Search This Blog

Monday, January 2, 2023

HUYU NDIYE "MAMA WA KUIGWA

 






Rehema alifika nyumbani mbio mbio na kumkuta mama yake aliyekua migombani akipalilia viazi vyake, "Mamaaa, hodi hodi humu nyumbani" aliita Rehema, "Naaaam, karibu nan jirani?" aliuliza mama yake Rehema, "Ni mimi mwanao Rehema mama" alijibu Rehema. Mama aliacha shughuli zake shamban na kurudi haraka, alimkuta mwanawe kaja nyumbani kutoka mjini anakoishi na mmewe ila cha ajabu kaja kidharura katika hali inayoonesha hayupo sawa yani atokako hali si shwari.

"Haya nieleze mwanangu nini kimekusibu waja mbio mbio kwangu kwa dharura kama kasuku"aliuliza mama Rehema," Dah ndoa imenishinda mama nimechoka mwanaume hashikiki nimeamua kurudi nimechoka visa mimi bora nikae nyumbani mama "alieleza Rehema. Mama yake alimuangalia namna alivyokua kavaa kikahaba akamwambia," Mwanangu kwa nini unanidhalilisha hivi, mmeo alivokuja kukuoa kijijini alikuchukua ukiwa na tabia njema na maadili mema, nani amekubadilisha namna hii huko mjini, hebu tizama hata mavazi uliyovaa yasivyo na staha "Rehema alitaka kujitetea," Ndio mavazi ya mjini mama mume ananionea tu sijabadilika"aliongeza.

Mama yake akamwambia, "Tulipata habari kuhusu ndoa yako, mmeo alitupigia simu zaidi ya mara 7 katika nyakati tofauti tofauti akitueleza kuwa umebadilika sana hushikiki tena umeungana na makundi ya mashangingi, unashinda kwenye masalun unazurura mji mzima katika mabaa na gesti unagawa unyumba humheshimu tena, leo ndio tulikua twapanga kukaa kikao kuzungumzia tena suala lako sasa nashangaa mbio mbio umerudi kulikoni??! "

"Hapana mama ananisingizia, mme kajaa wivu yule" alijitetea Rehema huku akiigiza kulia, ghafla mama yake alipokea simu, alikua ni mume wa Rehema

anapiga mama akapokea, "Mama sijui nikwambieje ila hakika mwanao sijui ana mapepo gani, yaani leo amenitia aibu ambayo sitokaa niisahau, kafumaniwa na mme wa mtu gesti kakimbia anasakwa mji mzima na vijana ndugu wa mke mwenye mume, mimi pia nimemtafuta sijamuona ndio nmetoka kuripoti polisi".

Mama alistaajabu sana kumbe Rehema alifikia hatua ya kutembea na waume za watu, "Pole sana mkwe wangu usijali amini yupo salama tutafanya juu chini arudi nyumbani kesho mimi na baba yake tutakuja huko kumpa kiapo cha mwisho" Mama Rehema alijibu, "Haya mama nashukuru sana ila kiukweli Rehema nampenda sana nisingependa kumuacha chondechonde mje mnisaidie kumfunda upya atulie" Mume wa Rehema alijibu.

Baada ya kukata simu mama Rehema alimgeukia mwanaye kwa hasira akamtandika vibao kama 7 vizito, akamwambia, "Mshenzi sana mtoto wewe, unapata mwanaume anaekupenda kweli alafu unaleta nyodo na mashauzi, hivi umesahau alipokutoa kijijini umepauka kama kiroba cha korosho? Pamoja na umaskini wako na elimu ya la 7 akakuridhia leo wamdharau? Hivi unafikiri yeye alikua mwehu kukuhudumia unapendeza ndio uwape penzi wa nje? Huo uzuri wako nani angeuona kama sio matunzo yake, Mwanangu Chunguza kabla ya kuamua, waza kabla ya kutenda, uzuri wako utakufanya uringe na upate mwanaume unaemhitaji ila tabia yako ndio itakayoamua ni kwa muda gani huyo mwanaume atakua na wewe. Uzuri huvutia kila mwanaume, ila tabia ndio itakufanya udumu katika ndoa . Upendeleo hudanganya na uzuri ni batili...bali mwanamke amchae Mungu ndiye atakayesifiwa

Nakushauri rudi kamuombe mmeo msamaha tulia nae thamini upendo wake, hakika kama ameweza kukuvumilia mauchuro yote hayo uliyomtendea basi tambua hata ukiachana nae hutokaa umpate mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na moyo wa huruma na uvumilivu kama yeye, rudi kwako haraka kesho mimi na baba yako tutakuja huko mjini mnapokaa kuweka mambo sawa, shenzi sana wewe"mama Rehema alimaliza akaokota fimbo akamcharaza kama 15 za fasta miguuni zikaingia kweli kweli maana Rehema alikuwa kavaa kimini, "Na ukiharibu siku nyingine usikanyage hapa nje kwangu ntakuvunja miguu fisi wewe huna adabu" Mama Rehema alimfukuza huku akimuonya kwa ukali. Rehema alikimbia kwa aibu akilia ndala mkononi.

Funzo 😑

Ni wanawake wangapi wamesahau waume zao walipowatoa saivi wanajiona wazuri wanaleta nyodo na kuona waume zao sio wa hadhi yao wanawadharau na kuwasaliti kama Rehema?

Je! Wewe unaesoma mkasa huu ni mwanamke wa aina gani kwa mmeo, unathamini upendo wake au unachukulia kama udhaifu wake na kumsaliti kama Rehema?

Je! Wewe ni mshauri na mkufunzi wa aina gani au ndio mtetea maovu, jiulize ingekuaje kama mama Rehema angemtetea mwanae badala ya kumkemea na kumuadhibu

Ni wamama wangapi wana ujasiri wa mama yake Rehema, kusimamia ukweli kukemea maovu ya watoto wao katika jamii?

Ni wanaume wangapi wenye mapenzi ya kweli kama mume wa Rehema

wenye uwezo wa kumvumilia mke hata katika maswahiba makubwa na kuwa tayari kusamehe?

Tafadhali kama umeupenda mkasa huu toa japo neno moja la pongezi kwa MAMA YAKE REHEMA kwa ujasiri na msimamo alioonyesha kukemea maovu ya mwanae Rehema kisha SHARE post hii iwafikie wamama wote katika jamii.

0 comments:

Post a Comment

BLOG