peku. Bwana Peku alikuwa akifuga masharubu na ndevu, na
alikuwa mweupe na mnene. Urefu wake ulikuwa kiasi cha futi sita. Tabia yake
hakuwa mtu wa hisani na huruma, alikuwa akiwaonea na kuwadhulumu watumishi wake
bila ya kiasi. Ilivyokuwa katika mji huo wa Barani hapakuwa na kazi za
kuwasaidia watu kuendesha maisha yao, isipokuwa huko kwenye tawi jipya la
biashara, Bwana Peku aliweza kupata watu wengi wa kufanya kila namna ya kazi,
lakini kazi zenyewe zilikuwa zimoto kabisa, kwani mtu yeyote alikuwa hapati kazi
mpaka atie sahihi mkataba ufuatao:
0 comments:
Post a Comment