"Kulikuwa na binti mmoja msomi tena alikuwa anatoka familia ya kitajiri sana,alikaa muda mrefu bila kupata muenzi wa maana yaani wa kumuoa maana kila aliyekuwa anampata aliishia kudanganywa na mwisho wa siku wanaolewa wengine,, aliishi katika maisha yale kwa muda mrefu sana huku akilini mwake akiwa anawaza kuolewa na mtu msomi tena tajiri pengine zaidi yake,, Siku zilizidi kwenda huku umri wake ukizidi kusonga, Kijana mmoja aliyekuwa na maisha ya chinì huku akiwa na bahasha ya khaki mkononì,ilionekana alikuwa anatokea kwenye moja ya ofisi kuomba kazi japo alikuwa mnyonge sana,alipoangalia pembeni alimuona Deborah na kuvutiwa sana nae akaamua kumfuata akamwambia kama alikuwa yupo tayari kumuoa, Debora alicheka kwa dharau ila akawaza kitu, kwa kuwa alikuwa na pesa aliona amkubalie kijana yule ili aolewe angalau awe na heshima kwa marafiki zake, alimuomba kijana yule kwenda kutoa taarifa kwa wazazi wake, yule kijana kwakuwa alitokea kumpenda sana yule binti hakusita, alitafuta nguo alizøona zingemfaa akavaa kisha akaongozana na rafiki yake hadi nyumbani kwa wazazi wake na Debora.
********
"Uzuri wa wazazi wake na debora hawakuwa na maneno mengi sana, walimuuliza mwanao kama yupo tayari kuolewa na kijana yule naye akakubali, maandalizi ya ndoa yalianza huku Debora akitumia ghalama zake kuhakikisha ndoa inakuwa ya kufana ili kuweka heshima kwa marafiki zake, hatimae siku ya ndoa iliwadia huku ikionekana kuwa ndoa ya kifahari sana,, kijana yule aliyekuwa akiitwa Faustine alikuwa na furaha sana kumpata mwanamke aliyekuwa akimpenda sana kutoka ndani ya moyo wake..
__BAADA YA NDOA__
"Baada ya ndoa, Debora alimwambia Faustine kuwa asingeweza kuishi nyumba aliyokuwa amepanga Faustine hiyo ikamlazimu Fau kuhamia nyumbani kwa Debora kwani tayari alikuwa ameshakopa mjengo kutoka shirika la serikali la Taifa (NHC) Kwa makubaliano maalum, maisha yalianza kusonga huku Debora akianza vimbwanga vyake kila kukicha, kwakuwa yeye ndo alikuwa akileta asilimia themanini na tano ya mahitaji yote ya ndani 85% hivyo ilimpa kiburi ya kutamba na kujiona yeye ndo yeye,, Ilikuwa ni mwiko kwa ndugu zake na Faustine kwenda kumsalimia ndugu yao kwani mara zote waliondolewa kwa maneno na matusi ya hapa na pale, hatimae Hata vyumba vya kulala kila mtu akawa analala chumba chake wakati huo tayari Debora alikuwa na ujauzito wa Faustine, japo alijaribu kuutoa mara nyingi lakini ilishindikana na hatimae Akaamua kusubiri kujifungua huku kazi zote za ndani zikigeuka kuwa za Faustine,,, miezi tisa ilifika hatimae Debora akajifungua mtoto wa kike ambaye alikuwa na matatizo ya mdomo kwani ulikuwa upande huku miguu ikiwa haina nguvu, ni wazi alikuwa mlemavu,, Debora aliöna kama ni laana kubwa sana kwake,
"Baada ya miezi miwili kupita tangu debora ajifungue, vituko vilizidi sana kwa Faustine, Akiwa amelala alijikuta akiota ndoto ya kutisha iliyomfanya kukurupuka usingizini na kutoka chumbani kwake, alipofika sebuleni alisikia kelele za mahaba chumbani kwa Debora, huku akishangaa kuona mtoto akiwa amelazwa kwenye sofa bila hata kufunikwa nguo yoyote, Faustine alimsogelea mtoto wake na kumbeba vizuri huku akirudi chumbani kwake na kuchukua shuka lake na kumfunika mtoto kisha akarudi na kukaa kwenye sofa, baada ya muda alimuona Debora akiwa amemshika mwanaume mmoja aliyekuwa na tumbo kubwa wakienda kuoga,
"Unawaona wanaume sasa,, wee utaendelea kukaa hum na kulea kitoto chako hicho kilemavu, tena najuta kuzaa na wewe maana nadhani ndo sababu ya mimi kuzaa mtoto mlemavu,, na siku siyo nyingi nitamuua"
"Alizungumza Debora maneno yaliyomtoa Faustine machozi, akufukuzae hakwambii toka, Faustine alirudi chumbani kwake na kubeba baadhi ya nguo zake kisha akamuweka mtoto vizuri mkononi huyoo akaanza kutoka, alishangaa alipofka mlangoni kuona akisukumwa nusu amdondoshe mtoto,,
"TENA UMEJIONGEZA, UNAIONA HII SUMU, NILIKUWA NAWAUWA WEWE NA MWANAO"
Alifoka Debora na kumfanya Faustine kutabasam huku akianza safari yake talatibu kwenda kwa rafiki yake angalu ampatie hifadhi kwa huo usiku mmoja, wakati akiwa anavuka barabara akiwa na mawazo mengi alijikuta akiguswa na gari iliyomfanya kuanguka na kupoteza fahamu,
***********************
"Alikuja kushtuka akiwa hospital huku pembeni yake akiwepo mdada mmoja ambaye alikuwa na tabasam pana usoni mwake, cha kwanza alichouliza ni mtoto wake, dada yule aliongeza tabasam kisha akamjibu,
"Mtoto yupo salama, na anafanyiwa matibabu ya miguu yake Faustine, maana imeonekana wakati wa mimba mama wa mtoto alikuwa anatumia chemicals kali kwa lengo la kuidhuru mimba, na atakuwa sawa baada ya wiki tatu"
Alijibu dada yule, kitendo cha kuitwa jina lake kilimshangaza zaidi Faustine,
"Umenijuaje dada?"
Aliuliza Faustine,
"Mimi ni mkurugenzi wa kampuni fulani, kuna siku ulikuja kuomba kazi na ukakuta nafasi zimeisha, kwa jinsi nilivyoona vyeti vyako siku ile kuna nafasi imepatikana na nilikuwa nawaza nitakupata wapi, kwani namba yako haukunipa, nashukuru mungu kwani siku nakuparamia na gari ndo siku nilipokupata tena"
alijibu dada yule, na kuamsha furaha ya Faustine kwani alikuwa haamini alichokuwa anakisia hapohapo nguvu za kuinuka zikapatikana na kujikuta akikaa kitako kitandani,,
______BAADA YA WIKI TATU______
"Zilipita wiki tatu mtoto akaruhusiwa huku miguu yake ikiwa imekaza vizuri kabisa,wakati huo tayari Faustine alikuwa ameshaanza kazi, huku kampuni ikimpa nyumba za kuishi na kumuhamisha mama yake kijijini na kuhamia mjini na kuwa Ndo mlezi wa mtoto,,
"Siku zilizidi kusonga faustine akapata taarifa juu ya wazazi wa Debora waliokufa kwa ajari ya gari"
_____BAADA YA MIAKA MINNE____
"Ilipita miaka minne, siku hiyo Faustine akiwa ndani ya gari lake yeye mama yake na mtoto wake wakiwa wanaenda mjini, walipita karibu sana na nyumba aliyokuwa akiishi Debora, alishangaa kuona watu wengi wakiwa wamejaa nje ya nyumba ile wakiwa na sale za kazini,,alipoangalia aligundua walikuwa ni wafanyakazi wenzake, kwakuwa alikuwa rikizo haikumzuia kupita ili aone nini kinaendelea, aliegesha gari yake pembeni kidogo ya nyumba ile akashuku, wafanyakazi wenzake walimsalimia kwa heshima sana kwakuwa yeye ndo alikuwa mkuu wao alipoangalia pembeni aliona vyombo vikitolewa ndani ya nyumba ile na kurundikwa nje, alipouliza aliambiwa aliyekuwa amepewa mkopo ameshindwa kukamilisha malipo baada ya kufukuzwa kazi, wakati wanaongea Faustine alimuona debora akiwa anatoka ndani huku akilia kwa huzuni sana, wakati huo alikuwa na mkono mmoja tu tena ukiwa hauna vidole vyote,,Faustine alishangaa sana huku akitamani kujua nini kilimpata binti yule ambaye nae baada ya kumuona Faustine aliangua kilio zaidi na kuwafanya wafanyakazi wenzake na faustine kushangaa
"FAUSTINE MUME WANGU NISAMEHE BABA, HAYA NDO MALIPO YANGU,YULE MWANAUME ALINIKATA MKONO WANGU BAADA YA KUNIKUTA NINA MWANAUME MWINGINE,SIWEZI KUFANYA KAZI TENA,WAZAZI WANGU WALIKUFA NA NDUGU ZANGU KUGAWANA MALI ZOTE"
alizungumza kwa uchungu Debora wakati huo mtoto alishuka na kumuacha bibi yake ndani ya gari kisha akakimbia hadi alipokuwa baba yake na kumkumbatia,,
"FAUSTINE HUYU NDO MWANANGU"?
Aliuliza debora
"Faustine hakujibu kitu zaidi ya kuwaamru vijana wake kurudisha vitu vya Debora ndani na kumuahidi angemlipia deni lililokuwa limebaki,ila alikuwa amechelewa kwani Debora alianguka hapohapo na kuanza kutokwa na damu puani na mdomoni bila shaka alikuwa ameshakunya sumu Kali sana,, alimgusa mwanae na kutamka maneno haya
"NISAMEHE MWANANGU,USIFANYE KAMA MIMI NILIVYOMFANYIA BABA YAKO, HESHIMU MTU YEYOTE BILA KUJALI HALI YAKE KWA MUDA HUO,NISAMEHE PIA FAUSTINE NA NASHUKURU KWA KUMTUNZA MWANETU"
baada ya kutamka maneno yale Debora alikata roho pale pale.
_______funzo____
USIMDHARAU ALIYE CHINI YAKO LEO,KWANI HUIJUI KESHO YAKE/YAKO
MWISHO
0 comments:
Post a Comment