Ali
alikua amesimama pembeni ya kaburi la Mama yake, alijitahidi kuzuia machozi
lakini yalitoka yenyewe. Nikweli alikua anamchukia sana Mama yake kutokana na
mambo aliyokua amemfanyia lakini bado alikua ni Mama yake na kuna kitu kilikua
kinamuambia mpende.
Miaka sita ilikua imepita tangu kutengana na Mama yake. Alikua amemaliza kidato cha sita yuko tu mtaani anateseka baada ya kukosa mkopo wa kumpeleka chuo.
Alilazimika kukaa mtaani kufanya vibarua huku akiishi kwa shida. Wakati huo alikua akiishi yeye na Mama yake tu ambaye alikua anaumwa mara kwa mara hakuweza kumlipia ada. Mara alikuja Baba mmoja, alikua akimfahamu, ni jirani yao tajiri ambaye alikua anaishi huko mjini.
Alikuja akitaka kumsaidia akisema kua yeye ni Baba yake, Ali hakumuelewa kwani tangu akiwa m mdogo Mama yake alimuambia kua Baba yake alifariki. Yule Baba alikasirika sana na kufoka akasema yeye ndiyo Baba yake na Ali alipombana Mama yake basi alisema nikweli yule ni baba yake.
Yule Baba alisema alikua hafahamu kua ana mtoto mpaka watu walipomuambia na alienda pale kumchukua. Ali alishangaa sana kwa Mama yake kuruhusu aishi maisha ya mateso mlo mmoja kila siku wakati Baba yake alikua tajiri kiasi kile.
Mama yake alibaki kimya akimuomba tu msamaha. Ali hakua tayari kumsamehe aliondoka na Baba yake ambaye alinza kumsomesha chuo, hakuwasiliana tena na Mama yake mpaka alipofariki dunia ndipo alilazimika kuja kutembelea kaburi lake hata mazishi yake hakuhudhuria.
Alikua na hasira naye, alishakata mawasiliano naye hata aliposikia anaumwa sana. Hata Mama yake alipomuomba kua ampelekee wajukuu zake bado hakumpelekea na Mama yake alikufa huku akisononeka kuona mtoto wake wapekee kamkataa.
Ali hakujali, aliendelea na maisha yake na Baba yake na familia yake mpya ambayo ilikua ikimjali sana. Mara kadhaa alitaka kwenda kumsalimia Mama yake lakini Baba yake alimkataza akimuambia kuwa amewapotezea muda sana kutokumuambia Baba yake.
****
Ali alitembelea Kaburi la Mama yake kisha kurejea mjini, maisha yaliendelea lakini miezi sita baada ya Mama yake kufariki Baba yake alianza kuugua, alipelekwa India na kugundulika ana matatizo ya figo. Watoto wote walipimwa na wote hawakua wanafaa kumpatia Bbaa yao figo kasoro Ali.
Hakua na hiyana hakufikiria hata mara mbili, alitaka Baba yake aishi hivyo alimtolea figo moja. Lakini pamoja na kumpa figo Baba yake alifariki wiki mbili baadaye. Lilikua pigo kubwa sana kwa Ali kwani bado alikua hajaishi naye vizuri na kufurahia mapenzi ya Baba yake.
Lakini baada ya Baba yake kufariki mambo yaliabdilika, familia nzima ya upande wa Baba yake ilimtenga, walisema hawamtambui na alifukuzwa kazi katika kampuni ya Baba yake, yeye na wanae pia walifukuzwa katika nyumba ile na katika urithi hakuambulia chochote.
Ali alichanganyikiwa akijua ni laana ya Mama yake aliamua kurudi kwenda kudhuru tena kaburi la Mama yake. Hapo ndipo alipokutana na Mama yake mdogo na kumuelezea kila kitu. “Nilijua tu wale si watu wema, kwa walichomfanyia Mama yako nilishangaa hata yeye kukuruhusu uende…”
Alia lishangaa kwani hakujua chochote. Ndipo Mama yake mdogo alipomhadithia mkasa mzima kwanini Mama yake alimficha. Alimuambia wakati Mama yake akiwa ndiyo kamaliza darasa la saba, kafaulu basi Baba yake alikua Kijijini.
