Search This Blog

Monday, January 2, 2023

KIFO CHANGU MWENYEWE

 






......Naikumbuka vema ile siku ya mimi na wewe kuanza ukaribu zaidi licha ya kuwa tulikuwa tunasoma wote kuanzia kidato cha kwanza.

Monica hakika siwezi kuisahau siku hiyo ya graduation ya kumaliza kidato cha nne mimi na wewe pamoja na wanafunzi wenzetu.Siku ambayo nilikuomba tucheze pamoja nawe ukakubali na ndio ukawa mwanzo mzuri sana wa mimi na wewe kuingia kwenye mahusiano.Nilikuambia NAKUPENDA nawe ukakubali kuwa unanipenda japo ulitaka nisikusumbue kwa chochote mpaka tutakapomaliza mtihani wetu wa kidato cha tano

Nilikubali na hata mimi nilitaka iwe ivyo kwa sababu wote tulikuwa katika kipindi cha mwisho.

Hatimae lenye mwanzo halikosi mwisho mtihani wa kidato cha nne uliisha na sasa tukawa wanakijiji.Ni kweli japo tulikuwa hatuna kitu na tulikuwa bado tunategemea wazazi lakini mapenzi yetu yalikuwa ya dhati kabisa.Nilikupenda nawe ukanipenda na maisha yetu yale duni ya kijijini.Kwenu mlikuwa na uwezo kidogo sana na nakubuka baba yako alikuwa mwenyekiti wa kijiji na ni nyumba pekee iliyokuwa na solar pale kijijini japo ilikuwa ya nyasi.

Maisha hayakuwa magumu katika familia zetu kwani kama ilivyokawaida sisi watu wa kijijini mara nyingi tunaishi kwa kutegemea ukulima na ufugaji hivyo kuhusu chakula kilikuwepo kwa wingi

MIEZI ilienda huku mapenzi yetu yakiwa moto moto na kujikuta nimekukabidhi moyo wangu wote na sasa hatimae matokeo ya mtihaninwetu wa kidato cha nne yalitoka.

Kwa bahati mbaya wote tulijikuta tumepata daraja la nne yaani division 4 japo katika point ulikuwa umenizidi maana mimi nilipata four mbaya sana na wewe ulipata ile ya kwanza kwanza.

Sikuwa na kingine cha kufanya niliamua niungane na baba yangu katika shughuri za kilimo ili angharau nipate maisha niweze kukuoa kama nilivyokuahidi.Monicah ulifurahi sana kusikia nakuambia kuwa baada ya miaka miwili nikiweka mambo yangu sawa nitakuoa.Nilijituma katika kilimo na baba kupitia mashamba ya kwetu huku tukilima kwa ng'ombe.

Mungu si athuman mwaka wangu wa kwanza wa kilimo niliweza kupata gunia 70 za mahindi na vigunia vichache vya maharage na karanga.

Monicah ulikuwa mstari wa mbele katika kunitia moyo katika shughuri zangu.Ulinipoza kwa penzi tamu lililozidi kuozesha moyo wangu kwako.Nilijikuta nakupenda sana mwanamke wa ndoto zangu.Ulinipa ushauri kila mara ulionipa nguvu.Hatimae ukaniambia niuze hayo magunia baadhi kisha nifungue duka la bidhaa ndogo ndogo za nyumbani pale kijijini maana kijiji kizima hakuna aliekuwa na duka kubwa la kuweza kutoa bidhaa kwa wingi.Hakika hapo ndipo nilipoukubali ule msemo wa kuwa MBELE YA MAFANIKIO YA MWANAUME BASI KUNA MWANAMKE NYUMA YAKE.Hakika Monicah nilifungua duka na kuleta bidhaa kwa wingi.Duka ambalo nilifanikiwa kwa asilimia 100 katika mauzo.Hatimae siku zikaanza kusogea za ahadi ya mimi kukuoa na hata mipango ya hela ya mahali ilikuwa tayari imeanza kukaa vizuri.

MONICAH naikumbuka vizuri siku ile umekuja chumbani kwangu ukiwa umeshikilia tangazo la nafasi za kusoma katika chuo kimoja cha kusomea maswala ya NURSING.

Vigezo na alama za ufaulu zilizokuwa zimetajwa zilikuwa zinaendana kabisa na alama za ufaulu wako wa masomo yako.Monicah nakumbuka siku yenyewe uliniomba ujalibu kuomba endapo watakubali uende ukasome na kunitaka mipango ya ndoa niiailishe.Nilikubali na na kufuata ushauri wako kwa sababu nilipenda pia kuona unakuwa mwanamke msomi kwangu.Mungu alikubaliki ulichaguliwa kwenda kusoma Nursing katika chuo kilichopo mjini.Masomo hayo yalikutaka usome kwa muda wa miaka miwili kisha uhitimu.Miaka miwili kwangu si haba kuvumilia nimpendae.Uliniambia na kuniahidi kuwa ukimaliza tu masomo yako utahakikisha ahadi yangu ya mimi kukuoa wewe inatimilika.Nilikubali japo moyoni mwangu wasi wasi kubwa ilikuwa endapo kama utakutana na wanaume huko mjini wakakuteka na kukuchukua kusha ukasaliti penzi langu itakuwaje.Nilimuachia mola haya yote nikiamini yeye Muweza wa yote ataweza kukulinda wewe na penzi letu.

Monica ulianza mwaka wa masomo mapenzi yakiwa moto moto bado mimi na wewe.Tuliwasiliana kila mara hukubadilika wala hukushusha hadhi ya penzi langu.Ilifikia kipindi nilijiuliza hivi huyu anasoma chuo ambacho huko mjini hakuna wavulana.Maana hukuonyesha dalili za kubadilika wala kunichoka na kunisaliti.Kwa bahati mbaya baba yako ambae ni mwenyekiti wetu wa kijiji aliugua ugonjwa wa kukohoa damu kutokana na kazi nzito za kilimo alizokuwa anafanya na pia uvutaji wa sigara nguvu zilimuisha akawa ni mtu wa nyumbani.Alikuwa hana kazi yoyote ya kuingiza kipato.Hapo ndipo hela ya kukusomesha wewe ilipoanza kukosekana sikuona shida kuingilia jukumu la kukusomesha wewe kupitia duka langu.Nakumbuka Monicah niliuza duka mpaka nikakosa mtaji wa kuliendeleza na hatimae kufilisika.Sikuona shida kufunga duka au kufilisika kwa sababu nilijua nasomesha mke wangu wa baadae.Nililudi kwenye shughuri za kilimo na umwagiliaji ili angalau niendelee kukutumia hela za wewe kujitunza na kusoma ili umalize masomo.Nilijituma saana wakati huo duka langu nikiwa nimefunga Mungu alinisaidia nilifanikiwa kuwa napata hela na kukutumia.

Miaka miwili ilitimia hatimae ulimaliza mafunzo yako ya Nursing.Ajira nazo zilikuwa nyuma yako.kutokana na upungufu wa wauguzi hasa maeneo ya kijijini.Serikari ilikupangia kazi katika kituo cha zahanati kilichopo kijijini kwetu.Hatimae ulilejea kijijini kwetu na kuanza kazi.

Nakumbuka nilikuomba sasa nikuoe japo sikuwa na kitu na duka nilikuwa nimefunga kazi pekee niliyokuwa nimebaki nayo ni kilimo cha umwagiliaji wa bustani huku nikisubiri mvua zije nilime.Monicah uliniomba kuwa nikuoe baada ya shughuri za mavuno kuisha ili kuokoa gharama za ununuzi wa chakula wakati wa harusi na badala yake tutatumia kile nilichovuna.Pia ulinipa sababu kuwa hiyo itakusaidia na wewe kuwa tayari umeizoea kazi na pia utakuwa na hela itakayoweza kuchangia katika harusi.Hakika yalikuwa mawazo ya busara na pia niliyachekecha kichwani mwangu na kuona kweli yanamantiki.

MONICAH namlaani sana kalani muhesabisha Sensa Mathias ambae alikuja kijijini kwetu na gari lake kwa ajili ya kufanya kazi ya kuhesabu sensa.Hakuwa na sehemu ya kufikia hivyo ilibidi afikie kwa baba yako akiwa kama mwenyekiti wa kijiji.Mlimpa hifadhi yeye pamoja na gari lake.

Monicah ni nini ulichotamani kutoka kwa kalani Mathias?.Au ni lile gari alilokuja nalo pale kijijini kwetu?.Je au ni usomi wake kuliko mimi?.Pengine labda ni uvaaji wake nadhifu kuliko mimi.

