"NILIFANYA
BIASHARA YA VIPODOZI NA MISUKULE"
Mara
tu bbaada ya kumaliza kidato cha nne Angel aliwaacha wazazi wake Shinyanga na
kwenda Dar es salam kukaa kwa shangazi yake.
Angel
alivyokua na rika la miaka kumi nane alikua na kijiuso kidogo, macho makubwa
ambayo kila wakati yalionekana kama yanatoa machozi, Alikua ana pua ndogo
nyembamba chini ya pua hiyo kulipangika safu mbili za midomo ambayo haikutulia
kwa kutabasamu kila Mara.
Urembo
aliokua nao Angel miaka ile hauwezi jirudia ni saw a alichezea shilingi
Chooni.
***
Dar
aliishi na shangazi yake maeneno ya Msasani osterbay, mboga tatu kwao haikuwa
tabu kama ilivyo sifa ya eneo lile.
Ushamba wa huko alikotok ulimjaa akawa hatoki ndani kama mwali anayesubiria kuolewa.
Ushamba wa huko alikotok ulimjaa akawa hatoki ndani kama mwali anayesubiria kuolewa.
Jogoo
wa shamba hawiki mjini lakini anaweza kulijua jiji kwa kupitapita,Angel mwaka
mmoja wa kukaa Dar alikua ashaanza kubadilika tabia, mule ndani pakawa ni kituo
cha kulalia tu atokapo kuzurura kwenye jua kali pasipo sababu.
Urembo
aliokua nao ANGEL hakuna mwanaume atakayempita asigeuke nyuma kumuangalia
wanaume wakaanza kumjua na kumpigia misele ya kila namna ila kitu kilichovutia
kwa yule binti hakukurupuka kuparamia mpenzi.
Mwishoni
alijikuta anampenda kijana mtanashati na mwenye kazi nzuri ya afisa msaidizi wa
mawasiliano katika kampuni ya AIRTELL pia yule kijana aliona ni bahati ya kupata
msichana wa ndoto yake.
Kila mmoja alionesha hisia na upendo kwa mpenzi wake si ANGEL wala PATRIC mpenzie.
Kila mmoja alionesha hisia na upendo kwa mpenzi wake si ANGEL wala PATRIC mpenzie.
Upendo
wao ulimea katika kipindi cha miezi mitano maamuzi ya Angel kwenda kumtambulisha
Patrick kwa shangaze yake wakayafikia hawakuchelewa jambo lile Shangazi wa Angel
alilikubali bila kipingamizi
"Nafurahi
wanangu kuwa na maamuzi ya busara, kwani mngekua kimya nisingemjua mkwe wangu,
siwezi kataa uhusiano wenu najua mmependana na kufanana kabisa ilimradi Patrick
ufanye mpango wa haraka umuoe Angel" ni maneno aliyowaambia siku hiyo jambo
ambalo waliliweka kichwani kila mmoja akifikiria wataoana lini.
Haikuwa
changamoto kubwa katika mahusiano yao changamoto ilikua kwa Angel ambaye kwa
kipindi chote kile hakuwa na kazi ya kufanya zaidi ya vibarua vya hapa na pale
kama kuwafulia wahindi magagulo yao.
Siku
moja akiwa na Patrick aliamua kuongea kuhusu kazi ambayo itamletea faida kubwa
ili wajikimu katika maisha kama wakifunga ndoa
"Mpenzi,"
alita Angel akiwa kamshika mkono Patrick wakitembea katika fukwe za coco
beach.
"Niambie
mke wangu mtarajiwa" aliitikia Patrick kwa sauti ya mahaba na ya
upole.
"Maisha
ya kufanya kazi za vibarua yamenishinda miaka inaenda wala sioni faida yake"
alilaalmika Angel
"Mh
sasa tutafanyaje?"
"Tufanyaje,
naomba mtaji nifungue hata biashara"
"Angel
unajua biashara inahitaji moyo kuna kupata na kukosa faida na hasara,
kustahimili uvumilivu wake unaweza" aliluza Patric baada ya wazo alilitoa Angel
kumkaa kichwani
"Baby
najua, ndio maana nimekwambia nataka biashara"
"okay
unapenda kufanya biashara gani?"
alifikiri
angel kabla ya kujibu swali lile
"Biashara
nzuri ninayoina ni kuuza VIPODOZI" alijibu
"Vipodozi? hiyo ina kazi nzuri ya biashara?"
"Ndio mpenzi" Siku zote mwanaume huwa dhaifu kwa mwanamke Patrick hakuwa NA njia ya kukwepa swala lile.
"Vipodozi? hiyo ina kazi nzuri ya biashara?"
"Ndio mpenzi" Siku zote mwanaume huwa dhaifu kwa mwanamke Patrick hakuwa NA njia ya kukwepa swala lile.
"Sawa
nimekuelewa nitaenda kukopa bank nikifungulie duka la vipodozi katika soko la
Kariakoo" Angel aliposikia vile aliruka na kumkumbatia Patrick asiamini maneno
yake.
Baada
ya wiki kadhaa kupita jitihada za Patrick kukopa bank zikafanikiwa.
Hakutaka
kuupoza ule mkopo moja kwa moja aliacha kazi zake siku hiyo na kuanza kulisaka
soko la kariakoo kutafuta Frame nzuri ya biashara.
Siku
hiyo ilikua ni ya bahati kwake alikua frame iliyokua katikati ya soko lile mtu
anahama hiyo hiyo ndio aliioda akapangisha.
Baada ya kufanya vile alimfanyia Angel surprise ya kumuonesha akimwambia mzigo wa vipodozi ashaagiza baada ya siku kadhaa utatua bandarini.
Baada ya kufanya vile alimfanyia Angel surprise ya kumuonesha akimwambia mzigo wa vipodozi ashaagiza baada ya siku kadhaa utatua bandarini.
Furaha
aliyokua nayo Angel siku hiyo haikua ya kawaida akiona maisha yanaenda kuwa
mazuri. Jambo zuri atakalofanya angel hakusita kumtaarifu shangazi yake kwani
bado alikua anaishi kwake.Shangazi yake alimpa baraka tele hasa kwa Patrick
aliyejitolea kumsaidia.
Wiki
mbili baada ya Frame kupangishwa Angel alikua ndani ya duka likiwa limesheni
vipodozi vya aina mbali mbali hasa mafuta ya lotion ya kujipaka.
Kariakoo
kuna biashara ya namna zile nyingi na ushindani uliokua katika soko lile
yahitaji ujasiri.
Angel
alikua anauza bidhaa zake kwa kusua sua sana hakutegemea kama itakua vile yeye
alizani ukifungua duka basi siku hiyo hiyo bidhaa zote zitanunuliwa.
Miezi
kadhaa kupita faida aliyokua anapata kwa mwezi ni ndogo kuliko ukiangalia
wafanya biashara wenzake walileta bidhaa mpya kila mwezi yeye yapata miezi
mitatu vipodozi alivyoanza navyo ni vile vile.
"Mpenzi
hii biashara sikujua kama ni nzito hivi tangu nianze napata visenti vya kula na
kuvaa tu faida haionekani" ni siku moja akiwa kitandani alimuandikia Patrick
massage.
"Hee
mara hii ushaanza kulalamika?, biashara ndivyo ilivyo mwanzo mgumu lakini
ukizidi kumuomba mungu ipo siku utauza mamia kwa mamia, kumbuka bado mkopo
hatujaurejesha, usivunjike moyo mpenzi" yalikua ni majibu ya Patrick akijitahidi
kumfariji Angel.
Walichart
sana usiku ule kuhusu MAPENZI yao lakini Angel hakukublia kabisa kuona biashara
yake inaenda namna ile.
"Hapana
kesho lazima niende kwa Mwajuma, anieleze anafanya nini mpaka anauza vile"
Alongea kimoyo moyo Angel.
Mwajuma
alikua ni rafiki wa Angel hakupishana sana kiumri ila Mwajuma aliionesha ana
umri mkubwa isipokua mwili ndio uliomfanya alingane na Angel. Walikutana
kariiakoo nae akiwa ni mfanya biashara ila si ya vipodozi kama Angel.
