Search This Blog

Monday, January 2, 2023

UPENDO WANGU UMENIPA UKILEMA

 






SIMULIZI FUPI : UPENDO WANGU UMENIPA UKILEMA


Ni mwaka mmoja tu umepita tangu mimi Aisha nifunge ndoa na Mume wangu Ally.Mwanzo maisha yalikuwa mazuri kiasi kwamba nilitamani hata tusizeheke wala kufa lakini ghafla mwenzangu alianza kubadilika.Nilimchunguza nikajua kuwa tayari ananisaliti na ana mwanamke mwingine nje.
Nilichukulia tu kama kawaida ya wanaume kutokuridhika lakini nilichojivunia ni kuwa mimi ndie mke halali na mwenye pete kidoleni hao wengine ni wapita njia na wala hata siku moja hawataweza kusogea kwenye mji wangu zaidi ya kuishia kuchezewa tu na kuachwa,Pamoja na hayo yote japo niliwaza sana na kuwa na hofu endapo sasa mme wangu ataniletea magonjwa ya zinaa itakuwaje.
Ila niliishia kujipa moyo na kutupilia mbali mawazo kama yale na zaidi ya hapo sikutaka hata kumuuliza mme wangu chochote kuhusu huyo mwanamke alienae nje,Niliishia tu kusema mimi ni mke halali na nina mamlaka na Ally wangu.


Sikujua kama ukimya ule na upendo ule kwa mume wangu baadae utakuwa mateso makubwa sana.
Siku moja nikiwa nimekaa sitting room naangalia Tv niliona sms imeingia kwenye simu yangu na namba ni ngeni.Niliifungua Sms ile na kukuta ujumbe unaosema"Achana na Mume wako vinginevyo tutakuachanisha".Nilijiuliza sana hii namba ni ya wapi na inatoka wapi sikupata jibu.Lakini moja kwa moja wazo likaja huyu ni mchepuko wa mume wangu yule ambae nilikuta sms zake kwenye simu ya mume wangu.Sikutaka hata kujibizana nae kwa sababu niliona ni ujinga na wala sikutaka hata kumuuliza chochote mume wangu japo sms ilikuwa ni ya vitisho.Niliona tu kuwa huyu mdada hana jipya kakosa la kufanya zaidi ya umalaya wake na anataka tu kunigombanisha na mme wangu.Sikutaka hata siku mmoja mimi na mume wangu tuje tugombane au nimuwekee kinyongo chochote.Nilichokuwa napenda ni kumuona mume wangu anafuraha siku zote hilo tu lilinifanya nijisikie raha na kujiona kuwa nina mume nimpendae hivyo sikutaka kujua au kusikia ni wanawake wangapi wanatoka na mume wangu na anawahonga kiasi gani haya yote sikuyataka.
Hivyo niliamua kuifuta ile sms wala nisibaki nayo kwenye simu.Kufanya hivyo kumbe ndio nilikuwa nazidi kujichimbia zaidi kaburi.


SIKU moja wakati natoka saloon kutengeneza nywele zangu mida ya saa moja inaelekea saa mbili usiku.Nilikuwa kwenye kiuchochoro napita ili nikatokezee barabara kubwa kisha kupanda pikipiki nielekee nyumbani.
Nikiwa kwenye kale ka uchochoro ghafla wadada watatu walijitokeza na kunizuia njiani.
Kabla sijafanya chochote mmoja wao aliniziba mdomo kisha kunivuta pembeni.Nikiendelea kutahayaruki mwingine alinishika kwa nguvu zaidi nisiweze kufanya chochote kisha yule kiongozi wao akaniambia"Si nilikutumia sms uachane na mumeo ukaniona mimi fala.Anaefaa kuolewa na mumeo sio wewe ni mimi hapa sasa leo tutakufundisha"Nikiwa siwezi kuongea chochote kutokana na kuzibwa mdomo yule dada alitoa kitu kama chupa yenye maji maji.Nilitamani kupiga kelele lakini ilishindikana.Nilitamani niombe msamaha lakini ilishindikana zaidi nilibaki kutoa macho kuangalia nini anataka afanye.Nikiwa nimetoa macho yangu nilishangaa kuona anaitikisa ile chupa kama mtu anaechanganya dawa kabla ya kunywa.
Mara ghafla bila huruma mwanamke yule alinipulizia dawa ile machoni mwangu ambapo muda huo nilikuwa nimeyatoa zaidi kwa ajili ya kushuhudia tukio.Niliyafumba kwa maumivu makali sana ya ile dawa aliyonipulizia na ghafla macho yangu yakaanza kuuma.Nilijalibu kufumbua angalau nione kitu ama hakika huo ndio ulikuwa mwisho wangu wa kuona DUNIA


Nilisikia sauti ya yule mwanamke akisema"Na bado leteni nyundo".Moja kwa moja nikajua sasa wananimalizia uhai wangu.Nyundo kali ilitua katika mguu wangu wa kulia na kusababisha maumivu makali sana katika mwili wangu.Nilipiga kelele ya kuungurumia ndani kwa ndani kwenye tumbo pasipo hata kutoa sauti kutokana na Maumivu makali niliyoyapata.Kabla hata maumivu ya mguu huo hayajapoa mara........


.....Nyundo ilinyanyuliwa na kunivunja mguu wa pili.Hapo maumivu yalizidi zaidi na kujikuta naanza kulia ijapokuwa tayari ni kipofu."Hii ndio dawa yake".Walisema wale wanawake huku wakicheka kisha kuniachia na kunikimbia.Nilianza kulia damu nyingi zilinitoka miguuni nilipiga kelele hatimae nikazimia.
Nilikuja kupata fahamu na kujikuta nipo mazingira ya tofauti.Nilijaribu kufumbua macho lakini sikuona kitu.Nilisikia kelele za hapa na pale na hatimae nilisikia sauti ya mama ikisema"Jamani mwanangu amezinduka".Mara pia nilisikia sauti ya mume wangu ikinitakia pole huku kwa mbaali mama alianza kulia.Niliuliza niko wapi hapa,Mama alichukua jukumu la kunielezea."Uliokotwa na wasamalia wema na kukufikisha hapa kisha wakatumia simu yako kumpigia mme wako kuwa upo hospitarini leo ni siku ya pili tangu uletwe hapa ulikuwa umezimia mwanangu nilijua nimeshakupoteza."Mama alianza kulia kwa kwikwi kitendo kilichosababisha na mimi nianze kulia"Ona mwanangu dunia vile mbaya wamekuvunja miguu na pia wamekuharibu macho sijui umewakosea nini mwanangu".Maneno haya ya mama yalinifanya nizidi kulia zaidi hasa baada ya kusikia nimekuwa kilema wa milele.


Yote haya yamesababishwa na hawala wa mume wangu.Nilijisemea moyoni,sikutaka kusema chochote zaidi ya kukaa kimya na wao kuamini kuwa ni vibaka ndio walionitendea haya.
Nilikaa hospitali takribani wiki mbili nikihudumiwa na hatimae nililuhusiwa.
Nilipotoka hospitarini moja kwa moja nilifikia kwa mume wangu lakini cha ajabu nilikaa siku ya kwanza na ilipofika siku ya pili Mume wangu aliniambia niende nyumbani na Mama nikakae kule mpaka nitakapokaa vizuri na miguu itakapoungana vizuri nitarudi.Aliniambia kuwa pale hamna mtu wa kusema nikae nae na kuniangalia hivyo bora niende nyumbami mama yupo.Alinipa maneno ya faraja kuwa japo kuwa nimepoteza macho lakini mimi bado ntabaki kuwa mke wake hivyo nitakapopona vizuri nitarejea nyumbani na atafanya mpango zaidi ikiwezekana tusafiri nje ya nnchi nikatibiwe macho.
Nilikubariana na nikasafiri mpaka mkoani kwetu na mama na wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi miwili.


ZILIPITA kama wiki mbili hivi tangu niludi kwetu.Siku moja usiku sikuamini baada ya mume wangu kunipigia cm na kuniambia"Mimi na wewe basi tena,Siwezi kuwa na mke kilema taraka zitakufuata huko huko".Kisha simu ikakata.Nilishindwa kuitafuta namba nimpigie tena kwa sababu ya upofu wangu.nilibaki nalia tu.Nilimuelezea mama yangu hayo maneno nae akanitia maneno ya faraja na kunifanya nipunguze kulia"Mwanangu angalia vilema wote vile wanavyotengwa na jamii wewe sio wa kwanza,Maadam nipo mimi mwanao nitakulea mwanangu Mungu atakusaidia tu utapona zaidi mshukuru Mungu kwa yote wewe pia sio wa kwanza kuachika ipo siku Mungu atasikia kilio chako utapona na kusimama na kuona tena mtumaini Mungu."
Hakika maneno haya yalikuwa ya faraja sana kwangu.Siku hazikupita na kweli niliachika kwa Mume wangu nilianza maisha ya kukaa nyumbani na mama yangu huku nikijuta ni bora toka mwanzo ningefungua kesi,Ni bora toka mwanzo nisingempenda mume wangu kiasi hiki,Ni bora ningeusema ukweli wote yaliyonikuta.Upendo wangu ka kukaa kimya kwangu kumeniponza.Nashukuru Mungu nilijifungua salama na nina Mtoto japo nae nasikia kaoa tena nadhani atakuwa yule mwanamke alienitendea mabaya haya.Sifa na shukrani naludisha kwa mola japo sioni.
Lakini napenda kuacha ujumbe huu kwa jamii na kuwauliza wanaume.KWANINI HAMTOSHEKAGI??


ASANTENI......


MWISHO

WARIDI LA MAPENZI

 






Tukusuma Mpoki alikuwa amesimama kwenye baraza la nyumba yake, uso wake ukiwa umekunja ndita, jasho likimtiririka, na macho yake yakiwa yanabubujikwa na machozi. Alikuwa amejifunga kanga moja tu kati ya eneo la kifuani na kiunoni na hivyo kuonesha mapaja yake yaliyonawiri vizuri na hivyo kulidhirisha kwa kadamnasi umbo lake lake la nyigu. Chini ya kanga hiyo alikuwa amevaa chupi ya rangi nyekundu. Licha ya upepo wenye joto la jiji hilo la bandari salama kumpulizikia bila kukoma Suma aliendelea kusimama kwenye baraza la nyumba hiyo. Hakujali watu waliokuwa wamesimama upenuni wakimshangaa binti huyo wa Kinyakyusa akiwa katika hali ya hasira na aliyekuwa akipaza sauti yake akimtukana mumewe bila kufunga breki. Mkono wake wa kushoto uliokuwa umevikwa bangiri za rangi ya dhahabu ulikuwa umekunjwa kwenye kiwiko na kuegeshwa kama gari la kijapani kwenye kiuno cha binti huyo kilichokuwa kimehifadhi vyema mviringo wa makalio yake uliokuwa kama vitunguu maji vinavyolimwa kule Tukuyu.



Mkono wake wa kulia ulikuwa umeinuliwa juu, huku kidole cha kati kikining’inia hewani utadhani kimepigiliwa msumari katika staili ya kumzodoa mtu. Kucha zake ndefu zilizopakwa rangi nyekundu inayong’ara zilionesha ni jinsi gani Suma (kama alivyozoea kuitwa mtaani) alivyokuwa anajijali. Nywele zake ndefu zilizosukwa kwa mtindo wa rasta zilining’ia mabegani kama nywele za simba jike. Suma alikuwa amekasirika, na hasira yake ilionekana wazi siku hiyo. Hakuna aliyewahi kuhisi kuwa dada huyo anaweza kuweza kumpaka mtu hadharani namna hiyo.



“Toka hapa, unadhani mwanamme peke yako” Alifoka binti huyo huku sauti yake yenye lafudhi ya mbali ya kinyakyusa ikipasua anga la eneo hilo la Chang’ombe.



“Yaani kukupenda wewe ndio imekuwa nongwa, mwanamme gani huridhiki, kama penzi langu hulitaki si uende huko huko ulikolala jana, firauni mkubwa, kama unafikiri huyo malaya wako anaweza kukupenda kama nilivyokupenda sasa mbona umerudi hapa?” Aliendelea kubwata bila hata ya kumeza mate. Sauti yake ikiwa kavu na isiyoonesha kujali nani anasikiliza au nani anamuangalia. Watu walifurahia sinema hiyo ya bure.



Hatua kama kumi hivi toka mlango wa nyumba yake ambayo ilikuwa ni ya mwisho ikipakana na nyumba za Polisi za Chang’ombe alikuwa amesimama Sospeter Mkiru, mdomo umemdondoka utadhani amemuona mzee Ole wa Usiku wa Balaa, na mkononi akiwa bado ameshikilia shati la lilikuwa limechanika mgongoni baada ya Suma kulishindilia kucha za uhakika.



“Jamani Suma nisamehe mpenzi sitarudia tena” Alisema Sosi huku maneno yake yakitoka kwa kukwamakwama kama maji yanavyotoka kwenye mpira wa kumwaligia maua. Soni zilimshika. Alijikaza kisabuni huku akibembeleza apewe nafasi nyingine.



“Nikusamehe mara ngapi nyang’au mkubwa we!” Dada Suma utadhani ametiwa ufunguo aliendelea kumpaka. “Jamani hata uvumilivu una mwisho. Mimi sasa basi, nenda huko unakokwenda kila siku utanletea magonjwa bure miye”



“Tafadhali Suma nisamehe mke wangu” Sosper alianguka na kupiga magoti kwenye mchanga uliokuwa unajoto. Alijaribu tena kumbembeleza binti huyo.



“Nenda kafilie mbali, hayawani mkubwa” Suma alisema huku akimwelekeza Sosi kwa kidole kuondoka hapo. Hayo yalikuwa ni maneno ya mwisho ambayo Sospeter aliyasikia toka kwa Suma Mpoki. Alimuona Suma akigeuka na kuelekea ndani ya nyumba.



Sosi alijua kuwa safari hii amevurunda kweli kweli. Uchungu ulianza kumpanda pole pole na donge la hasira ya kumpoteza waridi lake na mpenzi wake wa toka shule lilimkaba shingoni. Alijihisi kuwa amejidhulumu penzi na anastahili adhabu hiyo kali. Alitamani amkimbilie Suma na kujiangusha miguuni mwake na kumwomba radhi huku akijigaragaza. Akili yake ilianza kwenda kwa kasi akijiuliza ni shetani gani lilimwingia hadi kumfanya kwenda kulala na mwanamke waliyekutana kilabuni na kumuacha mpenzi wake wa damu? Alijihisi kizunguzungu. Kama mtoto mdogo Sosi aliunganisha vidole vya mikono yake kichwani huku shati lake akilibeba begani. Watu waliokuwa wamesimama kushuhudia tukio hilo walianza kujipangua taratibu huku wengi wakimuonea huruma Sospter na wengine wakisema wazi kuwa “amejitakia” mwenyewe. Wachache hawakuficha dhihaka yao kwani walimcheka hadharani na kumuona kweli huyo jamaa wa kuja. Sospeter aliapa hatarudi tena mitaa hiyo kwa aibu aliyoipata Chang’ombe. Akiwa haangaliki anakokwenda, Sosi alijikuta yuko katikati ya barabara ya Chang’ombe huku magari yakijaribu kumkwepa, na watu wakimrushia matusi ya kila aina hata matusi yasiyosajiliwa. Gari aina ya Fuso ambalo lilikuwa limeshehena mashabiki wakitoka uwanja wa Taifa lilijitahidi kufunga breki na kumkwepa kwa ustadi mkubwa. Sauti ya breki zake ziliumiza masikio ya watu. Mlio wa mshtuko wa watu ulitanda angani, huku watu wakishika vichwa vyao na wengine kufumba macho wasione kile kilichokuwa kitokee.. Sospeter hakupata nafasi ya kukwepa Fuso hilo, kwani alirushwa juu kama kopo tupu la kimbo. Alipotua kwenye lami yenye mashimo mashimo, mwili wake ulikuwa hauna ishara yoyote ya uhai ndani yake. Watu walikimbilia hapo kuangalia kilichotokea, huku kina mama wakipiga kelele ya kilio wakiwaficha watoto wao wasishuhudie jambo hilo.



Bila kusogea hata sentimeta moja, Suma alijisemea moyoni “Ukome!” Suma aligeuka kwa haraka huku akiangua kilio alichokuwa amekizuia kwa muda na kuingia ndani ya nyumba ambayo alikuwa anaishi na wadogo zake. Mwili wote ulikuwa unamtetemeka huku hisia ya furaha ya kisasi na hatia ya uovu vikimkaba rohoni. Moyo wake ulikuwa umejeruhiwa kwa mapenzi na kumbukumbu ya mapenzi ilimuumiza mtima. Alijihisi amepoteza muda mrefu na kijana Sospeter ambaye walikuwa wakiishi kama mume na mke. Alijidharahau na kujiona kweli “amepatikana” kwa kukubali penzi la kijana huyo chakaramu. Aliapa moyoni mwake kuwa hatopenda tena, kwani wanaume ni kama mbwa. Aliendelea kulala kitandani huku ameukumbatia mto huku moyo wake ukipaza sauti ya kilio chake mbele za Mungu. Aliendelea kulia hadi alipopitiwa na usingizi huku akiwaza jinsi alivyokutana na Sosi kwa mara ya kwanza.



* * *



Ilikuwa mwaka 1992 kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo ya Sekondari Tanzania ngazi ya Mkoa ambayo kwa mara ya kwanza yalikuwa yanafanyika kwenye shule ya Sekondari ya Karatu iliyopo pembezoni mwa barabara iendayo mbuga maarufu ya Serengeti nje kidogo tu ya mji wa Karatu. Wakati huo mji wa Karatu ulikuwa bado ni Wilaya ndogo katika mkoa wa Arusha. Shule karibu ishirini za Sekondari kutoka kila kona za mkoa wa Arusha zilikuwa zinawakilishwa kwenye mashindano hayo ambayo hatimaye yangeteua timu ya mkoa ambayo ingewakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano ya UMISETA yaliyokuwa yanafanyika baadaye mwaka huo huko Morogoro. Sospeter alikuwa ni golikipa namba moja wa timu ya Soka toka shule ya sekondari ya Singe iliyoko Babati. Sifa zake zilienea kwenye mashindano hayo kwani aliokoa penati tano katika mechi mbalimbali ambazo ziliifanya timu yake kushiriki katika mashindano hayo. Hata hivyo sifa hizo hazikumfanya awe anajipendekeza au kujiona yeye bora zaidi. Nje ya uwanja alikuwa ni kijana mcheshi, mwenye kupenda utani, lakini anayeheshimu kila mtu. Akiwa kwenye lango alikuwa ni tishio kwa timu ya ugeni kwani alikuwa na manjonjo ya Juma Pondamali na udhibiti wa goli wa Idi Pazi. Alikuwa na mbwembwe golini kiasi cha kuwafanya washambuliaji wa timu ya ugeni kupenda kujaribu mashuti ya mbali kwani wakimsogelea huwa anawazogoa na kuwatania kiasi cha kuwafanya wakasirike na hivyo kushindwa kutilia mkazo ufungaji magoli. Kwa mtindo wake huo watu walimfananisha na aliyewahi kuwa golikipa wa Coastal Union, Duncan Mwamba.



Upande mwingine kulikuwa na timu ya Netiboli toka shule ya Sekondari ya Kilutheri ya Dongobesh wilayani Mbulu. Kati ya shule zote zilizowakilishwa kwenye mashindano hayo timu ya Dongobesh ndiyo ilionekana kutoka mbali zaidi na wachezaji wake kuonekana ndio washamba zaidi. Hata hivyo watoto wengi wa wakubwa ambao walikuwa watundu huko mijini walitupwa huko kwenye shule hiyo ya bweni iliyozungukwa na kijiji cha kale cha Dongobesh. Timu yao ya Netiboli ilikuwa inacheza vizuri lakini sifa kubwa ilikuwa inatokana na dada aliyekuwa akicheza nafasi ya senta, alikuwa ni gumzo hapo Karatu. Kwanza kwa sababu ya uzuri wake na umbo lake la kimalaika. Wenyewe walimpachika jina la Angel hadi wengine walidhania ndio jina lake halisi. Alikuwa na mvuto wa ajabu kwa wavulana na wasichana. Lakini pamoja na sifa zake zote Suma alikuwa anaakili darasani na tangu aingie shule ya Dongobesh hajawahi kushika nafasi chini ya pili. Alikuwa akipishana na kijana mmoja ambaye baadaye alijulikana kwa kazi yake ya uandishi, hadithi, na utunzi mbalimbali kwenye mtandao wa kiintaneti.



Dongobesh walikuwa wanacheza mechi ya mwisho dhidi ya timu ya Madunga ambayo ilikuwa ni mpinzani wa jadi. Sospeter kwa kuitikia mwito wa rafiki zake waliokuwa wanamsifia Suma aliamua kwenda kuangalia mechi hiyo, siyo kwa ajili ya kuona nani atashinda bali kuona kama kweli hizo sifa za Suma zilikuwa ni za kweli au ni porojo tu za kwenye Umiseta. Alipofika na kumuona jinsi binti huyo alivyokuwa anapendeza katika mavazi yake ya netiboli ambayo yalimfanya aonekana kama amepotea toka Mbinguni na wanamtafuta, Sosi alijikuta akimkodolea macho dada wa watu utadhani ameona hazina ya mfalme Solomoni. Sosi hakutaka kuangalia kitu kingine chochote na alijikuta anaungana na wadau wengine kushangilia kila Suma alipokuwa akitoa pasi na kudaka mpira. Mara mbili alijikuta anagonganisha macho yake na Suma ambaye na yeye alianza kumwangalia na kila akidaka mpira basi anaweka madoido kidogo kumlingishia Sosi (kama ilikuwa kweli au hayo ni mawazo ya Sosi tu miye sijui).



Mechi iliisha kwa timu ya Dongobesh kushinda na furaha kubwa ilitawala upande wa mashabiki wa Dongobesh wakiongozwa na shabiki aliyejipachika Sospeter Mkiru. Ilikuwa ni furaha kubwa kwani timu ya Dongobesh haijawahi kuifunga Madunga kwa miaka mitano mfululizo hivyo ilikuwa ni furaha kwa mwalimu wa Michezo Michael Tluway wa shule hiyo. Aliyekuwa na furaha zaidi ya Sosi alikuwa ni matroni wao Vera Akonaay. Wakiwa katika shamrashamra za kusherehekea Sospeter alitembelea kumwelekea Suma aliposimama mbele yake alijikuta ananyosha mkono wa pongezi kwa kapteni huyo wa Dongobesh.



“Hongera Sana kapteni” alisema Sosi huku moyo ukimwenda kasi utadhani aliyefukuzwa na simba mwenye njaa.



“Asante sana” Alijibu Suma huku akijaribu kuachilia mkono wa Sosi ambaye alikuwa kama amemng’ang’ania.



“Umecheza vizuri kweli” alijikuta akisema maneno yasiyo na kichwa wala mguu.



“Ndiyo, ila kulikuwa na mtu ananikodolea macho utadhani amepoteza kitu na mimi nimemfichia” Alisema Suma huku mikono yake akiifunga pamoja kifuani. Sosi alishindwa kujizuia kuangalia kifua cha Suma ambacho kilikuwa kimetuna kwa matiti yaliyolala kama paa nyikani na kama midomo ya hua wawili chuchu zake zilionekana kwa mbali. Sosi alimeza fundo la mate kwa aibu.



“Wala usisema maana nilichopoteza nimekipata” Alisema huku akijikaza. Waliweza kuona macho ya watu yakiwaangalia imekuwaje watu hao wawili wazungumze. Na vijana wengi walishangazwa ni jinsi gani Sosi alikuwa na ujasiri wa kuzungumza na binti mrembo kama huyo. Wengine walikiri kuwa kama kulikuwa na mwanafunzi yoyote kwenye mashindano hayo ambaye angeweza kumsimamisha Suma basi alikuwa ni Sospeter.



“Umekipata? Na ulipoteza nini?” alihoji Suma huku macho yake yakimganda kijana wa watu. Moyoni alijisemea kuwa alikuwa ni kijana mzuri, msafi, na jasiri maana vijana wengi walikuwa wanaogopa hata kumsalimia. Walijiona hawafai mbele zake.



“Nimepoteza akili yangu baada ya kukuona, na nadhani nimepata mke kwa maisha yangu yote” Kama mtu aliyepagawa pepo wa mahaba Sosi hakujua maneno hayo yametoka wapi, maana yalibubujika kama chemchemi ifukayo maji ya mapenzi.



“Wacha we!, yaani kuniona tu umeona na mke kabisa!?” Aling’aka Suma huku akikunja uso wake kwa kushangaa na kwa kukutwa hakujiandaa kwa maneno hayo. “Usiniambie umeshaona na watoto na wajukuu?” Aliendelea huku akiangua kicheko.



“Tena watatu, wawili mapacha” Alisema Sosi huku akihesabu kwa vidole vitatu kwanza, kisha viwili. Suma aliendelea kucheka huku akishikilia mbavu zake kwani hajawahi kukutana na mvulana aliyejua anachotaka kama huyo. Mara mmoja wa wanatimu wa Suma walimuita ili waende kubadili nguo na kujiandaa kwa chakula cha jioni.



“Ungependa kula na mimi na tupige soga zaidi” Aliuliza Sosi kabla Suma hajakimbia.



“ah..wenzangu wataningoja” alijibu Suma



“Hapana, tunaweza kwenda kijijini na kununua cha hotelini, mie leo sili dona lao” alijibu Sospeter huku moyoni akiombea kwa miungu yake Suma akubali.



“We, tutawezaje kutoka kambini si ni kujitakia matatizo? Huoni geti kali?”Aliuliza kabla hajakubali baada ya ushawishi wa Sosi. Sospeter alimhakikishia kuwa hawatagundulika na wakakubaliana wakutane saa moja baadaye kwenye lango kuu la shule. Sospeter alianza kutafuta njia ya kuweza kutoka na kurudi jioni hiyo bila kujiletea matatizo yeye mwenyewe na Suma.



Baada ya kuhangaika kufikiri nini cha kufanya aliamua kwenda kwa mzee mmoja wa Kimang’ati aliyekuwa zamu kulinda lango la shule hiyo. Wala hakumchelewesha alimpatia shilingi mia tano na kumuomba chonde chonde amruhusu yeye na Suma waweza kwenda na kurudi kabla ya muda wa kulala ambao ilikuwa ni saa nne kamili za usiku. Mzee wa Kimang’ati kumbe hizo zilikuwa zake. Alizifinyanga hizo pesa kiupole na kuziweka mfukoni. Alimwambia akiwaona wanakuja basi atajifanya anazunguka upande wa pili na geti atalisogeza upande kidogo tu. Na kweli hivyo ndivyo ilivyokuwa kwani Sosi na Suma walipofika hapo majira ya moja za jioni wakati giza ndio limeanza kuingia kwa nguvu na kunyamazisha sauti za ndege yule mlinzi alizunguka upande wa pili wa kibanda na kujifanya hakuona kitu na pale tu walipotoka alifanya haraka kufunga geti kwa kufuli. Alikaa kuwasubiri warudi.



Kesho yake kama moto ulioanzishwa na cheche, uvumi mkubwa ulienea kati ya wachezaji kuwa Sospeter na Suma walienda kufanya ngono kijijini. Ulianza kama utani na mwisho chumvi zikaongezwa, limao, na pilipili. Na wengine wakanyunyiza na amdalasini. Mara habari zilipowafikia Suma na Sosi, hawakuchelewa kwenda kwenye ofisi ya Mkuu wa Kamati ya Mashindano. Walipofika walikuta walimu wao wa michezo wakiwa tayari wamewatangulia. Walimu walifurahi kuona vijana hao walivyomakini na walivyoamua kuweka mambo sawa kabla hajaaribika zaidi. Waliwaelewesha walimu kuwa hakukuwa na kitu kama hicho na walikwenda kwenye kale ka mgahawa kalioko gulioni. Walikiri kutoroka na kwa hilo ndilo kosa pekee ambalo walimu walikubali, na katika kuwapa adhabu waliwasimamisha kucheza mechi moja moja kwenye timu zao. Jambo hilo basi likazimwa kimya kimya na kiutuuzima. Hata hivyo, ule uvumi tu wa kuwa walikwenda kufanya ngono ulikuwa kama umewapa hamu na wakaamua kufanya kweli. Tatizo lilikuwa ni muda na mahali, maana kila kona kulikuwa na wanafunzi na shughuli.



Hawakupata nafasi ya kuweza kujificha mahali na kupeana mapenzi hadi siku ya mwisho ya michezo ambapo timu ya kina Suma ilichukua ubingwa na ile ya kina Sosi ikishika nafasi ya pili. Wakati michezo inafungwa rasmi ukumbi ulilipuka kwa furaha mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa kati ya wanamichezo waliochaguliwa kuwakilisha mkoa wa Arusha kwenye mashindano ya Taifa Morogoro walikuwemo Sosi na Suma. Sospeter alitangazwa kuwa Kapteni wa timu ya mkoa. Kambi ya timu hiyo ilikuwa ni Arusha, kwenye shule ya sekondari ya wavulana wenye vipaji ya Ilboru.



Kabla hawajaondoka Karatu, walikuwa bado wanatafuta nafasi ya kupeana tunda walilokatazwa. Nafasi ilijileta karibu saa moja kabla ya kuondoka hapo. Wakati wanafunzi wanaagana, Suma na Sospeter walienda kwenye mojawapo ya vyumba vya madarasa ambapo kulikuwa hakuna mtu, tena mchana kweupe. Walienda mmoja mmoja bila mtu yeyote kuwashtukia. Kilikuwa chumba cha kidato cha tano C kilichotazama upande wa shamba la shule hiyo.



“Kuna mtu amekuona” Sospeter aliyekuwa ametangulia alimuuliza Suma aliyekuwa amevaa sweta zito la rangi ya damu ya mzee, suruali ya jeans iliyokuwa imechakaa magotini na viatu vya raba vya rangi nyeupe ambayo ilikuwa imechafuliwa na vumbi la Karatu na kuvifanya vionekane vya rangi ya udongo.



“Hamna, ulitaka kusema nini huku kwa kificho” Aliuliza Suma kwa aibu huku macho yake yakiangaza angaza kwenye madirisha. Hakukuwa na mtu na sauti za wanafunzi zilikuwa zinasikika kwa mbali wakiimba nyimbo mbalimbali za kufurahia kambi hiyo.



“Nilitaka nikubusu kabla hatujaondoka, maana tukiondoka hapa itakuwa ni michezo tu ili tupate ushindi kwa mkoa” Alisema Sosi huku akimvuta karibu Suma. Suma alijifanya hataki lakini alikuwa anataka. Moyo ulikuwa ukimuenda kasi, na tumbo kama limejaa vipepeo! Viganja vyake vililowa kwa jasho licha ya baridi la mji huo uliokuwa karibu na lile shamba maarufu la Shangri La ambalo linamilikiwa na kina Christian Jebsen na Dr. Klatt.



“Tukibambwa je?” Aliuliza Suma huku akifungua mikono yake kumruhusu Sosi amkumbatie na kumvuta karibu. Alimwangalia Sosi machoni kwa macho yaliyolegea ambayo yalikuwa yanaita “njoo”!



“Hakuna mtu huku” Sosi alijibu huku akimwangushia Suma busu la taratibu, lenye unyevu kwenye midomo ya binti huyo iliyopauka. Suma alijiui kwa taratibu na upole wote huku akiguna kwa msisimko uliompitia kama umeme kuanzia utosini hadi kwenye nyayo. Alijikuta miguu yake imenyong’onyea. Moyo ulizidi kumdunda. Alijihisi kutekenywa sehemu ambazo ni bora zisitajwe hadharani. Akafungua mdom o wake zaidi na ndimi zao zikakutana, zikagongana na kuanza kuvingirishana utadhani ziko kwenye mashindano ya mabusu. Walipeana denda huku mikono yao ikipapasana mgongoni, kichwani, na karibu kila kiungo kingine cha mwili. Sospeter alijikuta “anazidiwa” kwani mzee aliyekuwa amelala aliamka utadhani kifaru mwenye hasira. Suma aliweza kuhisi kutuna kwa suruali ya Sosi, kitu ambacho kilimpagawisha.



“Wewehh…!”ndicho pekee alichoweza kusema. Akiendelea kurushiana mabusu na mpenzi wake huyo mpya, Suma aliianza kufungua suruali ya kodirai ya rangi ya maziwa aliyokuwa amevaa Sosi, mikono yake iliyobaridi ilijitumbukiza kama kwenye pango la nyoka na kumchomoa nyoka pangoni! Alikuwa ametuna na kuvimba kama chatu aliyekuwa tayari kummeza mtu. Sospeter alijikuta nusura aanguke kwani ubaridi wa mkono wa Suma ulikuwa kama hamira kwenye uanamuwe wake. Mzee alikuwa amefura na kupwita pwita kama chura aliyetoka majini!



“Suma, nakupenda” Alijikuta akisema bila hata kujua kweli alimaanisha au alikuwa amezidiwa na mfadhaiko. Suma akitumia kidole chake cha pili alimfunga mdomo na kumwambia “shhhhhh”. Sospeter alijikuta amekuwa na ububu wa ghafla. Kabla hajajua kilichoendelea, Suma allichuchumaa mbele yake, huku akizurusha nywele zake nyuma, kama mtumbuiza nyoka, alilichukua joka hilo, na kuliingiza mdomoni mwake. Kwa ufundi uliokubuhu, alianza kulipa burudani ya mwaka. Suma alifanya ufundi wake kwa joka hilo na kabla huyo chatu hajatema sumu yake alimchomoa mdomoni. Kichwa cha chatu huyo kilikuwa kimetuna, huku mrenda mrenda ukiwa unachuruzika. Suma alisogea kidogo na kuteremsha suruali na nguo ya ndani aliyekuwa amevaa hadi mguuni na kuchomoa mguu mmoja na kuuweka upande. Kwa mikono yake miwili aliinamia dawati, huku akishikilia kiti cha dawati hilo makalio yake akiwa ameyabong’oa. alinama kama anachuma mboga. Sospeter hakufanya ajizi, kama morani wa kimasai, alitupa mkuki wake wa raha, uliokita kunakotakiwa kwa ulaini kama kisu kikichomekwa kwenye siagi. Suma, nusura adondoke.



Mara kwa mbali walisikia sauti za mlio wa viatu zikielekea kwenye maeneo ya darasa walilokuwa wakifanya mapenzi.



“Harakisha” Suma alimwambia Sospeter ambaye kwa hakika hakuhitaji kuambiwa kwani aliangoza mwendo na haikumchukua muda alifika kunakofikwa, huku mwili wake na misuli ikigangamaa na mishipa ikimtoka usoni. Hawakuwa na muda wa kufarahia raha hiyo bali walipandisha suruali zao haraka haraka huku sauti za viatu zikiwa karibu kabisa. Kwa haraka wachuchumaa chini ya hilo dawati. Waliokuwa wanapita wakapita. Suma na Sospeter wakaagana na kukimbia kuwa basi lao.



“We Sosi ulikuwa wapi watu wanakutafuta, mchumbako yuko wapi?” Aliuliza mratibu wa Umiseta mkoa Mwl. Genda Gundi (alizoea kuitwa GG)



“Na mimi nilikuwa namtafuta yeye” Sospeter alijibu huku akiingia ndani ya basi ambapo kila mtu alikuwa anamshangaa alikuwa wapi muda wote huo wakati watu wanamtafuta. Alienda na kuketi mwisho mwa basi hilo na washirika wake.



Kwa mbali waliweza kumuona Suma akija huku amebeba mikoba yake. Alipofika kitu cha kwanza alimuuliza Mwalimu GG kama amemuona Sosi kwani alikuwa anamtafuta na hawezi kuondoka. Akaambiwa Sospeter ameshafika hapo na yuko ndani ya basi.



* * *



Penzi lao lilikua taratibu na miaka miwili baadaye walifunga pingu za maisha kabla tu ya kuanza masomo ya Chuo Kikuu. Waliishi pamoja Dar-es-Saalam wakati wote wa masomo hadi walipohitimu shahada zao za kwanza mwaka 1998. Wote waliajiriwa jijini hapo, Sospeter akifanya kazi katika idara ya Takwimu huku Suma akipata nafasi ya Ualimu katika shule ya sekondari ya Lugalo. Watu walionea wivu kwa jinsi walivyokuwa chanda na pete wakipendana kuliko kumbikumbi au njiwa. Waliheshimiana na kusaidiana katika kila hali. Ndio uchungu huu uliokuwa umekita kwenye moyo wa Suma akiwa bado amelala kitandani. Machozi yaliendelea kumbubujika.



“Suma, Suma, amka” Sauti ya upole ya kiume ilimshtua usingizini.

“Mume wangu Sosi” Suma aliendelea kulia huku akigalagala kitandani.

“Nini tena Suma, mbona unalia usingizini” Sauti hiyo iliendelea kuuliza huku mikono ya mtu huyo ikimtikisa, “umeota jinamizi mpenzi” Iliendelea sauti hiyo.



Suma hakuamini kusikia sauti hiyo, kwani haikuwa sauti ya mtu mwingine isipokuwa ya mume wake wa ndoa Sospeter Mkiru. Alifumbua macho yake taratibu kuangalia kama alikuwa bado anaota au ni kweli. Sospeter alikuwa ameketi kwenye ukingo wa kitandani huku akimuangalia mkewe kwa hofu na mahaba makubwa. Hajawahi kumuona akilia usingizini hata mara moja. Moyoni alijua ndoto yoyote aliyokuwa ameota hinti huyo ilikuwa ni mbaya kweli.



“Mpenzi, haya ni ndoto gani hiyo imekufanya ulie usingizini” alihoji huku kwa kutumia kidole gumba akimfuta machozi Suma.



“Jamani, hivi ni wewe kweli?” Suma aliinuka taratibu akaanza kuupapasa uso wa Sosi kuamini kama kweli ni yeye. Kwa mbali aliweza kusikia sauti za watoto zikicheza mchezo ya kombolela huku mlio wa magari ulisikika kwa mbali ukishindana na sauti za watoto hao. Alikuwa amelala na kanga moja tu kwani alijitupa kitandani baada ya kuoga akimsubiri mumewe atoke kazini.



“Ni mimi mpenzi” Sospeter alijibu kwa upole huku akimrushia busu. Alikumbuka mara ya kwanza kumbusu Suma miaka ile kule Karatu. Busu lake lilikuwa bado tamu na lenye mvuto usiochuja. Suma alimkumbatia mumewe na kumwomba Mungu amuepushe na mikosi yote, na maneno yote ya wamtakiao mabaya. Aliamua kumsimulia ndoto yake. Alipomaliza, alimuangalia mpenzi wake na kusubiri atasema nini.



“Mama Grace, tangu nikuone wewe kule Karatu sijaona mwanamke mwingine” Alisema kwa sauti ya kumhakikishia. “sijatamani wala sijaota kutamani mwanamke mwingine. Wote ninaowaona nikiwalinganisha na wewe, nitaendelea kukuchagua wewe hadi kaburini” Alisema huku macho yake yakilengwa na machozi. Suma alijikuta anatokwa na machozi tena, ingawa safari hii yalikuwa ni ya huba na furaha. Alimuuliza Mungu ilikuwaje astahili mwanamme namna hiyo.



Suma aliinuka kitandani, na kabla hajasimama vizuri kanga yake iliyokuwa bado imemning’inia mwilini ilidondoka, na kumwacha mtupu kama alivyozaliwa. Mwili wake wenye rangi ya maji ya kunde uliangaza kama mbalamwezi. Sosi alimuangalia mara moja na hamu yake ikamzidia. Alimvuta karibu huku yeye akiwa bado ameketi, alifungua miguu yake na kumsimamisha Suma katikati yake huku mikono yake ikiwa imezunguka makalio ya mviringo wa tufe. Alianza kumbusu tumboni , mapajani, huku vidole vyake vikiendelea kuyaminya minya makalio ya binti huo. Suma alinyanyua mguu wake wa kushoto na kuuweka juu ya ukingo wa kitanda. Harufu ya uanamke wake ilimwingia Sosi kama manukato ya thamani kutoka Yemeni. Kama fundi wa kukuna, Sosi alianza “kukuna nazi” na kukuna alikuna! Suma aliamua kujitupa kitandani, na kwa mahaba yasiyokifani walishirikiana tendo la ndoa bila hofu ya kubambwa au kufaminiwa. Hiyo ndiyo ilikuwa raha ya ndoa. Walipomaliza walijikuta wamelowa jasho utadhani walikuwa wanakimbia mchakamchaka.



“Haya niambie safari yako ya hospitali ilikuwaje” Sospeter alipata akili ya kuuliza kwani Suma alikuwa aonane na Daktari kwa uchunguzi wa kawaida.



“Una uhakika unataka kujua” Aliuliza kwa sauti ya upole iliyoficha jambo.



“Kido, nisingeuliza kama nisingetaka kujua” Alisema huku akimgeukia mkewe na kumtazama usoni. Suma aliuma mdomo wa chini kwa aibu za kike. Alimwangalia mumewe kwa mapenzi na kwa hamu.



“Unakumbuka wale mapacha uliokuwa unawazungumzia?” alimuuliza kwa haraka. Ulikuwa mtego ambao Sosi alinaswa kirahisi.



“Mapacha gani” aliuliza bila kujumlisha mbili na mbili.



“Kurwa na doto” Suma alijibu akicheka na kumuangalia usoni. Kama mtu aliyezibuliwa Sosi alifungua macho yake utadhani yako tayari kuchomoka kama ya Scooby Doo!



“Acha utani mama Grace!” Alisema



“Wala sikutanii, nimebeba mapacha!” Alisema kwa fahari kama mtu aliyetimiza wajibu wake. Sospeter alianza kucheka, kufurahi, na kushangilia utadhani amefunga goli lililoipeleka timu yake kwenye kombe la dunia Ujerumani! Alimvuta mke wake karibu na akiweka mkono wake kwenye tumbo la Suma, aliomba sala ya shukurani na baraka kwa viumbe hao wa Mungu. Mawazoni alianza kutafuta majina kama wote wakiwa wa kike, wa kiume au mchanganyiko. Suma alienda bafuni pembeni mwa chumba chao ambako alijisafisha na kubadili nguo. Alipotoka alikuwa anawaka. Alivalia gauni lake la rangi ya zambarau ya kifalme lenye madoa meupe, lilikokatwa kifuani kwa mtindo wa V na hivyo kuonesha kontua za matiti yake. Lilikuwa fupi lililombana kiunoni na kuishia magotini. Nywele zake zilizokuwa zimesukwa rasta zilidondoka mageni mwake utadhani binti ya mfalme. Alikuwa amejitia rangi nyekundu ya mdomo na wanja wa kope na nyusi. Alimalizia kwa kutinga viatu vyake vyenye ndefu kiasi huku vikiwa na kamba zilizozunguka miguu yake. Alikuwa na usafiri wa nguvu. Alisimama mbele ya kioo huku akijivisha hereni na mkufu uliokuwa na kito cha Tanzanite kifuani. Sospeter alijikuta akienda na kusimama nyuma yake, akimkumbatia toka nyuma, Suma alizungusha shingo yake na midomo yao ikagusana kwa busu lenye utamu wa pepo.



“Grace amesheenda kwa shangazi yake” Aliuliza Sosi



“Binamu zake walikuja kumchukua mara tu baada ya kutoka shule” Alijibu Suma. Jioni hiyo Sosi alimwambia wataenda kwenye ukumbi wa muziki ambako wana Sikinde walikuwa wanapiga. Suma alitangulia, na kufungua mlango wa mbele. Alipofungua nusura moyo wake ulipuke kwa mshtuko. Mbele yake kulikuwa na gari jeupe la kifahari la Limo, huku dereva wake akiwa ameshikilia mwamvuli mbele ya nyumba hiyo, akiwa naye amevalia suti nadhifu ya rangi nyeupe. Waswahili walikuwa wamekaa nje ya nyumba zao wakisubiri muda huo. Suma alimgeukia mpenzi wake na kupiga kelele ya furaha, machozi yakimtiririka tena. Waswahili walijikuta wakipiga makofi na vigelegele. Sospeter alimnong’oneza mpenzi wake, “Happy Valentine my love”! Suma aliishiwa nguvu. Waliingia ndani ya gari huku waswahili na watoto wa mtaani wakipiga minja na vigelegele. Moyoni, Suma aliapa atamrudishia fadhila mumewe usiku huo.



Mwisho

BAD VALENTINE

 






SIMULIZI FUPI : BAD VALENTINE



Niliamka asubuhi sana, baada ya kuoga na kuvaa suruali yangu nyeusi na tshirt nyekundu yenye michirizi meusi mabegani, niliingia stoo na kuchukua jembe, jembe ambalo lilikuwa limeanza kuota kutu kwa kutotumiwa muda mrefu.



Nilitoka nje na jembe langu mkononi, nilitembea kwa miguu taratibu kuelekea Sinza makaburini. Makaburi ambayo hayakuwa mbali sana na nyumbani kwangu nilipokuwa nakaa, Sinza kwa Remmy.



Nilifika Sinza makaburini, sehemu ambako kulikuwa na makaburi mengi sana. Nikatafuta kaburi nililokuwa nalihitaji miongoni mwa makaburi yale mengi, nililiona. Lilikuwa kaburi ambalo halijasakafiwa vizuri, lakini jina la mtu aliyehifadhiwa katika kaburi lile lilisomeka vizuri. Lydia Michael.

Tarehe ya kuzaliwa; 15/4/1990 Tarehe ya kufariki; 14/2/ 2012







Niliweka jembe langu pembeni, nilipiga magoti mbele ya kaburi lile. Nilifumba macho nikiwa nimeangalia juu, na kuanza kuongea peke yangu.



"Lydia mpenzi, kwanini uliamua kuondoka mapema sana. Kwanini uliamua kuniacha peke yangu Lydia. Bado nazikumbuka ahadi zako Lydia. Uliniahidi tutakuwa mume na mke. Tutaanzisha familia na kuzaa watoto, Lydia.



Lydia ulikuwa mwanamke wa kipekee sana kwangu. Mwanamke uliyenipenda kwa dhati nikiwa sina chochote kile. Lydia mwanamke mwenye upendo usiomithilika.



Nakumbuka ulikubali kuishi na mimi nikiwa sina kitu kabisa. Nilikuwa sina kazi yoyote, ningepata vipi kazi ilhali sikuwa na elimu? Nilikuwa naelekea kuwa mtoto wa mtaani, baada ya wazazi wangu wote wawili kufariki kwa ugonjwa wa hatari wa Ukimwi. Ugonjwa



ulioondoka na roho za wazazi wangu wote wawili, ugonjwa ulioniletea uyatima nikiwa mdogo sana.



Kwa bahati mbaya zaidi ugonjwa huu ulikuja na kitu kibaya sana. Unyanyapaa!



Wakati dunia mzima ikinitenga kwa kudai eti nina maambukizi ya virusi vya Ukimwi, virusi nilivyoambukizwa na wazazi wangu, lakini Lydia hukunitenga mpenzi.



Usiku ambao ndugu zangu walinifukuza katika nyumba iliyojengwa kwa jasho la wazazi wangu, nd'o usiku niliokutana na wewe Lydia, ukiwa unatoka kuuza maandazi yako sokoni Kariakoo. Nilikueleza matatizo yangu huku machozi yakinitiririka mithili ya maji.

Nakumbuka uliniangalia usoni na kunijibu maneno

matatu tu..



"Tutaishi Pamoja Allen" Na ilikuwa hivyo, ulinikaribisha kwako Lydia.



Tuliishi pamoja katika kibanda dhaifu kilichopo pale Jangwani. Nakumbuka tuliishi maisha magumu sana!



Mara nyingi tulilala na njaa, mara nyingine tulinyeshewa na mvua, mara nyingi tulichomwa na jua, mara nyingi tulisumbuliwa na vibaka.

Lakini tulipambana!



Tuliendelea kuishi pamoja mpenzi ingawa kwa shida.



Siku moja asubuhi, nakumbuka nilikuaga asubuhi kuwa naenda kutafuta. Nilikupiga busu mwanana katikati ya paji lako la uso tukiwa tumesimama pale mlangoni, mlango wa gunia chakavu. Nikatamka.



"Ubaki salama mpenzi wangu Lydia"



Nilienda kutafuta Lydia, ndio...nilienda kutafuta, lakini sikupata!.



Saa sita mchana nilikuwa narudi nyumbani nikiwa nimechoka sana, nimechoka kwa uchovu wa kutembea kwa miguu, nimechoka kwa kukosa hata shilingi mia tano. Nikiwa nimeweka mikono yangu nyuma, huku upepo mkali ukipeperusha shati langu dhaifu lililochanika kwa nyuma. Halikuwa shati, ilikuwa bendera.



Karibu na manzese darajani niliokota kitu, kipande cha gazeti. Niliokota kipande kile bila kujua kwanini nakiokota, kipande kile cha gazeti kilichorejesha furaha yangu. Katika kipande kile cha gazeti la Dumizi kulikuwa na jina langu, ilikuwa ni orodha ya watu walioitwa kazini kufanya kazi ya kuchora vibonzo katika gazeti hilo maarufu nchini Tanzania. Niliwehuka..



Nilikimbia mbio kuelekea nyumbani kwetu, kwa wewe mpenzi wangu Lydia. Nilikuwa na furaha isiyo na kifani, nilikimbia njiani huku watu wote wakiamini nilikuwa chizi. Sikujali mshangao wao, sikujali macho yao, sikujali zomea na makelele yao, nilichojali ni kwenda kushea furaha yangu na wewe mpenzi wangu Lydia.



Nilifika nyumbani, nilikukuta umesimama mlangoni Lydia. Nilikurukia kwa furaha, tukadondoka mpaka chini. Tulichafuka vumbi tupu.



Nakumbuka uliniuliza kwa upole kilichonifurahisha kiasi kile, nilikujibu nimepata kazi mpenzi katika gazeti la Dumizi. Hukuamini!

Sijui ni kwanini hukuamini Lydia, ni wewe ndiye uliyenambia nina kipaji kikubwa sana cha kuchora. Ni wewe ndiye uliyenishauri nishiriki katika mashindano yale yaliyoandaliwa na gazeti la Dumizi, na kila siku ulikuwa unaniambia ni mimi ndiye nitakayeibuka mshindi. Sasa Kwanini hukuamini Lydia nilivyokwambia kuwa nimepata kazi katika gazeti la Dumizi.



Nakumbuka usiku wa manane uliamka Lydia. Ulinipapasa mgongoni taratibu, kwa sauti ya upendo ulinambia.



"Allen mpenzi, umepata kazi. Siyo kwamba siamini kama umepata kazi, naamini sana, una kipaji kikubwa sana cha kuchora vibonzo, na siku zote niliamini wewe



ndiye utakayeibuka mshindi. Hakuna anayekufikia kwa kuchora katika nchi hii. Hakuna kabisa!

Lakini mpenzi wangu nina hofu, hofu ya kuachwa. Unaniahidi hutonitesa baada ya kupata kazi?.

Unaniahidi hutonisaliti?, unaniahidi Allen?.



Nilikuwa nimechoka sana, hivyo nilikujibu kwa kifupi, nikiwa nimekereka kwa kukatishwa usingizi..



"Siwezi kukusaliti Lydia!" Niligeuka upande wa pili na kulala.



Na ilikuwa kweli, niliajiriwa katika gazeti la Dumizi, kama mchora vibonzo. Tukahama kwenye kila kibanda dhaifu pale Jangwani, na kuhamia kwenye nyumba ya kisasa, Sinza kwa Remy.



Tuliendelea kuishi pamoja na wewe Lydia mpenzi wangu. Lakini sasa sikuwa nakuangalia kwa jicho la mke tena, nilikuwa nakuangalia kwa jicho kama mfanyakazi wangu wa ndani.







Wiki moja tu ilitosha kunambia kwamba Lydia haukuwa wa hadhi yangu. Ulikuwa mshamba sana, ulikuwa huna mvuto wa kuishi na mtu maarufu kama mimi. Pesa inabadilisha tabia ya mtu, pesa ni kitu kibaya sana hasa ukikipata katika umri mdogo tena bila kutarajia. Pesa ilinibadilisha.



Kubadilishwa na fedha siyo tatizo, tatizo ilinitoa mwangani na kunisukumia gizani. Ilinitoa kuwa mwanaume mpole, mstaarabu na mwenye busara, na kunipeleka kuwa mwanaume mkorofi, kiburi na mlevi. Nilianzisha tabia mpya, tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani. Tabia iliyochochewa na pombe, tabia iliyochochewa na mabaamedi. Tabia mbaya kabisa ambayo sikuwa nayo kabla. Lakini yote hayo ulivumilia Lydia.



Ikapita miezi, ikaja saa baada ya kupita siku kadhaa, saa mbaya zaidi katika maisha yako. Saa ambayo nilithubutu kuingiza mwanamke katika nyumba yetu, niliingiza mwanamke wakati wewe ulikuwepo.

Tulikukuta upo sebuleni unasali, tulikusonya kwa



pamoja, hatukujali ulichokuwa unachokifanya. Tulikaa pale sofani, tulianza kushikanashikana wakati wewe unasali.

Ulimaliza kusali, kwa hekima kubwa uliondoka bila kusema chochote, bila kufanya chochote, sikuwa najua kabisa kiasi gani ulikuwa unaumia, nilikuwa naona sawa tu kwa kila nilichokuwa nakifanya.



Siku ile tulilala sebuleni na yule changudoa niliyomchukua Kona baa, bila wasiwasi wowote. Lakini mimi sikukoma!



Siku ya pili nilikuja tena na mwanamke mwengine. Nakumbuka nilikukuta umelala chumbani. Nilikufukuza kama mbwa huku nikikutukana matusi makubwa sana. Nilikutukana matusi bila sababu maalumu. Lakini hukubisha Lydia. Ulinyanyuka taratibu pale kitandani na kwenda sebuleni. Ulilala sebuleni siku ile ilhali mimi nikilala chumbani, tena na changudoa!



Ulikuwa mwanamke wa ajabu sana Lydia, pamoja na yote hayo haukuonesha dharau kabisa kwangu, ulinijali, na mbaya zaidi ulizidi kunipenda!



Ni mwanamke gani duniani mwenye moyo kama wako, mwanamke anayeweza kuvumilia visivyoweza kuvumilika kama nikivyokufanyia wewe. Ni mwanamke gani?



Nakumbuka siku moja, siku iliyoanza kwa manyunyu ya mvua, sikumbuki ilikuwa juma ngapi, aahhhh leo nimekumbuka, ilikuwa jumamosi, ndiyo...kulikuwa na disco katika ukumbi wa Ambiance pale Sinza Africa sana.

Mimi nilienda, wewe nilikuacha umelala.



Nilirudi saa kumi usiku, kama kawaida yangu nilirudi na mwanamke, naye alikuwa changudoa. Changudoa mbaya zaidi katika maisha yangu! Tuligonga sana mlango pale nje, ilitunyeshea sana mvua pale nje.

Hukuja kufungua mapema. Labda ulilala sana kwa ajili



ya mvua, au labda ulikuwa umechoka kwa kazi nzito ulizofanya mchana, au yote hayo kwa pamoja.

Lakini baadae ulitufungulia, baada ya kuita sana. Ulitutizama mimi na yule mwanamke, changudoa niliyemuokota tu njiani. Sijui nimlaumu nani, eti nilijifanya nampenda sana mwanamke yule kuliko wewe. Labda nilikuwa nimerogwa! Yule mwanamke naye alifanya jambo la ajabu sana pale mlangoni.

Alikupiga kofi la nguvu sana usoni, eti akidai

umechelewa kutufungulia mlango. Nilitegemea labda utafanya kitu kikubwa sana. Lakini haikuwa hivyo kwako Lydia. Ulitoa maneno yaliyonishangaza sana.



"Naomba mnisamehe, sikusikia mlivyokuwa mnaniamsha"



Tuliingia ndani tukikokotana na yule mwanamke, mwanamke nisiyemjua, mwanamke asiyenijua.

Mwanamke aliyeingiwa na tamaa za mali zangu ghafla tu baada ya kuingia ndani, na kutamani kunimiliki kabisa, ili azimiliki mali zangu.



Baada ya nusu saa tu za kukaa chumbani aliniaga anaenda chooni, kumbe hakuwa anaenda chooni. Alikufata wewe pale sebuleni changudoa yule mwenye roho mbaya sana. Alikukuta umelala Lydia. Changudoa yule wa ajabu alikuziba mdomo na pua kwa mkono yake mipana. Ulikuwa dhaifu sana Lydia. Ulijitahidi kujitoa bila mafanikio.

Nikiwa kule chumbani nilisikia miguno yako, lakini sikujali kabisa, Lydia mpenzi ulifariki kifo kibaya sana wakati nilikuwa na uwezo mkubwa sana kukusaidia. Ulifariki siku kama ya leo, siku ya Valentine. Kwangu siku ya Valentine ni siku mbaya zaidi duniani.



Maana siku ile nilikuwa na uwezo wa kufanya kitu ili usiwawe, lakini sikufanya kitu chochote. Cha ajabu nilimpongeza yule mwanamke, nikimuona shujaa kwa kukuuwa wewe, mwanamke nikiyekuchukia sana tangu siku nilipoajiriwa na gazeti la Dumizi.



Baada ya ile ajira tu nilikuwa nasema hivi, katika vitu viwili nikivyovichukia zaidi duniani, ni wewe na shetani. Tuliificha ndani maiti yako usiku ule na mchana kutwa.







Usiku wa manane uliofuata tulienda kukufukia na yule baradhuli. Hatukukuzika Lydia, tulikufukia kama mnyama!



Lydia mpenzi, unafikiri mapenzi yetu yalidumu na yule mwanamke, wewe hukuwepo lakini malaika wako alikuwepo, hatukufikisha hata wiki na yule mwanamke.



Siku ya nne tu nikiwa na yule mwanamke, Nilikuja kugundua siri kubwa sana toka kwa yule mwanamke. Kumbe alikuwa anatumia dawa ya kurefusha maisha( ARVs), nilizozifuma katika mkoba wake. Ishara kwamba ameathirika na virusi hatari vya ugonjwa wa Ukimwi.

Sikumwambia.



Nami nikaenda kupima pale Angaza. Majibu yalipotoka, yalikuwa machungu mithili ya shubiri, na mimi nilikuwa nimeambukizwa virusi hatari vya ugonjwa wa Ukimwi. Ugonjwa uleule uliowauwa wazazi wangu wote wawili.



Nakubali nilistahili kupata adhabu hii, au pengine adhabu kubwa zaidi ya hii, kutokana na vitendo vibaya sana nilivyokufanyia mpenzi wangu Lydia. Leo nimekuja hapa kukwambia maneno haya.



"Nimegundua wewe ndiye mwanamke uliyenipenda, uliyenijali na kuniheshimu zaidi duniani. Natamani siku zirudi nyuma ili nikwambie haya, lakini siwezi, haiwezekani kurudisha siku nyuma. Naomba msamaha kwa yote niliyokufanyia Lydia, pesa na umaarufu vilinisukuma kwenye tamaa, tamaa mbaya! Pesa na umaarufu vimeniletea gonjwa hili lisilo na tiba.

Ningetulia na wewe nisingelia leo hii. Najiahidi sitokuwa na mwanamke mwengine tena hapa duniani mpaka nitakapokufuata Lydia ulipo, ili nije huko uliko tuishi wote Lydia. Nakuahidi nitaishi peke yangu katika maisha yangu yote yaliyobakia, ili nisiwaambukize watu wasio na hatia ugonjwa huu hatari, ili nilitunze penzi lako Lydia. NAKUPENDA SANA LYDIA.'



Nililimia kaburi la Lydia Michael, kisha nilirudi nyumbani.



Mwisho.



Halfani Sudy. 14/2/2015

TANGA USIKU WA MANANE

 






Mimi si mshirikina na mambo ya imani za jadi ziambatanazo na mambo ya kichawi kwangu ni kama hadithi za Hisopo na visa vya sungura na fisi. Katika pitapita yangu hapa yote hapa Bongo hata hivyo, nimekutana na watu wengi ambao wanaapa kwa majina ya wazazi wao na wengine hata wanaapia vifo cha watoto wao kuwa ati wamewahi kuona mambo ya kichawi au kushuhudia maluweluwe ya wataalam wa jadi. Hata nilipoenda masomoni kuanza kidato cha kwanza kule Ufipani watu walinishangaa na kuniasa niombe uhamisho kwani kule Sumbawanga “kwa wachawi ndio wenyewe”. Maneno yao hayakunitisha wala kunikatisha tama. Nilienda na bila hofu yoyote ile nilianza na hatimaye kumaliza masomo ya sekondari pale Kaengesa Seminari. Kwa muda wote huo sikupata kujikuta nimechanjwa usiku au nywele zangu zimenyofolewa “kitaalam”.



Bila shaka unajiuliza ni kwanini nimekuambia mimi si mshirikina. Nimesema hilo awali kabisa ili ujue kuwa nitakachokusimulia hapa ni ukweli, ukweli mtupu, na sikingine bali ukweli tu na hadi leo hii zaidi ya miaka kumi na tano baadaye sijapata maelezo ya kuniridhisha na yenye kunituliza akili yangu. Nimejaribu kwa kila namna kutafuta maelezo ya kisayansi ambayo yanaweza kuelezea kilichonisibu lakini hadi leo hii sijapata nadharia nzuri ambayo haivuji itakayoweza kuelezea kila kilichonitokea usiku ule ambao bado naukumbuka kama vile jana.



Baada ya kumaliza elimu ya sekondari kule Sumbawanga niliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita pale Sangu ambako nilihitimu. Nilijikuta nimekubaliwa kuchukua mafunzo ya Ualimu kule Butimba Mwanza na baada ya miaka mitatu nilipata cheti changu cha ualimu ambacho nilijivunia sana. Tangu nilipokuwa mdogo nilipenda sana kufundisha, hivyo watu walipoanza kuniita “mwalimu Shija” nilijisikia fahari sana na kutiwa moyo. Kituo changu cha kwanza cha kazi kilikuwa ni Tanga, shule ya Msingi Mbuyuni iliyoko ndani ya kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia nje kidogo ya mji wa Tanga pembeni kidogo ya barabara iendayo Dar-es-Saalam.



Ulikuwa umepitwa mwezi mmoja tangu nihamie Tanga toka nyumbani Mwanza na baada ya kukaa hotelini kwa wiki moja nilijikuta nimepata chumba cha kupanga eneo la Majani Mapana karibu na Uwanja wa ndege. Umbali toka nyumbani hadi shule ni kama kilometa tano hivi na usafiri wangu hapo mwanzoni ulikuwa ni Baiskeli (kama hujafika Tanga basi hujui jinsi baiskeli zinavyotumiwa). Ilikuwa ni mwezi wa saba, wiki ya kwanza ya mwezi, siku ya Ijumaa nilienda Pongwe kuchukua gari ambalo Mzee wangu alininunulia kama zawadi ili linisaidie kwa usafiri katika mji huo wa watu wa pwani. Wakati huo Tanga hakukuwa na vidaladala kama ilivyokuwa katika miji mingine mikubwa. Lilikuwa ni gari kuku aina Vokswageni mgongo wa kobe lakini lililotunzwa vizuri na mapadre wa kirosmini wa pale Parokia ya Pongwe.



Niliondoka Pongwe baada ya kula chakula cha jioni na Fr. John (aliyeniuzia gari) kwenye majira ya saa moja hivi. Giza lilikuwa limeshaanza kuingia katika mji huo uliotulia na uendao pole pole wa Tanga. Nilikuwa nimejawa na furaha sana kuwa na usafiri huo kwani nilijua sasa nitaufurahia mji wa Tanga kwa uhakika. Licha ya mshahara wangu, mzee wangu alikuwa akinitumia fedha kidogo za kunisaidia (yeye alikuwa ni Meneja wa Shirika la Mafuta la BP kule Mwanza). Nilipofika eneo la Maweni  kama maili kumi na tano toka Tanga mjini – ni kweli kuna mawe mengi sana – (karibu na lile gereza) nilimuona kwa mbali mtu akijaribu kuomba lifti na nilipokaribia niliweza kuona alikuwa ni mama na mtoto wake na vimizigo vyao. Kutokana na ukarimu niliopewa Tanga niliona nitakuwa ninafanya dhambi kumkatalia lift dada huyo, hivyo nilisimama baada ya kuwapita kwa mita chache hivi. Nilirudisha gari nyuma hadi walipokuwepo.



“Kaka habari yako” Alinisalimu dada huyo aliyekuwa amejitanda kanga ya vipande viwili huku kipande cha pili cha kanga kikiwa kimefunikwa kichwani na kuangukia mgongoni.



“Nzuri, mnakwenda wapi na usiku huu” Nilimuuliza huku lafudhi yangu ya kisukuma ikiwa ni dhahiri.



“Tunaenda Chumbageni” Alinijibu dada huyo huku akimvuta mkono binti mdogo wa kama miaka saba hivi.



“Haya ingieni” Nilimjibu huku nikitoka ndani ya gari langu na kuwasaidia kuweka mizigo yao kwenye boneti iliyo mbele ya mgongo huo wa kobe. Harufu ya manukato mazuri ilipenya ndani ya pua yangu, ilikuwa ni harufu ya yasmini. Haikuchukua muda tulianza safari ya kwenda Tanga mjini.



“Unaitwa nani” Nilimuuliza huku nikimuangalia kwa pembeni.



Kwa kumwangalia kwa karibu licha kigiza kilichokuwepo niliweza kutambua mara moja kuwa dada huyo alikuwa shombe, kwani licha ya ngozi yake kuonyesha kuchanganya damu, bali nywele zake zilikuwa ni za kiarabu (alikuwa ameiteremsha ile kanga aliyojitanda kichwani). Mashavu yake yalikuwa yameumuka sawia, huku macho yake yakiwa yamefunikwa kwa wanja. Midomo yake iliiva kwa rangi nyekundu ya mdomoni, na sikuweza kujizuia bali kukiri moyoni mwangu kuwa huyo dada alikuwa ni mzuri wa kuzaliwa.



“Naishwa Zainabu” Alinijibu.



“Mimi naitwa Mwl. Shija” Nilimjibu, huku nikiweka mkazo kwenye cheo cha ualimu na kujifanya mimi ni mtu miongoni mwa watu.



“Yaani wewe mwalimu? Mbona iko kazi basi” alisema huku akicheka kwa aibu.



“Mbona unacheka tena, kwani sifai kuwa mwalimu” nilimdodosa, huku nikijikuta nimefurahia kicheko chake cha kebehi.



“Si kwa ubaya, ila naona wewe ni kijana mdogo kujipachika cheo cha mwalimu” alifafanua huku kwa kutumia vidole vyake akiliweka neno “mwalimu” kwenye nukuu.



“Dada Zainabu, udogo si hoja” Nilimjibu. Nilimtaka anitambulishe huyo binti mdogo ambaye alikuwa ameanza kusinzia kwenye kiti cha nyuma.



“Huyo ni mtoto wa dadangu, tulienda kumuona baba yake pale Gerezani. Yuko kifungoni” Alinijibu na kunipa sababu ya wao kuwepo kule Maweni.



Aliniomba kama ingewezekana nimpeleke pale Masiwani na Kiwanda cha Chuma ili amrejeshe mtoto huyo kwa dadake, kasha nimpeleke Chumbageni. Kwa kweli sikuwa na haraka na nilifurahi kuwa na mtu wa kuzungumza naye kwani kwa karibu mwezi mzima nimekuwa nikizungumza zaidi na walimu wenzangu na wanafunzi. Haikuchukua muda mrefu hatimaye tulifika Masiwani, na Zainabu alimwamsha yule binti mdogo (anaitwa Saida) na kumpeleka ndani nyumbani kwa dadake. Miye nilisubiri nje na wala hakuchelewa kama nilivyohofia. Alipotoka nje dada yake alifuatana naye na alinipungia mkono kunisalimia na kuniasa.



“Uwe mwangalifu asikuzungushe usiku kucha huyo, mpeleke tu nyumbani” Alisema dada yake Zainabu kwa sauti ya kicheko. Nilimhakikishia kuwa hamna maneno na nitamfikisha salama mdogo wake huko kwake Chumbageni.



* * *



Tulikuwa tunakaribia eneo la Chuda karibu na kivuko cha reli ndipo vituko vya usiku huo viliponianzia. Kiza kilikuwa kimeshatanda na hakukuwa na mbalamwezi na mwanga wa pekee ulikuwa ni wa taa za rangu ya njano zilizokuwa kwenye milingoti mirefu pembeni ya barabara.



“Dada yako naona ni mtu mcheni kweli” Nilimwambia Zainab ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti cha abiria huku akionekana mwenye fikara nyingi.



“Nakuambia, ana vituko sana Aisha” Alinijibu huku akinitajia jina la dada yake.



Tuliendelea kuzungumza kidogo hadi niliposikia honi ya treni ikiashiria kuwa treni ilikuwa karibu kufika mahali hapo. Niliamua kuongeza mwengo ili niweze kupita kabla ya treni kwani sikutaka kuzidi kuchelewa. Kwa bahati nzuri niliweza kufika pale kabla vya vyuma vya vizuizi kuteremka na kutenganisha barabara na reli. Hata hivyo kama vile nuksi, gari langu lilizimika katikati ya reli. Nilijaribu kuliwasha tena bila mafanikio kwani sauti ilikuwa ni ya betri iliyokuwa. Moyo ulianza kunienda kasi, kwa mbali niliweza kuona taa ile kubwa ya mbele ya kichwa cha treni ikiibuka toka viwanda vya sabuni, karibu na uwanja wa Saba Saba.



“Fungua mlango toka nje!” Nilimpigia kelele Zainabu aliyekuwa bado ameketi huku amekodoa macho yake kuangalia mbele.



Alikuwa kama amepigwa bumbuwazi wala hakunisikia wala kuonyesha dalili ya kufahamu hatari iliyokuwa inatukabili. Treni ilikuwa imeanza kukaribia huku ikipiga honi kwa nguvu zaidi. Nakajaribu kufungua mlango wangu nao uligoma, nikajaribu kufungua mlango wake huku nikimtingisha, bila ya mafanikio yoyote. Nilihisi kizunguzungu na akili kuniruka.



“Zainabu, Zainabu” Nilimuita kwa sauti kali huku jasho likinitoka.



Niliweza kuliona treni likiwa umbali wa kama mita mia moja hivi huku likiendelea kujaribu kufunga breki na kupiga honi yake kwa nguvu zaidi. Bila ya shaka dereva wa treni alituona na alijaribu kwa uwezo wake wote kutuashiria tutoke hapo relini. Haikuwezekana. Nilijaribu kwa kutumia ngumi kuvunja vioo vya gari bila ya mafanikio. Ama kweli, siku ya kufa nyani miti yote huteleza, nilijikuta nikijiambia. Nilimuangalia Zainabu aliyekuwa bado ametulia kwenye kiti chake akiwa bado anaangalia mbele bila ya hofu yoyote au kuonyesha tahadhari. Niliweza kuhisi mtingishiko na mtetemeko wa reli wakati treni imetukaribia huku mwanga wa taa yake kubwa ikitumulika. Niliamua kukata tama kwani nilijua huo ndo ulikuwa mwisho wa maisha yangu. Nilijalaumu moyoni kwanini nilimpa lifti binti huyo mkosi, kwani kama nisingempa lifti ningekuwa nimetulia zangu nyumbani mida hiyo na nisingekuwa kwenye hatari ya namna hiyo.



Treni ilikuwa imetukaribia kabisa kama mita kumi hivi toka tulipo na hakukuwa na jinsi ya kuikwepa au yenyewe kusimama. Zainabu alinigeukia kwa haraka utadhania yule “Mtambaaji wa Usiku (NightCrawler)” kwenye vitabu vya X-Men. Aliikunjua mikono yake kwa kasi ya mwanga na kunikumbatia kabla tu treni halijagonga Vokswageni yangu.



“Kash Kash” Alisema neno hilo haraka kwenye sikio langu kama kwa kuninong’oneza, wakati treni ilipoligonga gari letu kwa nguvu zote.



Nilifumba macho yangu wakati wa mgongano. Sikusikia gari kutikikisika au sauti ya “bam”! Kulikuwa na ukimya wa ajabu nikiwa mikononi mwa Zainabu. Nilipofumbua macho yangu, tulikuwa bado tumekumbatiana ndani gari langu huku mabehewa ya treni yakipita ndani yatu kama vile tulikuwa ni mizuka. Niliweza kuona viti, watu, na kila kitu ndani ya treni huku treni ikiendelea kwenda kwa kasi. Sikuamini macho yangu, treni ilipita “ndani yetu” bila ya kutudhuru. Lilipofika behewa la mwisho, tulijikuta bado tuko katikati ya reli huku treni likiendelea mbele. Zainabu aliniachia na kurudi kitini na kuendelea kukodoa macho yake mbele. Nilitamani nipige kelele, sikuweza. Nilijaribu kuwasha gari tena na kwa jaribio moja tu, gari liliwaka na huku koo langu limenikauka kwa hofu nilianza kuendelea na safari.



“Zainabu, nini kimetokea pale” Nilimuuliza kwa sauti ya kutetemeka huku nikiegesha gari pembeni ya barabara ili kuvuta pumzi. Sikuamini kama nilikuwa bado hai, ndotoni, au ndo nshakufa na roho yangu bado inatangatanga.



“Unafanya nini?” Badala ya kujibu swali langu, alinirushia swali.



Nilimuambia siendi kokote hadi aniambie nini kimetokea pale, kwanini treni halikutugonga licha ya kwamba tulikuwa katikati kabisa ya njia yake. Niliegesha gari langu kama nilivyoadhimia huku vionjo vyangu vyote vikipiga kelele ya tahadhari. Nilitoka nje ya gari na kusimama pembeni huku nikihema kwa nguvu mikono yangu ikiwa imeagama kwenye dirisha la Zainabu ambaye hakutoka ndani ya gari. Aliendelea kuketi huku ameangalia mbele.



“Usitake kujua mengi Mwalimu Shija, hii Tanga” Aliniambia kwa sauti ya upole lakini iliyo thabiti.



Aliniambia si salama kuegesha hapo bali niendelee nimfikishe kwake Chumbageni na nihakikishe nimefika nyumbani kwangu kabla ya saa sita za usiku kwani anahisi kuna mabaya mengi yatatokea. Nilimwambia siendi kokote hadi anipe maelezo ya kutosha.



“Angalia nyuma yako!” Aliniambia kwa sauti ya kunitahadharisha na shari huku macho yake akiyaelekeza nyuma yangu ambapo na mimi sikuweza kujizuia bali kugeuka kufuatia alikoangalia.



Mwili ulinisisimka na nywele zikanisimama kwa ghafla utadhani paka aliyeona mbwa asiyemjua. Sikuweza kumuona mtu yeyote au kitu chochote bali nilihisi kama vile kuna mtu kasimama nyuma yangu. Kwenye kona ya jicho langu la kushoto nilihisi nimeona kivuli cha mtu au kitu kikinipitia karibu na kunitia kiza. Mwili ulipigwa na ubaridi wa ghafla na kwa sekunde chache sikujua nimeona nini au nimaluweluwe. Kabla sijamuuliza Zainabu “kulikoni” nilisikia kitu kizito kikinipiga kwenye kisogo na sikuwa na uwezo wa kukikwepa kitu hicho bali nilianguka chini kama gunia la mchanga.



Nilipozinduka nilikuwa nimeketi kwenye kiti cha dereva cha gari langu kana kwamba sikuwa nimeenda mahali popote. Gari lilikuwa limeegeshwa mbele ya nyumba kubwa ya rangi nyeupe ya “Msajili” ; (hizo ni nyumba za NHC kule Tanga) na mara moja nikatambua mahali nilipo kwani upande wa kulia kwa mbali niliweza kuona nyumba maarufu za mbao za pale Chumbageni kwenye kijiji kilichojulikana kama “Kijiji cha Miaka 20”. Zainabu alikuwa bado yupo pembeni yangu, na alikuwa akijiandaa kufungua mlango ili atoke.



“Mwl Shija asante sana” Alisema huku akitoka ndani ya gari hilo.



Sikuwa na kauli na ulimi ulikuwa umeganda kwenye taya la mdomo wangu. Nilijikuta nikimeza fundo kubwa la mate nikimuangalia Zainabu ambaye sasa alikuwa amezunguka mbele na kuja upande wa dirisha la dereva. Dirisha langu lilikuwa wazi. Aliinama kana kwamba alitaka kuniambia kitu. Kule kuinama kwake kulinipa nafasi ya kuangalia kifua chako na matiti yake yaliyokuwa yananing’inia kama embe bolibo; hakuwa amevaa sidiria. Alliegesha mikono yake kwenye ukingo wa mlango huku akiniangalia machoni, nilijifanya sikukiona kifua chake.



“Tutaonana baadaye” Alisema na kunyanyuka kuelekea iliko nyumba.



Sikuelewa alimaanisha nini aliponiambia “tutaonana baadaye” Nilimwomba Mungu kusiwe na baadaye. Alipoanza kukatisha kwenye baraza la nyumba hiyo niliweza kusikia mlio wa ‘ko ko ko’ kama vile mtu aliyevaa viatu vya mchuchumio. Nina uhakika moyoni mwangu Zainabu hakuwa amevaa viatu hivyo kwani alikuwa amevaa viatu vya wazi. Nilitazama miguu yake nione alivaa viatu gani vyenye kutoa mlio utadhani mbao ikigonga sakafu. Moyo ulinipasuka kwani sikuyaamini macho yangu. Zainabu hakuwa amevaa viatu vya mchuchumio bali miguu yake ilikuwa ya kwato za ng’ombe. Sikutaka ushahidi wa ziada. Niliingiza gia na kukanyaga mafuta sikutaka kuangalia nyuma wala nini na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi kuelekea nyumbani Majani Mapana. Moyoni, nilijikuta nikianza kusali sala ya “Baba Yetu” na ile ya “Salamu Maria”. Nilijikuta najifunza “Kukemea” kama walokole huku nikirudia maneno ya “Ushindwe katika Jina la Yesu”. Sikujua kama usiku huo ndio utakuwa wa mwisho kwangu duniani au kama nitaamka na kuiona Jumamosi. Sikujali sheria za usalama barabarani wala hofu ya ajali, kwani nilitaka kufika kwenye chumba changu ambako ningejihisi niko salama.



Kutoka eneo la kijiji cha miaka ishirini nilichukua barabara ya Pangani hadi karibu na stesheni ya treni ambako nilikata kona kulia na kuchukua barabara ya Morogoro na bila kufanya ajizi, nilikaza mwendo na kukanyaga mafuta kama nimepagawa kuelekea nyumbani. Ilikuwa nimekaribia lile eneo ambalo “nusura nipate ajali” pale Chuda, karibu kabisa na kituo cha mafuta cha BP. Kwa sababu fulani sikutaka kuangalia pale relini, macho yangu niliyakaza mbele. Nilipopita tu pale kiwanda cha sabuni, nilihisi kaubaridi kakinipuliza shingoni kwangu. Nilidhania nimeacha mojawapo ya madirisha ya gari wazi, na kwa haraka nikaangalia pembeni, na kukuta madirisha yote yamefungwa. Nywele zilinisimama tena, na mara moja nikajua kuna tatizo.



“Mwalimu Shija” Iliniita sauti ndogo ya kike, iliyonishtua utadhania nimeona mzimu wa Sokoine!



Nilijikuta nafunga breki ghafla huku gari likiserereka upande wa kushoto wa barabara. Ilikuwa inakaribia saa nne nusu za usiku wakati tukio hilo liliponikuta. Niliangalia kwenye kiti cha nyuma na kumkuta bindi mdogo Saida akiwa amekaa upande ule ule wa gari kama vile alivyokuwa ameketi wakati tunatoka Maweni. Nina uhakika Saida tulimshusha kula Masiwani kwa mama yake, na ninaapa mbele ya Mungu kuwa tulipoondoka Masiwani ilikuwa ni mimi na Zainabu tu. Jinsi gani Saida aliingia ndani ya gari sijui na sitaki kujua. Nilifumba macho yangu huku nikiyafikicha. Nilipoyafumbua tena na kuangalia ndani ya gari, Saida alikuwa ametoweka jinsi ile ile alivyoingia ndani ya gari. Sasa nilijua kuwa aidha nimeanza kurukwa na akili au ndo nimefanywa ndondocha.



Kulikuwa na watu kadhaa waliolikaribia gari langu kuangalia ni tatizo gani. Waliniuliza kama kila kitu kiko sawa au nahitaji msaada, niliwaangalia nikitamani niwaeleze yaliyonisibu na kuwaomba msaada. Kwa kiburi changu cha Kisukuma sikuweza. Niliwaambia tu kuwa nilikuwa nimesinzia kidogo kwenye usukani nilitaka nipate upepo kidogo kwani nina safari ndefu ya kwenda Korogwe usiku huo. Waliniponiacha nilivuta pumzi kidogo na niliangalia tena ndani ya gari kuhakikisha hakukuwa na mauzauza mengine. Nilipohakikisha kuwa hakuna kitu nilianza tena msafara wa kuelekea nyumbani Majani Mapana. Moyoni nilimuomba Mungu anisaidie nifike salama, na akinifikisha salama basi Jumapili iliyofuata nitaenda Kanisani.



* * *



Ilikuwa ni saa nne na nusu za usiku nilipojikuta nafungua mlango wa chumba changu kilichokuwa uwani kwenye nyumba ya Mzee Sudi karibu na duka la Mpemba pale Majani mapana. Niliingia ndani na mara moja nilienda kujitochea maji ya kunywa na kukata kiu cha muda mrefu kilichokuwa kimenikaba. Kwa sababu fulani, niliingia sebuleni, na chumbani, kuangalia kuwa hakukuwa na kitu chochote cha ajabu. Dari langu halikuwa na tundu wala nini. Kwa mara ya kwanza kwa muda wa masaa karibu matano nilijikuta najihisi niko salama. Nilivuta pumzi na kujisemea kwa kimombo “what a day?”!



Nilikuwa na njaa ile mbaya, na sikutaka hata nikae chini. Niliondoka mara moja kwa mguu kwenda kwenye duka la Mpemba kwani pembeni ya duka hilo kulikuwa na msururu wa kina mama na vijana kadhaa waliokuwa wakifanya biashara mbalimbali za vyakula. Meza zilipangwa kiustaarabu huku koroboi zikitoa mwanga hafifu kwenye genge hilo. Niliagiza samaki wa kukaanga, wali wa nazi na maharage ya nazi. Nilikaa pembeni chini ya taa iliyokuwa ikizungukwa na vijidudu na kula chakula changu huku akili yangu ikinizunguka utadhani gurudumu lililochomoka kwenye baiskeli. Nilihisi kichwa kikianza kuniuma. Nilitingisha kichwa changu na kujisemea tena “what a day”. Baada ya kula kwa haraka haraka nilianza kujikongoja taratibu kuelekea nyumbani ili nipumzike maana ilitosha kwa siku moja kupata msisimko wote huo.



Saa tano na robo hivi, nilijikuta nikijilaza kitandani kwangu huku moyo wangu ukianza kutulia. Kwa sababu fulani nilijikuta nashindwa kupata usingizi kwani akili yangu ilikuwa inajaribu kutafuta maelezo ya kina ya kile kilichonitokea jioni hiyo. Licha ya jitihada zangu kutaruta maelezo ya kujiridhisha nilijikuta nagonga mwamba. Niliendelea kujigeuza geuza hapo kitandani kwa karibu saa nzima. Ilikuwa ni majira ya karibu saa sita na nusu za usiku, nilihisi harufu ya yasmin ikiingia chumbani mwangu. Ilikuwa ni harufu ya manukato aliyokuwa amejipaka Zainabu. Nilijaribu kufumbua macho yangu katika giza la chumba changu bila ya mafanikio Nilijitahidi kuamka sikuweza. Nilijaribu kujitingisha kidogo, mwili wangu uligoma. Nilikuwa nimepigwa ganzi.



“Kash Kash!” Sauti ya kike ilisema kwa upole na kwa ulaini, na kabla sijasema au kufanya chochote usingizi mzito uliniingia.



Haikunichukua muda nilijikuta nimeanza kuota. Sikutarajia ndoto hiyo, kwani niliota mimi na Zainab tuko kwenye ghorofa kubwa na ndefu, lililokuwepo pembeni ya bahari ya Hindi, huku tukiwa tumekumbatiana kimapenzi kwenye kitanda cha sufi chenye mashuka ya hariri. Nilikuwa nimelala chali bila nguo yoyote ile huku Zainab naye akiwa uchi wa mnyama amelala pembeni yangu kuangalia upande wa bahari. Mwili wake ulikuwa ni laini na ngozi yake nyororo. Shingoni alikuwa amevaa mkufu wa dhahabu ulioendana na hereni zake, na bangili alizokuwa amevaa mkono wa kushoto. Kwa kweli alikuwa ni malkia wa malkia wote. Nililala nyuma yake huku matako yake yakiwa yamejibamiza mbele ya kiuno changu. Joto lake lilinipa ashki kupita kiasi na nilijikuta mzee akisimama na kupiga saluti.



Pole pole nilimgeuza na kumlaza chali huku nikitumia miguu yangu kumpanua. Zainab hakukaidi bali aliinyanyua mikono yake kunikaribisha kwa kunikumbatia. Alikuwa amelowa ile mbaya, na nilipojaribu kuingia, niliteleza kama vile sime inavyochomekwa kwenye ala. Sikuweza kujizuia nilianza kumkatikia, na binti huyo wa damu iliyochanganya hakuwa mwanafunzi. Kwa mahaba makubwa tulipeana mapenzi huku harufu ya maji ya chumvi  toka Bahari ya Hindi ikijaza chumba chetu. Moyoni nilisahau yote yaliyonisibu na wala sikuwa na kumbukumbu nayo. Zainabu alibana miguu yake kiunoni kwangu huku akijiviringisha kunileta miye chali. Na mimi sikukaidi kwani napenda mwanamke akiwa juu yangu na kama anajua kutumia alichojaliwa na mama yake. Zainabu alikuwa ni mwanamke wa jinsi hiyo. Alianza kunipa mavitu hadi nusura nipige kelele za furaha. Nilifumba macho yangu kufurahia penzi hilo la mtoto wa Kitanga.



Mikono yangu iliendelea kuchezea matiti ya binti huyo wakati yeye akiendelea na “vitu vyake”. Nilizungusha mikono yangu mgongoni mwake ili niendelee kumpapasa kwa raha. Viganja vyangu vilihisi vitu kama magamba mgongoni mwake. Nilijaribu tena na kugundua kuwa binti huyo alikuwa na magamba mgongoni. Mara moja nikahisi mwili wa binti yule umepoteza joto lote na umekuwa baridi kama barafu. Yeye alikuwa hajali aliendelea na shughuli. Sikuweza kuendele niliacha kumchezea mgongo na kufumbua macho yangu. Naapa maajabu haya mwanadamu hapaswi kuona na baadaye kusimulia.



“Kash Kash” Alisema tena.



Na mara hiyo chumba kizima kilijazwa na mwanga uliotoka ndani ya mwili wa binti huyo. Ulikuwa ni mwanga wenye rangi ya mbalamwezi angavu. Nilipomuangalia usoni, ndipo nilipojikuta roho ikinitoka. Zainabu alikuwa na jicho moja kwenye paji la uso wake, huku mwili wake ukiwa nusu toka juu hadi chini. Titi moja, mkono mmoja, mguu mmoja, nusu ya kila kitu. Nilimsukuma kwa nguvu na kumuondoa kifuani mwangu. Sikuweza tena kujizuia bali nilipiga ukelele kama mtoto mdogo, kuomba msaada.



Nilizinduka usingizini huku nikihisi mwili wangu wote ukipigwa na upepo mkali, na niliweza kuona kuwa jua limeanza kutoka kwani ilikuwa ni asubuhi ya siku ya Jumamosi. Nilipoangalia vizuri niligundua kuwa sikuwa chumbani kwangu, wala ndani ya nyumba, wala ndani ya hoteli. Mwenzenu nilijikuta juu ya mti wa Mbuyu huku nguo zangu zikiwa zinaning’inia kwenye matawi yake. Chini ya mti huo kulikuwa na kikundi cha watu wamezunguka wananiangalia na bila ya shaka walikuwepo hapo kwa muda mrefu.



“Baba karibu Tanga” Sauti ya mzee mmoja ilisema kwa sauti.



“Naomba msaada jamani, mniokoe” Niliomba kwa sauti ya kimasikini na nisiye na uhakika kama wanaweza kunisaidia.



Haikuchukua muda mrefu wasamaria wema hao walinisaidia kuteremka kwenye mti huo mkubwa. Sikuhitaji kuambiwa nilikuwa wapi kwani niliweza kuona wachuuzi wakianza kuleta mazao yao kwenye soko maarufu la matunda mjini Tanga. Nilikuwa pembeni kidogo ya soko la Makorola karibu kilometa kumi na tano toka nyumbani Majani Mapana. Walinipa shuka nikajisitiri. Yule mzee aliyenikaribisha Tanga alinichukua chemba na kuniuliza yaliyonisibu. Nilimweleza tangu mwanzo wa mkasa hadi dakika ile. Muda wote huo mzee hakuonyesha kushtushwa au kushangazwa. Nilipomaliza nilimsikiliza alichonacho. Mzee huyo aliniambia kuwa kilichonisibu ni shetani wa Mahaba aliyewahi kuwa mke wa Jini la Kiarabu la Kash Kash. Sikuwa wa kwanza kukutwa na masahibu kama hayo.



Nilimuuliza kama kuna dawa au madhara yoyote yaliyonipata baada ya kukutana na jini lile. Kwanza kabla ya kunijibu alitaka kujua kama nilifanya mapenzi na jini hilo kwenye ndoto. Nilimjibu ndiyo. Alisikitika sana. Aliniambia kuwa “nimeteuliwa” na jini hilo, na kwa sababu hiyo Kash Kash hataniacha nilale na mwanamke mwingine yoyote yule hadi kifo. Kwa vile nimelala na mke wake (Zainabu) basi jini hilo limeweka dai kuwa nisioe au kulala na mwanamke mwingine yoyote yule. Nilimuuliza mzee huyo kama kuna kitu chochote ninachoweza kufanya kujikinga au kujiondoa na laana hiyo.Aliniambia kuwa njia pekee ni kwenda Mabokweni kwa Sheikh Hamza Hamdani anayeweza kunipa dawa na kuniagua.



Nilifunga safari siku hiyo hiyo kwenda Mabokweni, kijiji kilichoko nje kidogo ya mji wa Tanga kwenye barabara ya kwenda Mombasa. Nilipewa masharti kadhaa ambayo ilinichukua karibu miaka mitatu kutimiza, na hatimaye ile laana ilivunjwa baada ya mimi na mimi kumtafuta mtu mgeni wa Tanga na kumtupia jini hilo. Leo hii niko salama, kwani mara tu ya kukamilisha matakwa hayo ya kijadi, niliamkua kuondoka mji wa Tanga na kurudi kwetu Mwanza. Leo hii nimeoa na nina mtoto mmoja. Anaitwa Shida. Mke wangu anaitwa Zabibu.



MWISHO

KIFO CHANGU MWENYEWE

 






......Naikumbuka vema ile siku ya mimi na wewe kuanza ukaribu zaidi licha ya kuwa tulikuwa tunasoma wote kuanzia kidato cha kwanza.

Monica hakika siwezi kuisahau siku hiyo ya graduation ya kumaliza kidato cha nne mimi na wewe pamoja na wanafunzi wenzetu.Siku ambayo nilikuomba tucheze pamoja nawe ukakubali na ndio ukawa mwanzo mzuri sana wa mimi na wewe kuingia kwenye mahusiano.Nilikuambia NAKUPENDA nawe ukakubali kuwa unanipenda japo ulitaka nisikusumbue kwa chochote mpaka tutakapomaliza mtihani wetu wa kidato cha tano

Nilikubali na hata mimi nilitaka iwe ivyo kwa sababu wote tulikuwa katika kipindi cha mwisho.

Hatimae lenye mwanzo halikosi mwisho mtihani wa kidato cha nne uliisha na sasa tukawa wanakijiji.Ni kweli japo tulikuwa hatuna kitu na tulikuwa bado tunategemea wazazi lakini mapenzi yetu yalikuwa ya dhati kabisa.Nilikupenda nawe ukanipenda na maisha yetu yale duni ya kijijini.Kwenu mlikuwa na uwezo kidogo sana na nakubuka baba yako alikuwa mwenyekiti wa kijiji na ni nyumba pekee iliyokuwa na solar pale kijijini japo ilikuwa ya nyasi.

Maisha hayakuwa magumu katika familia zetu kwani kama ilivyokawaida sisi watu wa kijijini mara nyingi tunaishi kwa kutegemea ukulima na ufugaji hivyo kuhusu chakula kilikuwepo kwa wingi

MIEZI ilienda huku mapenzi yetu yakiwa moto moto na kujikuta nimekukabidhi moyo wangu wote na sasa hatimae matokeo ya mtihaninwetu wa kidato cha nne yalitoka.

Kwa bahati mbaya wote tulijikuta tumepata daraja la nne yaani division 4 japo katika point ulikuwa umenizidi maana mimi nilipata four mbaya sana na wewe ulipata ile ya kwanza kwanza.

Sikuwa na kingine cha kufanya niliamua niungane na baba yangu katika shughuri za kilimo ili angharau nipate maisha niweze kukuoa kama nilivyokuahidi.Monicah ulifurahi sana kusikia nakuambia kuwa baada ya miaka miwili nikiweka mambo yangu sawa nitakuoa.Nilijituma katika kilimo na baba kupitia mashamba ya kwetu huku tukilima kwa ng'ombe.

Mungu si athuman mwaka wangu wa kwanza wa kilimo niliweza kupata gunia 70 za mahindi na vigunia vichache vya maharage na karanga.

Monicah ulikuwa mstari wa mbele katika kunitia moyo katika shughuri zangu.Ulinipoza kwa penzi tamu lililozidi kuozesha moyo wangu kwako.Nilijikuta nakupenda sana mwanamke wa ndoto zangu.Ulinipa ushauri kila mara ulionipa nguvu.Hatimae ukaniambia niuze hayo magunia baadhi kisha nifungue duka la bidhaa ndogo ndogo za nyumbani pale kijijini maana kijiji kizima hakuna aliekuwa na duka kubwa la kuweza kutoa bidhaa kwa wingi.Hakika hapo ndipo nilipoukubali ule msemo wa kuwa MBELE YA MAFANIKIO YA MWANAUME BASI KUNA MWANAMKE NYUMA YAKE.Hakika Monicah nilifungua duka na kuleta bidhaa kwa wingi.Duka ambalo nilifanikiwa kwa asilimia 100 katika mauzo.Hatimae siku zikaanza kusogea za ahadi ya mimi kukuoa na hata mipango ya hela ya mahali ilikuwa tayari imeanza kukaa vizuri.

MONICAH naikumbuka vizuri siku ile umekuja chumbani kwangu ukiwa umeshikilia tangazo la nafasi za kusoma katika chuo kimoja cha kusomea maswala ya NURSING.

Vigezo na alama za ufaulu zilizokuwa zimetajwa zilikuwa zinaendana kabisa na alama za ufaulu wako wa masomo yako.Monicah nakumbuka siku yenyewe uliniomba ujalibu kuomba endapo watakubali uende ukasome na kunitaka mipango ya ndoa niiailishe.Nilikubali na na kufuata ushauri wako kwa sababu nilipenda pia kuona unakuwa mwanamke msomi kwangu.Mungu alikubaliki ulichaguliwa kwenda kusoma Nursing katika chuo kilichopo mjini.Masomo hayo yalikutaka usome kwa muda wa miaka miwili kisha uhitimu.Miaka miwili kwangu si haba kuvumilia nimpendae.Uliniambia na kuniahidi kuwa ukimaliza tu masomo yako utahakikisha ahadi yangu ya mimi kukuoa wewe inatimilika.Nilikubali japo moyoni mwangu wasi wasi kubwa ilikuwa endapo kama utakutana na wanaume huko mjini wakakuteka na kukuchukua kusha ukasaliti penzi langu itakuwaje.Nilimuachia mola haya yote nikiamini yeye Muweza wa yote ataweza kukulinda wewe na penzi letu.

Monica ulianza mwaka wa masomo mapenzi yakiwa moto moto bado mimi na wewe.Tuliwasiliana kila mara hukubadilika wala hukushusha hadhi ya penzi langu.Ilifikia kipindi nilijiuliza hivi huyu anasoma chuo ambacho huko mjini hakuna wavulana.Maana hukuonyesha dalili za kubadilika wala kunichoka na kunisaliti.Kwa bahati mbaya baba yako ambae ni mwenyekiti wetu wa kijiji aliugua ugonjwa wa kukohoa damu kutokana na kazi nzito za kilimo alizokuwa anafanya na pia uvutaji wa sigara nguvu zilimuisha akawa ni mtu wa nyumbani.Alikuwa hana kazi yoyote ya kuingiza kipato.Hapo ndipo hela ya kukusomesha wewe ilipoanza kukosekana sikuona shida kuingilia jukumu la kukusomesha wewe kupitia duka langu.Nakumbuka Monicah niliuza duka mpaka nikakosa mtaji wa kuliendeleza na hatimae kufilisika.Sikuona shida kufunga duka au kufilisika kwa sababu nilijua nasomesha mke wangu wa baadae.Nililudi kwenye shughuri za kilimo na umwagiliaji ili angalau niendelee kukutumia hela za wewe kujitunza na kusoma ili umalize masomo.Nilijituma saana wakati huo duka langu nikiwa nimefunga Mungu alinisaidia nilifanikiwa kuwa napata hela na kukutumia.

Miaka miwili ilitimia hatimae ulimaliza mafunzo yako ya Nursing.Ajira nazo zilikuwa nyuma yako.kutokana na upungufu wa wauguzi hasa maeneo ya kijijini.Serikari ilikupangia kazi katika kituo cha zahanati kilichopo kijijini kwetu.Hatimae ulilejea kijijini kwetu na kuanza kazi.

Nakumbuka nilikuomba sasa nikuoe japo sikuwa na kitu na duka nilikuwa nimefunga kazi pekee niliyokuwa nimebaki nayo ni kilimo cha umwagiliaji wa bustani huku nikisubiri mvua zije nilime.Monicah uliniomba kuwa nikuoe baada ya shughuri za mavuno kuisha ili kuokoa gharama za ununuzi wa chakula wakati wa harusi na badala yake tutatumia kile nilichovuna.Pia ulinipa sababu kuwa hiyo itakusaidia na wewe kuwa tayari umeizoea kazi na pia utakuwa na hela itakayoweza kuchangia katika harusi.Hakika yalikuwa mawazo ya busara na pia niliyachekecha kichwani mwangu na kuona kweli yanamantiki.

MONICAH namlaani sana kalani muhesabisha Sensa Mathias ambae alikuja kijijini kwetu na gari lake kwa ajili ya kufanya kazi ya kuhesabu sensa.Hakuwa na sehemu ya kufikia hivyo ilibidi afikie kwa baba yako akiwa kama mwenyekiti wa kijiji.Mlimpa hifadhi yeye pamoja na gari lake.

Monicah ni nini ulichotamani kutoka kwa kalani Mathias?.Au ni lile gari alilokuja nalo pale kijijini kwetu?.Je au ni usomi wake kuliko mimi?.Pengine labda ni uvaaji wake nadhifu kuliko mimi.

Monicah uliingia kwenye mapenzi ma kalani yule na kunisahau kabisa mimi, Ulianza kubadilika na kuwa unanitukana na hali yangu duni ya kimaisha.Ukasahau kuwa ni wewe na kusoma kwako ndio kulinifanya nishuke hivi.Sikuwahi kupenda mwanamke mwingine labda ndiyo ilinifanya niteseke hivi.Ukasahau ahadi zote za mimi na wewe kuoana.Ukapenda kupanda gari na kunipita nyumbani kwetu ili niumie roho.Naikumbuka siku ile niliyopiga magoti mbele yako nikiomba uachane na karani kwa sababu nakupenda.Nayakumbuka maneno yako machafu uliyonitolea ukisema"Unanini cha kunipa wewe? Kwanza biologia inasema ukioana na mtu ambae sio msomi unazaa watoto ambao hawana akili darasani hivyo siwezi kuoana na wewe mimi nataka msomi ili nizae watoto wenye akili darasni sio watoto wa kushika jembe.Tena usinifuatilie mimi sio hadhi yako".

Maneno haya ninayakumbuka mpaka leo nikiwa hapa kitandani.Nakumbuka mate yako usoni uliyonitemea siku ile kuwa sina hadhi sikuweza kukufanya chochote kwa sababu moyoni ulikuwa bado unaishi.

Hatimae ile ahadi ya kukuoa iliamia kwa Kalani Mathias Siku ambayo nilinyanyua shingo yangu kwa mbaali na kukuona unavishwa pete ukiwa umependeza na gauni lako zuri jeupe.Nilimwangalia Mathias ambae sasa alikuwa amechukua ndoto yangu ya kukuvisha pete.Roho iliniuma sana nilianza kulia pale msibani.Jamaa zangu walinibembeleza na kuniambia kwa kejeri"Demu hasomeshwi utakuja jinyonga"

Taratibu niliondoka mpaka chumbani kwangu na kufikia kuanza kulia.Lililia kama mtoto mdogo huku nikigeuza shuka langu kama kitambaa cha kufutia machozi.Sauti za mziki harusini zilinifanya nizidi zaidi kudondosha machozi na kuwa kama mkuki uliouchoma moyo wangu

Hatimae harusi iliisha na ukachukuliwa kwenda kuishi mjini na Mathias.Alikuachisha kazi serikarini na kukutafutia kazi katika hospitali ya mtu binafsi huko mjini.Nilikaa siku tatu nikinywa uji na kulala bila kufanya chochote zaidi ya kulia.Hatimae siku ya nne niliamua kuufariji moyo na kuona kama yote ni mapito na niliamua kuendelea na shuguri zangu za shamba

ULIPITA mwaka mmoja.Nikiwa dukani kwangu tena ambako niliweza kulima na kulifufua duka sikuamini kukuona mbele ya macho yangu Monica mwanamke niliekupenda.Ulikuwanumependeza na kunenepa rangi yako nyeupe ilizidi kung'aa kwa maisha ya mjini.Nilipokutazama usoni ulikuwa unalia,Ghafla moyo wangu ulianza kuumia kukuona unalia.Ukweli ni kuwa japo uliolewa lakini moyoni mwangu ulikuwa bado unaishi NILIKUPENDA SANA na sikuwahi kupenda mwanamke mwingine.Nilikuchukua na tukakaa chini kuongea kilichokusibu.Uliniomba msamaha sana kwa ulionifanyia na kuniambia yule mwanaume sio mtu bali ni shetani kutokana na alivyokuwa anakutesa baada ya kukuchoka.Ukaniambia kuwa ni tabia ya yule mwanaume kuwa hutamani na kudanganyishia ndoa kwa mali na utajiri alionao kisha huwaacha wanawake pindi anapowachoka.Ulilia na kunitaka tuludiane na kusahau yale ya zamani.Nilikuonea huruma kwa chozi ulilotoa na hatimae nikajikuta tena nipo penzini na wewe.

SIKUJUA KAMA kufanya hivyo nilikuwa najichimbia kabuli langu mwenyewe.Miezi mitatu ilipita Monicah ulianza kuugua homa nzito iliyokufanya uanze kushuka uzito ghafla.Wazazi wako walikupeleka zahanati kwa ajili ya vipimo Maskini kumbe ulikuwa UMESHAATHIRIKA wazazi wako walificha siri na kusema kuwa unasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.Sikujua kama tayari na mimi vijidudu vimeanza kunishambulia haikupita mwezi hali ya kiafya kwangu ilianza kuwa mbaya nguvu ya kufanya kazi ilinipungua na hata mwili wangu ulianza kudhoofika.Wazazi wangu walinichukua nikiwa hoi kitandani na kunipeleka hospitali ili kupima na ndipo nilipogundua kuwa tayari UKIMWI ulikuwa umeshanitafuna.

Nilianza kulia sana nikiwa hospitari, Nilitamani sana nikuone ili nikuulize maswali niliyokuwa nayo kwanini umeamua kuniua?

Nililudishwa nyumbani nikiwa hoi kitandani macho yangu yameingia ndani mbavu zangu zinaonekana na kuhesabika.Niliomba nijikongoje nije nilale na wewe pembeni yako huku wote tukiwa hoi ili nikuulize maswali mengi niliyokuwa nayo lakini nilipoomba kuonana na wewe nililetewa taalifa ya kuwa nyumbani kwenu kuna msiba na tayari ulikuwa umefariki.

SAWA najua umetangulia na mimi ninafuata hivi karibuni.Hakuna sehemu nyingine tutakayokutana zaidi ya kuzimu kutokana na dhambi zetu.Nikifika huko naomba unijibu maswali yangu ambayo pia ninawauliza na hawa wanawake ninaowaacha hapa duniani hivi punde

๐Ÿ‘‰Ni kwanini mnakuwa na tamaa ya mali na kutamani vitu ambavyo hamna uwezo navyo

๐Ÿ‘‰๐ŸปNi kwanini sisi tusio na kitu mnatuona hatufai sana kwenye mapenzi pindi nyinyi mnapokuwa na kitu

๐Ÿ‘‰Ni kwanini hamliziki na hali ya maisha yenu mliyonayo na kupenda kusaliti mapenzi ya dhati kwa tamaa ya vitu.

๐Ÿ‘‰๐ŸปKwanini mnakuwaga na dharau sana kwa wanaume wenye maisha ya chini pindi nyinyi mnapokuwa na hadhi kidogo ya maisha?

Maswali haya naimani itabaki kuwa fundisho duniani na pia kokote niendako nikikuona nitakuuliza ewe monicah Muuaji wa roho yangu



FUNZO

* * * * * * * * * * * * * *

.....Usitamani kuwa na baiskeli ikiwa uwezo wako ni kutembea kwa miguu.

Usitamani pia kuwa na pikipiki ikiwa uwezo wako ni kutembea kwa baiskeli

Usitamani pia kuwa na gari ikiwa uwezo wako ni kutembea kwa pikipiki.Ki vyovyote vile kwenye maisha usitamani kitu chochote ambacho huna uwezo nacho maana huwezi jua madhara yake baadae.

Nataka nikufundishe kitu kimoja.Nafikili ulikuwaga unapewa sana hela ya kula shule hasa ulipokuwa shule ya msingi.Huenda mzazi wako alikuwa anakupa kila siku mia au miambili.Sasa basi huenda siku moja mgeni alikuja kwenu akakupa hela kubwa zaidi kama shilingi 5000 ya kutumia.Kwa haraka haraka ukiulizwa kati ya mzazi wako na mgeni nani aliekupa hela kubwa utajibu ni mgeni.

Lakini nataka nikuambie mzazi wako amekupa mia mia kila siku mpaka umefika darasa la 6 na mgeni kakupa elfu 5000 ya siku moja leo umemuona mgeni wa dhamani sana kuliko mzazi ni kwasababu umesahau vile vidogo vidogo wazazi walivyokutendea kwa kikubwa cha siku moja

Ninamaana hii.Monicah alisahau thamani ya kusomeshwa na mpenzi wake kwa thamani ya gari ya Mathias na wakati tukikusanya pesa zile kidogo kidogo alizokuwa akipewa na mpenzi wake mpaka kufikia hatua ya kumaliza chuo ni zaidi ya thamani ya ile gari ya Mathias.

OKY Wacha niishie hapo kutoa fundisho maana nahisi kuna mtu kama vile hanielewi hata niongee vipi.


SIJAKUSALITI WEWE MUME WANGU

 








Sijakusaliti wewe Mume wangu....



Alimfuata mumewe chumbani, muda huo watoto walikua wameshalala. Mumewe alikuwa 'busy' akisoma gazeti. 



Akamtazama mumewe kwa macho yaliyojaa huruma na huzuni, akaanza kuongea. "Mpenzi wangu, kuna kitu nataka nikiri kwako."



"Kitu gani?" Mumewe akamuuliza huku macho bado yakiwa kwenye gazeti alilokuwa akisoma. Mke akaendelea "sijawa muaminifu." Mume akatupa gazeti pembeni na kusimama huku akimkodolea macho mkewe.



Akamsogelea na kumchapa kofi, kwa mara ya kwanza katika ndoa yao ya miaka kumi alimpiga mkewe. "Kwanini wewe mwanamke, ndoa ya miaka kumi watoto watatu, na kila kitu nakupa ndio unifanyie hivi kweli??"



Mume akaendelea kufoka "Umenisaliti? , Umenidharau sana" wewe ndiye kila siku umekua ukinisisitiza nikae mbali na wanawake, najitahidi kuwa muaminifu kwako kumbe mwenzangu kwa upande wako unanisaliti kweli??"



Akiwa anataka amkabiri kwa kofi jingine, wakasikia mtu akipiga hodi mlango wa chumbani kwao, binti yao wa kwanza wa miaka 9 aitwae Maria aliingia ndani. "Baba na mama kuna tatizo?" Maria aliuliza.



"Toka, toka nje" Mumewe alimfukuza binti yake! Binti akaogopa. Mama akamwambia " Maria mwanangu nenda ukalale kesho shule, kila kitu kipo sawa ee mama." Maria akaitikia kwa shingo upande na kutoka nje.



"Ehee niambie ni nani? Ni nani ambae unavunja nae uaminifu? Nipe namba zake za simu. Leo atanitambua" mume akaendelea kufoka na kumnyang'anya mkewe simu. "Nioneshe picha na namba yake ya simu haraka"



Mkewe akaichukua simu yake kutoka kwa mumewe, akaipekua na kumuonesha mumewe "Huyu ndio mwanaume ambae nimevunja nae uaminifu" mumewe akatazama simu na kuiona picha ya Biblia. Akashangaa..akauliza nini maana ya hii?



Mkewe akajibu "Ndio sijawa muaminifu kwa Mungu wangu, nimekua busy nikikupenda wewe tu mpaka nimemsahau Mungu. Yote ni jitihada za kuwa mke bora kwako"



Mke akakaa chini. Akaanza kuongea .....



"Tulipokutana mwanzoni nilikuwa namtumikia sana Mungu wangu. Na nakumbukuka kabisa uliniambia sababu kubwa ya kunkchagua na kunioa mimi ni kwa sababu nilikuwa namtumikia Mungu"



"Nilikupenda kwa sababu na wewe ulikuwa na hofu ya Mungu, tulikuwa tukisali pamoja, tukiombea mahusiano bora na kuwa na familia yenye tija.,"



"Mungu ametujalia na baraka tele, familia ina furaha, mali za kutosha, amekupa kazi nzuri, umemaliza na PhD yako hivi karibuni tu.



Mke akamtazama mumewe kwa macho ya upole yaliyojaa huzuni kubwa. Muda huo mumewe akashusha pumzi na kuketi kochi lilikuwemo mle chumbani.



Mke akaendelea....



"Miezi ya mwanzo baada ya ndoa yetu, tulikuwa tukisali pamoja kama familia, tukienda pamoja kanisani, semina mbalimbali na masomo ya Biblia."



"Ila sasa tumekana yale maandiko yasemayo 'chagueni leo mtakaemtumikia, mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA' ..tumezaa watoto, tunawalea alimradi tu, hawamjui Mungu na wala mlango wa nyumba ya ibada hawaujui."



"Kutokana na mafanikio tumebadili hata marafiki, tumeona marafiki wampendao Mungu kama ni wasumbufu. Tumeanza kuabudu mali, pesa na mafanikio"



"Angalia tulivyo sasa, tunanyumba kubwa ila Mungu hayupo. Umeanza kunipeleka maeneo ambayo ni chukizo kwa Mungu wetu, tumeanza kunywa sana pombe, ulevi wetu umekua aibu tupu kwa watoto wetu" Mume akatizama chini kwa aibu!



"Kwa sababu ya upendo wangu kwako, nikajikuta nafanya yale ambayo unayapenda nikifikiri kuwa mke bora ni kufuata kila jambo unalolifanya. Nikashindwa kabisa kukuombea, nikafeli kukurudisha kwa Mungu. Wote tukapotea!



"Nikapotea kiasi ya kwamba nikawa na majivuno, shallow na self-centered; yote nikifikiri kwamba mimi ni mke bora. Ila huyu sio mimi. Nimebadilika sana kutoka yule mwanamke uliyeniona kwa mara ya kwanza. Wote tumebadilika mno na tumepotea katika kiza kinene.



"Vyote hivi, Nyumba nzuri, magari, chakula kizuri tunachokula, pesa tulizonazo vimetufanya tumsahau aliyetupa. Mimi si kitu bila ya Mungu na nimejikuta na aibu kuu kwa usaliti huu juu ya Mungu wangu. Ndio nimemsaliti Mungu."



"Tumeanza kuwa na migogoro isiyokwisha ndani ya ndoa, yote haya ni kwa sababu MUNGU hayupo kati yetu. Tunaendesha upendo wetu sisi kama sisi na tunakolekea tutafeli kabisa!!



"Nataka nirudi kuwa mwanamke yule uliyenikuta mwanzo. Mwanamke mwenye hofu ya Mungu. Nimeikumbuka mno amani ya Mungu wangu. Nimekumbuka kumuabudu yeye. Nimekumbuka kusali na wewe Mume wangu. Ni ipi faida kwangu kuwa na ndoa nzuri lakini nimpoteze Mungu wangu? Ninarudi kwa Mungu."



Akaendelea.....



"Mwanamke anaenyenyekea na kuomboleza kwa MUNGU ndie atakaekuwa mke bora na mama bora kwa watoto wake. Apatae mke amepata kitu chema na amepata kibali kutoka kwa Mungu, sitaweza kukupa kibali kama sitarudi kwa Mungu wangu. Nataka maisha yangu na Mungu yarudi. Nataka Mungu arudi katika familia yetu!



Mke akamaliza kuongea huku machozi yakimtoka. Mume akainuka kutoka kwenye kochi, huku machozi yakimrenga akamfuata mkewe, akambusu kwenye paji la uso, akamkumbatia, akamfuta machozi na akamwambia;



"Nisamehe mke wangu, nisamehe kwa sababu mimi ni kichwa, na kichwa kikipotea na mwili hufuata kupotea kwa kichwa. Ulichagua kuolewa na mimi kwa sababu uliiona hofu ya Mungu ndani yangu. Hata mwenyewe nimekumbuka sana ule uwepo wa Mungu ndani yangu"



"Ndoa isiwe kizuizi katika njia yetu kumfuata Mungu. Mawazo kwamba unanisaliti yaliuralua moyo wangu vipande vipande. Sasa nashindwa ku-imagine Mungu anajisikiaje sisi tunavyokua sio waaminifu kwake"



"Mungu ametubariki na vyote hivi, ni kweli lazima tumrudie yeye. Namimi nataka kurudi kwa Mungu, nataka zaidi kutoka kwa Mungu wangu kuliko haya mambo ya kupita ya duniani hapa. Nataka mungu wa ujana wangu!"



"Samahani kwa kukuchapa kibao, ni hasira za kudhani unanisaliti kumbe hukua unamaanisha usaliti nilioufikiri mimi!"



Usiku ule walisali na kutubu pamoja. Wakaanza kuwafundisha watoto wao ukuu wa Mungu, familia ikawa na furaha na Mungu akarudi katika familia yao!



M W I S H O .



Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.

Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.

Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo."

BLOG