Monicah uliingia kwenye mapenzi ma kalani yule na kunisahau kabisa mimi, Ulianza kubadilika na kuwa unanitukana na hali yangu duni ya kimaisha.Ukasahau kuwa ni wewe na kusoma kwako ndio kulinifanya nishuke hivi.Sikuwahi kupenda mwanamke mwingine labda ndiyo ilinifanya niteseke hivi.Ukasahau ahadi zote za mimi na wewe kuoana.Ukapenda kupanda gari na kunipita nyumbani kwetu ili niumie roho.Naikumbuka siku ile niliyopiga magoti mbele yako nikiomba uachane na karani kwa sababu nakupenda.Nayakumbuka maneno yako machafu uliyonitolea ukisema"Unanini cha kunipa wewe? Kwanza biologia inasema ukioana na mtu ambae sio msomi unazaa watoto ambao hawana akili darasani hivyo siwezi kuoana na wewe mimi nataka msomi ili nizae watoto wenye akili darasni sio watoto wa kushika jembe.Tena usinifuatilie mimi sio hadhi yako".

Maneno haya ninayakumbuka mpaka leo nikiwa hapa kitandani.Nakumbuka mate yako usoni uliyonitemea siku ile kuwa sina hadhi sikuweza kukufanya chochote kwa sababu moyoni ulikuwa bado unaishi.

Hatimae ile ahadi ya kukuoa iliamia kwa Kalani Mathias Siku ambayo nilinyanyua shingo yangu kwa mbaali na kukuona unavishwa pete ukiwa umependeza na gauni lako zuri jeupe.Nilimwangalia Mathias ambae sasa alikuwa amechukua ndoto yangu ya kukuvisha pete.Roho iliniuma sana nilianza kulia pale msibani.Jamaa zangu walinibembeleza na kuniambia kwa kejeri"Demu hasomeshwi utakuja jinyonga"

Taratibu niliondoka mpaka chumbani kwangu na kufikia kuanza kulia.Lililia kama mtoto mdogo huku nikigeuza shuka langu kama kitambaa cha kufutia machozi.Sauti za mziki harusini zilinifanya nizidi zaidi kudondosha machozi na kuwa kama mkuki uliouchoma moyo wangu

Hatimae harusi iliisha na ukachukuliwa kwenda kuishi mjini na Mathias.Alikuachisha kazi serikarini na kukutafutia kazi katika hospitali ya mtu binafsi huko mjini.Nilikaa siku tatu nikinywa uji na kulala bila kufanya chochote zaidi ya kulia.Hatimae siku ya nne niliamua kuufariji moyo na kuona kama yote ni mapito na niliamua kuendelea na shuguri zangu za shamba

ULIPITA mwaka mmoja.Nikiwa dukani kwangu tena ambako niliweza kulima na kulifufua duka sikuamini kukuona mbele ya macho yangu Monica mwanamke niliekupenda.Ulikuwanumependeza na kunenepa rangi yako nyeupe ilizidi kung'aa kwa maisha ya mjini.Nilipokutazama usoni ulikuwa unalia,Ghafla moyo wangu ulianza kuumia kukuona unalia.Ukweli ni kuwa japo uliolewa lakini moyoni mwangu ulikuwa bado unaishi NILIKUPENDA SANA na sikuwahi kupenda mwanamke mwingine.Nilikuchukua na tukakaa chini kuongea kilichokusibu.Uliniomba msamaha sana kwa ulionifanyia na kuniambia yule mwanaume sio mtu bali ni shetani kutokana na alivyokuwa anakutesa baada ya kukuchoka.Ukaniambia kuwa ni tabia ya yule mwanaume kuwa hutamani na kudanganyishia ndoa kwa mali na utajiri alionao kisha huwaacha wanawake pindi anapowachoka.Ulilia na kunitaka tuludiane na kusahau yale ya zamani.Nilikuonea huruma kwa chozi ulilotoa na hatimae nikajikuta tena nipo penzini na wewe.

SIKUJUA KAMA kufanya hivyo nilikuwa najichimbia kabuli langu mwenyewe.Miezi mitatu ilipita Monicah ulianza kuugua homa nzito iliyokufanya uanze kushuka uzito ghafla.Wazazi wako walikupeleka zahanati kwa ajili ya vipimo Maskini kumbe ulikuwa UMESHAATHIRIKA wazazi wako walificha siri na kusema kuwa unasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.Sikujua kama tayari na mimi vijidudu vimeanza kunishambulia haikupita mwezi hali ya kiafya kwangu ilianza kuwa mbaya nguvu ya kufanya kazi ilinipungua na hata mwili wangu ulianza kudhoofika.Wazazi wangu walinichukua nikiwa hoi kitandani na kunipeleka hospitali ili kupima na ndipo nilipogundua kuwa tayari UKIMWI ulikuwa umeshanitafuna.

Nilianza kulia sana nikiwa hospitari, Nilitamani sana nikuone ili nikuulize maswali niliyokuwa nayo kwanini umeamua kuniua?

Nililudishwa nyumbani nikiwa hoi kitandani macho yangu yameingia ndani mbavu zangu zinaonekana na kuhesabika.Niliomba nijikongoje nije nilale na wewe pembeni yako huku wote tukiwa hoi ili nikuulize maswali mengi niliyokuwa nayo lakini nilipoomba kuonana na wewe nililetewa taalifa ya kuwa nyumbani kwenu kuna msiba na tayari ulikuwa umefariki.

SAWA najua umetangulia na mimi ninafuata hivi karibuni.Hakuna sehemu nyingine tutakayokutana zaidi ya kuzimu kutokana na dhambi zetu.Nikifika huko naomba unijibu maswali yangu ambayo pia ninawauliza na hawa wanawake ninaowaacha hapa duniani hivi punde

👉Ni kwanini mnakuwa na tamaa ya mali na kutamani vitu ambavyo hamna uwezo navyo

👉🏻Ni kwanini sisi tusio na kitu mnatuona hatufai sana kwenye mapenzi pindi nyinyi mnapokuwa na kitu

👉Ni kwanini hamliziki na hali ya maisha yenu mliyonayo na kupenda kusaliti mapenzi ya dhati kwa tamaa ya vitu.

👉🏻Kwanini mnakuwaga na dharau sana kwa wanaume wenye maisha ya chini pindi nyinyi mnapokuwa na hadhi kidogo ya maisha?

Maswali haya naimani itabaki kuwa fundisho duniani na pia kokote niendako nikikuona nitakuuliza ewe monicah Muuaji wa roho yangu



FUNZO

* * * * * * * * * * * * * *

.....Usitamani kuwa na baiskeli ikiwa uwezo wako ni kutembea kwa miguu.

Usitamani pia kuwa na pikipiki ikiwa uwezo wako ni kutembea kwa baiskeli

Usitamani pia kuwa na gari ikiwa uwezo wako ni kutembea kwa pikipiki.Ki vyovyote vile kwenye maisha usitamani kitu chochote ambacho huna uwezo nacho maana huwezi jua madhara yake baadae.

Nataka nikufundishe kitu kimoja.Nafikili ulikuwaga unapewa sana hela ya kula shule hasa ulipokuwa shule ya msingi.Huenda mzazi wako alikuwa anakupa kila siku mia au miambili.Sasa basi huenda siku moja mgeni alikuja kwenu akakupa hela kubwa zaidi kama shilingi 5000 ya kutumia.Kwa haraka haraka ukiulizwa kati ya mzazi wako na mgeni nani aliekupa hela kubwa utajibu ni mgeni.

Lakini nataka nikuambie mzazi wako amekupa mia mia kila siku mpaka umefika darasa la 6 na mgeni kakupa elfu 5000 ya siku moja leo umemuona mgeni wa dhamani sana kuliko mzazi ni kwasababu umesahau vile vidogo vidogo wazazi walivyokutendea kwa kikubwa cha siku moja

Ninamaana hii.Monicah alisahau thamani ya kusomeshwa na mpenzi wake kwa thamani ya gari ya Mathias na wakati tukikusanya pesa zile kidogo kidogo alizokuwa akipewa na mpenzi wake mpaka kufikia hatua ya kumaliza chuo ni zaidi ya thamani ya ile gari ya Mathias.

OKY Wacha niishie hapo kutoa fundisho maana nahisi kuna mtu kama vile hanielewi hata niongee vipi.


0 comments:

Post a Comment

BLOG