Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

NATAMANI MAMA ANGERUDI HATA KWA DAKIKA TANO

 





    Baada ya Mama yake kukazania kuja mjini ili kupafahamu Dar John alilazimika kumpeleka mjini. Siku moja mfanyakazi wake alipata msiba hivyo aliondoka nyumbani. Kwakua hakuwa akipika kwani alikua bize na kazi, John aliamua kumtoa Mama yake na kumpeleka katika Hoteli nzuri ya hadhi yake.

    Alimsaidia Mama yake mtu mzima kushuka kwenye gari mpaka kwenye ile Hoteli. Huko waliagiza chakula na kuletewa, Mama yake hakuweza kutumia Uma hivyo aliomba maji kunawa mikono, John alikasirika akisema Mama unaniaibisha lakini Mama hakuwa na namna alinawa na kuanza kula.

    Wakati wa kula, kutokana na uzee na ugonjwa wa kutetemeka mikono aliokua nao, chakula kilidondokea nguo na kudondokea chini, John alizidi kukasirika, aliona kama Mama yake anamuaibisha hivyo alimharakisha ale na kumnyanyua harakaharaka hata kabla hajashiba ili waondoke shemu ile.

    Kabla hajaondoka, alitokea Dada mmoja wa makamo ya John, yeye ndiyo alikua mmiliki wa hoteli ile baada ya kuachiwa urithi na wazazi wake. John alikua anamfahamu na alianza kwa kumuomba msamaha, kwa uchafuzi alioufanya Mama yake.

    Lakini yule binti hakumsikiliza, alimshika Mama yake John mkono na kumrudisha kukaa, alichukua chakula na kuanza kumlisha taratibu, baada ya hapo alimchukua na kumpeleka bafuni, akamsafisha nguo zilizondondokea chakula, kisha akarudi na kusafisha sehemu ambapo chakula kilimwagika.

    Kila mtu alimshangaa kwani kwa muonekano wake watu walijua kuwa atawatukana na kuwafukuza. Aliporudi wakati anajaribu kumpendisha Mama yake John kwenye gari, John alishindwa kuvumilia, aliamua kuuliza.

    Huku akifikiri labda yule binti amefanya vile kwakua anampenda alimuuliza kwanini umefanya hivi binti alimjibu. “Wazazi wangu wote wamefariki, hakuna siku hata moja ambayo inapita sitamani kama wangekua hai, nikawaona wakiwa wazee.

    Waugue na niwauguze, niwasafishe wakijichafua kwasababu ya uzee, niwalishe wakiwa wagonjwa. Wewe Mama yako amechafua tu meza na sakafu umekasirika lakini kwa uchungu nilionao wa kutokumuona Mama yangu ningeweza hata kuitoa hii Hoteli ili Mama yangu arudi tena hata kwa dakika tano tu.

    Najua hoteli nitapata nyingine lakini Mama siwezi kupata mwingine. Hivyo kabla hujaangalia watu wanamuonaje Mama yako, waza ipo siku hata wewe hutamuona kabisa na hapo ndipo utajuta kila siku ya maisha yako.

    Mtendee wema sasa ili siku akiondoka basi ujue anakuangalia huko aliko kwa tabsamu.” Binti alimaliza kuongea na kuondoka huku akimuacha John akiwa meduwaa tu kwani alidhanilabda binti anamtaka.

0 comments:

Post a Comment

BLOG