Yeye alikua anasoma chuo na siku moja alikutana na Mama yako kisimani akambaka, Mama yako hakusema kwa uoga lakini Bibi aligundua na kumuuliza, alipombana ndiyo akasema kila kitu. Kutokana na utajiri wa familia ya Baba yako basi waliogpopa kusema.
Mpaka pale ambapo Mama yako alipogundulika kua ana ujauzito. Walienda kwa Baba yake ambaye wakati huo alisharudi chuo lakini wazazi wake waliukataa, aliporudi tena miezi mitatu baadaye mimba ya Mama yako ilikua kubwa. Baba yako hakutaka Mama azae kwani aliona kama ingekua aibu.
Walijifanya kumchukua Mama ili wamtunzie nyumbani kwao, alipofika walainza kumtesa, kumpiga na walimpa vidonge ili mimba itoke, walimchanganyia kwenye chakula na mara tatu walijaribu kumtoa mimba lakini ilishindikana.
Hapo ndipo Mama yako alitoroka na kwenda kwa Bibi yako mdogo mpaka alipojifungua na familia ya Baba yako haikutaka kujishughulisha tena na Mama na walikukana kabisa. Mama yako hakutaka ujisikie vibaya kua umekataliwa na Baba yako ndiyo Maana hakukuambia kitu.
Pia Baba yako alipokuja Mama yako aliona ndiyo nafuu ya wewe kusoma ili upate kazi na uje umsaidie ndiyo atakuja kukuambia ukweli ukiwa na maisha yako. Lakini alisubiri na kusubiri hukurudi nyuma hata kwa salamu.
Ilikua ni ndoto ya Mama yako kufika chuo kikuu, na aliposhindwa alijua kua wewe utafika hivyo uliposhidwa kufika wakati umefaulu alikua tayari kufanya chochote ili ufike chuo kikuu ndiyo maana Baba yako alipokuja hakusema chochote ili tu ufike chuo kikuu.
Alifurahi sana aliposikia kua umemaliza chuo kikuu, ingawa alitamani kuwepo kwenye sherehe yako lakini alijua utarudi tu, alikata tamaa aliposikia umeoa bila hata kumuambia na tangu siku hiyo basi alijua kua ashakupoteza.
Ali alilia sana, alimlaumu Mama yake kwa kutomuambia ukweli kwani kama angejua sio tu asingeenda kwa Baba yake bali hata nagemuua. Lakini hakua na namna, ilikua ni lazima maisha yaendelee, alirudi mjini kutafuta kazi nyingine.
Alipata kazi na kuanza maisha yake, baada ya kuchunguza sana ndipo aligundua kuwa, kumbe Baba yake alishajua kua ana matatizo ya figo na atahitaji mtu wa kumpa hakutaka kupata kutoka kwa watoto wake wa ndoa ndiyo maana alimtafuta Ali ili kuwa kama mtu wa kumpa figo.
Aliumia zaidi alipogundua kuwa watoto wengine hata hawakupimwa alipimwa yeye tu ndiyo maana hata kwenye uithi hakupewa chochote kwani hakukua na mapenzi yoyote kutoka kwa Baba yake. Hayo yalizidi kumuumiza huku akimkumbuka Mama yake ambaye ndiyo pekee alikua na mapenzi ya kweli kwake.
**** MWISHO.
Wanawake wanavumilia mengi kwaajili ya watoto wao, wanaume wengi hujifanya Baba watoto wanapokua wakubwa lakini hawajui changamoto ambazo wanawake hupitia kwaajili ya furaha za watoto wao, huweka rehani furaha zao kwaajili ya watoto..

0 comments:
Post a Comment