Search This Blog

Monday, January 2, 2023

NILISHINDWA KUMLINDA MKE WANGU

 








"Kijana mmoja alipata uhamisho kikazi kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine baada ya boss wake kufungua tawi jipya, wakati huo alimuacha mke wake ambaye ndo kwanza walikuwa na mwezi mmoja tu tangu wameoana hivyo kienyeji, yaani bila wazazi wao kufaham,, kijana yule aliyekuwa anaitwa Juma alijitahidi kumshawishi boss wake kutengua uhamisho ule lakini ilikuwa ni ngumu sana japo Juma hakujua ni kwanini, boss wake na Juma alimuongeza hadi mshahara na kumvutia zaidi Juma kwani Elimu yake ilikuwa ndogo hivyo aliona hiyo ni bahati kubwa,

"baada ya kushauriana na mkewe hatimae walikubaliana huku mkewe akimuahidi Juma angeomba uhamisho kazini kwake pia ili amfuate mume wake, Siku ya safari iliwadia huku Juma akimuaga mkewe Jacky na safari ya kwenda mkoani mwanza ikianza, Wakati akiwa ndani ya basi Juma alikuwa akimuwaza zaidi mkewe Jacky huku mara kwa mara akipoteza Furaha kabisa...

***********

"Hatimae Juma alifika kazini kwake, mwanzoni haikuwa rahisi yeye kuishi peke yake kwani alikuwa ameshamzoea sana mke wake, muda mwingi alikuwa akimpigia simu mke wake na kumuulizia kuhusu kuomba uhamisho lakini Jacky alishindwa kumpa jibu la kueleweka, Hatimae miezi mitatu ilipita Juma akapata rikizo, hakutaka kumuambia mkewe kwani alipanga kumfanyia suprise ambayo yeye aliamini ingekuwa ni suprise kubwa sana, alimnunulia nguo na maua mengi mazuri, kisha akaenda kupima afya yake kama kawaida na kukuta akiwa safi kabisa,

Kutokana na umbali wa safari wa mwanza to Dar, alijikuta akifika saa sita kasoro usiku, alichukua bodaboda na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwake huku akijihisi mwenye furaha sana na muda wote alikuwa akitabasamu kila akikumbuka anaenda kuonana na mke wake kipenzi sana ambaye wameona miezi michache tu iliyopia, Bodaboda ilimshushia hadi nje ya nyumba yake,alishangaa baada ya kuona gari ikiwa imepaki nje ya nyumba waliyokuwa wamepanga,

*******

"Juma alikuwa akimuamini sana mke wake, kwahiyo hakuwazia chochote kuhusu gari ile, alilisogelea dirisha la chumba cha mke wake ili agonge,, ila kabla hajalifikia vizuri alisikia sauti za mahaba zikiwa zimekitawala chumba kile, hapo ndipo joto la mwili wake lilipopanda na kujikuta akilegea, begi alilokuwa amelibeba lilianguka, huku Juma nae presha ikipanda na kuanguka hapohapo, kishindo cha Juma kiliwashtua Jacky na mwanaume wake ambaye walikuwa mapumziko baada ya kufika safari yao ila hawakujali sana waliendelea na raha zao bila kujua kama Juma ndiye aliyekuwa ameanguka nje,,,

"Baada ya baridi la nje, Juma alishtuka saa kumi na moja asubuhi na kujikuta chini, aliinuka na kujikung'uta vumbi huku akiyakumbuka maneno ya mama yake,

"HATA SIKU MOJA USIKUBALI KUFA KIZEMBE MWANANGU, SIYO KWAMBA MUUWAJI HADI AKUWEKEE SUMU AU KUKUCHOMA KISU BALI HATA ASIYEJALI UTU WAKO NI MUUWAJI PIA, UKIMGUNDUA ADUI YAKO NI RAHISI KUMSHINDA"

"Maneno yale yalimkaa vizuri sana akilini mwa Juma, wakati anawaza hayo ghafla mlango wa nyumba yake ulifunguliwa, roho ilimuuma alipomuona jacky akiwa ameshikwa kiuno na boss wake, cha kushangaza Jacky hakushtuka zaidi ya kumkumbatia boss wake kwa dharau huku wakifunga mlango na kuingia ndani ya gari lao, kabla hawajaondoka Juma alifungua begi lale lililokuwa na zawadi za Jacky kisha akasogea hadi karibu na gari na kuzirusha kupitia dirishani,

"Unanichafulia gari langu bhana, nyie wanaume suluari sijui mpojeee alaaah"!

Ni maneno aliyozungumza Jacky na kuzidi kumuumiza zaidi Juma ambaye aliamua kuondoka na kurudi stand kisha akapanda gari za kwenda kijijini kwao...

****

"Haikuwa rahisi Juma kumsahau Jacky wake hadi jitihada kubwa za mama yake zilipofanyika na kuamua kumpeleka mwanae mjini kwa baba yake mdogo ili kumtafutia kazi nyingine, kutokana na Elimu ya Juma haikuwa rahisi kupata kazi na alikaa kwa muda kidogo kabla hajapata kazi kama ya mwanzo ya hotel, alifanya kazi ile kwa muda mrefu huku akimsahau kabisa Jacky na kujikuta akipata mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni askari polisi,, mapenzi yao yalidumu kwa muda mrefu hadi wakapanga kwenda kutambulishana kwa wazazi wao., juma ndo alikuwa wa kwanza kumpeleka Binti yule nyumbani kwao na kumtambulisha kwa mama yake, Zamu ikafika kwa Juma kupelekwa nyumbani kwa mchumba wake huyo mpya ambaye alichukua nafasi ya Jacky, waliongozana huku Juma akivaa nguo za heshima sana hadi nyumbani kwa akina Jane, walifika nyumbani pale na kumkuta mama Jane akiwa anajiandaa kutoka, walipomuuliza aliwajibu anaenda kituo cha polisi kwani wamemkamata mtu anayesambaza virusi vya ukimwi kwa nguvu, na tayari hata mwanae ameshamuambukiza hivyo wamemshtakì, Jane aliposikia hivyo aliungana na mama yake, hivyohivyo hata Juma naye hakutaka kumuacha Jane wake muda huo, waliongozana hadi kutuo cha police ili kumuona huyo mtuhumiwa,, Moyo ulimwenda mbio Juma alipomuona boss wake akiwa ndo mtuhumiwa mkuu, aliangalia pembeni akamuona Jane akikumbatiana na Jacky huku akiita" Dadaaa" wakati huo machozi yakimtoka...

"Hapo ndipo Juma alipogundua kuwa Jane na Jacky ni mtu na dada yake,,,

"Moyo wa Juma ulienda mbio zaidi baada ya macho yake kukutana na macho ya Jacky yaliyokuwa yamevimba kwa kilio huku yakiwa yamejaa machozi, Juma alitumia muda huo kuitazama mikono ya Jacky hapo akafanikiwa kuona moja ya ua alilowahi kumchukulia kama zawadi,inaonekana ua lile Jacky alikuwa anatembea nalo kila sehemu kama kumbukumbu kwake, Baada ya Jacky kumuona Juma,alimuachia dada yake Jane na kipiga hatua akasogea hadi alipokuwa Juma,kisha akapiga magoti huku akilia kwa uchungu sana,,

"Juma baba, najua nilikuumiza sana ila haya ndo malipo yangu ya usaliti,nilishi

ndwa kuridhika na kidogo ulichokuwa unanipa na nilichokuwa nataka,ona sasa hali yangu ilivyobadilika, sina kazi,sina mali,nilipokuwa naishi nilifukuzwa baada ya kushindwa kulipa kodi,kibaya Zaidi nimepata maambukizo na nimekupoteza pia wewe mwanaume uliyekuwa na msimamo kwangu,mwisho wa yote nawatakia maisha mema ya ndoa wewe na dada yangu"

maneno yale yaliwatoa machozi wote,sio mama,Juma wala Jane, wote walijikuta wakilia kwa nguvu na kimfanya Juma kugundua lengo la boss wake kumhamisha kikazi ikikuwa ni kumpata kiurahisi Jacky alijilaumu kwa kushindwa Kumlinda mke wake,, hakuwa na kinyongo zaidi ya kumsamehe ingawa tayari sasa alikuwa kama shemeji yake na siyo mke tena,,,,

____FUNZO_____

=>We kama mwanaume unamlindaje mchumba/mke wako dhidi ya hatari kama hizi?

=>Tamaa siyo nzuri,ridhika na unachokipata kwa muda huo kwani hujui mungu kakupangia lini ridhiki yako

=>Usikubali kuuza utu wako kwa kitu.


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG