Jamaa mmoja alielekea sokoni kununua kondoo Kwa ajiri ya sikukuu ya Iddy. Pindi alipokuwa akirudi nyumbani,kondoo wake akakimbia. Yule jamaa akamfukuzia mpaka yule kondoo akaingia katika nyumba moja ya mama mjane mwenye watoto yatima. Baada ya watoto kumuona kondoo kaingia ndani, wakafurahi na kuanza kuimba: [emoji207]Kondoo wa eid ! kondoo wa eid ! kondoo wa eidi !. Mama yao alikuwa chumbani, akawajibu wanae: Hakuna kondoo wa eid. Muhusika wa kuwanunulia kondoo wa eidi hivi sasa yupo mchangani.{Akikusudia baba wa watoto hao aliye fariki na kuwaacha watoto na mke}. Pindi yule mama alipo toka sebuleni,kweli akakuta kuna kondoo na watoto bado waendelea kushangilia. Ghafla yule jamaa mmiliki wa kondoo akafika katika nyumba ile, akapiga hodi na kukaribishwa. Lengo lake lilikuwa ni kumchukua kondoo wake aliye mkimbia. Lakini kutokana na hali halisi aliyo ikuta kwa watoto wale, Kwanza kabisa nyumba yao ilikuwa ikionesha ya kwamba wahusika ni fukara mno,lakini vile vile furaha waliyo kuwa nayo watoto wale , ilimfanya yule jamaa awaonee huruma watoto wale na kujisikia aibu kumchukua yule kondoo !!! Akamwambia yule mama: Hii ni sadaka yangu kwenu, Kwa ajili ya Eid. Yule mama akafurahi sana na watoto wake kwa kupata kitoweo cha iddi. Yule jamaa ikambidi arudi nyumbani kwake na kuchukua fedha nyingine, ili aweze rejea kwa mara nyingine sokoni na kununua kondoo wa iddi.
Baada ya kufika sokoni, akakuta kuna gari ndio inashusha kondoo wengine. Akasubiri mpaka walipo maliza kuwashusha wale kondoo. Baada ya hapo akaanza kuchagua kondoo munasibu kwa ajili ya iddi. Kuna kondoo mmoja alipendezwa nae. Lakini alikuwa ni mkubwa na kanona kulikoni kondoo wa mara ya kwanza. Kutokana na hivyo akawa na khofu,je fedha yangu niliyo nayo itatosha kumnunua
kondoo huyu??? Wacha nimuulize muuzaji.
Mteja: "Ebwa ee kondoo huyu ni kiasi gani?"
Muuzaji: "Hebu chagua vizuri,ndiye uliye ridhika nae?."
Mteja: "Naam nimeridhika na huyu, Anauzwa kiasi gani?"
Muuzaji: "Kondoo huyu nitakupatia bure, Kwani baba yangu aliniuSia ya kwamba, Pindi nitakapo fika sokoni na hawa kondoo,Mtu wa kwanza kuchagua kondoo nisimuuzie, bali nimpatie bure ikiwa ni sadaka !!! kutokana na hivyo kondoo huyu ni bure kwako,hongera ndugu yangu."
Jamaa akarudi nyumbani na kondoo wake akiwa na furaha ya hali ya juu.
FUNDISHO!!!
[emoji841]Hivi ndivyo yalivyo malipo ya wema na sadaka,malipo yake huwa si yenye kuchelewa.Tatizo ni kwamba sisi wanaadamu Baadhi ya nyakati huwa hatuyahisi malipo hayo.
[emoji841]Sadaka hizo hazito punguza katika mali zetu, bali itakuwa ni sababu ya kuongezeka mali zetu
[emoji843]Kumbuka kutoa ni moyo si utajiri[emoji843]
MWISHO
0 comments:
Post a Comment