Msichana mmoja alikuwa na mpenzi wake, alimpenda sana sababu kijana alikuwa mtanashart na mcha Mungu. Malengo yao yalikuwa waje kuoana baada ya muda wa msichana kumaliza masomo yake.
Kijana huyu alijitoa sana kwa binti hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini kiukweli alikuwa anampenda sana msichana yule kwa dhati, alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauli kuhusu mipango ya maisha na alikuwa akimuombea kila alipopata nafasi ya kuomba.
Kijana huyu alijitoa sana kwa binti hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini kiukweli alikuwa anampenda sana msichana yule kwa dhati, alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauli kuhusu mipango ya maisha na alikuwa akimuombea kila alipopata nafasi ya kuomba.
Si hayo tu bali alijitahidi kumfurahisha mchumba ake kwa zawadi mbalimbali na shida pia zilizokuwa zikimkabili mara kadhaa, kijana kiukweli alikuwa amependa na alikuwa na pendo la dhati kwa binti yule.
Siku moja binti alikuwa anasheherekea siku ya kuzaliwa kwake..., hivyo akaarika ndugu,jamaa na marafiki zake akiwemo na mpnzi wake.
Wageni wote walifika kwa wakati, isipokuwa yule kijana alichelewa kidogo.., Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mchumba ake hajafika kumsifia, kwa kuweleza wale marafiki na wageni waliofika njisi kijana yule alivyokuwa mhimu kwake, akamsifia sana na akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya sherehe yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafisi yake.
Baada ya muda kijana akaingia na kuketi high table.. ,muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho kutoa zawadi. Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya msichana kumsifia sana yule kijana.
Kijana aliamka na kutoa mfuko, kila mtu alitaka kujua kilichokuwa ndani ya mfuko huo, mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate!!!!,
Lahaula... Watu wote wakastaajabu.... Mkate????!!!!!!!, lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate msichana akaanza kulia, akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemwaibisha,
Akiwa analia kwa kwikwi alimkwida shart lake na kumvua tai, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa!!!.
Masikini..... Yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota, kisha akarudi high table kwa huzuni na unyonge, baada ya kufika high table alisema maneno haya
"baby nashukuru sana kwa yote yaliyotendeka hapa huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii ya kuzaliwa, lakini kama dhahili ungelitambua thamani ya zawadi hii ndogo usingefanya haya"!!,
Baada ya kusema hayo kijana alifungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyokuwa amevificha ndani ya mkate ule, kwanza akatoa ufunguo wa gari ambalo alikuwa amemununulia mpnz wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya sikukuu ya kuzaliwa kwake!!!.
Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema " nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika khari yeyote,
Nilipanga leo nikuvishe pete hii ili kuelekea kwenye ndoto yetu ya ndoa, ila kwa kuwa uliangalia nje uliona mkate badala ya pete hii ya thamani iliyokuwa ndani, naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata, nashukuru kwa yote uliyonifanyia nimekusamehe nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza, kisha akachukua mkate wake na kuondoka, msichana akaomba msamaha lakini tayari alikuwa ameshachelewa!!!!.
MORAL OF THE STORY..!!
Usimdharau mtu/kitu kwa kukitazama nje, Mungu huangalia thamani ya mtu ndani lakini wanadamu huangalia thamani ya mtu kwa nje. Thamani ya mtu/kitu ipo ndani na si rahisi kuonekana!!,
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa mtazamo wa harakaharaka!!..., wanaokudharau leo na kukuona mkate ipo siku watagundua haukuwa mkate wa kawaida.... kuna vigi vya thamani ndani yako!!.
Wote wanakudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima!!!!,
"TUFUNDISHANE MEMA"
0 comments:
Post a Comment