Search This Blog

Monday, January 2, 2023

ALAZWE PEMA PEPONI

 




SIMULIZI FUPI - ALAZWE PEMA PEPONI





Juhudi zangu za hapa na pale za kumlaghai binti huyu aingie kwenye himaya yangu ni kama zilikuwa zimegonga mwamba, niliamini kwamba kila neno tayari nimetumia katika kamusi yangu ya longolongo nilizojifunza jijini.



Ulikuwa mfadhaiko mkubwa sana yaani nilipokuwa mjini haikunichukua muda mrefu sana kumhangaikia msichana sasa hapa kjijini inakuwaje?



"Nina mchumba wangu mjini…" ndio lilikuwa jibu lake siku zote binti huyu aliyeitwa Gift, hakuwa na uzuri wa kutisha hata kidogo lakini kwa pale kijijini aliongoza. Na mimi matamanio yangu yalinifanya nimwone kuwa ni mrembo.



"Eti ana mchumba mjini kha! mbona hata mi mjini nimefika, tena mi hadi Dar nimegusa japo kwa wiki moja tena nimemuona Diamond ambaye yeye anaishia kumuona kwenye luninga, huyo mchumba huenda mwisho wake hapo Musoma mh! Musoma napo mjini huyu mjinga nini??" ndivyo niliwaza, sikuamini likizo yangu ya mwezi mzima nimeambulia patupu yaani naondoka bila kumfaidi mtoto huyu wa kijijini.





Alikuwa mwembamba sana wa umbo lakini kifua kilikuwa kipana sijui kwa nini, miguu yake ilikuwa na dizaini flani ya 'matege tusijuane' nywele ndefu zilizoenda saluni miezi mingi iliyopita zilishikilia mamlaka ya kichwa chake ‘under sketi’ yake ilikuwa ndefu kuliko sketi aliyokuwa amevaa na kibaya zaidi kila moja na rangi yake, kiasi flani alifanana na misukule bandia tunayodanganywa kwenye magazeti ya udaku huko mjini kuwa imetolewa na wachungaji mashuhuri wanaojipa majina ya mitume na manabii huku wengine wakifikia hatua ya kujiita Miungu watu.



Licha ya yote hayo huyu mtoto kama akipata mtu wa kumpeleka saluni haki ya mama ni mzuri wewe, hivi unafahamu ladha ya binti mwenye ‘matege tusijuane’, achana na wale wenye ‘matege mbinuko’ hao hawana ladha sana kama hawa ninaozungumzia mimi.



Kweli Gift apate mtu wa kumtunza mbona asingejutia sema kwenye kile kifua ndo sielewi kama palikuwa na ujanja. Natambua wachina wana madawa ya kuongeza matiti kuhusu kupunguza.mh!!! hata sielewi!!



* * * *



Msiba wa babu yake Gift haukuwa wa kusikitisha sana kwani alikuwa anakaribia kutimiza miaka 95 umri ambao ni wachache sana kuufikia hivyo tuliamini siku zake zilikuwa zimefika. Mimi pamoja na vijana wengine pale kijijini tuliungana katika shughuli nzima ya kuchimba kaburi hadi maziko kwa ujumla. Baada ya maziko, wengine walirejea makwao, lakini mimi na kundi jingine tulirudi kwenye msiba nyumbani kwao Gift. Kwa ajili ya kuendelea kutoa mchango wa hapa na pale ikiwa kuna tatizo linaweza kujitokeza. Sisi ndio tulikuwa vijana na ule ulikuwa wajibu wetu!!



Majira ya saa nne usiku nilikuwa chumbani kwa Gift nikimfariji. Pembeni alikuwepo dada yake.



"Jamani mi ngoja nikacheze karata nje" dada yake Gift aliyeitwa Janeth aliaga na kutoka nje, pale ndani nikabaki mimi na Gift, roho ikaniambia hiyo, kama ni mpira wa miguu basi ilikuwa ni penalti dakika ya tisini, goli la pekee la ushindi, hiyo ndio nafasi iliyobaki kujaribu bahati kama kweli Gift amenizidi ujanja ama inawezekana. Nikamshukuru Janeth kimyakimya.



"Koroboi imeisha mafuta." Gift alisema baada ya kuona inafifia aliichukua akaitikisa kweli haikuwa na mafuta akawa ameirudisha mahali pake.



"Ngoja tuizime eti!" nilizuga kuuliza wakati tayari nimepuliza. Giza likatawala!!



“Mjini tanesko huku mafuta safi sana!!!” nilijisemea baada ya giza kuchukua hatamu.



Giza likachukua nafasi yake na ujasiri ukaongezeka maradufu aibu ikajificha hakika hiyo ndio ilikuwa nafasi ya kufanya uzinzi na Gift.



Gift alikuwa amelala na mimi nimekaa, taratibu mkono wangu ukapata kishawishi nikapapasa hadi nikatua kwenye mikono yake migumu iliyokomaa, bila shaka ni kutokana na kilimo cha mikono, hata hakushtuka basi nikausogeza hadi kifuani pake nikasalimiana na mzigo wa titi moja nikalinganisha na matiti ya vitoto vya Mwanza viwili ama vitatu vikiunganisha matiti yao ndo yanamfikia Gift. Nikaguna kisha nikendelea si unajua tamaa tena!!!



"Jamani Baraka kuna watu nje watatusikia, acha!!" alilalamika Gift nikacheka gizani kicheko cha kimya kimya nikayakariri maneno yake ‘watatusikia’ “Kumbe na yeye anajua kinachoendelea”, mi wala sikumjali nikapeleka na mkono wa pili weweeee! kifua kikubwa raha jamani dah! nikashangaa msimamo wangu wa kupenda chuchu ndogo ukianza kuyumbishwa na joto lililotoka pale ndani. Ulaini wake ukaitesa mikono yangu, uzito wake haukunisumbua!!!



Gift akawa anahema kwa kasi nikatamani kupanda pale kitandani lakini nikahofia aibu ya kuporomoka kutoka katika kitanda kile cha kamba. Sikukiamini kabisa japo alikuwa amenambia awali kuwa kitanda kile walikuwa wanalala watatu wakati mwingine. Imani ikagoma!!



Kwa jitihada nikamshusha hadi chini kwa kumbeba. Alikuwa mzito wewe!! Si alikuwa keshalegea!! Akiwa bado hoi nikaupeleka ulimi wangu masikioni mwake bila kujalisha ameyasafisha masikio yake au la!! Gift akatoa milio ya mtu mwenye kifafa ambaye yupo katika hatua za mwisho kupoteza fahamu, nikautoa ulimi sikioni nikahamishia kwenye shingo yake iliyokuwa na ladha ya chumvichumvi kutokana na jasho la kutwa nzima katika harakati za maziko, hata sikuhofia chumvi hiyo kwani nimeshazama chumvi kali kuliko hiyo tena si mara moja wala mbili, watoto wa Mwanza si ndio burudani yao. Chumvi hiui haikunitisha!! Nikainyonya!!!



Wamenifundisha tabia mbaya hao!!! Niliwawaza watoto wa Mwanza nikawahukumu!!!



"Mamaaaa mamaaaa" alipiga mayowe kwa nguvu, nikakurupuka pale lakini sikuweza kutoka alikuwa amenishikilia bila shaka alikuwa anataka huduma yangu. Nilijivuta ili nitoke lakini wapi Gift sijui hata alikuwa amezitoa wapi nguvu zile.



"Acha kulia Gift eeh" nilibembeleza kwa uoga, lakini Gift aliendelea kulalamika kwa sauti ya juu, kelele zilifika hadi nje, hofu ikanitawala sana nilikuwa naenda kuaibika msibani sasa mtoto wa kiume mimi.



Watu wakaanza kulia huko nje wakiamini Gift anamlilia marehemu babu yake. Laiti kama wangejua tiba ya kilio chake nadhani pangekuwa hapatoshi.



"Jamani Gift ukilia utakuwa unakufuru sasa imetosha tumwombee babu ALAZWE PEMA PEPONI" nilizungumza hayo kwa sauti ya juu huku nikitoka nje baada ya kujinasua mikononi mwa Gift… nikimuacha Gift akiwa ndani analia kwa uhitaji tayari alikuwa ameiondoa kanga yake akabakia na mchupi mkubwa uliokuwa umelegea kiunoni, watu wakaingia kumbembeleza baada ya kuwa wamesikia maneno yangu yaliyowachoma. Mimi tayari nilikuwa nje, hamu zote zikiwa zimeniisha.



Sikuamini nimekwepa aibu hiyo japokuwa nilishindwa kutimiza lengo langu la kumfaidi Gift.Kesho yake nikaondoka asubuhi na mapema kurudi shuleni na kurudi hapo kijijini sikutamani tena.



Maana waliyoyakuta huko ndani walijua wao wenyewe mi sitaki kujua.





MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG