Search This Blog

Wednesday, December 21, 2022

JINSI YA KUIPATA FURAHA

 





    SIMULIZI FUPI SANA: JINSI YA KUIPATA FURAHA



    Kundi la takribani watu hamsini, wanaume kwa wanawake walihudhuria semina ya mambo ya kijamii.

    Lakini baada ya kufika katika hiyo semina mtangazaji mwenyekitii akaifungua hiyo semina kwa zoezi dogo.

    Akakusanya mapulizo (balloons) hamsini, akamkabidhi kila mmoja la kwake kisha akawapatia kalamu (marker pen) zinazofanana wino na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake katika pulizo lake.

    Baada ya kila mmoja kuandika, mapulizo yale yakakusanywa na kuwekwa katika chumba kimoja kikubwa.

    Kisha mtangazaji akawaambia ndani ya dakika tano kila mmoja awe amepata pulizo lenye jina lake.

    Watu waligongana, wakakanyagana, kila mmoja akilalamika kivyake akishika hili na kuliacha akienda huku na kule bila mafanikio. Hakuwepo wa kumuuliza maana kila mmoja alijikita katika kutafuta la kwake!!

    Baada ya dakika tano hakuna hata mmoja aliyekuwa amepata pulizo lenye jina lake.

    MWENYEKITI akabadilisha zoezi, akasema kila mmoja achukue pulizo lolote kisha amtafute mwenye jina hilo na kumpatia pulizo lake.

    NDANI ya dakika tano kila mmoja alikuwa ameletewa pulizo lake na yeye alikuwa amepeleka lisilokuwa lake kwa mwenye jina husika. Kila mmoja akafurahi na kuridhika.

    HAYA YANATOKEA katika maisha yetu… kila mmoja amejikita katika kuitafuta furaha yake na kamwe asiipate kisha anabaki kunung’unika.

    IPO HIVI!! FURAHA yetu imeegemea katika furaha za watu wengine.

    WAPE WATU FURAHA WANAYOHITAJI NA WAO WATAKUPA FURAHA YAKO!!

    **Barikiwa sana siku ya leo ewe mdau huku ukiamini kuwa huwezi kujitafutia furaha yako iwapo wewe unawanyima wengine furaha yao!!!

UWE SAUTI YAO

 





    Kengele ya kutoka darasani iligongwa, wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza kutoka madarasani huku wakifukuzana wengine wakipiga kelele ilimradi shwangwe tu.

    Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufundisha shule za hatua hiyo. Ilikuwa ni shule ya serikali. Jicho langu liliangukia katika sura ya msichana mdogo, nguo zake chafu. Alikuwa analia. Alikuwa peke yake na hakuwa na yeyote wa kumbembeleza. Mimi kama mwalimu sikutaka kujisogeza karibu naye sana. Kwanza nilikuwa mgeni. Nikaachana naye.

    Siku iliyofuata tukio kama lile likajirudia. Msichana yuleyule wakati ule uleule wa kutawanyika, alikuwa analia sana. Mwishowe aliondoka huku akiwa analia. “Mbona mwenzenu analia?” nilimuuliza mwanafunzi mmoja.

    “Huyo ni mama kulialia..” alinijibu huku anacheka.......

    Haikuniingia akilini hata kidogo kuwa yule binti analia bila sababu. Siku ya tatu nikaanza kujiweka karibu naye. Muda wa mapumziko nilimwita nikamnunulia chai, alikuwa ananiogopa na hakutaka kuniangalia machoni. Sikumuuliza lolote juu ya tabia yake ya kulia lia kila anaporuhusiwa kurejea nyumbani. Hata siku hiyo pia alilia vilevile. Wenzake wakawa wanamzomea. Akili yangu iligoma kuamini kuwa binti yule analia bila sababu.

    Kwanini alie wakati wa kutawanyika tu?? Hapana si bure. Nikaendelea kujiweka karibu naye. Mkuu wa shule akafikishiwa taarifa kuwa nina mahusiano ya kimapenzi na yule mtoto.

    Moyo wangu na Mungu pekee ndio walikuwa mashahidi. Nilikosa cha kujibu. Nilijaribu kujiweka mbali naye lakini moyo ulinambia kuwa kuna jambo natakiwa kulijua. Nikaendelea kuwa karibu naye. Hatimaye mkuu wa shule akanisimamisha kufundisha pale kwa tabia yangu ya kufanya mapenzi na mwanafunzi. Nilijitetea lakini sikueleweka. Nikamwachia Mungu……

    Licha ya kusimamishwa kazi, niliendelea kufuatilia nyendo za yule binti aliyeitwa Janeth. Kila alipotoka shule nilimvizia njiani na kumnunulia chakula, kisha tunazungumza kidogo. Aliponiamini kama kaka yake ndipo nikajieleza dukuduku langu.

    “Janeth…” nilimuita.

    “Bee kaka ….” Aliitika huku akinitazama.

    “Nyumbani unaishi na wazazi.”

    “Ndio naishi na mama..baba huwa anasafiri safari.”

    “Mama yako ana watoto wangapi?”

    “Mama yangu alikufa….alikufa nikiwa mdogo hata simkumbuki” Alijibu kwa sauti ya chini.

    “Kwa hiyo unaishi na mama mdogo.”

    “Ndio.”

    “Unampenda mama mdogo?”

    Swali hili likaikatisha furaha ya Janeth. Akaanza kulia, alilia bila kukoma, Janeth alilia kwa uchungu hadi nikajisikia vibaya. Nilimbembeleza kisha sikumuuliza tena. Siku zikaenda bila kumuuliza chochote..

    Baada ya siku kumi, ilikuwa siku ya michezo pale shuleni, hivyo hapakuwa na masomo. Janeth alichelewa kuja shule, nilimngoja uwanjani, hadi alipofika majira ya saa nne. Nikamwambia twende kunywa chai. Siku hiyo nilimpeleka mbali kidogo, tukanywa chai, kisha tukakaa mahali palipokuwa wazi.

    Nikaleta tena mjadala mezani. Ni kuhusu maisha ya Janeth. Alikataa kabisa kusema lolote, nilimshawishi sana.

    “Usiogope mimi ni kaka yako.” Nilimpooza. Janeth badala ya kusimulia akaanza kulia tena.

    “Ataniua mama nikisemaaaa” alilalamika. Nikambembeleza hatimaye akanieleza jinsi anavyonyanyaswa na mama yake. “Mama hanipendi hata kidogo, ananipiga na kuninyima chakula, hapendi nije shule, vyombo tunavyotumia usiku hataki nivioshe usiku na hataki niwahi kuamka asubuhi, nikiamka natakiwa kufanya kazi zote, kufagia uwanja, kudeki nyumba, kuosha vyombo kisha ndipo nije shule. Baba akiwepo anajidai kunijali sana…” Alijieleza.

    “Ni hayo tu Janeth….niambie kila kitu.”

    “Akijua ananiua alisema….”

    “Kwani amewahi kukutesa vipi..”

    Ni hapa Janeth alivyozungumza huku analia kilio ambacho hakitatoka masikioni mwangu kamwe.

    Siku moja, alichelewa kuamka, ilikuwa siku ya mapumziko. Mama yake alipomwamsha, aliitika na kupitiwa usingizi tena bila kutegemea.

    Mama aliporejea mara ya pili, alikuwa na mti mkavu, alimpiga nao kichwani na popote pale katika mwili bila kujali ni maumivu kiasi gani anayapata mtoto yule, alipoona hiyo haitoshi akamvua nguo kwa kuzichanachana,kisha bila huruma akausokomeza katika sehemu za siri ukuni ule, aliuingiza hovyohovyo, ukuni huo ulikuwa wa moto.

    Yeyote mwenye moyo wa nyama ajifikirie ukuni wa moto ukazamishwa sehemu za siri za mtoto wa darasa la sita. Ama hata isiwe mtoto wa darasa la sita, iwe kwa mwanadamu yeyote yule.

    Nilitokwa machozi.

    Nikawahi kujifuta hakuona.

    “Baba yeye alisemaje….” Nilimuuliza kwa upole.

    “Baba ni mkali na hapendi kunisikiliza na mama aliniambia nikiambia mtu ananiua mara moja.” Alijibu kwa huzuni kubwa huku machozi yakimtoka.

    “Nikija na dada yangu tunaweza kukuona ulivyounguzwa..”

    “Ndio…” alinijibu huku akitikisa kichwa.

    Sikutaka kulaza damu nikampigia simu rafiki yangu wa kike.

    Nikamuuliza kama yupo kwake, alikuwepo.

    Nikaongozana na Janeth.

    Tukafika, Janeth akatoa nguo zote.

    Ilihitaji moyo wa kijasiri sana kutazama mwili wa Janeth mara mbilimbili.

    Alitisha, hakika alikuwa ameunguzwa vibaya na vidonda vilikuwa havijapona vizuri.

    Vingepona vipi wakati hakuwa akipata tiba yoyote…

    Dada yule alishindwa kujizuia alimlazimisha Janeth twende kwa mama yake amkabiri na kumpa kipigo. Nikamzuia.

    Hata mimi nilikuwa na hasira kali. Lakini sikutaka kuiruhusu ifanye kazi.

    Nikachukua kamera, nikampiga picha Janeth katika yale makovu makubwa na mabichi

    Mbio mbio nikaenda polisi, kituo cha haki za watoto nikaelezea mkasa ule huku nikishindwa kujizuia machozi.

    Nikawaonyesha na picha.

    Tukaongozana nao hadi nyumbani kwao Janeth.

    Mama yule akakamatwa bila kutarajia.

    Nilitamani kumrukia nimng’ate lakini haikuruhusiwa.

