Ni mimi Aisha nayazungumza maneno haya Leo nikiwa na maumivu mazito sana yanayouchoma moyo wangu, nililingia uzuri wangu, sura yangu iliyokuwa nyembamba na nyororo ilinifanya nivutie kwa kiasi kikubwa,
Na lile umbo langu lilivyokuwa nene kuanzia maeneo ya mgongoni kushuka chini liliyavuta macho ya vijana wengi na kuyashusha katika umbile lile zuri kwa hali ya matamanio.
Uzuri wangu ulinipa umaarufu ukafanya nikajawa na kiburi uku nikiwadharau watu na kuwaona ni takataka hawawezi kunifikia hata kidogo.
Nani ambaye akumjua Aisha? kila aina ya nywele nilizosuka zilinipendeza niliweka wiving refu lilinikaa vyema niliweka fupi pia nalo lilinipendeza vizuri kabisa.
Ni ukumbi upi wa starehe ambao hawakumjua Aisha? nilikuwa nikifika tu watu wanaanza kushangilia uku wengine wakitamani japo wanishike hata Mkono tu ila hawakupata nafasi hiyo.
Nilikuwa nikitembea kwa maringo sana uku nikiyatikisa makalio yangu kwa umahili wa hali ya juu watu walishangaa uku wakisema......
"Aisee kweli Aisha kabarikiwa sio kwa mtikisiko huo yaani kama tetemeko la ardhi limepita katika mwili wake."
Acheni Leo niendelee kuyazungumza haya katika hali ya upweke, Aisha mimi nilikuwa nikiongwa majumba na Magari ya kifahari nikajioni Mimi ndio Mimi hakuna Mrembo kama Aisha, hatimaye niliamua niutoboe ulimi wangu pamoja na kitovu changu na kupachika heleni.
Nilitembea na kila rika sikuweza kubagua mpaka umri wa Baba yangu Mimi nilipita nao tu cha msingi niliangalia pesa na sio kitu kingine.
Jamani kiukweli Aisha nilipeta sana kila mtaa niliopita nilikuwa nikiacha harufu ya pesa na hata mwili wangu ulikuwa ukinukia marashi ya Paris niliyokuwa nikiyaagiza uko Paris Nchini Ufaransa.
Kiukweli Aisha sikutaka kuharibu umbo langu na kila nilipopata mimba niliweza kuitoa haraka ili nisiharibu tumbo langu likawa kubwa nikapoteza ule mvuto wangu, nilifanikiwa kutoa mimba kama sita hizo ni ambazo nazikumbuka ila kuna baadhi nimezisahau.
Aisha Mrembo Mimi mwili wangu ulizidi kunipa rahaa kwa jinsi watu walivyokuwa wakinisifia na wengine kutamani wapate mke kama Mimi.
*****************************************************
BAADA YA MIAKA MITANO KUPITA.
Aisha yule wa zamani sio yeye tena Bali alionekana akiwa amedhoofu sana.
Aisha alikuwa amebaki Gofu la mtu yaani Fremu ya mtu Mabega yamemwanguka kama mkongwe Amekonda na kukondeana Mabaki ya mtu, Amebaki mifupa Mja huyo ni kifefe Ameregea parafujo za mwili.
Aisha alikuwa ni mtoto wa pekee kwa mama yake ndipo siku hiyo mama yake akamuita binti yake kisha akamueleza,
"Mwanangu Aisha kama unavyoniona mama yako naumwa sana sina muda mrefu katika ulimwengu huu ivyo naomba uniletee mjukuu nimuone na kumpa Baraka zangu zote kisha ntaweza kufa kwa amani.
Aisha alihuzunika sana baada ya kuyasikia maneno hayo ndipo akakumbuka zile mimba alizokuwa akitoa machozi yakaanza kumbubujika, Aisha alianza kuugua na asijue tatizo ni nini lile umbo zuri likageuka na kuwa la ajabu Kama Dudu washa.
Aisha hatimaye alipata mchumba ili aweze kupata mtoto kama jinsi mama yake alivyomuelekeza, waliishi katika mahusiano takribani miaka mitatu pasipo ya kupata mtoto kitendo hicho kilimuumiza sana Aisha, ikabidi Mume wake na Aisha amwambie mkewe waende hospitalini wakajue tatizo ni nini...
Hatimaye walifika wakapewa hudumu na majibu pia wakapewa, kumbe tatizo lilikuwa kwa Aisha walivyofika nyumbani Aisha akafungashiwa mizigo yake na kuambiwa arudi kwao na ndoa ikawa imeishia hapo.
Aisha akiwa njiani kurejea kwao alikuwa akilia sana uku akisema "Naenda kumwambia Mama kila kitu.
"Baada ya masaa mawili Aisha alikuwa amefika kwao ila cha kushangaza alikuta umati Mkubwa wa watu akajua Labda kuna kikao ila aliposogea anakuta ni Mama yake mzazi kafariki kumbe Aisha walimficha baada ya kujua kaenda hospitali.
Aisha nguvu zilimuishia alilia kwa sauti kubwa uku akisema "Mama yangu nisamehe nimekosa sana Mimi, kwanini umeamua kuondoka mapema pasipo ya kujua sababu ya Mimi kutokupata mtoto,
Jamani mama yangu mwanao najuta sana uzuri wangu Leo umeniponza sina thamani tena katika Dunia hii nitakuwa mgeni wa nani Mimi, Wanaume wote walionipenda kipindi Kile Leo hawanitaki tena Hata simu zangu hawapokei, wanaobahatika kupoke kabla ya salamu uniambia " Nikusaidie nini Wewe Malaya."
Jamani mama yangu Dunia Leo inanifundisha katika hali ya maumivu makali sana, kweli leo nimekubali kwamba .......
"Mungu hamfichi mnafiki " Leo Aisha Mimi nimeumbuka, jamani Masikini ya Mungu Aisha Mimi "nilisahau ubaharia kwa sababu ya unaodha" Nionee huruma Dunia najua nimekosa sana na sistahili hata kusamehewa, niliishi kwa ila kama kikwapa kunuka pasipo kidonda, jamani Leo Aisha nimeamini ......
"kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia" Heri kuliwa na simba, kuliko kuliwa na fisi. Dunia kwanini Afua ni mbili kufa au kupona siamini kwamba mema na mabaya ndio ulimwengu.
Mama yangu mwanao kizazi changu kimeharibika na kuoza vibaya sana, jamani naumia sana yote hayo yamesababishwa na mimba nilizotoa kweli ujana maji ya moto ni nani atakayekubali kunioa tena Aisha Mimi niliyepoteza mvuto mwili na nafsi vimechoka,
Kweli Dunia haitaki Pupa kwa maumivu nayoyasikia Mimi ni wakufa tu ni nani ataniuguza Mimi kama mama yangu umefariki na sijui kama umenisamehe kuondoka pasipo Mimi kukuletea mjukuu.
Najuta sana sina wa kumlaumu adhabu na maumivu yote yawe juu yangu mpaka siku ntakapoiaga Dunia hii iliyonilipa kwa Yale niliyoyafanya, acheni nilie msinifute machozi niacheni tu Dunia iniadhibu na kunijeruhi nasema upumzike kwa Amani Mama yangu nami nakufata uko ulipoelekea siku sio nyingi; Mwenyezi awabariki Nyooooote.
****** JIFUNZE *****
0 comments:
Post a Comment