Search This Blog

Monday, January 2, 2023

SITOSAHAU

 






Nilikuwa ndani ya chumba changu kidogo katika kiti changu nimeinamia meza ndogo! mkononi nikiwa nakalamu nikiendelea na kuandika mfululizo wa riwaya zangu mtetezi kutoka kinte kitabu cha tatu kijulikanacho kama NITAKUUA KWA MKONO WANGU CHAKA ghafla simu yangu iloko kwenye charg inaita naipuuzia nami naendeleza na uandishi kabla ya kuita tena.na achana na kuandika naenda kuipokea....ZUBERI mimi ni mpenzi wa story zako ongera kaka nilifatilia story ya kweli ya maisha yako ilinivutia sana nami naitaji nikusimulie yangu! ambayo katu sitokaa niisahau MAPENZI! MAPENZI! MAPENZI! Kijana yule akaacha kuongea akaanza kulia...moyo wa huruma ukanijaa nikawa nambembeleza.nika anza ku record kila alichozungumka! alianza kwa kujitambulisha kwa jina la MWALIMU MESHACK! kisha akaendelea
"MERY!,MERY! MERY! MERY Moyo wa kupenda ukishapenda ni vigumu kuundoa upendo uliojenga kiota kwenye moyo wa apendaye malipo ya upendo wangu yamekuwa ndo haya MERY? sithaminiki hata mbele ya ndugu zangu! sithaminiki hata mbele ya rafiki zangu yote sababu ya KUKUPENDA wewe! umenifanya fukara!,nisiye na kitu hivi unakumbuka?! mara ya kwanza mimi na wewe kuonana ni chuo cha ushirika MUCCOBS nikichukua corze ya uasibu mimi nikiwa katika DIPLOMA nawe ukiwa katika SERTIFICATE unakumbuka kabisa? pale niliposhindwa kuzizuia HISIA zangu za mapenzi juu yako pale macho yangu yaliposanifu umbo lako lililojijenga no 8,macho yako madogo yaliyolegea pale utazamapo,matiti yako madogo kama yanayoanza kuchipukia miguu minene itamanishayo pindi uiangaliapo,uzuri wa asili usiyetumia vikorombwezo kujichubua,mrefu kiasi ndiyo! ilikuwa ni lazima kwa mwanaume KUKUPENDA au pengine kuitaji kuwa karibu nawe kwa namna yeyote ile unajua! MERY haikuwa raisi kukupata kiuraisi si mimi pekee niliyekupenda chuoni pale NO! si mimi pekee niliye diriki kukufata na kukwambia NAKUPENDA ni msururu mrefu wa wanaume walodiriki kuifungua mioyo yao kwa mapenzi mazito dhidi yako aukuweza kudiriki kuwakubalia wote.
MERY si mimi pekee niliyekupenda no! si mimi pekee niliodiriki kukufata na kukwambia NAKUPENDA ni msururu mrefu wa wanaume waliodiriki kuufungua mioyo yao kwa mapenzi mazito dhidi yako aukuweza kudiriki kuwakubalia wote,ulinichagua mimi kwa kuwa uliniona nina faa katika kundi lile la wanaume ukasema UNANIPENDA! je ni kweli ulinipenda? la asha! sidhani kama kweli ulinipenda yupo ulompenda aloamua kukusomesha na hata kukutafutia field zote na kukuaidi kazi pale utakapohitimu! kama ulimpenda ni kwa nini ulikubali kunipa nafasi ambayo katu ulijua ungeniumiza moyo wangu hata pale nilipokwambia NAKUPENDA hukushindwa kunikatalia,badala yake ukanikubalia amakwel mapenz ni usanii.....ni kweli nilikupenda,moyo wangu nkakuzawadia!
Kwa nini ulishindwa kuuthamini? heti unanipenda na ukadiriki hata nyumbani kwenu kunipeleka kwa minajili ya kunitambulisha nikiwa na kiroba changu cha sukari nilikubali kuja kwenu kujitambulisha,mapenz ni nguvu ya mioyo miwili sidhani kama kweli moyo wako ulikuwa na nguvu juu yangu.moyo wangu uliteketea pale niliposikia wazaz wako waliponambia awaniitaji kwamba utaolewa na yule aliyekulipia ada! dah! niliumia sana MERY haikuwa kazi raisi kulivunja penzi langu kwako,niishi bila uwepo wako kwangu yah! nilimaliza mafunzo yangu na kufanikiwa kupata kazi ya uasibu katika kanisa la angalkana MOSHI kuwa muasibu wao na pia nilikuwa mwalimu mzuri wa kwaya nikapata jina jipya la mwalimu MESHACK maisha yalisonga MERY nikakusahau wanakwaya wakanichangia milioni 15 kama pongezi na ushawishi kwangu kama mwalimu wao ndipo nilipoamua kwa moyo wangu kuachana na maswala ya uasibu kwa kuwa ilikuwa ni kazi ya lawama,kazi ilojaa ubadhirifu katika sadaka niliamua kufungua super marketi na kuuza vitu mbalimbali nakumbuka kabisa ile siku nilipokutana na mdogo wako alipokuja na kunieleza juu yako kuwa ULIOLEWA.je nini kiliendelea usikose sehemu ya mwisho ya story hii ya kweli ilomtokea mwalimu meshack.coment like,share uwezavyo.
Nakumbuka kabisa ile siku nilipok Nakumbuka kabisa ile siku nilipokutana na mdogo wako alipokuja na kunieleza kuwa uliolewa,na bwana yule kakuacha na kukutelekeza nilikuchukua na kukuweka katika min super market yang kumbe ni kosa nilifanza MERY? baada ya kukukabidhisha super market yang sikutaka kukuingilia kwa kuwa nilikuamini nilikuwa ni kiongoz wa kwaya sikutaka kuwa karibu na wewe ndo ukaamua kunitapeli? au kwa kuwa ulompenda alikuongopea thamani yangu ukaiondoa mawasiliano na alokusomesha ukuyataka,mkanitapeli na kuamua kutoroka kwenda kuishi na yule mwanaume bila kuukumbuka unyama alokufanyia! ama kweli mapenz ni upofu! ni kweli mapenz yana nguvu zaidi ya kitu chochote.uliponiporomosha kimaisha.hata nilipokutana na wewe kwa mara ya kwanza dukani kwako hukutaka kunisaidia kwa chochote.umeyashusha maisha yangu sina mbele wala nyuma chanzo ni wewe MERY kila la kheri ila kwa ulonitendea SITOSAHAU abadan.alimalizia kuongea mwalimu MESHACK kwa uzuni.
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG