Siku moja baba mmoja alikuta gari yake aina ya Hammer nyeusi,,ikiwa imechorwa chorwa kwa jiwe,, aliyefanya hivyo ni mtoto wake. baba huyi alipatwa na hasira sana na kuamua kupiga vidole vya mwanawe mpaka akaumia na baadae akampeleka hospitali. Lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi daktari akasema kuwa hakuna uwezekano ila ni kuvikata tu hivyo vidole. Basi mtoto akakatwa vidole vyake vyote. Sasa akiwa wodini amelazwa na anaendelea na matibabu akamuuliza baba yake swali lifuatalo. " eti baba hivi vidole vyangu vitaota tena vingine?" Baba badala ya kujibu swali akaanza kulia sana na kumkumbatia mwanae. Akawa na mawazo sana na akarudi nyumbani ili baadae arudi tena hospitali. Alipofika nyumbani akaanza kukagua gari lake na kuangalia pale ambapo mwanae amechora ndipo akakuta kumbe mwanae aliandika maneno yafuatayo. " I LOVE YOU BABA" akiwa na maana nakupenda sana baba. Basi pale baba akazidisha kilio. Aliporudi hospitali akamkuta mwanae na baada ya kumsalimia akaambiwa tena na mwanae ILOVE YOU DAD. Baba kwa uchungu akamjibu mwanae kwa kusema I love you too my son. Akauliza mtoto. Baba uliona ripoti yangu ya shule nilikuwa naongoza somo la hisabati, ila kwa sasa sitasoma tena hisabati mpaka vidole vyangu vitakapoota kwa sababu kwa sasa siwezi kuandika. Baba akaendelea kulia..
MWISHO
0 comments:
Post a Comment