SIMULIZI FUPI - FIKIRIA KABLA YA KUTENDA
John ni kijana mwenye umri wa miaka 30. Ana shahada ya uzamili (Masters) ktk masuala ya Usimamizi wa biashara, na kwa sasa anafanya kazi kama Mkurugenzi wa fedha kwenye shirika moja la kimataifa hapa nchini. Hajaoa bado, lakini ana nyumba mbili nzuri za kuishi hapa jijini. Moja Mbezi Beach na nyingine Kimara.. Ana gari 2 za kutembelea na 3 za biashara.. Anamiliki duka moja la nguo Kariakoo na jingine la simu Mlimani city.. Ni mcha Mungu, mpole na mtanashati.. Ni miongoni mwa vijana waliofanikiwa kimaisha. John ana rafiki yake aitwae Michael.. Huyu ni Afisa Mtendaji mkuu (CEO) wa Shirika moja la ndege hapa nchini. John na Michael wamekua marafiki kwa muda mrefu.. tangu utotoni.. Wamekua pamoja, wamesoma pamoja tangu chekechea hadi chuo kikuu. Hata masomo yao ya juu (masters) walisoma pamoja Marekani licha ya Michael kupata ufadhili Australia, lakini alikataa kwenda ili tu akasome na John Marekani. Walipendana kama mapacha licha ya kuwa hawakuwa ndugu wa damu.. Ukimkosea John umemkosea Michael and its vice versa.! Waliitwa mapacha walipokua shuleni kwa namna walivyopendana. Kila mmoja alimheshimu mwenzie na kila mmoja alijitahidi asimkwaze mwenzie.. Kila mmoja amefanikiwa kutokana na juhudi za mwenzie.. upendo wao ulikua wa kweli kutoka kwenye vilindi vya mioyo yao.. Walimpenda Mungu na wote walikua viongozi wa jumuiya za vijana makanisani mwao.
Baada ya kuona wamefanikiwa kimaisha John akashauri watafute wenzi wa maisha...that means waoe.. Michael akasema anahofia kuoa kwa haraka kwani anaweza kupata mke atakayeharibu urafiki wao.. Mke asiyejua walikotoka na hivyo kuleta mfarakano baina yao... Akamshauri John wasubiri kwanza hadi WAKATI WA BWANA ULIOKUBALIKA.. John hakumuelewa Michael kabisa, na akadai tayari ana mchumba na anampenda sana.. Michael akamuuliza kwa muda gani wamekuwa pamoja, John akajibu miezi 6. Michael akasema Miezi 6 haitoshi kumchunguza mwenzi wa maisha lakini John akasisitiza anampenda... Mipango ya harusi ikafanyika na Michael akachagua kuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi ya John.. Lengo lake likiwa kusimamia harusi ya rafiki yake na kuhakikisha inafanikiwa.
John akamshauri Michael "tafadhali nawe tafuta mwenzi uoe ili usiwe mpweke. Ni dhahiri sasa nitakua karibu zaidi na mke wangu kuliko wewe. Majukumu ya kifamilia nayo yatanibana, hivyo tafuta mwenzi ili upunguze upweke..." Michael akajibu "Nimemuomba Mungu anipe mke atakayenifaa.. Bado nasubiri jibu lake. Siwezi kuoa ili tu niepuke upweke,.maana ndoa ni zaidi ya kuondoa upweke.. Nahitaji mwenzi wa maisha, sihitaji mtu wa kuniondolea upweke.."
Siku moja John akiwa katoka Michael akampigia simu kuwa yupo nyumbani kwake. John akamuomba amsubiri maana yuko mbali kidogo ila atarudi. Mke mtarajiwa wa John nae alikuanyumbani kwake, hivyo John akamshauri Michael apige story na shemeji yake hadi atakaporudi. Lakini John aliporudi nyumbani hakumkuta Michael, akamkuta mchumba wake analia.. alipomuuliza kulikoni akasema Michael alijaribu kumbaka... John akawaka kwa hasira... kwa kuwa alimpenda sana mchumba wake na kwa kuwa hakumkuta Michael nyumbani akaamini maneno ya mchumba wake.Akiwa amechanganyikiwa akaendesha gari kwa kasi kwenda kwa Michael. Ile kufika akamkuta Michael kajilaza kwenye sofa.
Lakini kabla hajamuuliza chochote, akampiga kichwani na chupa ya mvinyo aliyokua ameshika mkononi... Michael akaanguka na kuzirai.. Akakimbizwa hospitalini ambako ilionekana amepata athari kubwa ndani ya kichwa hivyo alihitaji upasuaji.. John akiwa amefura kwa hasira akarudi nyumbani kwa mguu na kuiacha ile gari kwa Michael, maana alipewa zawadi na Michael siku ya birthday yake.. hivyo akamrudishia zawadi yake maana aliona mtu aliyejaribu kumbaka mchumba wake hawezi kumpa zawadi. Kwa kuwa hakuwa na gari aliweza kuingia hadi ndani bila mchumba wake kumsikia wala kumuona... Alipofika akamkuta anaongea na simu "yes Jenny nimemkomesha.. atajuta kukukataa...Nimemwambia John kuwa alitaka kunibaka, John akawaka hasira na kwenda kumfuata... najua huko ni kivumbi na jasho na urafiki wao utaisha leo shosti..." Alipomaliza kuongea na simu na kugeuka akamuona John.. Akapanick maana hakutegemea... John akamwambia usiseme lolote maana nimesikia yote. Kumbe Jenny alikua rafiki yake mchumba wa John.. Na alipenda kuolewa na Michael lakini Michael alimkataa ili kulinda urafiki wake na John.. sasa ile hasira ya kukataliwa ndo wakapanga kuwafarakanisha.
. John alipojua ukweli akajilaumu sana kwa maamuzi ya haraka aliyochukua.. akiwa mnyonge,.na majuto moyoni akakimbia hospitalini ili akamuombe Michael msamaha. Alipofika akakutana na nesi akamzuia.. John akapaza sauti huku akibubujikwa na machozi "tafadhali naomba niruhusiwe nikamuombe Michael msamaha.. Najua amepoteza fahamu na hawezi kunisikia. Lakini naamini nafsi yake itanisikia na kunisamehe kwa ukatili niliomtendea.. Ooh Michael my friend urafiki wetu wote nimeshia kukupeleka ICU..Nisamehe Michael sikujua..."akalia kwa uchungu John. Mara daktari akatokea. John kwa shauku akamuuliza "dokta Michael anaendeleaje??" Daktari akamuangalia John kwa huruma kisha akasema, "Nasikitika kukujulisha kuwa Michael amefariki dakika chache zilizopita baada ya damu nyingi kuvujia kwenye ubongo.." Kisha akaongeza "tumejitahdi kwa kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha yake lakini imeshindikana.." John akakamatwa na kutupwa gerezani anakotumikia kifungo cha maisha..
UJUMBE.!
Kuwa makini unapotafuta mwenzi wako wa maisha. Wengi huharibu mahusiano yao na rafiki zao, ndugu zao au wazazi wao kisa wameoa/kuolewa. Usiruhusu mke/mume awe chanzo cha uadui kati yako na ndugu zako, wazazi au rafiki zako. Ukiona mke/mume ni chanzo cha uadui na ndugu zako ujue huyo mke/mume ana roho ya mfarakano (spirit of confusion).
Pilli, unapopata tatizo kwenye mahusiano kuwa na subira.. Usiharakie kufanya maamuzi. Mara zote maamuzi ya haraka humgharimu mtu baadae. Ona John ktk umri mdogo wa miaka 30, anaenda kumalizia gerezani maisha yake yote yaliyobaki hapa duniani. Mali zake, elimu yake, cheo chake, heshima yake na vyote alivyovijenga maishani ni kazi bure, just for a single mistake. Bila shaka huko gerezani alipo anatamani siku zirudi nyuma ili afanye maamuzi mbadala lakini haiwezekani tena... Itz over and out..!!
Mungu akubariki unayesoma ujumbe huu. Kama umeoa/kuolewa amuondolee mwezi wako Spirit of Confusion, na kama hujaoa upate mke/mume asiye a spirit of confusion. Upate mtu atakayewapenda rafiki zako, ndugu zako na wazazi wako na kuwathamini..
Kumbuka "asiyewapenda wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini.." Hivyo muombe Mungu umpate atakayewapenda wa kwenu. Stay blessed.!!
0 comments:
Post a Comment