    Sheria ikafuata mkondo. Janeth akaanza kupokea tiba rasmi baada ya kila kitu kuwa wazi.

    Yule mama akahukumiwa kwenda jela miaka tisa..hadi wakati huu ninaposimulia kisa hiki cha kusikitisha bado anasota jela.

    Mume wake alitozwa faini kubwa kwa kosa la kutofuatilia maendeleo ya mtoto wake kiafya……..ilikuwa bahati ya mtende sana kwake kunusurika na jela

    Mimi nilirudishwa kazini, kwa heshima kubwa. Heshima ya kumkomboa mtoto.
    JIFUNZE! Akina JANETH wengi wapo mtaani kwako…..usiwaangalie na kuwaacha tu…hebu jaribu KUWA SAUTI YAO….hawawezi kusema…hebu sema badala yao…….wanalia kisikie kilio chao……. Usipokuwa sauti yao watateseka milele na chozi lao litakuwa juu yako wewe usiyejali watoto wa wenzako kwa kuamini kuwa mtoto wa mwenzio si mtoto wako!!
    MWISHO

CHOZI LA MILELE.

 





    Binadamu unapozaliwa tu uhai wako na amani yako huishi kwenye mikono ya mama alie kuzaa japo mungu anakuwa ndio mlizi mkuu wa maisha yako.



    Mama anapo amua kukufupishia uhai wako anaweza kutimiza kwa dakika chache haijalishi kwa kukupa sumu au kuziba pumzi kwa muda mrefu hii itategemea ni jinsi gani amekusudia kukufupishia uhai .



    Wasichana wengi huchukua jukumu la kuharibu na kuzitoa mimba zao zinapokuwa changa kwa msukumo wa mazingira yaliyo mpelekea kupata mimba ile ama kwa sababu ya ugumu wa maisha na mazingira magumu anayo ishi,.

    Wasichana wengine huenda mbali na kufanya maamuzi magumu pale anapo ilea mimba miezi tisa na kujifungua salama baada ya hapo humtupa mtoto na kumuacha katika mazingira hatarishi nae anaondoka na kutokomea, hufumba macho na kuyasahau mateso ya kutunza mimba ndani ya miezi tisa na yale machungu ya kujifungua .



    Sijui ni ujasiri gani wanao utumia akina mama au ni roho mbaya kiasi gani wanayo kuwa nayo wakati ule wanapo watupa watoto walio wazaa wenyewe tena kwa uchungu....na sikitika sana kwani hata mama yangu alinitupa nikiwa mtoto mdogo mchanga akiniacha mazingira hatarishi .



    Mungu msamehe mama yangu na wanawake wote wanao toa mimba na kuwatupa watoto....

    Mimi ni Baraka matata. mwandishi na mtunzi wa simulizi hii ni ndugu Iddi Siraji  na imehaririwa na Lizbertha Maseke.



    sasa isome na ujifunze.



    Jina la baraka nilipewa na yule mama mgumba baada ya kuniokota nikiwa mtoto mchanga na kunifanya kuwa mwanawe mpendwa wa pekee na kwa hakika alinipa upendo ambao ulipindukia na alinipa malezi ambayo yalistahiki kwa kila mtoto japo alikuwa na maisha duni akijishughulisha na kilimo akiwa na mumewe mzee matata.



    Yalikuwa ni maisha duni ya kutegemea kilimo cha mkono lakini baba na mama yule walijitahidi kunisomesha kwa kidogo kilicho patikana huku nami nikifanya bidii kwenye masoma na kuwasaidia kilimo kila nilipo rudi kutoka shule,.



    Siku zote mama alinihimiza nisome kwa bidii kwani elimu ni urithi wa milele.



    "Mwanangu nipo tayari kuuza hata mashamba ili mradi tu usome na ufike mbali...unadhani nisipo kupa elimu utapata urithi gani wa thamani pindi nikifumba macho" aliongea kwa kunisisitizia na kunifanya niwe makini sana ninapo kuwa darasani.



    Mbali na kuwa saidia kulima wazazi wangu nilikuwa nina bustani zangu za mboga ambazo kila jumapili nilienda kuuza sokoni na kujipatia pesa ndogo zilizo niwezesha kununua vifaa vya shule na mafuta ya taa ya kibatali changu cha  kusomea usiku.



    Hatimae juhudi zangu zilizaa matunda ni pale tu nilipo faulu kwa kishindo kutoka la saba kwenda kidato nilikuwa mwanafunzi wa  pili kati ya wanafunzi sita wa kwanza akiwa ni mtoto wa kike wa mwalimu mkuu wa shule ile ilio kuwa chini ki elimu na uhaba wa walimu.



    Mama na baba mzee matata walifurahi kupita kiasi nina uhakika furaha yao ilizidi ya kwangu, waliuza mazao yaliyo patikana msimu ule kisha pesa iliyo patikana walininunulia vifaa vya shule na kunilipia ada ya shule kwani kipindi hicho cha mwaka 2005 elimu haikuwa bure kama sasa.



    Hatimae siku zilifika nikajiunga na wenzangu katika shule ile ya sekondary....Bado mama alinisisitizia kuhusu swala la kujituma katika elimu huku safari hii akinisihi sana nijiepushe na makundi ya vijana wasio na maadili , nami nilizingatia hayo, siku zika songa nikijituma kwenye masomo pamoja na kazi za nyumbani.



    ***--**



    Kama ilivyotokea mwaka 2005 basi ndivyo ilivyo jirudia mnamo 2009 kwani kwa mara nyingine nilifanikiwa kuziweka ndoto zangu mahala pazuri kwa kufaulu kutoka kidato cha nne kwenda cha tano.



    Safari hii furaha yangu haikudumu sana kwani iliyayuka baada ya kujua kwamba kulikuwa na uwezekano wa kutoendelea na masomo kwa sababu ya ada kubwa na shule niliyopangiwa ilikuwa mbali sana.

    Wazazi wangu wapendwa hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama zile, nilijikuta nikikata tamaa machozi yakinitoka kila siku zilivyo karibia za kujiunga na kidato cha tano.



    Siku moja baba aliniletea karatasi kadhaa na kuniambia ni chukue kalamu kisha nijaze ma swali ya form ile kisha niambatanishe na cheti changu cha kidato cha nne,

    nami nilifanya vile nikajaza karatasi ile ilio sheheni maswali yalio nihusu mimi na elimu yangu , baada ya kufanya hivyo baba aliichukua barua ile na cheti changu na kuuondoka navyo bila kuniambia anapeleka wapi hii ni kawaida yake mzee matata huwa haweki mipango yake wazi hivyo sikutaka kujisumbua kumuuliza.



    Baada ya siku sita tangu nijaze barua ile tulipokea ugeni wa watu ambao hakika walitoka serekalini tukawakaribisha,

    "naona mmekuja mabwana...kijana mwenyewe ndio huyu" mzee matata aliongea baada ya kusalimiana na watu wale huku akinielekezea kidole mimi.

    watu wale waliniuliza maswali kadhaa yenye misingi ya elimu wakijenga maada ya juu ya masomo ambayo huwa naya fanya vyema .



    Nami niliwajibu kadri nilivyo weza.

    walipo ridhishwa  walitazamana na kuafiki

    "Ok mzee matata mwanao atajiunga  kwenye hiyo shule kwa msaada wa kitengo chetu hivyo aanze maandalizi" aliongea mmoja wa watu hao na hapo nilishindwa kuivumilia ile furaha iliyo ripuka ghafla kwenye moyo wangu.



    Mzee matata alikuwa amefanya jitahada kubwa sana kwa kwenda kuomba msaada wa mimi kusomeshwa na alifanikiwa watu wale niliohisi wa serekalini walimkubalia nami nilitakiwa nikajiunge na wenzangu kwenye ile high school tena nilitakiwa nikaishi bweni.



    Huo ndio ulikuwa msaada mwisho wa mzee matata!! msaada katika mafanikio yangu kwani nikiwa nipo shule miezi tisa tangu niondoke nyumbani nililetewa taarifa mbaya yenye kuumiza moyo wangu mzee matata alikuwa kapata ajali ya kugongwa na gari ! maskini mzee matata aliaga dunia na kumuacha mama mjane huku akiniachia kilio cha aina yake.



    Nililia sana baada ya kupokea habari ile  na uongozi wa shule ukanifanyia msaada wa usafiri wa haraka ili niwahi mazishi.



    Hayati mzee matata tulimzika katika hali ya udhuni iliopindukia huku akimuachia mama kilio kisicho bembelezeka.



    Baada ya kumzika baba yangu mpendwa sasa macho yangu yalimuangalia mama yangu mpendwa ambaye nae hali yake kiafya haikuwa nzuri alikuwa kanyongea sana tena alidhohofika, hali ile ilinifanya nisitamami kurudi shule nikae kumuuguza mama yangu mpendwa, lakini mama alilipinga hilo na kuniamuru nirudi shule niendelee na masomo huku akidai udhoofu ule alionao ni sehemu ya ukiwa wa kufiwa na sio ugonjwa



    Maskini mama kipenzi alipenda sana nisome kuliko kitu kingine , sikuwa na pingamizi kwani mitihani ilikuwa imekaribia ikanilazimu nirudi shule na kumuacha mama akilelewa na wanakijiji.



    Wakati nikiendelea na mitihani shuleni nililetewa taarifa kuwa hali ya mama sio nzuri amelazwa hosptal hii ikanilazimu kumalizia mitihani haraka kisha nikarudi kijijini kwenye hospital aliyo lazwa mama.



    Hali ya mama haikuwa nzuri hata kidogo alikuwa taabani akisumbuliwa na maradhi ya moyo bila shaka  ni kutokana na kifo cha baba.



    Nikiwa na muuguza mama hospitalini pale siku moja alfajiri iliniita jina langu nami haraka nikaitika.



    "Mwanangu baraka kunakitu nataka ni kujuuze leo hii" aliongea ni kauliza ni kitugani mama ?



    "Unajua nilimpenda sana baba yako mzee matata na nilimkabidhi moyo wangu wote kwani ni wazi yeye pia alinipenda sana pengine kupita mimi kwani alikubali kuhama na mimi na kuondoka mkoa alio zaliwa akiepuka maneno ya ndugu zake walio mshawishi aniache na aoe mwanamke mwingine kwani mimi nilikuwa ni mgumba nisie weza kushika mimba" mama aliongea na kunyamaza kidogo kisha akaendelea"



    "mzee matata hakukubaliana nao kabisa akahama nami kutoka mkoa aliozaliwa, ndugu zake wasijue tume hamia wapi .baba yako alinipenda sana kufikia hatua ya kukubali kuishi nami bila kupata mtoto lah! mzee matata alikuwa na upendo wa kweli kwangu.

    siku moja usiku nilitoka nje kukojoa  kukiwa na hali ya mvua, na wakati narudi ndani nilisikia sauti ya mbwa akiunguruma huku akiburaza kitu nilipuuzia na kutaka kurudi ndani lakini hapo nikasikia chafya ya mtoto mchanga haraka nikawasha kurunzi yangu yenye mwanga hafifu  nikasogea upande huo ! masikini nilikuta kuna mtoto mchaga akisukwa sukwa na mbwa akiwa katupwa nilimfukuza mbwa huyo kisha nikamuita mzee matata tukamchukua huyo mtoto na kuingia nae ndani kwani mvua ilikuwa imeanza kunyesha bila ya mimi mvua ile ingechukua uhai wa mtoto au mbwa ange mdhuru mtoto huyo tukampa jina la BARAKA na kukufanya kuwa mwanetu mpendwa ukiwa ni baraka kutoka kwa mungu" Moyo wangu ulipata mshtuko mkubwa sana na kukumbwa na simanzi mara dufu baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa mama na muda huo mama aliendelea kunisimulia

    "mama yako alikuzaa akakutupa akiwa anaona hufai ila sisi ulitufaa japo hatuku kuzaa ila tulikufanya kuwa mwanetu ....baraka mimi sio mama yako ila nakupenda sana"



    kufikia hapo nilikuwa na lia tu huku nikiwa siamini kuwa yule sio mama yangu  kilio kile kilichukua takribani dakika ishirini

    "HAPANA MAMA WEWE NA MZEE MATATA NDIO MLIO NIZAA HAYO MANENO SIYAAMINI NAKUPENDA MAMA" niliongea huku nikilia lakini mama alikuwa kimya... naaam kimya cha milele!! alikuwa amesha iaga dunia akiniacha na chozi la milele.



    Tayari mama alikuwa amefariki.



    Mama yangu alitangulia mbele za haki akiniacha kwenye kilio kikubwa nililia sana zaidi ya unavyo fikiri msomaji, mbaya zaidi mama alikuwa amefichuwa siri nzito kuwa mimi waliniokota , swala lile liliniumiza sana ni bora asingeniambia kwani mimi nawajua wao ndio wazazi wangu na mpaka leo hii naandika haya moyo wangu una kiri kuwa wale ni wazazi wema japo hawakunizaa.



    Ulikuwa ni msiba mkubwa sana kijijini pale , nae mama tulimzika karibu na kaburi la mumewe mpendwa mzee matata.

    Baada ya mazishi yaliyo hudhuliwa na watu wengi huku waalimu kadhaa walio nipenda wakishiliki mazishi yale kisha nikarudishwa shuleni ili nika pumzike bwenini kwani pale kijijini sikuwa na ndugu mwingine  tofauti na wazazi wangu walio tangulia.



    Hapo shuleni nilipewa wiki tatu za kupumzika kabla ya kurudi kwenye masomo...sikuwahi kuwaza kumtafuta mama yangu alie nizaa na kunitupa ila mara nyingi nilijiuliza ni kwanini alinitupa na kuniacha mazingira hatarishi .



    Nilirudi tena kwenye masomo huku hali yangu kiafya ikiwa sio nzuri lakini nilijikaza kuushinda wakati ule wa majonzi



    nilifanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha tano na sita na nilifaulu kwa matokeo mazuri kwenda chuo kikuu cha dar es salaam.



    Jiji la dar nilikuwa nalisikia tu kwenye  vyombo vya habari lakini sasa nilipata nafasi ya kwenda kimasomo huku gharama zote zikisimamiwa na watu wale walio tafutwa na hayati mzee matata .



    Miaka mitatu ya chuo ilinitosha kuhitimu vyema masomo yangu na kufikia hatuwa ya kuajiriwa kwenye kampuni ya wale wadhamini walio ni somesha huku asilimia ishirini na tano ya mshahara wangu wakichukuwa wao kama fidia .

    Yalikuwa ni mafanikio ya haraka sana kwani watu wengi huhitimu chuo kisha hupata tabu kwenye swala la kuajiriwa , nilishukuru sana kwa mungu huku nikiukumbuka msaada wa mzee matata , nilisikitika sana kwani wazazi wale walio nilea vyema walikufa bila kuyaona mafanikio yale.

    mshahara wangu wa kwanza niliuchukua na kwenda kijijini kujenga makaburi ya wazazi wangu wa pendwa na kuyaacha katika hali nzuri kisha pesa ilio bakia nikawagawia majirani ambao walikuwa bega kwa bega kwa mama yangu hadi umauti ulipo mfika, baada ya hapo nilirudi mjini ili kundelea na kazi.







    Tayari nilikuwa nimesha fanikiwa kujenga nyumba kubwa na kuna msichana nilikuwa nime muoa, msichana huyo nilimkuta katika maisha ya kifukara akiishi na mama yake kwenye nyumba waliopanga baba yake akiwa alisha kufa. yeye na mama yake walikuwa kwenye maisha magumu lakini moyo wangu ulipendezwa na binti yule nika muoa na kufanga nae pingu za maisha.

    kama wasemavyo wahenga ukipenda boga penda na ua lake, basi nilipo muoa binti yule nilimchukua na mama yake nikaishi nao nyumbani kwangu .



    Msichana yule aliyeitwa joyce alikuwa mke mwema kwangu aliniheshimu na alinipenda sana .tulifanikiwa  kupata mtoto wa kiume nae nikamuita MATATA ,



    Siku moja tukiwa wote mama mkwe na mimi na mke wangu niliamua kuwasimulia juu ya maisha yangu kwani walijua mimi ni yatima lakini hawakujua mengi ya maisha yangu.

    Siku hiyo niliwasimulia tangu nilipo tupwa na mama alie nizaa nyuma ya ua wa mzee matata kisha nikaokotwa na wazee wale wakanilea.

    stori ile ili wahudhunisha sana wakanipa pole, lakini nilikuwa nimefanya kosa kubwa kuwasimulia!!!!



    Ilikuwa ni siku ya pili tangu familia yangu niisimulie kuhusu maisha yangu , siku hiyo niliwahi sana kutoka kazini nikanunua zawadi za mwanangu na mahitaji ya mama watoto.  lakini nilipo fika nyumbani furaha yangu ili yayuka na kuzitupa chini zawadi zile , kwanza nyumba ilikuwa kimya kabisa tofauti na siku zote na nilipoingia ndani nikakutana na balaa.



    Kwanza nili muona mke wangu akiwa kalala sakafuni na mama mkwe alikuwa kalala kwenye kochi mwanangu matata akiwa kalala pembeni yake.



    Loh! hii sijawahi kuona usingizi namna ile itawezekana vipi wasinzie fofofo muda ule wa saa kumi za jioni!



    Haraka nikamsogelea mke wangu na nikamgusa kujaribu kumuamsha lakini hakuamka kabisa na mwili wake ulikuwa wa baridi!! , hata mama mkwe nae ile vile vile hadi mtoto wangu na wote wale hawakuwa wao ila ilikuwa ni miili yao tayari wamesha fariki.!!!!

    Nilichanganyikiwa sikujua nini kimetokea ila niliona karatasi ikiwa mkonomi mwa mama mkwe nikaichukua ilikuwa ni barua  haraka nikaifungua na kuisoma.

     

    Ndani ya barua ile nilikutana na jambo zito tena ilikuwa ngumu kuliamini na kulikubali kwani aliye iandika barua ile alikuwa ni mama wa mke wangu, aliandika kwamba yeye ndie yule msichana alie mtupa mtoto nje ya ua wa mzee matata !!!!!!, " Mwanangu kweli malipo ni hapa hapa duniani naona hata aibu kukutazama mwana nilie kutupa kisa ulikanwa na baba yako, jana ulipo simulia stori ya maisha yako nimejihakikishia kuwa wewe ndiwe nilie kutupa kisha nikakimbilia dar es salaam kuishi na mwanaume ambae na tulizaa huyu joyce ulie muoa naweza sema umemuoa dada yako ila wakulaaniwa ni mimi ...nisamehe kwa maamuzi nilio yachukua ya kuondoka na familia yako lakini nimefanya haya kwa kujiepushia aibu kwani wewe na mke wako ni mtu na dada yake japo baba tofauti ...nisamehe sana mwanangu ama hakika aibu kubwa imenikuta"



    LA haullah! yule ndie alikuwa mama yangu. kwa mara nyingine niliangusha kilio kizito cha kuipoteza familia yangu machozi yalinitililika naam MACHOZI YA MILELE ama hakika hili ni CHOZI LA MILELE.



    MWISHO.... 

BARUA YA MTOTO KWA MAMA YAKE

 





    BARUA YA MTOTO KWA MAMA YAKE

    *******:**;********

    Mpendwa Mama.

    Roho inaniuma, siamini kilichotokea. Nipo mbinguni sasa. Nilihitaji sana kuwa mtoto wako. Sijui nini kilichotokea nilipatwa na mshangao jinsi nilivyokuwa nikianza kukua. Nilikuwa katika giza lakini sehemu ambayo ni tulivu eti nimeambiwa ilikuwa ni sehemu inayoitwa mfuko wa uzazi.

    Nilijiona nikianza kukua vidole vya mikono na miguu. Sikuwa mbali na kukua kabisa kuwa mtoto kamili. Nilitumia muda mwingi kulala na kufikiri jinsi maisha yangu yatakavyokua baada ya wewe kunizaa.

    Hata hivyo siku za mwanzo kabisa nilijihisi na furaha sana kuwa sehemu ya nyama zako za mwili.

    Wakati nimo tumboni mwako nilikusikia mara kadhaa ukilia nataka ujue tu kuwa ulivokua ukilia na mimi nilikuwa nalia vile vile, muda mwingine nilikusikia ukilalamika kabla ya kuanza kulia sio siri nilikuwa nikikuonea huruma sana mama. Nilimsikia baba akikufukuza na kunikataa nilishangaa kwanini ulikuwa ukilia sana. Kuna siku ulilia siku nzima, niliumia sana siku ile. Sikujua kwanin hukuwa na furaha.

    Siku hiyo hiyo, kitu kibaya kilitokea. Kitu kama jinamizi kilikuja sehemu ambamo nipo ndani ya tumbo lako, nilikuwa nimetulia siku hiyo nikitafakari. Nilipatwa na hofu kubwa sana. Nilianza kulia, lakini hukunisaidia. Labda hukunisikia. Jinamizi lilizidi kunikaribia na nilizidi kulia mama!! Mama!! Mama!! Nisaidieeee lakini hukunisikia.

    Nililia! Nililia! Nililia! Mpaka nilipojihisi siwezi kulia tena. Jinamizi likaanza kukata mikono yangu. Nilipatwa na maumivu makali ambayo siwezi kuyaelezea mama!

    Nililia na kuomba jinamizi liniachie lakini halikuniacha, ndio kwanza likaanza kunikata miguu. Nililia sana lakini haukunisaidia wakati nilikuwa ndani ya tumbo lako.

    Japo nilikuwa katika maumivu makali. Nilikuwa nakufa! Nilijua kuwa sitaweza kuiona sura yako tena wala kukusikia ukinibembeleza na kuniambia kuwa unanipenda!

    Nilikuwa na mipango mingi kama ungenizaa, nilikuwa na mipango ya kukufuta machozi yako yote ambayo umekua ukikia mara kwa mara. Nilikuwa na mipango ya kukufanya uwe mwanamke na mama nwenye furaha. Sasa siwezi kutimiza mipango hiyo! UMENIUA MAMA! HUKUNIPENDA KAMA MIMI NILIVYOKUPENDA!.

    Mbali na vyote nilihitaji sana kuwa mtoto wako. Nimekufa kifo cha maumivu mno, sijui walikufanya nini mama mpaka ukawa katili vile, ila japo nilikuwa na maumivu makali nilitaka nikumbie kuwa nakupenda mama kabla sijafa ila nilishindwa n namna gani nikufikishie ujumbe huo unielewe.

    Na mwishoe sikuwa na pumzi tena za kukwambia chochote. NILIKUFA! Nilijihisi nikinyanyuliwa juu. Nilibebwa na malaika na kupelekwa katika sehemu ambayo ni nzuri sana. Nilikuwa bado nikilia. Lakini maumivu ya mwili yalikuwa yamekwisha.

    Baada ya hapo nilikuwa na furaha tena! Nilimuuliza malaika ni nini kilichoniua. Alinijibu kuwa ni "MTOA MIMBA" mimi sijui Mtoa Mimba ni nini, ila labda ndio jina la yule jinamizi aliyenitesa ndani ya tumbo lako na kuniua.

    Nimeandika barua hii kukwambia kuwa nakupenda mama na kukueleza ni jinsi gani nilitamani niwe mtoto wako. Nilijitahidi kweli Niishi. Nilitaka nami niishi niione Dunia ya mwenyezi Mungu, lakini nilishindwa Mtoa Mimba alikuwa na nguvu kunizidi mimi, alinivunja vunja mikono na miguu na kunitoa kwa nguvu tumboni kwako bila huruma wala ridhaa yangu.

    Ilikuwa ni vigumu sana kuishi, nataka ujuwe kuwa nilitaka sana kuishi na wewe mama! Sikutaka nife! Na pia mama nakukumbusha sana kuwa makini na huyo mtoa mimba ni muuaji mkubwa, anaweza kuja kukuua na wewe au akaharibu tumbo lako wadogo zangu wasiweze kuja kukaa humo!

    Nakupenda sana mama, na tambua kuwa nachukia kama na wewe utakuja kupata maumivu niliyoyapitia mimi kabla sijafa!

    Tafadhali mama uwe makini.

    Nakupenda.

    Ni mimi mwanao.

    "Nakuomba Nelea usitoe mimba yangu, Mungu akileta mtoto analeta na sahani yake"

NILIFANYA BIASHARA YA VIPODOZI NA MISUKULE

 





    "NILIFANYA BIASHARA YA VIPODOZI NA MISUKULE"
    Mara tu bbaada ya kumaliza kidato cha nne Angel aliwaacha wazazi wake Shinyanga na kwenda Dar es salam kukaa kwa shangazi yake.
    Angel alivyokua na rika la miaka kumi nane alikua na kijiuso kidogo, macho makubwa ambayo kila wakati yalionekana kama yanatoa machozi, Alikua ana pua ndogo nyembamba chini ya pua hiyo kulipangika safu mbili za midomo ambayo haikutulia kwa kutabasamu kila Mara.
    Urembo aliokua nao Angel miaka ile hauwezi jirudia ni saw a alichezea shilingi Chooni.
    ***
    Dar aliishi na shangazi yake maeneno ya Msasani osterbay, mboga tatu kwao haikuwa tabu kama ilivyo sifa ya eneo lile.

    Ushamba wa huko alikotok ulimjaa akawa hatoki ndani kama mwali anayesubiria kuolewa.
    Jogoo wa shamba hawiki mjini lakini anaweza kulijua jiji kwa kupitapita,Angel mwaka mmoja wa kukaa Dar alikua ashaanza kubadilika tabia, mule ndani pakawa ni kituo cha kulalia tu atokapo kuzurura kwenye jua kali pasipo sababu.
    Urembo aliokua nao ANGEL hakuna mwanaume atakayempita asigeuke nyuma kumuangalia wanaume wakaanza kumjua na kumpigia misele ya kila namna ila kitu kilichovutia kwa yule binti hakukurupuka kuparamia mpenzi.
    Mwishoni alijikuta anampenda kijana mtanashati na mwenye kazi nzuri ya afisa msaidizi wa mawasiliano katika kampuni ya AIRTELL pia yule kijana aliona ni bahati ya kupata msichana wa ndoto yake.

    Kila mmoja alionesha hisia na upendo kwa mpenzi wake si ANGEL wala PATRIC mpenzie.
    Upendo wao ulimea katika kipindi cha miezi mitano maamuzi ya Angel kwenda kumtambulisha Patrick kwa shangaze yake wakayafikia hawakuchelewa jambo lile Shangazi wa Angel alilikubali bila kipingamizi
    "Nafurahi wanangu kuwa na maamuzi ya busara, kwani mngekua kimya nisingemjua mkwe wangu, siwezi kataa uhusiano wenu najua mmependana na kufanana kabisa ilimradi Patrick ufanye mpango wa haraka umuoe Angel" ni maneno aliyowaambia siku hiyo jambo ambalo waliliweka kichwani kila mmoja akifikiria wataoana lini.
    Haikuwa changamoto kubwa katika mahusiano yao changamoto ilikua kwa Angel ambaye kwa kipindi chote kile hakuwa na kazi ya kufanya zaidi ya vibarua vya hapa na pale kama kuwafulia wahindi magagulo yao.
    Siku moja akiwa na Patrick aliamua kuongea kuhusu kazi ambayo itamletea faida kubwa ili wajikimu katika maisha kama wakifunga ndoa
    "Mpenzi," alita Angel akiwa kamshika mkono Patrick wakitembea katika fukwe za coco beach.
    "Niambie mke wangu mtarajiwa" aliitikia Patrick kwa sauti ya mahaba na ya upole.
    "Maisha ya kufanya kazi za vibarua yamenishinda miaka inaenda wala sioni faida yake" alilaalmika Angel
    "Mh sasa tutafanyaje?"
    "Tufanyaje, naomba mtaji nifungue hata biashara"
    "Angel unajua biashara inahitaji moyo kuna kupata na kukosa faida na hasara, kustahimili uvumilivu wake unaweza" aliluza Patric baada ya wazo alilitoa Angel kumkaa kichwani
    "Baby najua, ndio maana nimekwambia nataka biashara"
    "okay unapenda kufanya biashara gani?"
    alifikiri angel kabla ya kujibu swali lile
    "Biashara nzuri ninayoina ni kuuza VIPODOZI" alijibu

    "Vipodozi? hiyo ina kazi nzuri ya biashara?"

    "Ndio mpenzi" Siku zote mwanaume huwa dhaifu kwa mwanamke Patrick hakuwa NA njia ya kukwepa swala lile.
    "Sawa nimekuelewa nitaenda kukopa bank nikifungulie duka la vipodozi katika soko la Kariakoo" Angel aliposikia vile aliruka na kumkumbatia Patrick asiamini maneno yake.
    Baada ya wiki kadhaa kupita jitihada za Patrick kukopa bank zikafanikiwa.
    Hakutaka kuupoza ule mkopo moja kwa moja aliacha kazi zake siku hiyo na kuanza kulisaka soko la kariakoo kutafuta Frame nzuri ya biashara.
    Siku hiyo ilikua ni ya bahati kwake alikua frame iliyokua katikati ya soko lile mtu anahama hiyo hiyo ndio aliioda akapangisha.

    Baada ya kufanya vile alimfanyia Angel surprise ya kumuonesha akimwambia mzigo wa vipodozi ashaagiza baada ya siku kadhaa utatua bandarini.
    Furaha aliyokua nayo Angel siku hiyo haikua ya kawaida akiona maisha yanaenda kuwa mazuri. Jambo zuri atakalofanya angel hakusita kumtaarifu shangazi yake kwani bado alikua anaishi kwake.Shangazi yake alimpa baraka tele hasa kwa Patrick aliyejitolea kumsaidia.
    Wiki mbili baada ya Frame kupangishwa Angel alikua ndani ya duka likiwa limesheni vipodozi vya aina mbali mbali hasa mafuta ya lotion ya kujipaka.
    Kariakoo kuna biashara ya namna zile nyingi na ushindani uliokua katika soko lile yahitaji ujasiri.
    Angel alikua anauza bidhaa zake kwa kusua sua sana hakutegemea kama itakua vile yeye alizani ukifungua duka basi siku hiyo hiyo bidhaa zote zitanunuliwa.
    Miezi kadhaa kupita faida aliyokua anapata kwa mwezi ni ndogo kuliko ukiangalia wafanya biashara wenzake walileta bidhaa mpya kila mwezi yeye yapata miezi mitatu vipodozi alivyoanza navyo ni vile vile.
    "Mpenzi hii biashara sikujua kama ni nzito hivi tangu nianze napata visenti vya kula na kuvaa tu faida haionekani" ni siku moja akiwa kitandani alimuandikia Patrick massage.
    "Hee mara hii ushaanza kulalamika?, biashara ndivyo ilivyo mwanzo mgumu lakini ukizidi kumuomba mungu ipo siku utauza mamia kwa mamia, kumbuka bado mkopo hatujaurejesha, usivunjike moyo mpenzi" yalikua ni majibu ya Patrick akijitahidi kumfariji Angel.
    Walichart sana usiku ule kuhusu MAPENZI yao lakini Angel hakukublia kabisa kuona biashara yake inaenda namna ile.
    "Hapana kesho lazima niende kwa Mwajuma, anieleze anafanya nini mpaka anauza vile" Alongea kimoyo moyo Angel.
    Mwajuma alikua ni rafiki wa Angel hakupishana sana kiumri ila Mwajuma aliionesha ana umri mkubwa isipokua mwili ndio uliomfanya alingane na Angel. Walikutana kariiakoo nae akiwa ni mfanya biashara ila si ya vipodozi kama Angel.
    Yeye alimiliki maduka zaidi ya matatu ya nguo za kike na kiume akiwa anapata wateja wengi na kuingiza faida kubwa. Urafiki wao ulianza siku moja Mwajuma alienda kwenye duka la Angel kununua vipodozi wakajuana na angel ndipo alipoanzisha urafiki.
    Kesho yake Angel alitoka nyumbani kwa shangazi yake akiwa na mawazo ya kumuona Mwajuma aeleze kile anachotaka.
    Baada ya kufika dukani kwake alifungua nakusubiri mda uende ili amfate mwajuma kwani biashara yake haikua mbali na kwake.

    Lakini ilitokea kama Bahati siku hiyo Mwajuma alienda dukani kwa Angel.
    "Shoga angu Yale mafuta si yamenishiia nimekuja kununua mengine" alijitamba mwajuma aliyekua mzuri wastani mwili ulioja kwa kuridhika na hela, kavaa viatu vya mchuchumio funguo ya gari kaitumbukiza katika kidole cha mwisho.
    Angel alipomuona alimchangamkia zaidi ya siku zote.

    "eh! tena nilikua nampango wa kuja huko kwako shost" alidakia Angel

    "Kuna nini tena shoga, au unahisi natembea na bwana ako?' mwajuma alikuabl ni mtu wa utani sana kwa Angel licha ya urafiki wao.
    "Njoo kwanza tukae nikueleze vizuri"

    "mhh haya"walikubaliana wakaa kwenye viti pamoja.Angel hakujua aanzaje kumuuliza Mwajuma lakini mwishoni alipiga moyo konde.
    "Mwajuma tumekua marafiki kwa mda mrefu, kwa hiyo asinifikirie vibaya" alianza kwa kujihami Angel.

    "usiogope Angel wewe endelea" Angel alikaa vizuri akashusha sauti yake chini.
    "Shost, naona mwenzangu unauza kama unagawa bure yani wateja hawapungui dukani mwako,lakini angalia Mimi tangu nianze wewe ndio mteja wangu mkubwa, nisubiri mafuta yaishe ndio uje kununua,Kwa hiyo chonde chonde naomba siri ya uuzaji wako kama kanisani niende au kama msikitini niingie nimuombe huyo mungu uliyemuomba wewe" alipomaliza kusema vile Mwajua alicheka sana kiasi kwamba alinyanyua miguu juu.Angel hakutegema kwamba Yale maneno yatamchekesha mwajuma, alijua labda ndio atakamsirisha.
    "Angel ni hilo tu" aliuliza mwajua akipunguza kicheko.

    "Ndio shosti hilo sio dogo"

    "Ushamuomba mungu mara ngapi?" mwajuma alianza kumuuliza maswali
    "Mara nyingi tu"

    "umepata mafanikio gani toka umuombe?'

    "Ndio kama haya kidogo kidogo" alinung'unika Angel

    "Hivi una fikiri hakuna njia nyingine zaidi ya kumuomba mungu?'aliuliza mwajuma swali lilomtatiza Angel

    "una maanisha nini kusema hivyo?"
    "usiwe kama umekuja mjini Leo, usifikiri hapa kariakoo kila mtu anafanya biashara kwa kumtegeme mungu, njoo nikupe siri ya mafanikio yangu" mwajuma alimvuta Angel sikio nakulisogeza kwenye midomo yake.
    "Siri ni kwenda kwa mganga tu" Angel alichoropoka katika mdomo wa mwajuma kwa mstuko, maishani mwake hakuwahi kwenda kwa mganga wala kuwaza vile.
    "Kwa mganga?' aliuliza kwa nguvu mpaka mwajuma alimziba mdomo.
    "Shiiip bibieee, isiwe nongwa habari ndio hiyo, kama unahitaji kuwa kama mimi hiyo ndio siri yangu, na kwa uzuri nakupeleka mpaka kwake" alifoka Mwajuma. Swala lile lilikua ngeni kwa Angel ataanzaje kwenda kwa mganga. Alibaki ameduwaa asijue ajibu nini.
    "Embu nyanyuka unipe mafuta niende zangu, wewe endelea kujifikria ukizani mafanikio yanakusubiri" alisema mwajuma akinyanyuka ndipo angel nae alinyanyuka na kwenda kumtolea mwajuma mafuta yake.
    "shost bye,ukipata jibu usisite kuja kunieleza nipo wakati wowoate maana najua hapo nimekuacha njia panda" Mwajua alikua ni mtu wa kuongea mpaka anaondoka licha ya Angel kuwa kimya.
    Siku hiyo mchana iliisha akiwa anawaza maneno ya mwajuma kwenda kwa mganga.
    Ilipofika usiku akiwa kwa shangazi yake alitamani kumwambia lakini alisita.
    Alichukua simu ili amueleze Patrick habari zile nayo ikawa vile vile moyo ulisita.
    Kazi ikawa kwake yeye na nafsi zake kujibizana kwenda au kutokwenda usiku kucha akijigalaza kitandani asioate jibu mpaka usingizi ulipomchukua.
    Siku iliyofata akiwa dukani kwake nafsi ya kukubali kwenda ikashinda hakutaka kusubiri alimtafuta mwajuma dukani mwake na kumueleza kuhusu nae ampeleke kwa huyo mganga.
    Mwajuma hakuwa na hila alikubali na kumueleza asichelewe hiyo safari waende kesho yake wazo ambalo Angel aliliafiki.
    Bila ya Patrick wala shangazi yake kujua asubuhi ya kesho yake aliamka saa kumi na moja akimdanganya Shangazi yake anaenda kuchukua mzigo wa dukani huku Patrick asijue.
    Walikubalina na mwajuma kukutaa moroco kwani yule mganga anaishi Tegeta na mwajuma yeye anaishi Kinondoni.
    Sehemu waliyoahidiana walikutana na safari ya kweda kwa mganga ikaanza wakitumia gari ya Mwajuma.
    Kwa mganga walipofika Angel akielekezwa na mwajuma alieleza shida yake mganga bila kujali alimkabidhi dawa ya kuvutia wateja lakini kwa mashart makuu matatu.
    "Kwanza Akishaisindika ile dawa dukani mwake siku zinazofata akifungua duka muda wa kufunga uwe saa moja usiku na atakapofunga asirudi nyuma kulifungua.
    Sharti la pili hela atakazopata asizipeleke Bank wala kwenye taasisi yoyote ya kuhifadhi hela ajeengee kabati ndani ya hilo duka ahifadh huko

    Tatu asifungue duka lingine atumie hilo hilo moja ndani ya miaka miwili, akitaka kuajiri ajiri lakini sio nje ya hilo duka."
    Angel alikubali yale mashart bila kipingamizi wakarudi safari yao ile dawa iliyotakiwa aizindike ndani ya duka SAA moja usiku wa siku hiyo.
    Angel mchana wa siku hiyo hakuwa ametulia akihangaika mda ukimbie aiweke ile dawa. Mpaka SAA moja ilipofika alikua ashatembea vya kutosha mule dukani.
    Wiki moja baada ya kuweka dawa hali ya duka la angel ikabadilika ghafla wateja wakaanza kumiminika makumi kwa makumi akiuza zaidi laki tano kwa siku angali mwanzoni alikua anauza hata elfu hamsini haifiki.
    Mafanikio yake hakuacha kumueleza Patrick hasa alipotaka aagiziwe mzigo Mara mbili pale dukani kwani vitu vinaenda isivyo kawaida.
    Patriki akiwa hajui kilichotendeka alimshukuru muumba wake akimwambia Angel ni mungu alisikia kilio chao hivyo hawana budi kumshukuru lakini si kwa angel aliyetumia ushirikina.
    Ikapita mwezi, miezi sasa Angel akawa ni maarufu kariakoo nzima kwa biashara ile, Patricki akijisifu kupata mpenzi mchapakazi lakini kitu kilichomtatiza ni kuwa alipomuuliza Angel anaweka hela bank gani alionekana akikwepeshaa maswali Yale.
    Kitendo cha Patrick kuanza kumuuliza maswali Angel kikamfanya Angel aone kwamba Patrick anataka kumuingilia katika biashara yake akaanza kupunguza upendo taratibu zile SMS walizokua wanachart usiku zilififia kama kibatari kilichokosa mafutĂ .

    Patrick alipompigia au kutuma SMS mchana alijibiwa

    "Samahani mpenzi, niko bize na wateja" akimpigia usiku au kutuma SMS navyo alijibiwa

    "Samahani mpenz nimechoka sana nahitaji kulala" kitendo ambacho Patrick kilimkasirisha na kuona siku moja amuendeee huko huko dukani na ni afadhali asingeenda kwani alikuta wateja wanatoka na kuingia akisubiri amalize huyu anakuja mwingine mwishoni alikata shauri.
    "Angel kwanini usifunge duka tuongee maana siku hizi ata weekend hautaki kupumzika mpenz"

    "Hivi Patrick una akili? yani Mimi niache hela nikusikilize wewe utanipa nini zaidi ya kugombana, naomba ondoka nitakutafuta kwa mda wangu, ukiwa wewe hapa unaleta gundu wateja hawaji" maneno ya siku hiyo yalikupasua ngoma za Patrick asiamini yule angel alimuomba mkopo wa mtaji ata badilika vile hata kabla nusu ya mkopo haujarudishwa.
    Alijaribu kila namna akiona ni utani mwishoni Angel alitaka kupigia simu polisi ndipo Patrick aliondoka kwa machungu sana.
    Hela zikamjaza kiburi Angel hakukumbuka wazazi wake alitumia hela zike kuruka viwanja na mwajuma pamoja namatajiri wa kike.

    Swala lile Patrick alilipeleka kwa shangazi yake Angel na kumueleza jinsi angel alivyobadilika.
    "Pole sana mwanangu at a Mimi naona Angel alivyobadilika kwani siku hizi anakuja usiku wa manane kalewa nikuuumuliza ananitukana sijui kapatwa na nini"
    Walimjadili sana wakamkalisha Angel chini na kumuleza lakini jeuri ya pesa akawapuuzia alipomuona Shangazi yake anamzingua aliondoka kwa shangazai yake bila kuaga akiwa na kila kitu chake kwa kiburi alienda kununua nyumba kubwa ya mamilioni huko Masaki mwisho akanunua na gari Kali ya kutembelea kwa duka lile lile moja.
    *****
    Yapata mwaka NA NUSU sasa Angel hana mawasiliano ya shangazi yake wala Patrick wazazi wake nyumbani shinyanga wanalilia shida Ila yeye alijivinjari akiwa na haja humtafuta mwanaume yeyote anayempenda nakutoa haja yake.
    Duka limesheheni vipodozi mpaka vingine vikawa vinatolewa nje nakuingizwa aliajirivwafanyakazi wawili ambao aliwalipa mshahara mzuri.
    Hakuna anayejua siku ya ajali yake,

    Ilikua siku ya jumanne Angel akiwa katika duka lake baada ya wafanyakazi wake kuondoka alikua anahesabu hela za siku hiyo ili aweke kwenye gala lake lilikua mule ndani.
    Alifanya haraka haraka kwani ilikua yapata saa mbili kasoro na ilitakiwa duka lifungwe saa moja.
    Alipomaliza kuhesabu alizihifadhi sehemu anayoijua yeye kisha akatoka nje haraka na kufunga duka.
    Aliliendea gari yake iliyopaki pembeni akataka atoe funguo afungue mlango alipopapasa kwenye mkoba hakukuwa na ufunguo wa gari zaidi ya zile za duka alizoshika mkononi

    Alijipiga sachi kila sehemu akiangalia nyuma kama kadondosha lakini haukuwepo mwishoni alikumbuka kaufungia ndani ya duka.
    Alirudi tena dukani akiwa na funguo za duka akaanza kufungua duka akisahau mashart mengine ya mganga.
    Alifanikiwa kufungua lakini alipokuja kunyanyua macho kutazama mule dukani la hasha hakuamini macho yake.
    Alikutana na watu wa kutisha wamejaa mule dukani kama wateja. wale watu walifanan na misukukule, wakishika vile vipodozi vya mule dukani na kuvifanyia mauza uza kama wengine walivipakza vinyesi, wengine walipakaza makamasi.
    Idadi ya wale misikule haikuhesabika kila mmoja akishika kitu chake na kuvifanyia vitu vya ajabu.
    Angel hakustahimili tukio lile alijikuta anadondonda chini na kupoteza fahamu.
    Alikuja kuamka yuko kwenye kitanda cha hospatli alijaribu kujinyanyua lakini alishindwa akajaribu kuongea nayo akashindwa machoni mwake akamuona mwanamke kasimama na bakuli kumtazama vizuri alikua ni shangazi yake aliyemkimbia kipindi kirefu.

    Shangazi yake bado alimpenda alipata taarifa za angel kudondoka alienda hosptali aliyolazwa muhimbili.
    Madaktari walimuambia Shangazi yake kuwa Angel kapatwa na stroke, iliyomfanya mwili mzima usifanye kazi yani yeye ni wa kugeuzwa, kutolewa kinyesi na anajisaidia hapo hapo kitandani.
    Hiyo haikutosha walisema uwezo wake wa kusikia na kuongea itachukua mda mrefu na pia matibabu zaidi yanahitajika aende nchi za nje.
    Shangazi yake hana hela wala nini akaanza kufanya mpango wa kitafuta hela lakini duka lake siku ile alipodondoka liliungua lote ghafla,:moto ulisambaa na kufikia mpaka gari yake ikalipuka, kila kitu kilichokua ndani ya duka au gari kiliteketa kwa moto.
    Alichunguza marafiki wa Angel akawafata kuwaomba msaada lakini walidai hawana hela wala pia hawakuonekana hosptali kumtembelea Angel si mwajuma wala nani.
    Suluhisho la mwisho lilibaki ni kuuza nyumba ya Angel baada ya shangazi, ndugu na wazazi wa Angel kuafikikiana walikubali kuiuza jela zilizopatikana ndio zikampeleka Angel India kutibiwa.
    Licha ya kupelekwa India Angel alirudi Tanzania akiwa anasikia kwa umbali na kuonge kidogo, akawa kilema wakutembea na baiskeli.
    "Shanga.....zi, Patrick yuko wap" aliuliza siku moja akiwa anasukumwa na baiskeli na shangazi yake wakimsafirisha kwenda Shinyanga kijijini kwani maisha ya mjini katika hali ile ni magumu hasa mtu wa muangalia
    "Patrick, bado unamkumbuka?
    sasa hivi anaozea jela mwenzako, zile hela alizokopa alishindwa kurejesha akafungwa" Angel aliposikia hivyo akiwa anashusha maudenda kama tahira alianza kulia kwa kumkumbuka Patrick wake.
    Alijuta kwenda kwa mganga ule urembo wake ulipotea akawa na ngozi iliyokakamaa kama mzee angali ndio alikua ana umri wa miaka ishirini na tano tu.
    Iligundulika kuwa wateja waliokua wanaenda kununua vipodozi kwake walikua wanatolewa kafara kwa mwezi watano na akitolewa kafara anaekwa msukule ndani ya lile duka bila ya wateja wala Angel kujua.
    Angel alijutia na kunung'unika moyoni

    "KUMBE NILIFANYA BIASHARA NA MISIKULE" Kutoka kwenye ufahari leo hii anatembelea kibaiskeli, kwa kusukumwa, chakula analishwa, kuoga n vitu vyote anafanyiwa hana uwezo wa mwingine.
    Wale ndugu aliowatupa ndio wanamsaidia shughuli zote zile. Marafiki aliokua nao anaruka viwanja, gari ya kifahari ama ile nyumba vyote vilipotea kama upepo.

    *****MTAKA SABA NYINGI KWA PUPA,HUPATA MINGI MISIBA********mwisho****
    UJUMBE: Ni heri mtaji wa elfu kumi unaokuzailishia elfu hamsini ya faida kwa mwezi ya HALALI, kuliko

    Mtaji wa elfu kumi unaokuzalishi faida yamilioni kumi kwa wiki kwa HARAMU.
    Usiharakie Maisha kama rizki ipo ipo tu japo itacheleweshwa lakini MTUMAINIE MUNGU WAKO. usimtegeme mwanadamu mwenzako.

