Basi leo asubuhi nimemuona mrembo mzuri masikini hata hawezi
kugombania gari, nikaona hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko!
Nikapanda fasta nikawahi siti ya watu wawili halafu nikakaa
katikati ili akija nimpishe, dah! Si likatokea libabu moja limevaa miwani kubwaa
kama ya kukatia vitunguu likakaa! Duh linanuka tu sigara, Yule Mrembo akasimama,
limoyo likauma kweli!,
Daladala ilipofika Makumbusho nikaona lile Babu linashuka,
aisee kama zali na Mrembo akakaa! Jaman Bahati iliyoje!!
Nikalianzisha:
MIMI : Mambo Mrembo.
MREMBO : poa,
MIMI : Karibu Karanga (nikatoa viujugu vya kuzugia)
MREMBO: silagi huo Uchafu, labda Pop Corn na Clips.
MIMI: Ok naitwa Shidondofila Pangalashaba,
mwenzangu?
MREMBO: He he heee! Jina kama dawa!, mi naitwa Princess
Rihanna!
Wakati naendelea kupata majibu Machungu ghafla Nikaona Gari
imefika Namanga, kwa kweli kama huyu mrembo angekuwa anatoa majibu ya kuridhisha
ningeenda kushuka nae popote nikamwambia konda "Shusha Namanga" ,
sasa wakati nashuka nikashangaa kumbe na yeye anashuka hapo
hapo!
MIMI : haa kumbe na wewe unashuka hapa?
YEYE : so what?
MIMI : ok umekataa karanga zangu, basi twende hapo kwa Mama
ntilie tukagonge chai, andazi maharage,
YEYE : khaa! Unikome, mimi huwa natumia vitu kama Burger,
Kuku, sausages, Pizza, Egg Chops na Chipsi Mayai, yaani Uzuri Wangu woote
unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,
Dah Mrembo akasepa zake, nikaona hakuna Noma nikaagiza zangu
Maharage ya 200, maandazi mawili 200 na Chai ya 100, nikaacha kajero hapo
nikasepa.
Nimefika Kwa Shangazi akafurahi kweli kuniona.
SHANGAZI: mwanangu Shidondofila Karibu Baba!
MIMI: asante Shangazi
SHANGAZI: yule mwanangu wa mwisho unamkumbuka?
MIMI: Si yule Kipandauso?
SHANGAZI: huyo huyo!
MIMI : namjua vizuri, wakati anakuwa namuona, hata nepi
nimembadili, teh teh! yupo wapi siku hizi?
SHANGAZI : amekuwa mkubwa kweli, anasoma Hapo Chuo Cha Kodi
TRA pale karibu na ITV, ila yupo aliendae Chuo akahisi homa kaona arudi, ngoja
nimuite:
Kipandausooooo!!!
KIPANDAUSO: beeee Mama!
SHANGAZI : Njoo mwanangu, kuna Mgeni!
Hamad! Ndipo Macho yangu yakakutana na Yule Mrembo wa Kwenye
daladala, kavaa vitenge vya zamani vya Shangazi, hana Wigi tena, muda huu komwe
la ukoo linaonekana, komwe la babu yetu!
mrembo kashika sahani ya Maboga na kikombe cha uji wa
Mchele!,
Aliponiona Almanusura azimie!!!,
huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa Mwisho wa Mjomba Dindoyogo!,
ukipenda Muite Kipandauso Dindoyogo!
SHANGAZI : Njoo na Maboga ya kutosha na kikombe kingine cha
uji uje unywe na Kaka yako!
Dah! akarudi ndani kinoma noma kainamisha sura chini, mi
nikawa najiuliza wapi Pizza? Wapi Burger? Wapi Sausage?, anyway bado nipo hapa
kwa Shangazi mpaka kesho Nitalala huku....Usimdharau Mtu yeyote Ktk dunia
hii...
Mungu anakuona We kipandauso
MWISHO
0 comments:
Post a Comment