Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

Maji Yakimwagika Hayazoleki




    Alikuwepo kijana mmoja ambaye alikuwa na tabia nzuri sana machoni kwa watu. Kijana huyo alikuwa na adabu nzuri sana na kila jambo lake lilikuwa zuri, watu wote walimpenda

    kwa mwendo wake huu. Jinsi watu walivyompenda walikuwa wakimuandika kuwa wash wao baada ya kufa kwao. Watu wengi walimfanya wash, naye alikuwa akifanya kama alivyolusiwa. Kumbe vile mtu yule alikuwa mbaya sana kwa siri, alikuwa na tabia ya wizi ambayo watu hawakuijua. Mara moja aliwekwa wash na mtu mmoja na baada ya yule mtu kufa alianza kufanya yale aliyousiwa. Warithi wa yule maiti walibaini kuwa yule wash anaiba baadhi ya mali yao. Basi walimshitaki. Huko mahakamani aliachiliwa. Hakimu alisema, hasadiki kuwa mtu yule anaweza kuiba, kwani alikuwa maarufu kwa uaminifu. Baadhi ya mali ya yule maiti ilikuwa serikalini. Basi siku moja yule wash alikwenda akachukuwa, huko serikalini, shilingi elfu na alisema kuwa anataka kuwanunulia watoto wa huyo maiti nguo na chakula. Fedha hiyo aliitumia kwa haja zake tu wala hakuwapa hao watoto alichosema. Mama wa wale watoto alimwambia yule wash, mara kwa mara, kuwa watoto hawana chakula wala nguo, lakini yule wash alipuuza. Mama watoto alikwenda huko serikalini nafsi yake na kusema kuwa hali ya watoto ni mbaya kwa hivyo apewe pesa za chakula chao na nguo.



     Mshika fedha za maiti alistaajabu kuona ametoa shilingi elfu karibuni kumpa wash na ikawa zinakwisha. Alipomuuliza huyo mama watoto habari ya zile shilingi elfu mama watoto alisema hajui kitu cho chote kilicho husu fedha hiyo. Hapo hapo alipelekwa askari kwenda kumchukua huyo wash. Alipofika huko kwa mshika fedha na akamuona yule mama watoto alifahamu kuwa matata ya tayari. Kabla hajaulizwa neno aliruka na kumwambia yule mama watoto, 'Mimi ninatoka nyumbani kukuletea pesa za watoto, mbona sikukuona?' 'Ah! bwana, siku nyingi nimekuomba unipe pesa za watoto nawe unanipuuza, ilikuwaje leo kusema ulikuja nyumbani kunitafuta? Yule mama alijibu. Mshika fedha za maiti alimpeleka polisi na huko alishtakiwa kuvunja uaminifu. Hapo ndipo alipobainika uizi wake na ndipo maji yake yalipomwagika. Alijitahidi sana kutaka kuyazoa maji yake kwa kwenda huko na huku ili ajinusuru, lakini wapi! Maji yakimwagika hayazoleki. Kesi hii ilimkalia vibaya sana, aliweka mawakili kwa mali nyingi na vile vile alisema na yule mama watoto asimkalifishe huko kortini. Mama watoto alisema yeye hamkalifishi lakini hasemi uongo ila kweli tu. Basi kesi juu yake ya kuvunja uaminifu ilisikilizwa. Wash alijitahidi sana kuweka heshima yake kama zamani, lakini hakufuzu kabisa. Hakimu alimuona mkosa na akampa adabu ya kifungo cha miezi sita. Hadhi yake na heshima yake ilivunjika, hata alipofunguliwa watu hawakumuheshimu wala hawakumpenda
    Pseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

BLOG