BALAA

 





    "BALAA"
    " Miongoni mwa masiku katika juma,siku ambazo mara nyingi huwa ni siku

    zenye wingi wa watu ambao wanakua wanazunguka katika maene mbali mbali

    ya ndani ya hata nje ya mji kwa ajili ya mambo fulani fulani ambayo

    ndio huwa weka wao hapa mjini,hali kama hiyo mara nyingi haiishii kwa

    watu wa maofisini au wale wafanya biashara pekee bali huwa inaenda

    mpaka kwa wale wafanyakazi ambao wanakua wanafanya shughuli mbali

    mbali katika jamii kama vile Waalimu,madaktari na hata wale wafanya

    usafi wa maeneo yanayoizunguka jamii..
    *****
    Katika viwanja vya shul ya sekondari Tumani,shule ambayo imekumbwa na

    upepo mbaya wakuto kufaulisha mwanafunzi hata mmoja kwenda kidato cha

    tano tangu kuanzishwa kwake miaka nane iliyopita chini ya uongozi

    imara wa mkuu wa shule hiyo mwalimu.
    Bagamba Zeganda,mwalimu ambae

    alisifika saana kutokana na mipango mingi ambayo alikua akiwaeleza

    wazazi lakini mwisho wa yote utekelezaji ulikua ni sifuli,mpango ambao

    aliupanga kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka shuleni pale ulikua ni

    mpango wa kujenga maktaba kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kidato

    cha nne kwa ajili ya mitihani yao ya mwisho,kiukweli wazazi wa

    wanafunzi walitikia kwa mwitiko mkubwa ambao haikutarajiwa kuitikiwa

    kutokana na ubishi wa wazazi wale juu ya ule mpango mwingine wa

    chakula cha pale shuleni,mwalimu bagamba zeganda aliitisha mchango wa

    kila mzazi kuchangia shilingi elfu kumi kwa ajili ya ujenzi wa maktaba

    ile pamoja na ununuzi wa vitabu vya masomo ya sayansi,tena alisema

    hayo huku akiwapa upatu watoto wale kuwa huenda wote wangekua

    madaktari au wahandisi wakubwa kwa miaka ijayo! nani asiependa mwanae

    kua daktari?
    ni nani asietaka mtoto wake kuwa mwandisi? au ni mzazi

    gani asipenda mtoto wake kuja kuwa miongoni mwa watu wanaousudiwa

    saana katika taifa hili na hata bara la Afrika kama sio dunia nzima?

    hayo ndio maneno ya Bagamba wa Zeganda ambayo yaliwaingia kwa ufasaha

    wazazi wa watoto wale,walipanga mengi pamoja na wazazi wale na hatmae

    kutaja tarehe ya kikao cha mwisho cha michango na mipango..
    Yalikatika majumaa kadhaa na hatimae wazazi walikuja kwenye kikao kile

    ambacho kilipata chapuo kwa jina la kiingereza "create our future

    generation" neno ambalo lilikua zuri miongoni mwa wazazi pamoja na

    wale wahusika wenyewe ambao ni wanafunzi wa shule ile,baada ya wazazi

    kuwa wengi katika viwanja vile vya shule ndipo mkuu wa shule bwana

    Bagamba aliposimama nakuanza kutoa maneno ambayo yalijenga imani

    miongoni mwa wazazi wale "leo inaandikwa historia,zaidi ya wazazi 325
    kuchanga zaidi ya elfu kumi kwa kila mmoja!! kwa ajili ya ujenzi wa

    taifa la kesho linaloenda kwa sayansi na teknolojia" kiukweli maneno

    ya mwalimu yule yalimshawishi hata yule aliepanga kutoa 10000 kujihisi

    mkosaji na kujikuta hata akikopa kwa ajili ya kuongeza angalau ifike

    elfu20 au elfu15"
    ****************
    Baada ya mchano ule wazazi wote walirudi kwenye makazi yao huku wakiwa

    wanaamini hivi karibuni huenda shughuli ya ujenzi wa maktaba

    ungefanyika,na huenda wengi wa watoto wao wangekua wamepata mahala

    sahihi kwa ajili ya ufaulu wao katika mitihani ya kitaifa ambayo

    ingefuata...
    Siku zilienda na kulikua hakuna hata dalili yoyote ya kuanza kwa

    ujenzi wa maktaba,jambo ambalo lilianza kuwatia wasiwasi wazazi wa

    watoto wale,lakini hakuna hata mzazi mmoja ambae alithubutu kwenda

    shule kutoa malalamiko yake,haikueleweka kwa sababu gani wazazi waze

    hawakwenda kutoa malalamiko katika uongozi wa shule ile,kiukweli watu

    walio wengi waga hawapendi kufuatilia maendeleo hata yale ambayo

    wameshiriki kwa kuyatolea mchango na hiyo ndiyo kasumba ambayo wazazi

    wale walikua nayo!!!
    ****
    Baada ya mwalimu yule kupata mchano ule wa maktaba tena bila hata ya

    wazazi wale kupewa stakabathi kama uthibitisho!!! ndipo Zegamba

    alipoamua kutumia nafasi ile kama kile ambacho kilionekana kama neema

    kwa upande wake,baada ya kikao kile Mwalimu mkuu wa shule ya matumaini

    aliiandikia wizara ya elimu barua ya kuomba kustaafu kazi kwa kile

    kilichodaiwa kuwa umri wake ulikua umeenda saana pia mazingira ya

    shule ile hayakua rafiki,wizarĂ  haikutaka kufanya uchunguzi kuhisiana

    na hilo ila wao walichoamua ni kuandaa mazingira ya kumstaafisha

    mwalimu yule pamoja na kumwandalia usafili kwa ajili ya kumpeleka

    mahala ambapo angeenda kuishi baada ya kustafu,
    Siku chache baadae barua ya mrejesho ili rudishwa kwenye ofisi ya

    mwalimu yule huku ikiwa imempa uhakika wa kumwamisha na kumstĂ afisha

    katika shule ile,ilikua ni furaha kubwa moyoni mwake maana ilikua ni

    njia rahisi kwake kuondoka mahala pale,
    Safari za hapa na pale hazikuweza kukatika kwa mwalimu yule,tena

    safari hii haikua siri tena maana mkuu wa shule msaidizi alikua

    ameshajua kile ambacho kilikua kinafanya na mwalimu yule,ndipo

    alipoamua kuchukua maamuzi magumu dhidi ya mkuu wa shule hiyo,
    ************************

KAMANDA

 





    " KAMANDA "
    NGURUMO za radi zilizoambatana na miale kadha wa kadha hazikutofautiana sana na ile mizinga iliyopigwa miaka mingi nyuma.

    Ni miaka mitano sasa imepita, awali nilikuwa nikija peke yangu katika udongo huu ulionyanyuka juu katika namna ya kuunda tuta la aina yake lisilopendeza sana kutazama machoni.

    Sipo peke yangu leo katika tuta hili nipo na kiumbe mwingine ambaye angalau siku hii ya leo anaanza kupata maana halisi ya tuta hili.
    Naam ni kaburi ambalo walizikwa wanajeshi wapatao kumi na watano waliokufa katika vita huko Somalia, miili yao iliharibika vibaya kiasi kwamba haikutamanika kuaga na hivyo serikali ilitusihi sana tukubaliane na matokeo.

    Wanajeshi wote wakazikwa katika kaburi moja kubwa.

    Kati ya miili hiyo mmoja ulikuwemo mwili wako mume wangu, mume niliyelisahau jina lako la Amata na kukubatiza jina la Kamanda tangu ulipojiunga na jeshi na hatimaye kuwa mwanajeshi kamili.

    Hakika ulikuwa kamanda, sio tu kwa sababu ya gwanda ulizokuwa unavaa bali jinsi ulivyopigana kiume ilimradi familia yako iweze kuja kuishi maisha mazuri, ulisaidia upande wa familia niliyotoka ya kimasikini bila kujal;i nduguzo watasema nini. Hatimaye ukanioa il;i wakae kimya.
    Ukamanda wako haukuishia hapo, wakazi wa Mbagala wanakulilia hadi hivi sasa, kwa jinsi ulivyojitoa muhanga wakati ule lilipotokea tukio la mlipuko wa mabomu, watoto uliowaokoa hivi sasa wapo shule ya msingi, usingekuwa wewe wangekuwa chini ya madongo haya yaliyokufunika wewe.

    Kamanda!! Leo hii nimekuja hapa na ninayazungumza haya nikiwa na kamanda mwingine chipukizi, kamanda ambaye haukuwahi kumuona wala yeye hajawahi kukuona zaidi ya picha zako tu zilizojazana tele ndani ya ile nyumba uliyoijenga.

    Mara yako ya mwisho ulilibusu tumbo langu lililokuwa kubwa kiasi kutokana na ujauzito, ukasema kuwa iwe isiwe lazima nitazaa mtoto wa kike..... nikabisha nikasema nazaa kamanda wa pili.

    Amata mume wangu huko ulipo tambua kuwa nimekuzaa wewe tena na leo hii nipo na wajina wako aliyeniuliza sana juu ya wapi ulipo na nini kilikutokea.

    Amata!! Siamini kama kweli upo chini ya madongo haya kwa sababu sikuwahi kuushuhudia mwili wako uliodaiwa kuwa umeharibika vibaya mno.
    Kamanda nahisi upo hai na siku moja utarejea nyumbani ili umfunze wajina wako mambo mengi kuhusiana na jeshi, kwa sababu maswali anayoniuliza nakosa majibu, ananiuliza nini maana ya nyota, ananiuliza nini maana ya saluti. Nakosa majibu kabisa namjibu uongo leo, kesho anakuja na swali jingine.

    Na kinachonifanya niamini kuwa bado upo hai ni kitendo cha wajina wako kujitamba kila siku shuleni kuwa baba yake ni mwanajeshi na ni shupavu sana.

    Kamanda!! Naumia sana moyoni mwangu kwa maneno makali niliyiopewa na ninayoendelea kupewa kutoka kwa ndugu zako, Kamanda huwezi amini eti wanadai nahusika katika kifo chako eti kisa tu ile nyumba uliyoijenga uliandika jina langu hivyo hawana haki ya kunifukuza.

    Nakukumbuka sana kamanda uliniambia kuwa mtu akinikera basi sitakiwi kujifungia ndani na kuugulia huku machozi yakinibubujika badala yake nitembee na kukutana na watu ambao wapo upande wangu nizungumze nao na hapo nitapata faraja ya moyo.

    Basi sina haja ya kuwa nazunguka sana faraja yangu ni huyu wajina wako, kila nikikereka nakaa karibu naye na kumsikiliza jinsi anavyonisimulia sinema alizoziona......
    Kamanda!! Huko ulipo napenda pia kukushirikisha hili jambo ambalo nashindwa kulikemea kwa sababu sina nguvu katikati ya umma.

    Ni kuhusu thamani ya mtu baada ya kifo chake, Kamanda, eti licha ya kujitolea kote kule, kaburi lako wewe na wanajeshi wenzako mliokufa mkipigana vita katika nchi isiyokuwa yenu hata hayajasakafiwa, ninapozungumza na wewe haya mvua inanyesha na ni matope yametapakaa, natumia uzoefu tu kulitambua kaburi hili kwa sababu huwa nakuja mara kwa mara kukusalimia maana sina pengine pa kukupata na kukupa salamu hizi.

    Kamanda!!! Miaka yote nilikuwa nikifika hapa na kukueleza kuwa nimeukumbuka sana uwepo wako huku nikilikosa penzi lako maridhawa, lakini sikuwa hi kukueleza mengi yaliyojitokeza baada ya tukio hilo lililohusisha kifo chako na makamanda wenzako.
    Kamanda! nilikuwa Mwanza kwa ndugu zako, nadhani unajua jinsi gani ambavyo hawakuwa upande wanguy mara zote lakini kumbuka mimi tayari nilikuwa katika ukoo wako hivyo sikuwa na namna zaidi ya kwenda kuwajulia hali, na baada ya tukio ndipo nikatambua ni kwa nini ulinikataza kata kata nisiende kwa ndugu zako bila uwepo wako.

    Awali nilitengwa na dada zako, hadi mama yako alikuwa akinitazama kwa jicho la tofauti.... ila haya yote niliyapuuzia japokuwa nilikuwa naumia sana.

    Sasa ilipotumwa ile taarifa kuwa mmeuwawa mkiwa vitani, hapo kila mtu akanigeukia mimi kana kwamba ni mimi nilikulazimisha uende vitani!!

    Kamanda! nisiendelee kuzungumza haya kwa sababu yananiumiza sana, ila cha msingi elewa kwamba baadhi ya watu walinishauri niitoe hii mimba uliyokuwa umeniachia eti mimi bado kigoli niweze kuolewa na mtu mwingine kwa sababu nduguzo walikuwa wamenitenga kabisa.
    Kamanda! ningeweza kufanya kila kitu lakini sio kutoa kumbukumbu hii, hadi familia yangu ilinisihi kuhusu jambo hilo na hadi wakafikia hatua ya kusema kuwa hawatamlea mtoto ambaye ukoo wake umemkataa hata kabla hajazaliwa.

    Nikaamua kusimamia uamuzi wangu, yaani laiti kama ile nyumba ungekuwa haujaandika jina langu sijui tu ningepitia wakati mgumu kiasi gani.....

    Niliilea mimba hadi nikajifungua Kamanda, na hatimaye nikajiona nikiishi nawe tena katika mwili wa huyu mtoto wako.

    Ni miaka mitano na miezi kadhaa sasa Kamanda!

    Sijawahi kufikiria kuwa na mwanaume mwingine, nimeamua maisha yangu yote kumkabidhi Mungu.... nakumbuka uliwahi kuniambia sijui kuimba eti nina sauti mbaya... nahisi ulikuwa unanitania tu huwezi amini sasa naimba kwaya kanisani. Na wanakwaya wanasema najua kuimba....

    Basi hiki ndicho nilichoamua, nimeamua kumuimbia Mungu kwa mema yote ambayo ananitendea na ninamshukuru kwa yote yaliyopita.....
    Kamanda Amata! Ningeweza kuwa na mwanaume mwingine, lakini hakuna mwanaume kama wewe na simwoni akitokea mbele yanguhadi nitakapokutana nawe huko ulipo ama la ukirejea kutoka ile safari uliyoondoka miaka mitano iliyopita huku ukinipa ahadi kedekede kuwa utaniletea zawadi kutoka huko unapokwenda.

    Nazisubiri zawadi zangu Kamanda kwa sababu bado naamini upo hai, ila basi tu haujataka kurudi nyumbani kwako.

    Nimezungumza mengi sana Kamanda, naamini umenielewa na si jambo jipya wewe kunielewa ila siku hii ya leo mtoto wako wajina wako na kamanda mwenzako amenisihi sana kuwa kuna neno anahitaji kuzungumza na wewe, amesihi kuwa nisimwache nyumbani bali nije naye hapa anataka kusema na wewe.

    “Amata mwanangu, baba yako anaishi chini ya udongo huu, zungumza ulichotaka kuzungumza atakusikia na atakujibu sawa mwanangu!!!” nilimweleza mtoto wangu, mtoto ambaye naweza kukiri kuwa alikuwa wa aina yake akiwa na uwezo wa kufikiri mambo makubwa sana tofauti na umri wake wa miaka mitano, ni kweli hakuwa mzuri katika kuunganisha visa olakini alikuwa anaongea na kueleweka.
    Amata alisogea mbele ya tuta lile akapiga magoti akiniiga nilivyokuwa nimefanya mimi na hapo akaanza kuzungumza kwa sauti ya kitoto sauti iliyoniumiza sana hasahasa kile alichokuwa anakisema.

    “Baba kwa nini unaishi huku peke yako huku porini... nimekuja nikuchukue twende nyumbani.

    Nilimwambia rafiki yangu Lameck baba yangu ni mwanajeshi akabisha... nataka aje akuone, nikimleta lameck utatoka humu baba ili na yeye akuone... halafu baba nataka na mimi nikiwa mkubwa niwe mwanajeshi kama wewe.

    Nakusubiri utoke baba... kama mimi ni mtoto wako toka twende nyumbani.....”
    Alimaliza kuzungumza mwanangu Amata na kama masihara vile nilidhani tutaondoka, mtoto akagoma kuondoka kabisa alikuwa analia akiita babaa babaa!!

    Nilijaribu kumsihi sana nilimwongopea mambo mengi ilimradi tu aamini lakini kilio kilizidi kuwa kikubwa.

    Kilio cha mtoto huyu kulilia kuwa anamtaka baba yake kiliniumiza sana na mwishowe na mimi nikajikuta nalia nikimsihi Kamanda kama anakisikia kilio cha mtoto wake basi atoke na kumtuliza walau mara moja tu!!

    Lakini zaidi ya kelele za miti na ndege waliokuwa wanaruka hapa na pale hakuna jibu lililotoka. Palikuwa kimya... kimya kabisa!!

    Kamanda hakuwa pamoja na sisi!!

    Nikiwa sijajua nini cha kumfanya mtoto yule mara alianza kushangaa huku akirejewa na tabasamu.... na mara akazungumza.
    “Mama... baba amesema tutamkuta nyumbani... twende nyumbani mama twende!!” alinisihi mwanangu huku akinivuta mkono.

    Ilikuwa inastaajabisha sana hali ile, nikamfuata alichohamasisha tukaondoka.......

    Uzuri ni kwamba tulipokuwa garini alisinzia nadhani hii ilisababisha akasahau alichokuwa amesema tutakikuta nyumbani......

    Nilipofika nyumbani hata mimi roho ilikuwa inadunda nikitarajia kukutana na Kamanda wangu akiwa yu hai na tabasamu lake lile tamu la kupendeza.

    Lakini palikuwa kimya sana na hapakuwa na dalili ya mtu pale ndani.
    Nilipiga goti na kumshukuru Mungu kwani niliamini kuwa mwanangu alikuwa walau ameisikia sauti ya baba yake!!

    Nikamwandalia chakula akala kisha akalala.

    Nikaifunua ‘albamu’ nikazitazama picha kadhaa za hayati kamanda na kisha namimi nikaingia kulala.

    Nililala nikiwa naamini kuwa alipangalo mola haliwezi kuepukika na linakuwa na makusudi yake.....

    Nikaukumbusha moyo wangu kuwa usisononeke upya tena kwa sababu ya kukipoteza kipenzi cha moyo wangu!!!

    Wakati nataka kuzima taa nikageuka kumtazama yule mtoto wangu..... nikaiona sura ya baba yake tupu katika uso wake.

    “Kamanda Amata!!!” nikaita lile jina.... mtoto akatabasamu.

    Nikafarijika moyoni kuwa nilikuwa nimezaa mwanajeshi mwingine ambaye atashabihiana na baba yake kila kitu!!!
    LALA KAMANDA LALA UPUMZIKE UMEZALIWA UPYA TENA!!
    MWISHO!!!

BLOG