SIMULIZI FUPI : TUWAPENDE MAADUI ZETU
*Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila
mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama
unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili
vilevile.*
*Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari
na vitu vingine vya shule*
*"Wanafunzi wakakubali halafu kesho yake wanafunzi wakazibeba
zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi
sana.*
*Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu
ambao wanafunzi wanawachukia*.
*Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu* *akawaambia kila
mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake halafu aziache humo humo
ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo
nyumbani.*
*Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale
waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na
zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi yao*
*Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu
usiowapenda moyoni*
*kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya* *kwenye
begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo wako unayapata kwa kuubebesha mzigo wa
chuki dhidi ya watu.?*
*Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila
wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika* *na
kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokoko moyoni mwako. Moyo ni
kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na visivyo na
chuki ndani yake*
*Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe
maana ni moja ya virutubisho vya moyo wako,Samehe kwa anayekukosea na
kukukwaza.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment