SIMULIZI FUPI - MSIBA ULIVYOMUUMBUA SISTA DUU
Usingethubutu kumtongoza kirahisi rahisi kamahuna roho ngumu!! Alikuwa haoni hatari kukutukana hadharani na kukuandikia STATUS…. Kilichompa jeuri ni kwamba alikuwa anakubalika sana. Akiweka status wanaume wanaishobokea sana wanamsifia.
Lakini bila kificho alikuwa ni mrembo sana!! Sio kwenye picha zake pekee bali hata waliopata bahati
ya kuonana naye ana kwa ana walikiri kuwa Neema alikuwa msichana mwenye mvuto wa pekee.. Alijua
kupangilia nguo na zikaifanya shepu yake ionekane vizuri. Alijua kutembea haswaa!!
Kubwa zaidi alikuwa anajua kutafuna wakati wa kula chakula, achana na wasichana wengi ambao ni
warembo na bado wakiwa wanatafuna chakula wanaacha midomo wazi. Neema alikuwa ana kitu
kingine cha ziada. Alikuwa anajua kutabasamu!!! Na kama angeamua kucheka basi alikuwa hachoshi
kumtazama. Nayasema yote haya kwa sababu na mimi nilipata
nafasi ya kuonana naye!! Kabla ya kuonana naye nilitumia zaidi ya akaunti
nne kumtongoza!! Nililazimika kutumia akaunt tatu tofauti kwa sababu Neema alikuwa ananiblock katika
account nyingine, Neema hataki maswali ya kijingajinga eti una miaka mingapi, sijui unaishi na
nani? Neema anapenda maongezi ya moja kwa moja we kama huna jipya basi achana naye. Ukimkosoa
katika Status yake anakublock, ukijishaua kumwandikia ujinga kwenye WALL anakublock!!
Neema alikuwa Neema kweli. Akaunti ya kwanza nilijifanya mi najua kushauri,
alikuwa anatukanana na mtu nikamfuata inbox nikamwandikia, “Neema acha hizi mambo we kwa
urembo wako haupendezi ukitukana” baada ya dakika tano nikaingia inbox. He! Nikashangaa
Neema ametoa picha ama? Maana hapakuwa na picha. Mbona jina la Neema limekuwa jeusi!!
Hapo ndipo nikapata fursa ya kuusoma ujumbe… “We mwehu nini, nenda ukamshauri baba yako
ajiunge facebook labda ndo anaweza kunishauri sio uchafu kama wewe” Wacha nipagawe!! Nikataka
kumjibu nikaambiwa haiwezekani. Neema alikuwa ameniblock!!!
Si unajua tena mwanaume hakubali kushindwa!! Nikaona nimedhalilishwa sana, nikafungua akaunti
nyingine, hapa sikuweka picha nikamuADD Neema akanikubalia, nikajiunga na Team ya kuLIKE, kila
annachoandika Neema mi naLIKE huku nikimsifia hata ujinga. Nikimfata inbox namsifia status zake
Hapa tukawa marafiki tena!! Si nikawa na haraka nikaanza kumtongoza Neema kitoto, eti ooh mara
nimwandikie usiku mwema baby!! Mara morning lovely one!!
Neema akashindwa kunivumilia akaniandikia bonge moja ya status…halafu akanitaja kabisa.
Ninachoshukuru sikuwa natumia jina langu halisi.
Baada ya hapo akaniblock. Sikukata tamaa
nikafungua akaunti ya tatu. Huku sasa sikuremba nikayafuatilia maisha ya Neema nikagundua kuwa ni
mtoto wa kidosi kwao kuna pesa. Nami nikaingia kipesa pesa. Post nyingi za Neema alikuwa
akiandika mara: “@Home sweet home watching movie!”
“@Samakisamaki” “Oh! At Maisha club jamani Diamond mchokozi
huyu!!” “Anyone around nipo kitanda cha sita kwa sita
alone!!” Nikagundua kuwa alikuwa mtoto wa kishua haswa!!!
Hatimaye nikafanikiwa kukutana na Neema kwa mara ya kwanza, Blue Pearl hotel Ubungo. Hapa
ndipo nikajua kwa nini Neema anaringa!! Alikuwa mrembo haswa na kama nilivyosema awali alikuwa
na vitu vingi ambavyo wasichana warembo hawana hasahasa jinsi ya kutembea maana warembo
wengine wanatembea kibabe kama wanyanyua nondo!! Neema alijua jinsi ya kuibana miguu yake
kisha ikaunda herufi kama V. mapaja yake manene yalikibeba kiuno chake vyema.
Baada ya kukutana ndipo nikaanza kuwa nawasiliana na Neema mara kwa mara. Japo
nilikuwa sijawahi kufika kwao lakini kwa mazungumzo yake nilifika kimawazo. Mara nipo na
fundi wa kutengeneza AC…..yaani msumbufu huyooo!!! Mara yupo na daktari wa mifugo ng’ombe
wao anaumwa Mara anaelekea airport kumpokea baba yake. Hapa nikamuuliza akaniambia baba yake
anafanya kazi uingereza. Nikamuuliza pia kuhusu mama yake akadai ana
saluni kubwa ka kike Kampala. Sasa hapa Neema akawa akiniomba hela ya vocha natuma elfu tano
hadi kumi. Tukitoka naye najiandaa na laki mbili na ziada!!!
IKAFIKIA SIKU YA SIKU!!
KWANZA nilishangaa kuna wadada wawili
walimuandikia Neema neno POLE katika WALL yake, lakini ghafla sikuona tena ile post na wala Neema
hakuwajibu!! Mchana tena kuna wavulana wawili wakamuandikia maneno ya kumpa pole. Uzuri
mmoja alikuwa rafiki yangu!! Nikamnukuu jina ‘CHIDY Boy Wa Mbinga!!!’ ile narefresh tu page
nikakuta Neema amefuta zile post!! Nikashangaa kulikoni!! Mara akaweka post kuwa ‘ambaye anajua jinsi ya kufunga WALL please anisaidie!!” baada ya dakika kumi WALL ya Neema ilikuwa imefungwa!!!
Nikajiuliza kulikoni!! Lakini sikumuuliza maana Neema hataki kuulizwa mambo yake ya facebook,
ukimuuliza anakwambia ‘sisi ni wapenzi tayari mambo ya facebook ya nini?’ ukiangalia kweli.
Unaacha!! Upesi nikamtumia meseji Chidy, nikamuuliza
unampa Neema pole kwa nini. CHIDY: ah amefiwa na baba yake bwana huyo
demu!!! MIMI: Baba yake? Lini. CHIDY: Jana usiku kaka kwani vipi?
MIMI: aah hamna kitu lakini vipi unamfahamu vizuri!!
CHIDY: hamna kaka simfahamu vizuri ila kifacebook tu!! Sema kuna watu wanasema anakaa
Mwananyamala kisiwani. Tukachat sana na Chidy hadi naye akaniambia kuwa
aliwahi kumtongoza na amemlia pesa zake kweli. Nami nikawa muwazi nikamueleza kuwa ni mpenzi
wangu japo sielewi kwanini ananificha kuhusu msiba. Mimi na Chidy tukakutana na kuamua
kufuatilia kwanini huyu Neema anaficha jambo la muhimu kama msiba. Safari yetu ikaishia
Mwananyamala Kisiwani. Tukaanza kuulizia wapi kuna msiba, kwa sababu
tuliamini kwa kuwa Neema ni mtoto wa kishua basi hata msiba ule utakuwa kama harusi kubwa!!! Mimi
nikiwa na lengo la kumfanyia surprise mpenzi wangu!! Baada ya kuulizia tukapata misiba miwili,
mmoja wa mtoto mdogo na mwingine wa Fundi viatu maarufu. Hapakuwa na msiba wa mtu kutoka
nje wala!! Mh!! Tukashangaa ina maana haijajulikana kama kuna msiba au??
Hapa sasa tukaamua kwenda kwenye huo msiba wa Fundi viatu, Chidy alishauri. Kweli tukafanikiwa
kufika, tukakuta watu wachache kiasi, Chidy alikuwa amechafuka na matope tayari kutokana na njia
mbaya tuliyopita. Si unajua tena uzuri wa surprise, hakikisha unayemsurprise hakuoni kabla wewe
hujamuona.
Sisi tukaanza kuuliza ni nani amefariki, tukaambiwa baba mwenye nyumba.
Mh! Chidy akaninong’oneza. “Hapawezi kuwa hapa kaka!!” nami nikakubali tena.
Tukauliza jina la marehemu, wakasema ni mzee Peter.
Akili ikakimbia upesi. Neema anajiita facebook “Ney Petersonn Daughter”
He!! Sasa inawezekana akawa ni baba yake Neema kweli ama!!
Wakati hu ulikuwa unapita mchango kwa ajili ya jeneza, hali ilikuwa tata na umasikini ulinukia eneo
lile. “Chidy eeh tubaki hapa hadi kieleweke!!”
Tukaamua kubaki!! Mara kwa mbali nikasikia mlio. “Chidy, simu ya Neema hiyo nilimnunulia inaita…
Chidy ni hapa.” Mara akatoka nje Neema ninayemfahamu, alikuwa peku na kanga imechakaa!!
Kichwani amejitanda kilemba. “We Chimodoi wewe!! Chimodoi nitakubamiza na hicho kisimu chako
nasema!!” mwanamke mmoja wa makamo alimkaripia Neema. “Mama si ninapokea mara
moja.” Akajibu Neema. Mama yangu weee!! Kumbe ndo kwao Neema hapa!! Sasa alikuwa anajikweza
nini maskini weee!! Sisi tukapiga picha kadhaa, nyumba na mazingira!!! Hatimaye mwili ulifika, kwa
ajili ya kuagwa!!! Hatujui nani alinunua jeneza!! Neema alipomaliza kuaga ndipo tukauvunja
ukimya..yaani kwa jinsi alivyotusumbua kumbe maisha duni kiasi hicho alaa!! Tukamfikia,
nikamgusa bega akageuka!! Aisee hadi leo sijui kama aidha aligongwa na gari huko alipokimbilia,
hatukjui kama labda alipatwa na uchizi kwa mshtuko ama vipi. Lakini alitimua mbio ambazo
sijapata kuona msichana akitimua!!! Aliteleza mara moja akaanguka akasimama kisha akatoweka hadi
leo ninapoandika simulizi hii…. Nilitamani sana kumkimbilia Neema lakini nikahofia kuandika hadithi
ndefu ikakuchosha kusoma ewe rafiki yangu!!!
SOMO:
Jikubali maisha yako yalivyo ndugu…kama
unalala chini sio lazima utwambie lakini basi usidanganye. Misiba inaumbua nyie, usidanganye
kwenu mambo safi kumbe kapuku sisi tukija msibani hatutaangalia kama upo katika machungu
tutakuuliza tu!!! Utuonyeshe yale magari sita, utuonyeshe ile bustani ambayo huwa unasema ni
kwenu, utuonyeshe na geto lako lenye kiyoyozi!!! Mnapiga picha nyumba za kulala wageni mnaandika
HOME SWEETv HOME....Shauri zenu!!
MWISHO!!!
0 comments:
Post a Comment