Search This Blog

Sunday, January 1, 2023

MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO

 






SIMULIZI FUPI : MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO



Kulikuwapo na mama ambaye alikuwa na kijana mmojatu, kijana ambaye mama alitokea kumpenda sana harikadharika kijana naye kumpenda mama.



Lakini kutokana na mihangaiko ya maisha iliwapelekea wawili hawa mtu na mamaye kuishi mbalimbali. Kwakuwa mama alijitahidi sana kumsomesha kijana kwa bahati nzuri kijana alipata kazi na kwenda kuishi mjini huku mama akiwa kijijini. Hata hivyo umbali wao wala haukuwafanya wajisikie wapweke sana kwakuwa kijana alijitahidi sana kuwasiliana naye . Faraja ya mama ilimtengenezea maisha yenye furafa kijana wake kwa kiasi kikubwa akiwa mjini.



Baada ya muda Fulani kupita mama alianza kutengeneza dukuduku moyoni kwakuwa kila anapohitaji pesa za matumizi kwa mwanaye basi lazima aanze yeye kumueleza mwanaye kuwa anashida ya pesa. Utu uzima ni dawa, mama alikuwa katika misingi hiyo. Kabla ya kumueleza shida zake alikuwa anaanza kutumia utuuzima wake kwa kumuulizia hali ya maisha aliyonayo kijana wake mjini. Kila asikiapo kijana wake akilalamika kuwa mjini maisha ni ya ghari kwakuwa kila kitu kinanunuliwa hadi maji ya kupigia mswaki, mama hakuwa na nyongeza.



Kitendo kile kilimfanya mama alifute dukuduku lile, huruma ilimjaa juu ya mwanaye alitamani hata baadhi ya nyakati yeye awe anamtumia pesa mwanaye ila tu hakuwa na uwezo huo. Mahitaji ya mama hayakuwa makubwa sana pale nyumbani ila alikuwa anayakosa. Hakuweza kumueleza mwanaye shida zake kutokana na huruma aliyonayo juu ya mwanaye(wakina mama wengi ni wazito sana kueleza shida za pesa kwa wanao tofauti na wakina baba). aliamini wazi ingawa anafanya kazi ila bado anaishi kwa shida kutokana bado anajijenga kimaisha pili maisha ya mjini yanagarama sana. Aliendelea kumuombea mwanaye mafanikio.



Wakati mama akiwaza hayo juu ya kijanaye, kumbe mambo yalikuwa tofauti kidogo. Siyo kwamba kijana alikuwa hapati pesa kabisa za kumsaidia mama yake, rahashaa, bali pesa alikuwa anazipata ila hazikuwa nyingi kama alivyokuwa akihitaji. Kijana alikuwa mzito sana kumsaidia mama yake siyo kwa nia mbaya bali aliona siyo jambo zuri kumtumia mama pesa kidogo kidogo. mfano akimtumia mama yake Tsh.10,000/= ndani ya siku chache atatakiwa amtumie tena, kwake hakupendezewa na hilo.



Kijana hakuwa na mawazo mabaya na mamaye,alichokifanya ni kuanza kuwekeza pesa kwa njia mbali mbali mfano kuweka kibubu na kutenga mshahara aliokuwa akiupata, lengo ni kwenda kumuridhisha mamaye kwa mpigo (surprise).



Maisha yalisonga, kiajana anazidi kujiwekeza huku upande wa pili mama anazidi kuteseka.taarifa ilimfikia kijana kuwa mama yake anaumwa. Aliamua kufunga safari na kwenda kumuona. Ingawa alikuwa anaenda kumjulia khari lakini pia alichukua kiasi chote cha pesa alichojwekeza kwa muda mrefu na kufanya maandalizi ya nguvu kwaajili ya mamaye. Kiasi kingine cha pesa aliendanacho kwa lengo la kwenda kutatua shida ndogo ndogo.



Alipokwisha kufika matarajio yake yalikuwa tofauti sana. Badala ya kumjulia khari mamaye ambaye alikuwa akiumwa bali alifikia kuuaga mwili wa mamaye . tayari alikuwa ameshaaga Dunia. Ilimuuma sana kijana, alilia kwa uchungu huku akijilaumu kwa mengi juu mamaye ambaye walipendana sana.siyo sili kina alimpenda sana mama yake na alikuwa anatamani sana amfurahishe mama yake, hivyo moja ya njia sahihi ya kumfurahisha mama yake aliona ni ile ya kujiwekeza na kumfanyia Surprise. Kila alipokuwa akilia aliweza kuzungumza maneno machache sana “MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO”.



MWISHO.



********

FUNDISHO.

Vijana wengi wa sasa tunaishi maisha ya namna hiyo, maisha ya kudhani mama/mzazi anahitaji kikubwa ndipo aridhike. Tunaishi kwa mfumo wa mwisho wa mwezi ndipo nimuwezshe mzazi.



Vijana, sawa maisha ya sasa ni magumu. Lakini ukichunguza kwa kina mama aliyeko kijijini hana mahitaji makubwa kiasi kwamba wewe ukashindwa kuyamudu hadi ukajiwekeza kwa muda mrefu. Usione aibu wala usione kazi kumtumia mama yako ulichonacho. Sikuzote kidogo ukiwanacho, kwa asiye nacho ni kikubwa. Wazazi hasa wa kijini wanajitahidi sana kubana matumizi, Tsh.5000 utakuta anatumia hata wiki mbili. Sasa wewe unataka ujiwekeze hadi ifike laki sita ili atumia miaka?. Wengine utakuta anapesa kidogo ya hakiba, anawaza kumpa mama haimtoshi ila kwenye starehe anaenda kwa pesa ile.



Mfanye mama yako ni sehemu ya furaha yako,kama huna basi muombe sana Mungu upate, ila kama unacho usiseme hicho ni kidogo mama atakidharau. Mpe ulichonacho kisha jitume na kumuomba sana Mungu ili kesho upate kikubwa zaidi ya hicho na utamfanyia hiyo Surprise unayopanga kumfanyia mama yako.



Nimemtumia sana mama kwakuwa ndiye mhangaikaji mkubwa ndani ya nyumba. Binafsi nimepitia maisha ya U- bachelor , nakiri kuwa hamna kazi ngumu katika kuhakikisha unakula na kushiba kama kutafuta mboga. Hivyo kidogo unachokiona wewe, mama kwake kitatatua lile tatizo gumu la kupata mboga hakika atakuwa na furaha sana.



Ninaimani vijana wenye tabia hii ya kuwasahau wazazi wetu na kusubiri tupate pesa nyingi ndipo tuwakumbuke tupo, tukiendelea nayo tabia hii tutakuja kuwakumbuka Maiti. Siyo kwamba hatuwapendi wazazi wetu, tunawapenda sana ila kumfanya mama awe anatabia ya kukuomba kila mara kwako, wala siyo nzuri kwani huyo hajawa ombaomba. Alikusomesha au alikuwezesha sasa unajitambua unatakiwa utambue na wajibu wako kwake.TUBADILIKE



MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG