Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

JIJINI DAR ES SALAAM…!

    JIJINI DAR ES SALAAM…!ALICE, mwanamke wa Kimarekani, ambaye alizaliwa na kukulia Texas, mchana huu alikuwa ndani ya jengo la ghorofa tatu katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Mtaa wa Sokoine, akisubiri kutekeleza jukumu lililomtoa Texas, Marekani kiasi cha miezi mitano iliyopita.Ndiyo, alikuja Tanzania, jijini Dar es Salaam kwa lengo maalum, akiwa amelipwa dola 50,000 kama advansi na akikamilisha kazi aliyotumwa, atalipwa baki yake ambayo yeye na aliyemtuma walikubaliana.Alikuja kama mtalii, akashukia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Arusha. Wiki mbili za kwanza aliishi jijini Arusha. Wiki ya tatu alipaa hadi jijini Dar ambako pia alifikia katika hoteli ya kawaida lakini yenye hadhi ya kutosha kumhifadhi mtu wa aina yake.Akiwa katika mwonekano wa kujiamini, Alice mara kwa mara alipendelea kutembelea ufukweni eneo la Kigamboni mara mbili kwa wiki na mara moja akiingia katika kasino moja iliyokuwa mtaa wa Samora ambako alikesha.Wakati alipokuja Tanzania kwa jukumu hilo maalum, alibeba nguo zake chache pamoja na bastola ndogo ambayo haikubainika katika maeneo ya ukaguzi aliyopita. Vitu vingine ni vitambulisho vilivyomtaja kwa jina la Catherine John na siyo Alice Ronald.“Mzigo utakuja baada ya mwezi mmoja,” aliambiwa na mtu huyo aliyempa kazi hiyo maalum. “Katengeneze mazingira kwanza. Tanzania ni nchi ndogo sana na nina hakika ukiwa makini hakuna watakachoambulia kwako. Ninakuamini kuwa wewe ni mwanamke wa shoka. Kazi yako ya Afghanistan na Syria inatosha kunifanya nikupe kazi hii. Na ndiyo maana FBI walikuamini kwenda nchi kama hizo ulizotumwa.Mwezi mmoja baadaye mzigo alioambiwa utamkuta huko Dar ulifika. Ilikuwa ni silaha nzito, bunduki ya aina yake ambayo alipaswa kuitumia mara moja na akishakamilisha kazi hiyo, ataondoka mara moja.Jinsi silaha hiyo ilivyogawanywa vipande na kusafirishwa mpaka jijini Dar na kisha kuunganishwa tena ni mbinu iliyowaacha gizani wataalamu wote nchini.Kwa siku kadhaa, kwa kutumia mawasiliano na watu wa mtandao wake, Alice aliweza kujua kuwa kazi itafanyika saa saba mchana, siku fulani wakati mlengwa atakapokuwa anakuja katikati ya jiji kwa majukumu fulani akiwa katika gari aina Land Cruiser jeusi lenye namba ambazo alitajiwa, na kwamba, ataliona kwa usahihi gari hilo likiwa umbali hata wa kilomita mbili kutoka katika dirisha la hoteli hiyo na kuwaona wote watakaokuwa ndani kwa usahihi vilevile.Pia aliambiwa kuwa huyo mlengwa mara nyingi huwa akija katikati ya jiji, akitumia hilo gari, lakini pia mara nyingi huwa anatanguliwa na gari lingine ambalo pia alitajiwa namba zake au gari hilo ambalo ni kama la ulinzi huenda likawa nyuma yake.Kwa muda huu, Alice akiwa amekwishakunywa kahawa nzito, alitulia akiangalia saa na kuwa tayari kwa kazi iliyomleta Tanzania jijini Dar! Alikuwa amesimama kando ya dirisha akiwa tayari na silaha yake kwa minajili ya kutekeleza jukumu lake.Mara akaona upungufu wa magari katika barabara hiyo. Akiwa hapo dirishani, ghorofa ya tatu, aliweza kuona kwa umbali mkubwa wa barabara hiyo kuanzia eneo la kituo cha daladala cha Stesheni hadi kufikia hapo alipo.Gari lolote ambalo lingetokea upande huo angeliona kwa usahihi na hivyo asingepata shida kufanya lolote lile alilolidhamiria.Akayakumbuka maneno ya mtu yule aliyemtuma kuja Tanzania kukamilisha kazi hiyo kwa malipo ya dola ambazo kwa fedha zza Tanzania zilikuwa ni shilingi bilioni moja, milioni mia moja kumi na sita, na laki tano.“Kuna mtu anataka kutuharibia mambo huko Afrika Mashariki. Mtu huyo yuko kwenye nchi moja changa ya Tanzania ambayo ni jirani na Kenya. Kwa Afrika Mashariki naijua Kenya, nilishawahi kufika, lakini hiyo ya jirani naisikia tu. Sijawahi hata kutia mguu.“Hakikisha unafanya kazi hiyo kwa ufanisi na baada ya hapo silaha hiyo iache hapohapo chumbani. Ukiona umeshindwa, jimalize mwenyewe vinginevyo kuna mtu atakumaliza hukohuko. Kazi ni kwako!”Maneno hayo yalijirudia mara nyingi kichwani mwake akizingatia kuna malipo yaliyokwishaingia kwenye akaunti yake benki. Na alimjua vizuri huyo aliyemtuma kwa jinsi alivyo na mtandao mkubwa, kwa hali hiyo aliliamini pia tishio lake kuwa kama atashindwa kufanya kazia hii, kuna mtu atakayemuua bila ya kumjua!Mara mlio mdogo ukasikika katika mkufu wake shingoni. Akaushika na kuutazama. Kisha sauti ndogo ikatokeza, “Yuko umbali wa kilomita mbili….Uwe tayari… Yuko spidi kali ametanguliwa na gari dogo…” akatajiwa namba za gari hilo. Kisha, “Kazi imebaki kwako!”Haraka akajiweka dirishani, akijua kuwa mlango wake ameufunga na hivyo isingewezekana kwa mtu yeyote kuingia labda kama atatumia ufunguo bandia au wa akiba wa hoteli hiyo.Akaishika bunduki na kuiweka sawa. Akaiweka kofia yake kichwani vizuri na kuzinyoosha nywele zake ndefu nyuma yake.Akatabasamau kidogo alipoweka shabaha kwenye usawa wa barabara hiyo ambayo labda kwa kuwa siku hiyo ilikuwa ni sikukuu ya kidini, kulikuwa na upungufu mkubwa wa watu na magari.Aliinua bunduki na kuweka usawa wa gari moja dogo ambalo wakati huo ndilo pekee lilikuwa likija. Akacheka kidogo alipobaini kuwa aliwaona kwa usahihi wote waliokuwa ndani kupitia darubini kali za bunduki hiyo.Akaishusha bunduki huku akisema, “Haponi!”Kwa mara nyingine akatabasamu. Kisha akalikata tabasamu hilo na kuunda ule uso wake wa kikazi zaidi. Mwonekano ambao ulimtawala wakati alipokuwa Afghanistan ndiyo ukatwaa nafasi.Mara akasikia tena mlio mdogo kwenye mkufu wake shingoni. Mlio huo ukarudiwa mara mbili kwa namna ambayo aliijua kuwa ni ishara ya kumtaka awe makini zaidi.Sasa akaitwaa tena bunduki na kuiweka sawa. Mara akayaona magari mawili kwa mbali yakija. Alijiamini kwa kuwa alijua kuwa kwa uwezo wake wa shabaha kali ndiyo maana hata Wamarekani huysusan Shirika la FBI wamemkubali kwa asilimia mia moja!Akalenga kwa shabaha kali akitumia darubini kali ya bunduki hiyo ya kipekee! Akafanikiwa kuwaona kwa usahihi watu waliokuwa kwenye gari la pili. Akafanikiwa pia kumwona kwa usahihi zaidi mlengwa ambaye alikuwa ameketi kiti cha katikati, na akiwa katikati ya watu wawili ambao hakuwajua.Hakuhitaji kuwajuaa hao watu wengine, alikuwa na sura ya huyu mlengwa wake maalum.Akajiweka sawa na kufyatua risasi moja kwa shabaha kali!....******MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG