SIMULIZI FUPI: TIBA MBADALA
Dunia ilianza kugeuka taratibu, ikaanza kupandisha miguu juu huku na kichwa chini na hapo hapo ikilazimisha kutembea kwa kutumia hicho kichwa.
Tabasamu langu likaanza kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia za mume wangu tuwapo ndani na hata nje ya chumba chetu tulichokipachika jina la bustani ya Edeni wakati wa siku zetu za furaha.
Sasa siku hizo zilikuwa zimetoweka na chumba kile kugeuka kuwa tanuru la moto lisilofuka moshi wa aina yoyote ile.
Faki alikuwa amebadilika sana, ama nisiseme kuwa alikuwa amebadilika maana watu wote walisema kuwa yupo kama alivyokuwa siku zote.
basi alikuwa amenibadilikia mimi vibaya mno.
Kila jema nililojaribu kufanya likawa baya kwake, nikipika chakula kizuri atapambana awezavyo kukitoa kasoro. Na alizotoa kasoro hizo kimasimango katika namna ya kuniudhi mimi.
Nilipohoji kuna nini kinatokea alinieleza kuwa nimepika vibaya nijirekebishe.
Nikienda kurekebisha nywele zangu, labda niweke rasta. Usiku anatandika shuka chini analala, nikiuliza kulikoni anaanza kuzisimanga nywele zangu, mara anadai zinamuumiza mara anishangae mimi ni mwanamke wa aina gani nimejitandika marasta kichwani kwangu angali ni mazito sana.
Nilistaajabu hii haikuwa mara ya kwanza kuwa na rasta katika kichwa changu, iweje basi leo hii zilete matatizo katika ndoa yangu?
Niliumia sana, na kulipopambazuka nilizitoa rasta zile ilimradi tu kumfurahisha mume wangu niliyempenda sana.
Lakini hata hii haikuwa tiba muafaka juu ya hali ilivyokuwa inaendelea pale ndani.
Wasiwasi ukaniingia kuwa huenda mume wangu amepata mwanamke mwingine huko nje anayemsumbua kichwa ama kumpagawisha zaidi ya nilivyokuwa nafanya mimi.
Nikajaribu kuipigana vita hii kwa kuhamishia vita hii chumbani, nikapanga kupambana kwa ujuzi wangu wote ili nimzidi huyo mwanamke kahaba anayetaka kunipotezea mume wangu.
Siku hiyo nikakiandaa chumba vyema, nikakitandika kitanda vizuri kwa mashuka mapya na nikapulizia utuli uliokuwa na harufu ya kuvutia pua ambazo ni timamu.
Alirejea usiku majira ya saa nne, nikampokea kwa bashasha nikiwa na kanga yangu moja, nikamkokota hadi chumbani.
Alipofika akakishangaa chumba, nikadhani nimemkamata tayari nikajipongeza.
Ghafla akaniuliza ni kitu gani nimepulizia pale ndani kinatoa harufu ya kukera namna ile.
Nilichoka!
Hakuishia hapo akaanza kuninanga kuwa anashindwa kuelewa mimi ni mwanamke wa aina gani..... Akanisema kwa mambo mengi huku akionyesha wazi kukerwa na kile kilichotokea.
Kama masihara vile akachukua shuka na kwenda kulala sebuleni katika kochi.
Nilipagawa sana, nililia mno huku nikijiuliza ni wapi nilipomkosea mume wangu hadi amenibadilikia namna hii.
Hakutaka nimguse na alikuwa anahema juu juu mithiri ya simba anayekaribia kurarua windo lake.

Nilijaribu kutega mitego yangu nje ya nyumba ili nimjue mpinzani wangu na kisha kukabiliana naye ana kwa ana baada ya vita hii ya chumbani kugonga mwamba.
Mafanikio hayakuonekana, sikumjua adui yangu anayetaka kuniharibia ndoa yangu.
Nikajaribu kumshirikisha mama yangu mzazi ambaye ndiye pekee ninayemuamini kumueleza mambo yangu ya siri kubwa. Akashangaa sana lakini akanitia moyo kuwa nisichoke kupambana huenda kuna kitu niliwahi kumkosea nikitafute na kisha nipige goti kumwomba msamaha.
"Usije ukafanya makosa mwanangu ukaanza kujibishana naye huwezi kujua huenda kuna kosa umefanya na haujaligundua, jichunguze na ubadilike " Mama alinisihi kwa upole.
Nikaaga huku nikiwa sijaipata amani ya moyo hata kidogo.
Faki wangu alikuwa katika hatihati ya kunitoka katika himaya yangu.
Kila siku aliibuka na kisanga kipya, leo ananisema nimezidisha mafuta kwenye mboga, kesho yake nisipowekamafuta analalamika kuwa ndani kuna mafuta lakini ninakuwa na roho ya kimasikini ninaweka kwa kubania.
Nilichanganyikiwa sana!
Nikafuatilia kazini kwake huenda kuna jambo halipo sawa.
Nilipofika nikaambiwa siku tatu zilizopita alipokea zawadi kwa kuwa mfanyakazi bora na makini sana.
Nilikata tamaa!
Mtu hatari namna hii katika nyumba yake anawezaje kuwa mfanyakazi bora tena anayeitwa makini?
Nini kilikuwa kimemsibu Faki wangu?
Kila nilipotaka tuzungumze juu ya mahusiano yetu yanavyoelekea alikuwa hasemi maneno mengi badala yake alinisihi nijitahidi nibadilike.
Sasa nitabadilikaje bila kuelezwa bayana ni wapi nibadilike?
Niliteseka sana.......
Nilijaribu kuwatembelea rafiki zangu na kuwaomba wanieleze madhaifu yangu yote ambayo huenda ndo chanzo cha Faki kunibadilikia, walijaribu walivyoweza na mwisho waliishia kusema kuwa mimi ni mwanamke ambaye kila mwanaume angetamani kuwa naye.
Walisema kuwa nina tabia njema na sina tamaa halafu kubwa zaidi ni mstahimilivu.
Sasa Faki anataka nini jamani? nilijiuliza.
Kitandani hanitaki, katika meza ya chakula ananikosoa, katika mavazi ananisema.
Nilishindwa kufanya makisio ya jambo jipya nikabaki kuwa mtu wa kulia pindi Faki akiwepo ama asipokuwepo.

Ikafikia kipindi Faki akaagizwa kikazi kwenda mkoani, alinieleza kwa ufupi sana siku mbili kabla nimwandalie nguo anakaribia kusafiri. Akanitajia siku ya kusafiri.
Nikafanya kama alivyohitaji....
Usiku wa mwisho kabla hajasafiri akazikagua nguo.
Siku hii tukashiriki katika kisanga kipya, akaanza kunihoji nimeanza kujifunza kunyoosha nguo nikiwa darasa la ngapi, akaniuliza ikiwa nguo kwa ajiri ya safari ya kikazi nazijua.
Hakunipa nafasi ya kupumua akanisema sana. Nikalia hakunibembeleza.
Siku hii tena hakulala na mimi chumbani, akalala sebuleni na begi lake la safari huku likiwa na nguo zilezile alizonisema nazo.
Alfajiri nikausikia mlango ukifunguliwa.
Faki hakuniaga akasafiri!
Nilichanganyikiwa, nikahisi huenda si safari ya kikazi ananitoroka.
Nikataharuki kwa kujiona napoteza mume wangu wa ndoa dhidi ya malaya nisiyemjua.
Nikatoka mbiombio na nguo zangu za kulalia. Nikasema liwalo na liwe namfuatilia hivyohivyo hadi nijue anaelekea wapi?
Nilipotoka sikwenda hatua nyingi nikamwona naye anarudi, sijui kuna kitu alikuwa amesahau??
Nikajiuliza...
Alikuwa anatembea taratibu, hakuonekana kama mtu aliyesahau kitu.
Aliponiona akasimama, nilikuwa nalia sana na hakika nilikuwa nimechanganyikiwa.
Akaifungua mikono yake akaliacha begi lianguke chini.
Mikono ile iliashirikia alihitaji kunikumbatia....
Sikuamini, akatoa tabasamu.
Nilikuwa nimekosa kuliona kwa muda mrefu sasa, leo ananionyesha tabasamu? Nilistaajabu.
Akaniita kwa jina langu na kisha akamalizia kwa kusema 'Mke wangu kipenzi'
Moyo ukapiga kwa nguvu, Faki amebadilika?
Nikasogea huku siamini.
Akanikumbatia na kisha akanibeba katika mikono yake.
Akaanza kuniimbia nyimbo ya mapenzi ya enzi hizo iitwayo 'EMBE DODO'.
Tukaingia hadi ndani hakuniweka chini akaanza kuongea huku akionyesha furaha.
"Mpenzi.... ninakupenda sana. Sijawahi kukusaliti hata Mungu ananiona, sijawahi kukusema vibaya kwa mtu yeyote yule, halipo baya la kukusemea.
Unanikosha katika pande zote za nyumba yetu na hata nje ya hapo.
Baada ya kutambua kuwa wewe ni wangu na nikatamani uwe mimi ninavyotaka sikuwa na haja ya kwenda kuzurura huko nje kutafuta mwingine. Bali nilitakiwa kukuunda uwe ninavyotaka na moyo wangu uzidi kufurahi.
Ujue ilibaki kidogo tu nianze kuwa mpumbavu ninayelalamika kwa marafiki kuhusu mke wangu, lakini sikuuvuka mstari huo ili niwe mpumbavu. Nilisimama imara nikasema nguvu ya mabadiliko ipo katika mkono wangu, nikaamua kuitumia njia hiyo na imefanikiwa.
Suzana mama.... manyamanyama yako yalikuwa yananichukiza, nilijaribu kukwambia tuwe tunafanya mazoezi ukawa mbishi, uache kula vyakula vya mafuta ukakaidi, nikasema nitapambana uwe ninavyotaka. Nimefanikiwa....
Hakuna cha kuzidisha chumvi, hakuna cha rasta zinaniumiza, hakuna cha marashi yananukia vibaya, yote yaliyokuchanganya jibu ni hakuna.........
Zamani ulikuwa kibonge hata kukubeba kwa mahaba ya dhati kama hivi ilikuwa haiwezekani, sasa unaona raha ya kubebwa unaona kashepu kalivyoonekana vizuri, bila mimi nani angekupunguza hivi???" Alimaliza na kuanza kucheka, sikuwa naamini, nilikuwa nalia lakini hayakuwa machozi ya uchungu bali furaha.
Faki alikuwa wangu na akanieleza kuwa ni wangu zaidi ya niwezavyo kudhani.
Nilimkumbatia kwa ngiuvu, akajitoa katika mikono yangu na kuuendea mzani mdogo tuliokuwa tunaumiliki.
Akaniambia nisimame juu ya mzani.
Mungu wangu! nilikuwa nimepoteza kilo kumi na sita.........
Akaniongoza katika kioo chumbani, nilikuwa nachekacheka kama mjinga nikikosa neno sahihi la kumpa mume wangu.
Akanionyesha katika kioo kiasi gani nilikuwa nimependeza, akafungua begi lake na kisha akaitoa nguo mpya ya kike.
Akanisihi niivae kisha nijitazame.
Hamadi!! nilipendeza sana.... nilijua bila kusifiwa na yeyote nilikuwa nimevutia katika namna aliyohitaji Faki!
Nilipomaliza kujisanifu nikalitoa vazi lile.
Faki hakutaka nirudie kuvaa zile nguo za kulalia, akanibwaga kitandani huku nisijue ni muda gani naye alichojoa nguo zake.
Umeme ukakatika na kilichotokea kizani hakikuhusu wewe bali mimi na Faki.
Hata mwanga uliporejea sikuwa na neno la kumweleza Faki ambaye alijibatiza daktari anayetibu kwa kutumia TIBA MBADALA!!

Ngoja nimalizie hapa, kuhusu kama mwili ule ulirudi tena? Hayo ni yajayo si ya sasa.....
MWISHO!!!
0 comments:
Post a Comment