Yeye
alimiliki maduka zaidi ya matatu ya nguo za kike na kiume akiwa anapata wateja
wengi na kuingiza faida kubwa. Urafiki wao ulianza siku moja Mwajuma alienda
kwenye duka la Angel kununua vipodozi wakajuana na angel ndipo alipoanzisha
urafiki.
Kesho
yake Angel alitoka nyumbani kwa shangazi yake akiwa na mawazo ya kumuona Mwajuma
aeleze kile anachotaka.
Baada
ya kufika dukani kwake alifungua nakusubiri mda uende ili amfate mwajuma kwani
biashara yake haikua mbali na kwake.
Lakini ilitokea kama Bahati siku hiyo Mwajuma alienda dukani kwa Angel.
Lakini ilitokea kama Bahati siku hiyo Mwajuma alienda dukani kwa Angel.
"Shoga
angu Yale mafuta si yamenishiia nimekuja kununua mengine" alijitamba mwajuma
aliyekua mzuri wastani mwili ulioja kwa kuridhika na hela, kavaa viatu vya
mchuchumio funguo ya gari kaitumbukiza katika kidole cha mwisho.
Angel
alipomuona alimchangamkia zaidi ya siku zote.
"eh! tena nilikua nampango wa kuja huko kwako shost" alidakia Angel
"Kuna nini tena shoga, au unahisi natembea na bwana ako?' mwajuma alikuabl ni mtu wa utani sana kwa Angel licha ya urafiki wao.
"eh! tena nilikua nampango wa kuja huko kwako shost" alidakia Angel
"Kuna nini tena shoga, au unahisi natembea na bwana ako?' mwajuma alikuabl ni mtu wa utani sana kwa Angel licha ya urafiki wao.
"Njoo
kwanza tukae nikueleze vizuri"
"mhh haya"walikubaliana wakaa kwenye viti pamoja.Angel hakujua aanzaje kumuuliza Mwajuma lakini mwishoni alipiga moyo konde.
"mhh haya"walikubaliana wakaa kwenye viti pamoja.Angel hakujua aanzaje kumuuliza Mwajuma lakini mwishoni alipiga moyo konde.
"Mwajuma
tumekua marafiki kwa mda mrefu, kwa hiyo asinifikirie vibaya" alianza kwa
kujihami Angel.
"usiogope Angel wewe endelea" Angel alikaa vizuri akashusha sauti yake chini.
"usiogope Angel wewe endelea" Angel alikaa vizuri akashusha sauti yake chini.
"Shost,
naona mwenzangu unauza kama unagawa bure yani wateja hawapungui dukani
mwako,lakini angalia Mimi tangu nianze wewe ndio mteja wangu mkubwa, nisubiri
mafuta yaishe ndio uje kununua,Kwa hiyo chonde chonde naomba siri ya uuzaji wako
kama kanisani niende au kama msikitini niingie nimuombe huyo mungu uliyemuomba
wewe" alipomaliza kusema vile Mwajua alicheka sana kiasi kwamba alinyanyua miguu
juu.Angel hakutegema kwamba Yale maneno yatamchekesha mwajuma, alijua labda ndio
atakamsirisha.
"Angel
ni hilo tu" aliuliza mwajua akipunguza kicheko.
"Ndio shosti hilo sio dogo"
"Ushamuomba mungu mara ngapi?" mwajuma alianza kumuuliza maswali
"Ndio shosti hilo sio dogo"
"Ushamuomba mungu mara ngapi?" mwajuma alianza kumuuliza maswali
"Mara
nyingi tu"
"umepata mafanikio gani toka umuombe?'
"Ndio kama haya kidogo kidogo" alinung'unika Angel
"Hivi una fikiri hakuna njia nyingine zaidi ya kumuomba mungu?'aliuliza mwajuma swali lilomtatiza Angel
"una maanisha nini kusema hivyo?"
"umepata mafanikio gani toka umuombe?'
"Ndio kama haya kidogo kidogo" alinung'unika Angel
"Hivi una fikiri hakuna njia nyingine zaidi ya kumuomba mungu?'aliuliza mwajuma swali lilomtatiza Angel
"una maanisha nini kusema hivyo?"
"usiwe
kama umekuja mjini Leo, usifikiri hapa kariakoo kila mtu anafanya biashara kwa
kumtegeme mungu, njoo nikupe siri ya mafanikio yangu" mwajuma alimvuta Angel
sikio nakulisogeza kwenye midomo yake.
"Siri
ni kwenda kwa mganga tu" Angel alichoropoka katika mdomo wa mwajuma kwa mstuko,
maishani mwake hakuwahi kwenda kwa mganga wala kuwaza vile.
"Kwa
mganga?' aliuliza kwa nguvu mpaka mwajuma alimziba mdomo.
"Shiiip
bibieee, isiwe nongwa habari ndio hiyo, kama unahitaji kuwa kama mimi hiyo ndio
siri yangu, na kwa uzuri nakupeleka mpaka kwake" alifoka Mwajuma. Swala lile
lilikua ngeni kwa Angel ataanzaje kwenda kwa mganga. Alibaki ameduwaa asijue
ajibu nini.
"Embu
nyanyuka unipe mafuta niende zangu, wewe endelea kujifikria ukizani mafanikio
yanakusubiri" alisema mwajuma akinyanyuka ndipo angel nae alinyanyuka na kwenda
kumtolea mwajuma mafuta yake.
"shost
bye,ukipata jibu usisite kuja kunieleza nipo wakati wowoate maana najua hapo
nimekuacha njia panda" Mwajua alikua ni mtu wa kuongea mpaka anaondoka licha ya
Angel kuwa kimya.
Siku
hiyo mchana iliisha akiwa anawaza maneno ya mwajuma kwenda kwa mganga.
Ilipofika
usiku akiwa kwa shangazi yake alitamani kumwambia lakini alisita.
Alichukua
simu ili amueleze Patrick habari zile nayo ikawa vile vile moyo
ulisita.
Kazi
ikawa kwake yeye na nafsi zake kujibizana kwenda au kutokwenda usiku kucha
akijigalaza kitandani asioate jibu mpaka usingizi ulipomchukua.
Siku
iliyofata akiwa dukani kwake nafsi ya kukubali kwenda ikashinda hakutaka
kusubiri alimtafuta mwajuma dukani mwake na kumueleza kuhusu nae ampeleke kwa
huyo mganga.
Mwajuma
hakuwa na hila alikubali na kumueleza asichelewe hiyo safari waende kesho yake
wazo ambalo Angel aliliafiki.
Bila
ya Patrick wala shangazi yake kujua asubuhi ya kesho yake aliamka saa kumi na
moja akimdanganya Shangazi yake anaenda kuchukua mzigo wa dukani huku Patrick
asijue.
Walikubalina
na mwajuma kukutaa moroco kwani yule mganga anaishi Tegeta na mwajuma yeye
anaishi Kinondoni.
Sehemu
waliyoahidiana walikutana na safari ya kweda kwa mganga ikaanza wakitumia gari
ya Mwajuma.
Kwa
mganga walipofika Angel akielekezwa na mwajuma alieleza shida yake mganga bila
kujali alimkabidhi dawa ya kuvutia wateja lakini kwa mashart makuu
matatu.
"Kwanza
Akishaisindika ile dawa dukani mwake siku zinazofata akifungua duka muda wa
kufunga uwe saa moja usiku na atakapofunga asirudi nyuma kulifungua.
Sharti
la pili hela atakazopata asizipeleke Bank wala kwenye taasisi yoyote ya
kuhifadhi hela ajeengee kabati ndani ya hilo duka ahifadh huko
Tatu asifungue duka lingine atumie hilo hilo moja ndani ya miaka miwili, akitaka kuajiri ajiri lakini sio nje ya hilo duka."
Tatu asifungue duka lingine atumie hilo hilo moja ndani ya miaka miwili, akitaka kuajiri ajiri lakini sio nje ya hilo duka."
Angel
alikubali yale mashart bila kipingamizi wakarudi safari yao ile dawa iliyotakiwa
aizindike ndani ya duka SAA moja usiku wa siku hiyo.
Angel
mchana wa siku hiyo hakuwa ametulia akihangaika mda ukimbie aiweke ile dawa.
Mpaka SAA moja ilipofika alikua ashatembea vya kutosha mule dukani.
Wiki
moja baada ya kuweka dawa hali ya duka la angel ikabadilika ghafla wateja
wakaanza kumiminika makumi kwa makumi akiuza zaidi laki tano kwa siku angali
mwanzoni alikua anauza hata elfu hamsini haifiki.
Mafanikio
yake hakuacha kumueleza Patrick hasa alipotaka aagiziwe mzigo Mara mbili pale
dukani kwani vitu vinaenda isivyo kawaida.
Patriki
akiwa hajui kilichotendeka alimshukuru muumba wake akimwambia Angel ni mungu
alisikia kilio chao hivyo hawana budi kumshukuru lakini si kwa angel aliyetumia
ushirikina.
Ikapita
mwezi, miezi sasa Angel akawa ni maarufu kariakoo nzima kwa biashara ile,
Patricki akijisifu kupata mpenzi mchapakazi lakini kitu kilichomtatiza ni kuwa
alipomuuliza Angel anaweka hela bank gani alionekana akikwepeshaa maswali
Yale.
Kitendo
cha Patrick kuanza kumuuliza maswali Angel kikamfanya Angel aone kwamba Patrick
anataka kumuingilia katika biashara yake akaanza kupunguza upendo taratibu zile
SMS walizokua wanachart usiku zilififia kama kibatari kilichokosa
mafutà.
Patrick alipompigia au kutuma SMS mchana alijibiwa
"Samahani mpenzi, niko bize na wateja" akimpigia usiku au kutuma SMS navyo alijibiwa
"Samahani mpenz nimechoka sana nahitaji kulala" kitendo ambacho Patrick kilimkasirisha na kuona siku moja amuendeee huko huko dukani na ni afadhali asingeenda kwani alikuta wateja wanatoka na kuingia akisubiri amalize huyu anakuja mwingine mwishoni alikata shauri.
Patrick alipompigia au kutuma SMS mchana alijibiwa
"Samahani mpenzi, niko bize na wateja" akimpigia usiku au kutuma SMS navyo alijibiwa
"Samahani mpenz nimechoka sana nahitaji kulala" kitendo ambacho Patrick kilimkasirisha na kuona siku moja amuendeee huko huko dukani na ni afadhali asingeenda kwani alikuta wateja wanatoka na kuingia akisubiri amalize huyu anakuja mwingine mwishoni alikata shauri.
"Angel
kwanini usifunge duka tuongee maana siku hizi ata weekend hautaki kupumzika
mpenz"
"Hivi Patrick una akili? yani Mimi niache hela nikusikilize wewe utanipa nini zaidi ya kugombana, naomba ondoka nitakutafuta kwa mda wangu, ukiwa wewe hapa unaleta gundu wateja hawaji" maneno ya siku hiyo yalikupasua ngoma za Patrick asiamini yule angel alimuomba mkopo wa mtaji ata badilika vile hata kabla nusu ya mkopo haujarudishwa.
"Hivi Patrick una akili? yani Mimi niache hela nikusikilize wewe utanipa nini zaidi ya kugombana, naomba ondoka nitakutafuta kwa mda wangu, ukiwa wewe hapa unaleta gundu wateja hawaji" maneno ya siku hiyo yalikupasua ngoma za Patrick asiamini yule angel alimuomba mkopo wa mtaji ata badilika vile hata kabla nusu ya mkopo haujarudishwa.
Alijaribu
kila namna akiona ni utani mwishoni Angel alitaka kupigia simu polisi ndipo
Patrick aliondoka kwa machungu sana.
Hela
zikamjaza kiburi Angel hakukumbuka wazazi wake alitumia hela zike kuruka viwanja
na mwajuma pamoja namatajiri wa kike.
Swala lile Patrick alilipeleka kwa shangazi yake Angel na kumueleza jinsi angel alivyobadilika.
Swala lile Patrick alilipeleka kwa shangazi yake Angel na kumueleza jinsi angel alivyobadilika.
"Pole
sana mwanangu at a Mimi naona Angel alivyobadilika kwani siku hizi anakuja usiku
wa manane kalewa nikuuumuliza ananitukana sijui kapatwa na nini"
Walimjadili
sana wakamkalisha Angel chini na kumuleza lakini jeuri ya pesa akawapuuzia
alipomuona Shangazi yake anamzingua aliondoka kwa shangazai yake bila kuaga
akiwa na kila kitu chake kwa kiburi alienda kununua nyumba kubwa ya mamilioni
huko Masaki mwisho akanunua na gari Kali ya kutembelea kwa duka lile lile
moja.
*****
Yapata
mwaka NA NUSU sasa Angel hana mawasiliano ya shangazi yake wala Patrick wazazi
wake nyumbani shinyanga wanalilia shida Ila yeye alijivinjari akiwa na haja
humtafuta mwanaume yeyote anayempenda nakutoa haja yake.
Duka
limesheheni vipodozi mpaka vingine vikawa vinatolewa nje nakuingizwa
aliajirivwafanyakazi wawili ambao aliwalipa mshahara mzuri.
Hakuna
anayejua siku ya ajali yake,
Ilikua siku ya jumanne Angel akiwa katika duka lake baada ya wafanyakazi wake kuondoka alikua anahesabu hela za siku hiyo ili aweke kwenye gala lake lilikua mule ndani.
Ilikua siku ya jumanne Angel akiwa katika duka lake baada ya wafanyakazi wake kuondoka alikua anahesabu hela za siku hiyo ili aweke kwenye gala lake lilikua mule ndani.
Alifanya
haraka haraka kwani ilikua yapata saa mbili kasoro na ilitakiwa duka lifungwe
saa moja.
Alipomaliza
kuhesabu alizihifadhi sehemu anayoijua yeye kisha akatoka nje haraka na kufunga
duka.
Aliliendea
gari yake iliyopaki pembeni akataka atoe funguo afungue mlango alipopapasa
kwenye mkoba hakukuwa na ufunguo wa gari zaidi ya zile za duka alizoshika
mkononi
Alijipiga sachi kila sehemu akiangalia nyuma kama kadondosha lakini haukuwepo mwishoni alikumbuka kaufungia ndani ya duka.
Alijipiga sachi kila sehemu akiangalia nyuma kama kadondosha lakini haukuwepo mwishoni alikumbuka kaufungia ndani ya duka.
Alirudi
tena dukani akiwa na funguo za duka akaanza kufungua duka akisahau mashart
mengine ya mganga.
Alifanikiwa
kufungua lakini alipokuja kunyanyua macho kutazama mule dukani la hasha
hakuamini macho yake.
Alikutana
na watu wa kutisha wamejaa mule dukani kama wateja. wale watu walifanan na
misukukule, wakishika vile vipodozi vya mule dukani na kuvifanyia mauza uza kama
wengine walivipakza vinyesi, wengine walipakaza makamasi.
Idadi
ya wale misikule haikuhesabika kila mmoja akishika kitu chake na kuvifanyia vitu
vya ajabu.
Angel
hakustahimili tukio lile alijikuta anadondonda chini na kupoteza
fahamu.
Alikuja
kuamka yuko kwenye kitanda cha hospatli alijaribu kujinyanyua lakini alishindwa
akajaribu kuongea nayo akashindwa machoni mwake akamuona mwanamke kasimama na
bakuli kumtazama vizuri alikua ni shangazi yake aliyemkimbia kipindi
kirefu.
Shangazi yake bado alimpenda alipata taarifa za angel kudondoka alienda hosptali aliyolazwa muhimbili.
Shangazi yake bado alimpenda alipata taarifa za angel kudondoka alienda hosptali aliyolazwa muhimbili.
Madaktari
walimuambia Shangazi yake kuwa Angel kapatwa na stroke, iliyomfanya mwili mzima
usifanye kazi yani yeye ni wa kugeuzwa, kutolewa kinyesi na anajisaidia hapo
hapo kitandani.
Hiyo
haikutosha walisema uwezo wake wa kusikia na kuongea itachukua mda mrefu na pia
matibabu zaidi yanahitajika aende nchi za nje.
Shangazi
yake hana hela wala nini akaanza kufanya mpango wa kitafuta hela lakini duka
lake siku ile alipodondoka liliungua lote ghafla,:moto ulisambaa na kufikia
mpaka gari yake ikalipuka, kila kitu kilichokua ndani ya duka au gari kiliteketa
kwa moto.
Alichunguza
marafiki wa Angel akawafata kuwaomba msaada lakini walidai hawana hela wala pia
hawakuonekana hosptali kumtembelea Angel si mwajuma wala nani.
Suluhisho
la mwisho lilibaki ni kuuza nyumba ya Angel baada ya shangazi, ndugu na wazazi
wa Angel kuafikikiana walikubali kuiuza jela zilizopatikana ndio zikampeleka
Angel India kutibiwa.
Licha
ya kupelekwa India Angel alirudi Tanzania akiwa anasikia kwa umbali na kuonge
kidogo, akawa kilema wakutembea na baiskeli.
"Shanga.....zi,
Patrick yuko wap" aliuliza siku moja akiwa anasukumwa na baiskeli na shangazi
yake wakimsafirisha kwenda Shinyanga kijijini kwani maisha ya mjini katika hali
ile ni magumu hasa mtu wa muangalia
"Patrick,
bado unamkumbuka?
sasa
hivi anaozea jela mwenzako, zile hela alizokopa alishindwa kurejesha akafungwa"
Angel aliposikia hivyo akiwa anashusha maudenda kama tahira alianza kulia kwa
kumkumbuka Patrick wake.
Alijuta
kwenda kwa mganga ule urembo wake ulipotea akawa na ngozi iliyokakamaa kama mzee
angali ndio alikua ana umri wa miaka ishirini na tano tu.
Iligundulika
kuwa wateja waliokua wanaenda kununua vipodozi kwake walikua wanatolewa kafara
kwa mwezi watano na akitolewa kafara anaekwa msukule ndani ya lile duka bila ya
wateja wala Angel kujua.
Angel
alijutia na kunung'unika moyoni
"KUMBE NILIFANYA BIASHARA NA MISIKULE" Kutoka kwenye ufahari leo hii anatembelea kibaiskeli, kwa kusukumwa, chakula analishwa, kuoga n vitu vyote anafanyiwa hana uwezo wa mwingine.
"KUMBE NILIFANYA BIASHARA NA MISIKULE" Kutoka kwenye ufahari leo hii anatembelea kibaiskeli, kwa kusukumwa, chakula analishwa, kuoga n vitu vyote anafanyiwa hana uwezo wa mwingine.
Wale
ndugu aliowatupa ndio wanamsaidia shughuli zote zile. Marafiki aliokua nao
anaruka viwanja, gari ya kifahari ama ile nyumba vyote vilipotea kama
upepo.
*****MTAKA SABA NYINGI KWA PUPA,HUPATA MINGI MISIBA********mwisho****
*****MTAKA SABA NYINGI KWA PUPA,HUPATA MINGI MISIBA********mwisho****
UJUMBE:
Ni heri mtaji wa elfu kumi unaokuzailishia elfu hamsini ya faida kwa mwezi ya
HALALI, kuliko
Mtaji wa elfu kumi unaokuzalishi faida yamilioni kumi kwa wiki kwa HARAMU.
Mtaji wa elfu kumi unaokuzalishi faida yamilioni kumi kwa wiki kwa HARAMU.
Usiharakie
Maisha kama rizki ipo ipo tu japo itacheleweshwa lakini MTUMAINIE MUNGU WAKO.
usimtegeme mwanadamu mwenzako.
0 comments:
Post a Comment